KOMLA DUMOR AFANYIWA IBADA

Familia, jamaa, marafiki pamoja na wafanyakazi wenza wa mwandishi wa BBC aliyeaga dunia wiki mbili zilizopita, Komla Dumor, wanakusanyika hii leo mjini London kwa ibada maalum.

Ibaada hiyo itafanyika katika kanisa ya Matakatifu Martin katika eneo la Trafalgar Square mjini London.

Ibaada hiyo itahudhuriwa na maafisa kutoka ubalozi wa Ghana pamoja na raia wa Ghana wanaoishi London.

Komla Dumor ayekuwa mtangazaji na ripota wa BBC idhaa wa dunia alifariki kutokana na mshtuko wa moyo.

Viongozi na watu mashuhuri barani Afrika wamekuwa wakimsifu sana mwenda zake wakisema kuwa aliwakilisha Afrika vyema katika safu ya kimataifa kwenye sekta ya habari.

Baadhi pia wamesema kuwa Komla alikuwa mwandishi mahiri ambaye alikuwa mfano mzuri kwa vijana wanaochipukia kazi ya uandishi barani Afrika.

Unaweza kutazama ibaada hiyo hapa:http://goo.gl/BYkA2e

Kifo cha ghafla cha Komla Dumor kimewashtua wengi sana barani Afrika.

BBC imewapoteza waandishi wake wawili mahiri katika wiki mbili zilizopita akiwemo Ann Waithera aliyefariki kutokana na Saratani ya ubongo mjini Nairobi.