Polisi nchini Tanzania inawashikilia
watu wa nane kwa madai ya kuhusika
na mlipuko wa siku ya jumapili katika
kanisa Katoliki la Olasit viungani mwa
mji wa Arusha.
Miongoni mwa washukiwa ambao
wako mikononi mwa polisi ni raia
wanne wa Saudi Arabia, na wengine
wanne ni raia wa Tanzania.
Wakati mwandishi wa BBC Baruan
Muhuza akuzungumza akiwa
hospitalini mjini Arusha amesema
idadi ya watu waliofari dunia kufuatia
mlipuko huo ni wawili na wala sio
watatu kama ilivyoripotiwa hapo
awali.
Polisi mjini Arusha vile vile
wamethibitisha kuwa waliokufa wakati
wa tukio hilo la kigaidi ni wawili.
Kwa wakati huu polisi wanachunguza
ni kulipuzi aina gani kilitumika wakati
wa shambulizi hilo.
Lakini Baruan Muhuza ambaye
alitembelea eneo la tukio mbali na
majeruhi hakuna hasara kubwa
iliyotokea mahali hapo pia sakafi na
kuta za kanisa hilo hazikuchimbika
sana.
Kutoka Dar es Salaam Leornad
Mubali anaongezea kuwa watu wawili
sana wamethibitishwa kufariki dunia
katika mlipuko huo uliotokea majira ya
saa tano asubuhi katika kanisa katoliki
la Olasit nje kidogo ya mji wa Arusha
nchini Tanzania na wengine kadhaa
kujeruhiwa huku balozi wa papa na
watawa waliokuwa katika shughuli
hiyo maalumu ya uzinduzi wa parokia
mpya ya mtakatifu Yosefu mfanyakazi
wakinusurika pia .
Kwa mjibu wa Padri Festus
Mangwangi ambaye ni paroko
msaidizi wa kanisa katoliki jimbo la
Arusha mlipuko huo unapotokea
walikuwa tayari katika hatua ya
kubariki maji kwaajili ya uzinduzi wa
kanisa ulikuwa ukiongozwa na balozi
wa Papa Fransis.
Hata hivyo Padre Mangwangi
ameiambia BBC kuwa taarifa
walizonazo muda mfupi baada ya
majeruhi kukimbizwa hospitali watu
kati yao wamefariki huku wengine
wakiendelea kupatiwa matibabu katika
hospitali ya Mount Meru mjini
Arrusha.
Shughuli zote kuhusiana na ibada
hiyo zimesitishwa huku watalaalamu
wa milipuko na polisi wakiendelea na
uchunguzi kuhusiana na mlipuko
huo.
Bado hakuna taarifa zozote kuhusiana
na chanzo halisi cha bomu hilo ama
kundi lolote linalodaiwa kuhusika na
utegaji wa bomu hilo.
Hili ni shambaulio la kwanza la bomu
nchini Tanzania japo kuwa mwaka
huu pia kulikuwa na mtukio ya mauaji
ya Padre wa kanisa hilo visiwani
Zanzibar ambaye alipigwa risasi
wakati akiwa anajiandaa kuingia
kanisani.
Chanzo:BBC