Rais wa klabu ya Real
Madrid,Florentino Perez amewaambia
waandishi wa habari jumatatu jioni
kuwa Mourinho hatofukuzwa bali
wamekubaliana kumaliza mkataba
wao na kocha huyo raia wa Ureno.
Aidha Madrid, imeongeza kuwa
haijaanza mazungumzo na kocha
yeyote kwaajili ya kuchukua nafasi ya
Mourinho lakini vyanzo mbalimbali
vya habari za michezo zinamtaja
kocha wa PSG ya Ufaransa, Carlo
Ancelloti kuchukua jukumu la
kuifundisha Madrid msimu ujao.
Duru za kimichezo zinasema, Jose
Mourinho huenda akarejea nchini
Uingereza kuifundisha klabu yake ya
zamani ya Chelsea baada ya kuwepo
makubaliano baina yake na uongozi
wa klabu hiyo.