Baada ya Bunge kuahirishwa jana,
nje ya ukumbi hali haikuwa nzuri
baina ya Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge
wa Same Mashariki (CCM), Anne
Kilango Malecela.
Mtafaruku huo uliibuka baada
ya Kilango kusikika
akimtuhumu Lissu kwa
uchochezi, akisema kwamba
amekuwa mbunge pekee
anayeongoza kwa vurugu.
Maneno hayo hayakumfurahisha
Lissu ambaye alishindwa
kuvumilia na kumgeukia Kilango
kwa nguvu huku baadhi ya
wabunge wakishuhudia na
wengine wakimzuia Lissu.