Kipindi cha kwanza cha mchuano kiliisha bila mabao.
Wakati wa kipindi cha pili, Alex Oxlade-Chamberlain, aliweza kuingiza bao lake la kwanza msimu huu baada ya kuingiza pasi ya Santi Cazorla.
Palace walipata fursa ya kuingiza bao la kusawazisha lakini pasi ya kichwa ya Cameron Jerome iliokolewa na Wojciech Szczesny.
Oxlade-Chamberlain aliongeza bao la pili kutokana na pasi ya Olivier Giroud.
Matokeo hayo yanaiweka Arsenal kifua mbele kwa alama juu ya Manchester City, ingawa vijana wa Manuel Pellegrini,wanaweza kuchukua nafasi ya kwanza ikiwa watashinda Chelsea katika uwanjawa Etihad katika mechi ya leo.
Lakini Arsenal, wanaojitahidi kupata ushindi wa ligi, walipata pointi tatu na kusonga mbele ya Liverpool kwa pointi tatu.
Wanatarajiwa kumenyana na watani wao Manchester United baadaye.