MADAKTARI WAKUZA UKE KATIKA MAABARA

Madaktari nchini Marekani wamefanikiwa kuwatengezea wanawake wanne sehemu ya uke kwa njia ya kisayansi.Walitumia mfano wa seli ya uke na mifupa ya mwili kuweza kukuza uke huo katika maabara kwa kuzingatia wastani na umbo la kila mwanamke.

Baada ya matibabu hayo, wanawake hao wote inaarifiwa walielezea kupata hisia sawa na kamilifu,matamanio, kuridhishwawakati wa tendo la ndoa pamoja na kutopata maumivu yoyote wakati wa tendo la ndoa.

Wataalamu walisema kuwa utafitiwao, ambao matokeo yake yalichapishwa katika jarida la kisayansi la Lancet, ni mfano wa hivi karibuni wa nguvu za mbinu tofauti na za kisasa za matibabu.

Wanawake hao walizaliwa na uke ambao haukuwa umeumbika vyema yaani ulikuwa na kasoro ya maumbile , tatizo linalojulikana kama 'vaginal aplasia.'

Matibabu ya kisasa kwa tatizo kama hilo la kiafya yanaweza kuhusisha upasuaji ambapo ngoziau sehemu ya utumbo inatumika.

Celi zilichukuliwa kutoka kwa kizazi cha kila wanawake hao ambacho kilikuwa na kasoro ya maumbile na kukuzwa katika maabara ili kuweza kuzaana.

Picha za kizazi cha wanawake hao zilitumia kuwarekebishia uke wao.

Hili bila shaka ni jambo geni katika sayansi ya matibabu na piainatoa taswira ya mambo yatakavyokuwa katika siku za usoni.

Jambo la Kutumia celi za mwili kubadilisha maisha ya wagonjwa tayari limefanyika na kuwasiaidia wagonjwa kupata kibofu cha mkojo, mishipa ya damu na koo.

Sasa unaweza kuongeza kwenye orodha hiyo, uke na pua.