AFISA MASOKO COCA-COLA AUWAWA

OFISA Masoko wa Kampuni ya vinywaji ya Coca-Cola, Steven Mbilo (40), amefariki dunia baada ya kupigwa risasi maeneo ya kifuani.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, ACP Wankyo Nyigesa, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 12:00 asubuhi katika Kijiji cha Mtiri, Tarafa ya Ifwagi, wilayani Mufindi.

Nyigesa alisema marehemu baada ya kupekuliwa alikutwa na sh milioni 4.7 pamoja na simu yake ya mkononi.

Alisema hadi sasa watu wawili wanashikiliwa na Jeshila Polisi kutokana na kuhusishwa na mauaji hayo ambao ni Paschal Benedict(44) mkazi wa Tunduma na Seleman Juma (42) mkazi wa Soweto.

Alisema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ilikubaini chanzo cha kifo hicho.

Wakati huo huo, Aloyce Mlimakifye (60) mkazi wa Mtitu, amekufa maji baada ya kutumbukia kwenye Mto Kikonde.

Kamanda huyo alisema kuwa tukio hilo lilitokea janasaa 12:30 asubuhi katika kijiji hicho Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa huku akieleza kuwa chanzo cha kifo hicho kimetokana na ulevi.