SHERIA YA KUWEZESHA WAZAWA KWENYE GESI YAJA

RAIS Jakaya Kikwete amesema serikali ipokwenye hatua za mwisho za kuandaaa sheria, kanuni na taratibu kwa ajili ya uwekezaji wenye tija kwa wazawa katika sekta ya gesi na mafuta.

Alisema kazi hiyo itafanywa na Bunge laAgosti mwaka huu ambapo miswada ya sheria hiyo itajadiliwa.

Rais Kikwete alisema hayo Dar es Salaam jana wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 19 la mwaka lililozindua pia ripoti ya utafiti wa Shirika la Utafiti na Kupunguza Umaskini (REPOA).

"Baada ya kugundulika kwa zile kyubiki futi za ujazo milioni 46 wa gesi… kazi iliyopo ni kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya rasilimali ile kwa manufaa ya Watanzania wote inapatikana ili Oktoba mwakani nistaafu kwaamani," alisema Rais Kikwete.

Alisisitiza kwamba lazima serikali na wadau muhimu wa sekta hiyo wajiridhishe kwamba hakuna wizi ili kumletea mwananchi wa kawaida maendeleo na kuzuia hujuma, wizi na rushwa kwa lengo la kuleta matokeo chanya.

Akizungumzia tafiti zinazofanywa na REPOA alisema: "Tafiti hizi za kila mwaka zimekuwa na msaada mkubwa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo, wakulima na wananchi wa kawaida katika kufanya uamuzi sahihi kwenye maeneo."

Alisema kwamba Tanzania zipo ajira ndogo ndogo milioni tatu zinazohusisha wananchi milioni 5.2 huku kati yao asilimia 64 ni wanawake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA, Profesa Samwel Wangwe, alisema kwamba tafitihizi zinalenga kuwasaidia wananchi wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo ili kupunguza umaskini.

Alisema malengo ya tafiti pia ni kuongeza tija kwa kupata uzoefu kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni jinsi ya kujenga viwanda, usindikaji wa chakula na kupambana na tatizo la ajira hasa kwa vijana na wanawake.