Akizungumza na wandishi wa habari katibu mkuu kiongozi Mh Ombeni Sefue amesema serikali imesikitishwa sana kuona wapo baadhi ya watu wanaodhiriki kusema kuwa hati hiyo haipo.
Akasema pia kwamba ni kwa busara za mwenyekiti wa bunge maalum l katiba akiona kuna haja ya hati hiyo kupelekwa katika bunge maalum serikali ipo tayari.
Aidha akasema kuwa zipo hati ambazo serikali inazihifadhi kwa umakini mkubwa ili kuhakisha kuwa zinaendelea kubaki salama kwa kizazi cha sasa na kizazi kijacho.
Kiongozi huyo akaongezea kuwa ni matumaini ya serikali kuwa baada ya kuitoa hati hiyo hadharani watu wataendelea na mambo ya msingi yaliyopo mbele yao na siyo kuendeleza malumbano ambayo hayana tija kwa taifa.
Chanzo: ITV