WAPIGANAJI LIBYA WAVAMIA BUNGE

Watu waliokuwa wamejihami walivamia majengo ya bunge nchini Libya Jumanne jioni na kulazimisha wabunge kusitisha shughuli ya kumteua waziri mkuu mpya.


Maafisa wanasema kuwa wabunge waliondoka bunge punde waliposikia milio ya risasi.


Hatua ya kupigia kura waziri mkuu mpya imetokana na kujizulu kwa aliyekuwa waziri mkuu Abdullah al-Thinni, aliyeondoka mamlakani mapema mwezi huu baada ya yeye pamoja na familia yake kulengwa na wapiganaji.


Libya imekuwa ikikumbwa namgogoro tangu harakati za kumuondoa mamlakani hayati Muammar Gaddafi mwaka 2011.


Awali ripoti zilisema kuwa watu kadhaa walijeruhiwa katika mashambulizi siku ya Jumanne.

Haijulikani nani aliyehusika na shambulizi hilo.


Mwandishi wa BBC mjini Tripoli, Rana Jawad anasema kuwa bunge la Libya limewahi kuvamiwa na watu waliojihami katika kipindi cha mwaka mmoja unusu iliopita.


Wabunge wamekuwa wakitofautiana kuhusu kuteuliwa kwa waziri mkuu wakati shambulizi la Jumanne lilipotokea.

Tayari walikuwa wamefanya duru ya kwanza ya kura na kuwateua wagombea wawili kati ya saba.


Lakini duru ya pili ilipoanza ndipo watu hao waliposhambulia bunge na kulazimisha wabunge kuahirisha shughuli hiyo ambayo sasa itafanyika tarehe 4 mwezi Mei.

WEZI KUKATWA MIKONO NA WAZINIFU KUPIGWA MAWE

Serikali ya Brunei iliyo Kusini Mashariki mwa Bara Asia, itaanza kutumia sheria kali za kiisilamu.

Kiongozi wa nchi hiyo ya kiisilamu ambayo ni jirani na Malaysia ametangaza kuwa sheria hiyo itaanza kutumika kuanzia wiki hii.


Adhabu zilizo chini ya sheria za kiisilamu ni pamoja na kuwakata wezi mikono na kuwapiga mawe hadi kufa watu waliopatikana na hatia ya kushiriki Zinaa.

Sheria hii itatekelzwa katika awamu tatu katika kipindi cha miaka mitatu.

Umoja wa Mataifa tayari umeelezea wasiwasi wake kuhusu sheria hiyo.


Taifa la Brunei tayari linafuata sheria kali za kiisilamu kuliko hata nchi jirani kama Malaysia na Indonesia pamoja na kuharamisha uuzaji na utumiaji wa pombe.


Nchi hiyo ndogo ilio katika kisiwa cha Borneo, inatawaliwa na Sultan Hassanal Bolkiah na imepata utajiri wake kutokana na kuuza nje mafuta na gesi yake.

Takriban nusu ya waisilamu wanaoishi katika nchi hiyo ni raia wa Malaysia.


Sultani alinukuliwa akitangaza hatua ya kwanza ya kuanza kutumiwa kwa sheria hiyo akimshukuru Mungu na kuwatahadharisha wananchi kuhusu kuanza kutumika kwa sheria hiyo.


Sheria yenyewe itaanza kutumika katika kipindi cha miaka mitatu huku hukumu ya makosa ya kwanza ikiwa kifungo cha jela pamoja na kutozwa faini.


Katika awamu ya pili ndipo wahalifu wataanza kukatwa mikono kwa watakaopatikana na hatia ya wizi , huku awamu ya tatu ikihusu kupigwa mawe wazinifu na wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.


Sultani anayetawala kisiwa hicho ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani na tayari amewaonya watu kukoma kushambulia mipango yake kupitia mitandao ya kijamii.

Mfumo wa sheria katika mahakama nchini humo ni sawa na ule wa Uingereza.


Umoja wa Mataifa uliitaka serikali kuchelewesha mageuzi hayo ili kuhakikisha kuwa sheria hiyo inaambatana na sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu.

TSVANGIRAI AMTIMUA HASIMU WAKE

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe, Morgan Tsvangirai aliyetimuliwa kutoka katika uongozi wa chama chake cha MDC amesema kuwa hasimu wake katika chama hicho Tendai Biti, naye ametimuliwa pamoja na wanachama wengine 8.'Bwana Biti ni mtegemea tu cha wengine ambaye anatumiwa na rais Robert Mugabe,'' alisema Tsvangirai.


Mnamo siku ya Jumamosi, mrengo mmoja wa chama hicho unaoongozwa na Biti ulisema kuwa Tsvangirai, alisimamishwa uongozi wa chama kwa muda, kwa sababu ya kukosa uwezo wa kuongoza chama hicho.

Mgawanyiko katika chama cha MDC, unakuja baada ya chama hicho kushindwa vibaya katika uchaguzi uliofanyika 2013.


Uchaguzi huo ndio ulikuwa mwisho wa muungano uliokuwepo kati ya chama tawala Zanu-PF na MDC ulioundwa baada ya uchaguziwa mwaka 2008 uliokumbwa na utata.


Tsvangirai na Bwana Biti, ambaye ni katibu mkuu wa chama cha MDC walikuwa washirika kwa muda mrefu katika kampeini yao dhidi ya Mugabe, ingawa walitofautiana Julai mwaka jana.


Tsvangirai alisema Biti na wanachama wenzake aliowaita waasi, wameondolewa katika vyeo vyao kama wabunge.


"Alituhadaa, Mwanamume huyu hata haamini chochote isipokuwa mamlaka,'' alisema Tsvangirai kuhumusu Biti.


Mnamo siku ya Jumamosi mrengo wa bwana Biti ulisema kuwa baraza la chama cha MDC lilipiga kura kumondoa Tsvangirai kutoka katika uongozi wa chama hicho, wakisema kuwa chama hicho kimeguzwa na kuwa kama himaya ya mtu mmoja.


Kwa upande wake Tsvangirai alipuuza mkutano huo kama usio halali na ulio kinyume na katiba

Wafausi wengi wa MDC, wana wasiwasi kuwa malumbano hayo yanaweza kuimarisha utawala wa Mugabe na chama chake na wanatumai kuwa wataweza kusuluhisha tofauti zao.

AJINYONGA BAADA YA KUMKUMBUKA MKEWE

MKAZI wa Mtoni Kijichi, Richard Kijazi (36) amekutwa amekufa kwa kujinyonga chooni na kuacha ujumbe kwamba amejiua kwa sababu ya kumkumbuka marehemu mkewe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo, alisema jana kuwa Kijazi alijiua juzi saa 11:15 jioni katika maeneo ya Mtoni Kijichi, Wilaya ya Temeke.

Alisema Kijazi alikutwa amejinyonga kwa kutumia kitambaa cha nguo alichokitundika kwenye kenchi ya choo ya nyumba anayoishi.

Ujumbe uliokutwa katika eneo hilo ulisomeka:

"Hajahusika mtu yeyote kuhusu hili, nimemmiss Mama John wangu, nizikwe Dar es Salaam na Mchungaji Haule naomba ujumbe huu uheshimiwe."

Kwa mujibu wa Kamanda Kiondo, uchunguzi wa awali umebaini kuwa Mama John alifariki mwaka 2012 baada ya kuugua malaria na tangu wakati huo Kijazi alikuwa akijaribu kujiua na kuokolewa na ndugu zake.


Maiti amehifadhiwa katika Hospitaliya Temeke. Katika tukio jingine, Kamanda Kiondo alisema, Mwendesha Pikipiki, Said Jongo (32)amekufa papo hapo baada ya kugongwa kwa nyuma na gari aina ya Toyota Coaster lenye namba T412 ATJ.


Ajali hiyo ilitokea juzi saa 12:00 jioni katika Barabara ya Chamazi eneo la Charambe Magengeni, ambapo gari hilo likiendeshwa na mtu asiyefahamika akitoka Mabagala Rangi Tatu kwenda Chamazi, liligonga kwa nyuma pikipiki yenye namba T281 CKY ainaya Fekon, iliyokuwa ikiendeshwa na Jongo.

Mwili wa Jongo umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke na dereva wa gari hilo aliyekimbia baada ya ajali bado anatafutwa, gari liko katika Kituo cha Polisi Mbagala.


Katika tukio la tatu, mkazi wa Majohe aliyetambuliwa kwa jina la Erasmus Marshal (52), amekutwa amekufa chumbani kwake huku mwili ukiwa umeanza kuharibika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema mwili wa Minangi ulikutwa juzi saa 7:00 mchana huko Majohe Kichangani ukiwa umekaa kitandani huku umefunikwa shuka na mezani kwake kulikutwa mabaki ya chakula aina ya utumbo na soda ya Azam Malta.


Uchunguzi wa awali kwa mujibu wa Kamanda Minangi, umeonesha kuwa enzi za uhai wake alikuwa akiishi peke yake kwenye nyumba hiyo na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

MAJAMBAZI YAUWA POLISI WAWILI

ASKARI Polisi wawili kutoka Tarafa ya Usoke wilayani Urambo mkoani Tabora, wameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Suzan Kaganda, alisema mauaji hayo yamefanyika juzi saa 2: 30 usiku katika kijiji cha Usoke wilayani Urambo.


Kamanda Kaganda aliwataja askari waliouawa kuwa ni PC Shabani, mwenye namba G 3388 ambaye alikufa papo hapo baada ya kupigwa risasi na majambazi hao.

Mwingine ni PC Jumanne mwenye namba F.5179, aliyejeruhiwa tumboni na baadaye kufa jana saa 4asubuhi, katika Hospitali ya Rufaa yaMkoa wa Tabora Kitete, alikokuwa akipatiwa matibabu.


Akisimulia zaidi tukio hilo, Kamandahuyo alisema majambazi hao walikuwa watatu na kabla ya mauaji hayo, walivamia nyumbani kwa mfanyabiashara Ibrahim Mohamed, ambaye ni mkazi wa Usoke na kupora fedha taslimu Sh 1,200,000.


Mbali na uporaji wa fedha, pia walipora vocha za simu aina mbalimbali zenye thamani ya Sh 120,000 ambapo baada ya askari hao kupata taarifa ya uhalifu huo, walienda eneo la tukio kutoa msaada zaidi.


Kamanda huyo wa Polisi, alifafanua kuwa askari hao wakiwa mita chache kabla ya kufika katika eneo la tukio, walikutana na majambazi hao na kuanza kuwafyatulia risasi kwa kasi na kumuua PC Shaabani.


"Ndugu zangu waandishi wa habari hili ni pigo kubwa sana kwa Jeshi la Polisi, lakini naapa kuwasaka hadi kuwakamata wakiwa hai au wafu…tumechoka na uhalifu huu," alisema Kaganda.


Kamanda Kaganda alisema kabla ya mauaji ya askari hao, majambazi hao walifyatua risasi hovyo hewani kwa lengo la kuwatisha raia ambapo maganda 25 ya risasi aina ya SMG na SAR yameokotwa katika eneo la tukio.

Kutokana na mauaji hayo, Polisi mkoani Tabora wanaendesha msako mkali usiku na mchana, ambapo tayari hadi sasa watu watano wametiwa mbaroni na Polisi wakituhumiwa kuhusika na mauaji hayo.


Kamanda Kaganda alitoa mwito kwa wananchi mkoani Tabora, kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zitakazowezesha kuwabaini majambazi hao.


Akizungumzia mauaji hayo jana katika ofisi za Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshila Polisi, Paul Chagonja, alitoa pole kwa wananchi wote waliofiwa na ndugu zao.


Alisema Jeshi la Polisi limeanzisha msako mkali wa majambazi hao ili wakamatwe na kufikishwa mahakamani na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu wa aina yeyote ile, ili wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake.

WARIOBA ATAJA WASALITI WA MWALIMU NYERERE

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadilikoya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema wanasiasa wanaomtuhumu kwa kumsaliti Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuhusu Muungano, ndiyo wasaliti kwa kuwa waliingiza kwenye Katiba, mambo yanayo kinzana na makubaliano ya Muungano huo.


Jaji Warioba amesema usaliti huo ni pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuondoa mamlaka ya Bunge la Muungano katika utungaji wa sheria, kuitambua Zanzibar kuwa nchi inayojitegemea na kuongeza mambo ya Muungano bila kufuata Katiba.

Ametoa kauli hiyo kujibu mwendelezo wa lugha za kejeli na matusi anazorushiwa na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wengi kutoka CCM na baadhiya viongozi wa Serikali baada ya Tume aliyoiongoza kupendekeza muundo wa serikali tatu.


Akizungumza juzi usiku katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, Jaji Warioba alisema viongozi wa pande mbili za Muungano wanaomtuhumu, ndiyo waliouvuruga Muungano huo


"Mwalimu aliacha Bunge likiwa na mamlaka kamili, aliacha nchi ni moja, aliacha mambo ya Muungano 11 sasa yamekuwa ni 22, kwa bahati nzuri Rais Jakaya Kikwete alieleza bungeni hilo kwamba mambo hayo yaliongezekaje," alisema na kuongeza:

"Katika kubaini kuongezeka kwa mambo ya Muungano ndivyo ilikuwa inapunguza mamlaka kwa Zanzibar, mambo 11 yaliyoachwa na mwalimu yaliingizwa kikatiba lakini haya yaliyoongezeka yalipatikana kienyeji."

Jaji Warioba alisema enzi za uhai wake, Mwalimu Nyerere aliheshimu na kuilinda Katiba hivyo, walioivunja ndiyo wasaliti wa Muungano.


"Sasa kati ya mimi na wao ni nani msaliti kwa Mwalimu, angekuwapo (Mwalimu) ni yupi angeonekana msaliti wa Serikali ya Muungano? Wao ndiyo wameuvuruga, alichokiacha Mwalimu ni tofauti na kinachoonekana kwa sasa," alisema Jaji Warioba.


Kuhusu Bunge

Jaji Warioba alisema mipango mingi ya maendeleo inayopangwa ndani ya Bunge la Muungano inatekelezwa upande wa Bara pekee.


"Si hivyo tu, Bunge hilo linajadili mambo ya Bara tu na halihusishi upande wa Zanzibar. Zanzibar nayo inajadili mambo yake na kujiamulialakini jina la Bunge hilo ni Muungano," alisema Jaji Warioba.


Kutokana na mazingira hayo, Jaji Warioba alisema Zanzibar iliamua kuondoa mamlaka ya Bunge hilo katika utungaji wa sheria kupitia Baraza la Wawakilishi Zanzibar.


"Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema sheria zinazotungwa katika Bunge hilo zitatumika ndani ya pande zote za Muungano, lakini Zanzibar wakabadilisha hilo kupitia Katiba yao wakasema sheria zote zitakazotungwa ndani ya Bunge hilo, lazima zipitiwe tena na Barazala Wawakilishi," na kuongeza: "(Zanzibar) Hawakuishia hapo, wakafanya mabadiliko ya Katiba mwaka 2010 iliyovunja Katiba ikiitambua Zanzibar kama nchi kamili, ikaondoa mamlaka ya Rais wa Jamhuri kugawa wilaya na mikoa kwa Zanzibar tofauti na Katiba ya Muungano, kwa maana hiyo Zanzibar ikavunja nguvu ya Bunge la Muungano."


Aidha, alisema hatua hiyo ilionekana kuuvunja Muungano kwavitendo baada ya kuvunja mamlaka ya Rais na kutambua marais kamili katika nchi mbili tofauti.

"Kwa kawaida nchi inakuwa na amri jeshi mkuu mmoja ambaye anapigiwa mizinga 21, Jeshi la Muungano linapiga mizinga kwa marais wawili kitu ambacho hakiwezekani," alisema.


Malalamiko ya Watanganyika

Jaji Warioba alisema Kwa upande wa Tanzania Bara, walibaini malalamiko ya Watanganyika kuwa ni pamoja na kukosa fursa mbalimbali ndani ya Zanzibar. "Watu wa bara nao wanasema Zanzibar inashiriki Bunge la Muungano, inakagua miradi ya barana kuihoji lakini wao hawana nguvu ya kushiriki mambo hayo kwa upande wa Zanzibar," alisema.

)Aliongeza: "Mbaya zaidi wanasema Wazanzibari wanaweza kumiliki ardhi na kupata uraia kwa upande wa bara lakini haki hizo haziwezi kupatikana kwa Mtanganyika, njia pekee tukaona ni vyema Zanzibar nayo ilete mambo yake ndani ya Muungano lakini ikashindikana.

"Hoja ya takwimuJaji Warioba aliwataka wajumbe wa Bunge wasihangaike na takwimu badala yake wajibu maswali yaliyojitokeza kutoka kwa washirikawa Muungano."


Takwimu siyo tatizo, sisi hatukufanya jambo jipya, ila ilikuwani kama marudio tu ya Tume ya Nyalali, wanahoji takwimu hizo je, hawakuona dosari kwa takwimu za maoni ya asilimia 20 kwa jaji Nyalali?

Alisema Tume yake ilizunguka nchi nzima ikiwa na waandishi waliorekodi kwa tepu, video na maandishi kwa ajili ya kuweka kumbukumbu katika mtandao wa Tume.

UKAWA RUKSA ZANZIBAR

Hatimaye mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), uliokuwa umezuiwa kupisha sherehe za Muungano utafanyika leo katika Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja baada ya kupata baraka za polisi.


Mkutano huo awali ulikuwa ufanyike Aprili 19, mwaka huu lakini ukazuiwa na polisi kwa maelezo kuwa intelijensia yao ilionyesha kuwa kungekuwa na tishio la maisha ya watu. Hivyo walishauriwa wapange tarehe nyingine baada ya Sikukuu ya Pasaka.


Hata Aprili 23 ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika kwa mkutanohuo, ilikataliwa na polisi kwa madaikwamba askari na maofisa wa jeshi hilo walikuwa Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yaliyofanyika Aprili 26, mwaka huu.


Msemaji wa Polisi Zanzibar, Mohamed Mhina amethibitisha kuruhusiwa kwa mkutano huo na kuwataka wananchi watakaohudhuria kuwa watulivu kabla na baada ya mkutano.

"Tumewaruhusu kufanya mkutano huo lakini maandamano hayataruhusiwa kufanyika," alisema Mhina.


Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema mkutano huo utakaoanza saa 8 mchana hadi saa 12 jioni, utahudhuriwa na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, Freeman Mbowe na Dk Willibrod Slaa wa Chadema, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Dk Emmanuel Makaidi wa NLD.


Wengine ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, wawakilishi10 kutoka kundi la 201 na wanachama mbalimbali kutoka umoja huo.


"Tunakwenda kuwaelimisha wananchi nini maana ya Katiba, jinsi ya kulinda maoni yao waliyoyatoa yasichakachuliwe na kuwaeleza kwa nini tuliamua kutoka bungeni," alisema Mtatiro na kuongeza:

"Kesho (leo) tunafanya mkutano Unguja na keshokutwa (kesho) Pemba na tutatoa ratiba ya mikutano mbalimbali itakayofanyika Tanzania Bara kwa makundi tofauti."

Aprili 16 mwaka huu, Ukawa wakiongozwa na Profesa Lipumba walisusia Bunge la Katiba na kutoka nje kwa madai ya kutokuridhishwa na mienendo ya mjadala ya Bunge hilo.


Baada ya kutoka bungeni, walitangaza kufanya mikutano nchi nzima wakianzia Zanzibar.

SHERIA YA KUOA WAKE WENGI YAPITA KENYA

Sheria inayoruhusu wanaumekuoa wake zaidi ya mmoja, imepitishwa nchini Kenya.

Rais Uhuru Kenyatta ametia saini sheria hio licha ya malalamiko kutoka kwa vikundi vya wanawake nchini humo.


Taarifa kutoka katika ofisi ya Rais ilisema kuwa mswada huo ambao unaojumuisha vipengele kadhaa kuhusu ndoa , imekuwa sheria sasa.

Mswada huo ulioleta mageuzi katika sheria ya sasa , ilipitishwa na bunge mwezi jana kuidhinisha rasmi utamaduni wa ndoa ya zaidi ya mwanamke mmoja.


Taarifa ya Rais ilisema kuwa"ndoa ni muungano wa watu wawili mwanamke na mwanamume , ikiwa mume atataka kuoa mke mmoja au wawili, mwenyewe anapaswa kuamua. ''Mswaa wa awali, ulimpa mwanamke haki ya kwenda mahakamani kupinga mume wake kuoa mke wa pili, lakini wabunge wanaume waliungana katika kuunga mkono mswada huo.

Wakati mswada huo ulipopitishwa mwezi jana , wabunge wanawake waliondoka bungeni kwa Hasira baada ya mjadala mkali.

Viongozi wa baadhi ya makanisa pia wamepinga vikali mswada huo


Shirikisho la kitaifa la mawakili wanawake pia limesema kuwa litapinga sheria hiyo mahakamani.


Katika sehemu nyingi barani Afrika, kuoa zaidi ya mwanamke mmoja ni jambo la kawaida katika tamaduni nyingi sawa na hali ilivyo nchini Kenya na hata pia miongoni mwa waumini wa dini ya kiisilamu.

Wengi wanasema kuwa sheria hiyo inapiga tu muhuri wa utamaduni uliopo.

HATIMA YA SUDAN KUSINI EAC KUJULIKANA LEO

Mkutano wa kumi na mbili waviongozi wa Jumuiya ya AfrikaMashariki unaaanza rasmi hii leo mjini Arusha nchini Tanzania.

Miongoni mwa maswala muhimu yatakayojadiliwa ombi la Sudan Kusini kutaka kujiunga na jumuiya hiyo.


Mkutano wa mwisho kama huu uliofanyika mjini Kampala Uganda mwezi Novemba mwaka jana, uliweka bayana kwamba ni katika mkutano huuu wa Arusha, ambapo tarehe ya Sudan Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki itakapotangazwa.


Lakini wadadisi wanasema kuwa msukosuko wa kiuchumi pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe huenda ikawa sababu ya taifa hilo kunyimwa uanachama wa jumuiya hiyo. Hii ni baada ya machafuko ya wenyewe kwawenyewe kuzuka, na kusambaratisha nchi hiyo kisiasa na kiuchumi.


Maswala mengine yatakayojadiliwa ni ripoti ya mawaziri, mikakati ya kifedha katika kuiendesha jumuiya hiyo na mbinu za nchi wanachama kuendelea kupeana taarifa za kijasusi, katika juhudi za kupambana na tishio la ugaidi.

BUS LA HOOD LATEKETEA KWA MOTO

Abiria zaidi ya 55 wamenusurika kufa baada ya basi la Hood kuungua moto likiwa safarini kutoka mkoani Mbeya kwenda Arusha.


Zaidi ya abiria 55 waliokuwa ndani ya basi la kampuni ya Hood, wakisafiri kutoka Mbeya kwenda Arusha walinusurika kufa baada ya basi hilo kushika moto na kuteketea kabisa katika kijiji cha Kilolele, Chalinze mkoani Pwani.

Kufuatia ajali hiyo ya moto ya basi la Hood, mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijaelezwa.


Julai 2011, Kampuni hiyo ya mabasi ya Hood iliungua moto karibu na hifadhi ya Mikumi mkoani Morogoro ambapo watu watano walikufa kwenye basi hilo lililokuwa na namba za usajili T 762 AVL lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Arusha.


Katika ajali hiyo abiria 40 walijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa ya Morogoro kwa matibabu.

MAMA AWAUA WATOTO WAKE WATATU

Mama anayetuhumiwa kwa mauaji ya watoto wake watatu nchini Uingereza amewekwa rumande kwa ukaguzi wa kiakili kubaini ikiwa alikuwa timamu wakati wa mauaji hayo.


Tania Clarence, mwenye umriwa miaka 42, alihudhuria kikao cha mahakama kwa njia ya video akiwa gerezani akituhumiwa kwa mauaji mapacha wake wawili wenye umri wa miaka mitatu na mwanawe msichana mwenyemwiri wa miaka minne.


Watoto hao walemavu, walipatikana nyumbani kwao katika mtaa wa New Malden wakiwa wamefariki Aprili 22.


Mahakama pia ilisikia kuwa watoto hao walikuwa na ulemavu uliosababishwa na ugonjwa wa uti wa mgongo.


Mahakama iliambiwa kuwa watoto hao walifariki katika hali ya kuzuiwa kupumua.


Jaji Judge Brian Barker, alisema Bi Clarence anaweza kuondolewa jela na kuwekwarumande kufanyiwa uchunguzi na kupokea matibabu ya kiakili kwa sababu tukio hilo sio la kawaida


''Hio sio dhamana , lakini ninachoamrisha ni aweze kufanyiwa ukaguzi wa kiakili kuambatana na kifungu cha 35 cha sheria. Baada ya hapo anaweza kuwekwa rumande ili achunguzwe zaidi hali yake,'' alisema jaji.


Wendesha mashitaka waliambia mahakama kuwa polisi walikuwa wanasubiri matokeo ya uchunguzi wa maiti za watoto kabla ya kubaini chanzo cha vifo vyao.


Mahakama iliambiwa kuwa babake watoto hao alikuwa nchini Afrika Kusini na mwanao mkubwa wakati wa mauaji hayo.


Mahakama itasikia baadaye utetezi wa Bi clarrence ikiwa anakiri au kukana mauaji tarehe 15 mwezi ujao.

WANAFUNZI WALIOTEKWA WAVUSHWA NCHI JIRANI

Baadhi ya wasichana waliotekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram, wanaaminika kupelekwa katika nchi jirani.


Kiongozi mmoja katika eneo la Chibok ambako wasichana hao walitekwa nyara wiki mbili zilizopita, Pogo Bitrus, ameambia BBC kuwa watu kadhaa wamewaona watu waliojihami wakiwa wanavuka mpaka na washichana hao na kuingia Cameroon na Chad.


Baadhi ya wasichana walikuwa wamelazimishwa kuolewa na wapiganaji hao.


Bwana Bitrus alisema kuwa wasichana 230 bado hawajapatikana tangu tukio la utekaji nyara katika shule ya mabweni mjini Chibok katika jimbo la Borno wiki mbili zilizopita.


Kundi la wapiganaji wa Boko Haram limelaumiwa kwa tukio hilo ingawa bado halijasema chochote.


Bwana Bitrus, ambaye ni kiongozi mmoja wa eneo hilo,alisema kuwa wasichana 43 walifanikiwa kutoroka, wakatiwengine 230 bado wanazuiliwa.


Idadi hii bila shaka ni kubwa kuliko taarifa za awali zilizvyosema ingawa hakuwa na uhakika ikiwa idadi hiyo ni sawa.

Wanafunzi hao walikuwa wanajiandaa kufanya mitihani yao ya mwisho wa muhula na kwamba wako katiya umri wa miaka 16 na 18.


''Baadhi yao wamepelekwa nchini Chad huku wengine wao wakipelekwa nchini Cameroon,'' alisema bwana Bitrus.


Bwana Bitrus alisema kuwa kulikuwa na ripoti kwamba baadhi ya wasichana hao wamefanywa kuwa wake za wapiganaji hao.

MCHINA AJINYONGA KWA KUBORONGA KAZI

Raia mmoja wa China ambaye ni mhandisi katika Kampuni ya Ujenzi ya China Railway Bureua 15 Group inayojenga Daraja la Mto Kilombero, Qin Bao Feng amekufa kwa kujinyonga kwa kile kinachodaiwa ni baada ya kuboronga katika kazi.


Ilielezwa kuwa Feng aliamua kujinyonga baada ya nguzo za daraja alilokuwa akilisimamia katika ujenzi huo, kusombwa na maji, jambo ambalo aliona kuwa limemvurugia kazi yake.


Baadhi ya watu waliokuwa jirani na kambi hiyo, walisema baada ya kuharibika kwa kazi hiyo, wahandisiwenzake kutoka China, walianza kumtenga hali iliyomfanya ajione kuwa mpweke na hatimaye kuchukua uamuzi huo.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alisema tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita ndani ya kambi ya kampuni hiyo.


Alisema mwili wa marehumu ulikutwa ukining'inia kwenye dari ndani ya chumba alichokuwa analala na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo.


Kamanda Paulo alisema baada ya kuchunguza mwili wa marehemu walikuta karatasi iliyokuwa imeandikwa ujumbe kwa lugha ya Kichina.


Alisema kwa kuwa hakuna mkalimani aliyekuwa jirani na eneola tukio, polisi wanaendelea kumtafuta mtu wa kuutafsiri.


Alisema kwa sasa mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya St Francis iliyopoKilakala, Morogoro.

BABA AUA MTOTO KWA MAKONDE

Watoto wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti likiwamo la mtoto wa miaka mitatu aliyepoteza maisha baada ya baba yake kumchakaza kwa makonde.

Mtoto aliyefariki baada ya kipigo hicho ni Vanesa Njojowa wa Kijiji cha Isisi wilayani Mbarali mkoani hapa.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema tukio hilo lilitokea saa 5:00 usiku wa kuamkia jana baada ya kuzuka kwa vurugu katika familia.


Msangi alisema baba wa marehemu ambaye ana umri wa miaka 23 alizusha vurugu kubwa kwa mkewe na baadaye aliamua kutoa kipigo kwa mtoto na kusababisha kifo.

Baba huyo anashikiliwa polisi wakati mwili wa marehemu ulitarajiwa kuzikwa jana baada ya polisi na madaktari kufanya uchunguzi.


Katika tukio jingine, Msangi alisema mtoto anayekadiriwa kuwa na umriwa kati ya miaka minne na mitano, Festo Mbiga alifariki dunia baada ya kugongwa na lori eneo la Nsalaga Uyole jijini hapa.


Mtoto huyo aligongwa juzi alipokuwa akikatisha barabara na kwamba polisi wanachunguza chanzo cha ajali hiyo.

MENEJA BARCLAYS MBARONI KWA WIZI

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia watuhumiwa 13, wakiwamo mameneja wawili waBenki ya Barclays kwa tuhuma za kuhusika na wizi katika benki hiyo katika tawi la Kinondoni. Mameneja hao ni Alune Kasililika maarufu kama Mollel (28), mkazi wa Kimara Bonyokwa ambaye ni Meneja wa tawi hilo na Neema Bandari maarufu kama Bachu (28) ambaye ni Meneja Operesheni wa tawi hilo.

Kamishna wa Kanda hiyo, Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa watuhumiwa hao wanahusishwa katika ujambazi uliotokea Aprili 15, mwaka huu saa 3:30 asubuhi.Alidai katika siku ya tukio hilo, watuwenye silaha aina ya SMG na bastola waliingia katika benki hiyo na kupora Sh milioni 390.22, dola za Marekani 55,000, Euro 2,150 na Pauni 50.

"Majambazi hao waliwatishia kwa silaha watumishi wa benki hiyo na kuwaweka chini ya ulinzi na hatimaye kutoroka na fedha hizo kwa kutumia pikipiki aina ya Fekon," alisema. Alidai awali watuhumiwa hao walifika katika benki hiyo wakiwa na magari mawilimoja aina ya Opa lenye namba T421 BQV ambayo imekamatwa.


Kwa mujibu wa madai ya Kova, uchunguzi wa kina ulibaini kuwa Alune alishirikiana na Neema pamoja na watuhumiwa wengine kufanikisha tukio hilo, huku ikigundulika kuwa robo tatu ya fedha zote zilizoibwa zilichukuliwa kabla ya tukio hilo.

"Siku hiyo ya tukio ilikuwa ni utekelezaji ili kukamilisha njama zao, hawa walisakwa na vikosi mbalimbali maalumu ikiwa ni pamoja na Kikosi Maalumu ambacho ni kwa ajili ya kuzuia na kupambana na wizi katika mabenki jijini Dar es Salaam," alisema.


Aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Fredrick Lazaro (19), Kakamiye Julius (31), Iddi Nguvu (32), Sezary Massawe maarufu kama Msolopa, Boniface Ndaro maarufu kama Muumba (29), Erasmus Mroto maarufu kama Menyee (38), Deo Olomy (32), Mohamed Athumani (31), Joseph Mkoi (33), Lucy Amos maarufu kama Macha (30) na Grace Amon (39).


Alisema baada ya watuhumiwa hao kuhojiwa, baadhi yao wamekiri kuhusika na wizi huo na walipopekuliwa walikutwa na fedha kidogo ambazo ni sehemu ya mgawo waliopata baada ya tukio hilo."


Kabla ya tukio lile, imebainika kulikuwa na vikao mbalimbali vya maandalizi ya kufanikisha tukio hilo kabla ya siku hiyo.

"Matukio kama haya yanatudhalilisha, yanatoa picha kwamba Jeshi la Polisi na serikali tumeshindwa kuzuia uhalifu wa ainahii lakini kumbe ni kazi iliyofanyika ndani," alisema Kamanda Kova.

Alisema bado upelelezi unaendelea, hivyo wananchi waendelee kushirikiana na Polisi ili watuhumiwa wengine wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake.

Katika hatua nyingine, Kova alisema kwa sasa wataanza kuwachukulia hatua wamiliki wa hoteli zenye mabwawa ya kuogelea ambayo hayana uangalizi wakati watu wakiogelea.


Hatua hiyo inatokana na tukio la watoto watatu kufa wakati wakiogelea katika bwawa la kuogelea kwenye Hoteli ya Landmark iliyopo Mbezi Jangwani, tukio ambalo ni la juzi saa 11:00 jioni.


Alisema mtoa taarifa David Mboka (44) alisema akiwa hotelini hapo kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wake, Derrick Mboka (1) aligundua watoto hao ambao ni Ndimbuni Bahati (9), Eva Nicholous (9) na Janeth Zacharia (10) wametumbukia katika bwawa hilo.


"Matukio ya aina hii tunaanza kuyafanyia kazi na tunaanza na huyu, pia tunatoa onyo kwa wamiliki wengine ambao wana mabwawa ya kuogelea kuwa makini na maeneo hayo kwa kutoruhusu watoto kukaribia maeneo hayo," alisema Kova.

WAFANYAKAZI STRABAG WAGOMA WAKIDAI POSHO

Mradi wa mabasi yaendayo haraka huenda usikamilike kwa wakati kutokana na migomo ya mara kwa mara ndani ya kampuni hiyo ambapo zaidi ya wafanyakazi elfu moja wamegoma kushinikiza uongozi wa kampuni hiyo kuwalipa posho zao za takribani miezi nane ambazo zimedaiwa kulipwa kwa ubaguzi kwa baadhi ya wafanyakazi kutoka nje ya nchi.


ITV imefika makao makuu ya kamuni hiyo Strabag jijini Dar es Salaamu na kuwakuta wafanyakazi wakiwa wamezagaa huku ofisi za uongozi wa kampuli hiyo zikiwa zinalindwa na askari wenye silaha za moto ambapo baadhi ya wafanyakazi hao wamesema wameamua kugoma ili kushinikiza kampuni hiyo kuwalipa posho zao za zaidi ya miezi nane ambazo wamekuwa wakipigwa danadana bila kujua hatma yao.


Aidha wafanyakazi hao wameendelea kulaani kitendo cha uongozi wa kampuni hiyo kuendelea kulipa posho hizo kwa wafanyakazi wengine waliotoka nchi jirani bila kutambua ya kuwa posho hizo zipo kisheria na imesainiwa kwenye mikataba yao ambpo wanadai kila mfanyakazi zaidi ya laki tano huku wakiiomba serikali kuingilia kati ili waweze kupata haki yao.


Jitihada za ITV za kutafuta uongozi wa kampuni hiyo ili kufafanua juu ya madai ya wafanyakzi hao ziligonga mwamba baada ya baadhi ya viongozi kugoma kuongea na wengine kujifungia ndani.

Chanzo:ITV

HEROINE TANI 1 YADAKWA KENYA

Serikali ya Kenya imelalamika kuwa haikupewa taarifa zozote kuhusu dawa za kulevya zilizonaswa na wanajeshi wa Australia wanaoshika doria katika ufuo wa bahari Hindi , ufukweni mwa Kenya.

Hii ilijitoza katika mkutano kati ya waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohammed na balozi wa Australia nchini humo Bwana Geof Tooth aliyetakiwa na serikali kuelezea kuhusu tukiola kunaswa kwa dawa hizo.


Dawa hizo zenye uzani wa kilo 1,023 ambazo ni kiwango kikubwa cha dawa za kulevya kuwahi kunaswa katika pwani ya Afrika, ni za thamani ya dola milioni 289.


Zilinaswa Ijumaa zikiwa zimepakiwa katika mifuko 46 ambayo ilikuwa imefichwa kwenye mifuko ya Simenti


Ubalozi wa Australia umekanusha madai kuwa, manowari yake ya kijeshi iliingia katika eneo la bahari inayomilikiwa na Kenya na kunasa shehena ya dawa hizo.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, ubalozi huo umesemakuwa madawa hayo ya kulevya yalinaswa katika eneo la bahari inayomilikiwa na jamii ya kimataifa na kuwahakuna manowari yake iliyoingia Kenya.

Pia yalinaswa katika operesheni dhidi ya biashara ya kimataifa ya dawa za kulevya. Taarifa zilisema kuwa dawa hizo ziliharibiwa kwa kumwagwa baharini.


Taarifa hiyo imesema kuwa tukio hilo halina uhusiano wowote na Kenya na kuwa habari zilizochapishwa na vyombo vya habari nchini Australia kuwa madawa hayo yalinaswa karibu na kenya ilikuwa kutoa taswira tu ya eneo la tukio.


Shehena kubwa kuwahi kunaswa

Wiki iliyopita wanajeshi wa Australia walinasa mashua moja iliyokuwa imesheheni zaidi ya tani moja ya madawaya Heroine katika bahari ya hindi na taarifa hiyo inasema kuwa mashua iliyonaswa haikuwa na usajili wowote.


Ubalozi huo umekariri kuwa haukuhusika na operesheni hiyo ambayo ilifanywa na wanajeshi wa majini wa Australia wanaoshika doria katika bahari ya hindi chini ya mkataba wa kimataifa wa kupambana na uharamia na uhalifu katika bahari ya hindi.


Hata hivyo ubalozi huo umesema kuwa shirika la kimataifa la kupambana na uharamia na uhalifu CMF litaendelea kushirikiana na serikali ya Kenya hasa katika kuelezea zaidi operesheni yake.


Tangu shehena hiyo kukamatwa kumekuwa na shauku miongoni mwa maafisa wa ulinzi na wale wa wizara ya mambo ya nchi za kigeni nchini Kenya kuhusianana tukio hilo na madai kuwa kenya haikuhusishwa katika operesheni hiyo licha ya kutendeka katika eneo linalosemekana kuwa lake.

KIVUMBI CHA AFCON 2015 KUANZA KUTIMKA

Droo ya Kufuzu kwa kombe la mataifa bingwa Barani Afrika mwakani{ Afcon} imefanyika huko cairo Misri huku timu zote za kanda ya Afrika Mashariki zikiratibiwa kucheza katika mechi za mchujo kabla ya kushiriki mechi za kufuzu.

Kenya itachuana dhidi ya Visiwa vya Comoro ,Tanzania ipambane na Zimbabwe, Uganda imeratibiwa kutoana kijasho dhidi ya Madagascar nayo Rwanda ikivaana na Libya.

Raundi ya Kwanza

*.Liberia v Lesotho

*.Kenya v Comoros Islands

*.Madagascar v Uganda

*.Mauritania v Equatorial Guinea

*.Namibia v Congo

*.Libya v Rwanda

*.Burundi v Botswana

*.Central African Republic v Guinea Bissau

*.Swaziland v Sierra Leone

*.Gambia v Seychelles

*.Sao Tome e Principe v Benin

*.Malawi v Chad

*.Tanzania v Zimbabwe

*.Mozambique v South Sudan

Burundi kwa upande wake itachuana dhidi ya Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiratibiwa kuvaana na Namibia.

Baada ya kushiriki mkondo wa kwanza wa maondoano mataifa hayo tena yatalazimika kuchuana miongoni mwao ilikufuzu kwa awamu ya pili.

Mshindi wa mkondo huo wa pili ndio watakao jumuishwa katika makundi saba yaliyotajwa jana.

Raundi ya Pili

Liberia or Lesotho v Kenya or Comoros Islands

Madagascar ,Uganda v Mauritania ,Equatorial Guinea

Namibia , Congo v Libya , Rwanda

Burundi , Botswana v CAR , Guinea Bissau

Swaziland or Sierra Leone v Gambia , Seychelles

Sao Tome e Principe or Benin v Malawi , Chad

Tanzania , Zimbabwe v Msumbiji , Sudan kusini

Mechi za raundi ya kwanza zitang'oa nanga tarehe 6-18 Mei.

Mechi za marudio zitasakatwa wikiendi ya tarehe 30-31 Mei hadi Juni Mosi.

Katika mechi zitakazoibua hisia ni pamoja na mabingwa watetezi Nigeria ambao wameratibiwa kuvaana na Afrika Kusini.

Mahasimu wa jadi kaskazini mwa Afrika Tunisia na Misri wameratibiwa kukwaruzana nayo Ghana,ikitoana kijasho na Togo.

Aidha Ivory Coast itafungua kampeini yake ya kufuzu kwa dimba hilo lenye hadhi baranidhidi ya mahasimu wao wakuu Cameroon.

Droo ya Makundi:

Kundi A :
Nigeria,
Sudan,
South Africa
{Namibia vs Congo Brazzaville/Libya vs Rwanda}

Kundi B:
Mali,
Ethiopia,
Algeria
{ Sao Tome e Principe vs Benin/Malawi vs Chad}

Kundi C:
Burkina Faso,
Gabon,
Angola
{ Liberia vs Lesotho/Kenya vs Comoros Islands}

Kundi D:
Ivory Coast,
Democratic Republic of Congo,
Cameroon
{ Swaziland vs Sierra Leone/Gambia vs. Seychelles}

Kundi E:
Ghana,
Guinea,
Togo
{Madagascar vs Uganda/Mauritania vs Equatorial Guinea}

Group F:
Zambia,
Niger,
Cape Verde Islands
{ Tanzania vs Zimbabwe/Mozambique vs South Sudan}

Kundi G:
Tunisia,
Senegal,
Egypt
{ Burundi vs Botswana/ Central African Republic vs Guinea Bissau}

Mechi za makundi zitaandaliwa kati ya tarehe 5-6 Septemba na tarehe 10 Septemba.

Mkondo wa pili utaandaliwa kati ya tarehe 14-15 November na 19 November.

Washindi wawili katika kila kundi watajiunga na wenyeji Morocco mwakani kwenye kipute cha kuwania taji la taifa bingwa barani Afrika 2015.

TIMU YA TANZANIA CHINI YA MIAKA 20 YASONGA MBELE

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania kwa vijana wenye umri wa miaka 20 imesonga mbele kwenye safari ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la mataifa baada ya kuilaza Kenya kwa mikwaju ya Penalti 4-3 kwenye mechi ya marudiano iliyochezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo imelazimika kuingia hatua ya Penalti baada ya kumalizika dakika 90 mechi ikiwa sare ya 0-0 nandipo Tanzania ilipopata ushindi unaoisogeza kwenye raundi ya pili ya michuano hiyo inayofanyika kila baada ya miaka miwili.

Ushindi huo wa timu ya Tanzania ijulikanayo kana Ngorongoro Heroes umekuwa faraja kwa Watanzania baada ya timu yaTaifa ya wakubwa, Taifa Starskuchezea kichapo dhidi ya Intamba Murugamba ya Burundi Jumamosi kwenye mechi ya kirafiki ya maadhimisho ya miaka hamsini ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo Taifa Stars ilichapwa mabao 3-0.

Nalo Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limemtangaza rasmi kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars Martinus Ignatius Nooij ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuionoa timu hiyo huku kibarua chake cha kwanza kikiwa tayari kimeishatangazwa ambapo Taifa Stars itashuka dimbani dhidi ya Zimbabwe mwezi Mei mwaka huu kwa mechi ya awali ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa zitakazofanyika mwakani nchini Morocco mwezi Februari mwakani.

Tayari Kocha ametangaza majina ya wachezaji tisa wapya kuimarisha kikosi hicho huku beki maarufu wa timu ya Yanga, Kelvin Yondan akitemwa kwenye kikosi hicho baada ya kugoma kuripoti kambini, pasipo kutoa sababu za msingi za kutofanya hivyo.


Katika safari ya kuelekea Morocco hapo mwakani, Uganda itashuka dhimbani dhidi ya Madagascar, huku Burundi ikicheza dhidi ya Botswana, na Harambee Starsya Kenya itapepetana na Commoro, nayo Rwanda ikicheza dhidi ya Libya.

WAZIRI MKUU WA KOREA KUSINI AJIUZULU

Waziri mkuu nchini Korea Kusini amejiuzulu kutokana na vile serikali yake ilivyolichukulia swala lote la ferry iliozama siku kumi na moja zilizopita.

Chung Hong Won amesema kuwa kusalia afisini ni mzigo mkubwa kwake.

Bwana Chung alizomwa alipozitembelea familia za waathiriwa waliotoweka katika ferry hiyo ya Sewol,baada ya kuzama katika hali ya kutatanisha.

Takriban watu 200 wanadaiwa kufa maji katika tukio hilo huku zaidi ya mamia wengine wakiwa hawajulikani waliko,wengi wao wakiwa wanafunzi na walimu waliokuwa wakielekea katika ziara ya shule.

Wapiga mbizi bado wanaendelea kuwasaka waathiriwa chini ya ferry hiyo iliozama.Ripoti za awali zimedai kuwa watu wote wametolewa katika boti hiyo.

TSVANGIRAI ASIMAMISHWA UONGOZI MDC

Chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change MDC kimesema kimemsimamisha kiongozi wake Morgan Tsvangirai kwa kukiuka kanuni za kidemokrasia.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa MDC Tendai Biti kufuatia mkutano wa chama hicho uliofanyika katika mji Mkuu Harare.

Tangu mwaka 2009 hadi 2013 Bwana Tsvangirai alitumikia taifa la Zimbabwe katika nafasi ya Waziri Mkuu katika serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa kwa pamoja na Rais wa sasa Robert Mugabe.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilifikia kikomo mwezi julai mwaka 2013 baada ya Rais Mugabe kushinda kwa wingi wa kura katika uchaguzi wa rais na Tsvangirai kususia uchaguzi kwa madai ya udanganyifu.

Kushindwa kwake kulipunguza nguvu yake kama kiongozi ambaye alikuwa mshindani mkuu wa Rais Mugabe.

Waangalizi wanasema ndani ya MDC kumekuwa na mgogoro wa kiuongozi kwa miezi kadhaa.

Viongozi wengine wa ngazi za juu wameripotiwa kusimamishwa katika mkutano huo uliofanyika siku ya jumamosi na wanachama wengine wa chama hicho watachukua nafasi zao.

TANZANIA YAAZIMISHA MIAKA 50 YA MUUNGANO

Sherehe za kuhadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyozaa nchi ya Tanzania zimefanyika leo mjini Dar es Salaam na kupambwa kwa maonyesho mbali mbali ya kijeshi pamoja na halaiki zilizoandaliwa na watoto.

Marais wanne wa nchi za Afrika Afrika Mashariki akiwemo Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Pierre Nkurunzinza wa Burundi ni miongoni mwa marais waliohudhuria sherehe hizo.

Wengine ni Rais Joyce Banda wa Malawi, Mfalme Mswati III wa Swaziland, mfalme Letsie III wa Lesoto Makamu wa Rais wa Nigeria Mohammed Sambo, Makamuwa Rais wa Zambia Guy Scott,Waziri Mkuu wa Rwanda Piere Habumurenyi, Waziri Mkuu wa Misri Ibrahim Mahlab na Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki.

Katika maadhimisho yao pia kulikuwa na maonyesho ya silaha mbali mbali za kivita zikiwemo ndege za kivita pamoja na za kiraia.

Hata hivyo kilichovutia zaidi ni kikosi cha makomandoo wa jeshi la Tanzania ambao walionyesha umahiri wao kupambana na adui bila kutumia silaha na kuvunja vitu vigumu kwa kutumia kichwa pamoja na mikono.

Onyesho jingine lililotia fora ni askari wa miamvuli ambao waliruka kutoka kwenye ndege kwa kutumia miavuli na kutua katika uwanja wa sherehe.

PALESTINA KULITAMBUA TAIFA LA ISRAEL

Rais wa Palestina, Mahmuoud Abbas amesema serikali ya pamoja itakayowajumuisha kundi la Hamas, italitambua taifa la Israel na wajibu wa kitaifa pamoja na kutangaza kusimamisha machafuko.

Bwana Abbas amelimbia baraza kuu la chama cha kisiasa cha PLO, kwamba bado angelipenda kuendelea na mazungumzo ya amani na Israel.

Israil imesimamisha mazungumzo hayo baada ya kutangazwa kwa serikali ya pamoja ambayo itaongozwa na bwana Abbas na Hamas wanaotawala himaya ya ukanda wa Gaza.

Rais wa Palestina ametetea makubaliano hayo ya serikali ya pamoja na kusema hawezi kuwabana na kuwakana raia wake walioko Gaza na wala kukataa kuendelea na mazungumzo ya amani na Israil.

KINGUNGE AWATAKA KUFYATE WANAO MSHAMBULIA JAJI WARIOBA

Wajumbe wa Bunge Maalum wametakiwa waache kumsakama aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba na timu yake, kwani maoni alowasilisha si yake, bali ni ya wananchi.

Rai hiyo imetolewa Bungeni hapa leo na Mwanasiasa Mkongwe, MzeeKingunge Ngombale-Mwiru wakati akitathmini mwenendo wa Bunge hilo katika mjadala wa Rasimu ya Pili ya Katiba.


Mzee Ngombale-Mwiru amewatahadharisha wajumbe wasivuke mipaka, akiwaeleza hawakwenda Dodoma kuipiga vijembe timu ya Warioba, bali wana wajibu wa kuhakiki na kuboresha Rasimu ya Katiba Mpya.


"Kero ya wananchi kubwa kabisa ni kero ya umasikini," amekumbusha Kingunge, akiliambia Bunge kuwa wana wajibu wa kuhakikisha Katiba wanayoandika inaakisi matatizo haya na inazungumzia "hatma ya wananchi."

Huku hayo yakiendelea, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewataka wajumbe wa Ukawa walosusia vikao warejee Bungeni hapa, na wamalize tofauti zao ili Katiba ya Wananchi ipatikane.


Bunge hilo limeahirishwa hadi Agosti 05 mwaka huu, litakapokutana tena mjini hapa kwa miezi miwili ili kuhitimisha kazi waliyoianza ya kuandaa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

BUNGE LA KATIBA MPAKA AGOSTI 5

Bunge maalum la katiba limeahirishwa hadi agasti tano mwaka huu huku wabunge wa wakitahadharishwa kuacha kumshambulia aliyekuwa mwenyekiti wa iliyokuwa tume ya mabadiliko ya katiba jaji mstaafu Joseph Warioba au mjumbe yeyote binafsi wa iliyokuwa tume ya mabadiliko ya katiba.


Akitoa maoni kabla ya kuahirishwa kwa bunge hilo,mwanasiasa mkonge ambae pia ni mbunge wa bunge hilo, Mhe Kingunge Ngombare Mwiru, amewaomba wajumbe hao kuacha kushambulia mtu na wasitumie msimamo wa CCM kufanya hivyo kwani wanakitukanisha Chama cha Mapinduzi.

Aidha kuhusu kero zilizomo katika katiba ya sasa, Mhe Kingunge amesema kero kubwa kwa wananchi ni umasikini hivyo ametaadharisha katiba yeyote itakayo andikwa bila ya kukabili tatizo la umasikini itakuwa si katiba bora.


Kwa upande wake makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Mhe, balozi eif Ali Idd amesema serikali inatumia zaidi ya milioni 188 kila siku kwa kazi ya katiba ambapo sasa rais kwa ridhaa yake ameongeza siku 60 hivyo ni vyema wapunguze mijadala isiyoyalazima na kuzionea huruma fedha za walipa kodi.

Waziri mkuu mhe. Mizengo pinda amesema anashangzwa na baadhi ya watu wanao dai tanganyika wakati ilidumu kwa kipindi mwaka mmoja na nusu na kuwataka wabunge wasiwabeze wahasisi wa muungano wa tanzania,huku spika wa baraza la wawakilishi Mhe. Pandu Kificho akisisitiza yapo baadhi ya mambo ambayo binadamua anaweze kubahatisha la si uendeshaji wa nchi.


Katika mkutano huo mwenyekiti wa mkutano wa bunge maalum alilazimika kutumia mamlaka kwa kushirikiana na mwanasheria mkuu wa serikali kutengua kanuni mara mbili ili kutoa fursa kwa viongozi hao kutoa maoni yao na hatmaye kuliahirisha bunge hilo hadi Agosti 5 mwaka huu.

MAKOMANDO KUWASAKA WAPIGANAJI UKRAINE

Vikosi vya jeshi nchini Ukrain vimekuwa vikielekea mji wa Slavyask ambayo ni ngome ya makundi ya wapiganaji wanaounga mkono Urusi.

Wizara ya masuala ya ndani nchini Ukraine inasema kuwa imeharibu vizuizi vitatu vilivyowekwa na makundi haramu yaliyojihami kwenye mji wa mashariki wa Slavyansk.


Wizara hiyo inasema kuwa watu watano waliotajwa kuwa magaidi wameuawa.

Waziri wa masuala ya ndani nchini Ukrain Arsen Avakov amesema kuwa vikosi vya serikali vimefanikiwa kuwaondoa wanamgambo wanaoiunga mkono Urusi kutoka kwa majengo ya serikali katika mji wa Kusini Mashariki wa Mariupol.

Duru zinasema kuwa aneo la kati mwa Sloviansk ni tulivu.


Wapiganaji wanaotaka kujitenga na Ukraine wakati wakiunga mkono Urusi, wameendelea kuteka majengo ya serikali mjini humo.

Awali maafisa nchini Urusi walikuwa wameonya Ukrain kutokan na kuwachukulia hatua makundi yaliyojitenga.


Naye rais wa Marekani Barack Obama alinukuliwa awali akisema kuwa Urusi haikutii makubaliono ya Geneva yaliyokuwa na lengo la kuzima mzozo nchini Ukrain.

LUPITA MWANAMKE MREMBO ZAIDI 2014

Jarida la People limemtangaza Mkenya Lupita Nyong'o kama mwanamuke mrembo zaidi duniani mwaka 2014.

Lupita ambaye alishinda tuzo ya Oscar kwa uigizaji wake katika filamu '12 years a slave,' yuko kwenye ukurasa wa juu zaidi wa makala ya wiki hii ya jarida hilo.

Katika orodha yake ya wanawake 50 warembo duniani, Lupita amewapiku waigizaji maarufu akiwemo Kerry Washington, ambaye pia alishiriki katika filamu hiyo na mwanamuziki Pink ambao walikuwa katika nafasi ya 10 na 5 mtawalia.


Stacy Kiebler ambaye alisifikasana kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji nyota George Clooney, alishikilia nafasi ya nane.


Hatua ya Jarida la People ambalo huchapishwa kila wiki nchini Marekani na kusomwa na karibu watu milioni 40, kumkubali Lupita kama mwanamke mrembo duniani,ni kama tuzo kivyake kwa muigizaji huyo ambaye amegonga vichwa vya habari nchini Marekani tangu kushinda

Mtandao wa People.com, unasema kuwa muigizaji huyo alifurahia sana kutajwa na jarida hilo kama mwanamke mrembo hasa kwa sababu wasichana kama yeye watapata kuwa na matumaini ya kufanikiwa maishani kama yeye.


"Nimefurahi sana na hii ni fursa kuwafanya wasichana wengine wajihisi kuwa wana uwezo wa kufiia chochote maishani mwao.

MAREKANI YASIKITISHWA NA PALESTINA

Marekani inasema imesikitishwa na makubaliano kati ya makundi makuu Palestina ya kuiunda serikali ya Umoja.


Imeonya huenda hatua hiyo ikatatiza zaidi jitihada za amani. Uamuzi huo unalijumuisha kundi lenye msimamo kali za kidini, Hamas, unaliotawala eneo la Gaza na limetajwa na Marekani na Israeli kama kundi la kigaidi.


Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Marekani Jen Psaki amesema wakati wa kutangaza uamuzi hduo ndio unaotia wasiwasi.


Tangazo hilo limefanywa wakati ambapo Marekani ilikuwa ikijitahidi kushawishi Israil na Wapalestina kukubali kuendelea kufanya mashauriano ya amani ambayo hadi kufikia sasa hayajazaa matunda yoyote.


Bi Psaki amesema mapatano kati ya Wapalestina yatavuruga vibaya sana juhudi hizo na akatangaza kuwa itakuwa vigumu kwa Israil kufanya mashauriano nakundi ambalo haliamini kuwa Israili ina haki ya kuwepo kama taifa; jinsi wanavyoamini wanachama wa Hamas.

Alisema Serikali ya Marekani itaendelea kuchunguza kwa makini hatua zinazochukuliwa kuhusiana na uamuzi huo na Wapalestina siku na hata masaa yanayokuja.


Wamarekani na mataifa washirika wake wamesisistiza kuwa muda mrefu kuwa taifa lolote la Wapalastina inapaswa kuwa lile linaloshutumu vita, litambue Israil na kukubalia mapatano yote yanayohusisha taifa hilo la Wayahudi.


Wapalestina wanasisitiza kuwa umoja wao utampa uhalali zaidi Rais Mahmoud Abbas, kufanya mashauriano kwa niaba yao kwa sababu atakuwa akiwakilisha Wapalestina wote na wala sio baadhi yao tu.

MZEE KUUAWA KWA KUPIGWA MAWE

Mahakama moja ya kiisilamu katika jimbo la Kano nchini Nigeria, imemkuhuku kifo mzee mwenye umri wa miaka 60 kwa kupigwa mawehadi afe baada ya kupatikanana hatia ya kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 12.

Mwanamume huyo pia aliripotiwa kumuambukiza msichana huyo virusi vya HIV.

Hukumu kama hizi hutolewa chini ya sheria kali za kiisilamu na zimewahi kupitishwa ingawa utekekelezaji wake unakuwa mgumu.


Hukumu ambazo ziliwahi kutolewa hapo awali ziligeuzwa na kuwa kifungo cha maisha jela.

Mtuhumiwa Ubale Sa'idu Dotsa, alijitetea mahakamani Jumatano, akisema kuwa shetani ndiye aliyemsababisha kumbaka msichana huyo.

Alisema hakujua kama alikuwa ameambukizwa virusi vya HIV.


Dotsa alisema kuwa msichana huyo alimfanya kupata hisia alipotembelea duka lake mara kwa mara nyakati za usiku na ndio maana akambaka.

Hakimu Faruk Ahmed, alipuuza kilio cha mzee huyo aliyetaka mahakama kumsamehe.


Alisema mzee huyo kwa jina Dotsa alikuwa ametenda zinaa, kitendo ambacho adhabu yake ni mtu kuuawa kwa kupigwa mawe.

WATU WANNE WAUAWA KATIKA MLIPUKO JIJINI NAIROBI

Watu wanne, wakiwemo maafisa wawili wa polisi, wameuawa jana usiku mjini Nairobi baada ya gari walilolizuia kulipuka, lilipokuwa likielekea katika kituo cha polisi katika eneo la Pangani, jijini Nairobi.

Bomu la pili lilipatikana katika gari hilo baada ya mlipuko huo na wataalamu wa mabomu waliliharibu.


Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kuitambua miili ya washukiwa hao ambayo iliharibiwa vibaya kiasi cha kutoweza kutambulika.

Usalama umeimarishwa katika eneo hilo na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi.


Bosco Mugendi ana kibanda cha kuuza vitu vidogovidogo karibu na lango la kuingia kwenye kituo cha polisi cha Pangani kulikotokea mlipuko huo.

Alunukuliwa akisema:

"kile kilichonikuta katika kibanda changu ni nyama ya watu iliyonirukia halafu mimi nikatoroka na kutoka nje."

Mtaalamu wa maswala ya usalama jijini Nairobi, George Musamali, aliambia BBC kuwa maafisa wa polisi waliokuwa wakisindikiza gari kuelekea kituo hicho cha polisi walikuwa kwenye gari la washukiwa ambalo lililipuka baadaye.

MAJAMBAZI WAVAMIA KAMBI YA WACHINA NA KUJERUHI

Watu wanane wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na siraha za jadi mapanga na marungu wamevamia kambi ya Kampuni ya wachina wanaotengeneza Barabara kwa kiwango cha rami ya kutoka Mpanda hadi Sitalike Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi na kumjeruhi mlinzi wa Kampuni hiyo Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina mwandamizi msaidizi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea hapo Aprili 22 mwaka huu majira ya saa tano na dakika thelathini na tano usiku katika kambi ya kampuni hiyo iliyoko katika Eneo la kata ya Magamba Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi.

Alisema siku hiyo ya tukio watu hao wanane wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walifika kwenye kambi hiyo na kisha walimvamia mlinzi wa kampuni hiyo Joseph Sarangi na kumshambulia kwa kutumia silaha za jadi mapanga na marungu na kumjeruhi kwenye paji la uso na kichwani kufanikiwa kuiba betrii la gari aina ya Nissan lenye Namba 120 na kisha kutokomea kusikojulikana.


Alieleza kuwa jeshi la Polisi lilipata taarifa ya tukio hilo baada ya muda mfupi baada ya kuwa limetokea kwenye eneo hilo na walianza wawafatilia watu hao waliohusika na tukio hilo la ujambazi wa kutumia silaha hizo za jadi.

Kamanda Kidavashari alisema katika msako huo wa Jeshi la polisi siku hiyo hiyo walifanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa mmoja aitwaye Juma Athumani 23 Mkazi wa Mtaa wa Tambukaleli Mjini hapa.

Alisema baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo mmoja jeshi hilo bado linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine saba ambao walishiriki kwenye tukio hilo la ujambazi wa kutumia silaha za jadi.


Aidha alieleza kuwa mtuhumiwa Juma Athumani anatarajiwa kufikishwa Mahakamani mara baada yaupelelezi wa tikio hili utakapo kuwa umekamilika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake wa sheria

MAMA NA MWANAE WAFARIKI KWA KUPIGWA NA RADI

Mpanda Katavi

Wanawake wawili mama na Mtoto wake wakazi wa Kijiji cha Mnyagala Tarafa ya Kabungu Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamefariki Dunia baada ya kupigwa na Radi na Kufa hapo hapo wakati wakiwa njiani wakiwa wanatokea kwa jirani yaoKwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina mwandamizi Msaidizi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea hapo A prili 22 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili jioni kijijini hapo

Kamanda Kidavashari aliwataja waliokufa kwa kupigwa na Radi ni Migu Samwel 46 na mwanae wakike aitwaye Nsungulwa Kasanzu 15 wote wawili wakiwa wakazi wa kijiji hicho cha Mnyagala


Alisema kabla ya vifo hivyo vya mama na mwanae marehemu hao walikuwa wamekwenda kwa jirani yao kwa lengo la kumsalia na wakati wako huko waliona wingudogo la mvua likiwa limetanda hewani


Alieleza kutokana na kuwepo kwa wingu hilo dogo la mvua marehemu hao walimuaga jirani yao kuwa wanawahi kurudi nyumbani kwao kabla mvua ya haija anza kunyesha kwani waliondoka nyumbani huku baba mwenye nyumba akiwa hayupo alikuwa amekwenda kwenye shughuli zake za ufundi wa baiskel kijijini hapo katika eneo linaloitwa Center


Alifafanua wakati wakiwa wanaelekea i walipofika jirani na nyumba yao umbali wa mita 15 ndipo walipopigwa na radi na kufa hapo hapo ambapo mama alipigwa na radi sehemu ya kifuani na mwanae alipigwa na radi sehemu ya kichwani


Alisema baada ya kuwa wamepigwa na Radi na kufafa hapo hapo miili ya marehemu hao iliokotwa na majirani walikuwa wakipita kwenye eneo hilo baada ya mvua ndogo ilinyesha kuwa imekatika


Kidavashari alieleza majirani hao baada ya hapo walitowataarifa kwenye uongozi wa Serikali ya Kijiji ambao nao walifika kwenye eneo hilo nakisha walitowa taarifa za vifo vya marehamu hao kwa jeshi la polisi Wilaya ya Mpanda


Alisema miili ya marehemu hao ilitarajiwa kuzikwa jana kijijni hapo mara baada ya taratibu za kidaktari zitakapokuwa zimekamilika na jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limetowa wito kwa wakazi wa Mkoa huo huacha kutembea barabarabi wakati wa mvua na waepuke kupita karibu na miti

RIPOTI YAANIKA MAUAJI YA VYOMBO VYA DOLA

Matukio ya vyombo vya dola kutumia nguvu kupita kiasiyamezidi kuongezeka nchini na kwamujibu wa Ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2013 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), watu 34 waliuawa na watumishi wa vyombo hivyo katika nyakati tofauti.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa jana inaonyesha kuwa mauaji hayo yalitekelezwa na baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi, Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na sungusungu. Vyombo vingine vilivyotajwa katika matukio hayo ni polisi jamii na askari wa Wanyamapori. Pamoja na matukio hayo, pia askari wanane waliuawa na raia katika vurugu mbalimbali zilizohusisha pia kuvamiwa kwa vituo vinne vya polisi.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema matukio hayo yameongezeka kutokana na vyombo husika kutowachukulia hatua maofisa wake baada ya kutekeleza mauaji.

Hata hivyo, Msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Erick Komba alisema jana kuwa baadhi ya askari wa jeshi hilo waliobainika kutekeleza vitendo hivyo walichukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Isaya Mungulu alisema watatumia ripoti hiyo kujirekebisha zaidi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbaliza polisi.


*Maeneo ya mauaji

Dk Bisimba alisema sehemu kubwaya mauaji hayo yalitokea katika matukio baina ya askari na wananchi pia kupitia operesheni zilizotekelezwa na Serikali hususan Operesheni Tokomeza.

"Mambo makubwa matatu ndiyo yalikuwa na uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu; Operesheni Tokomeza na Kimbunga pamoja na vurugu za gesi mkoani Mtwara," alisema.

Alisema uvunjifu huo wa amani pia ulitokana na matamko ya viongozi wa Serikali ikiwemo kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda bungeni Agosti mwaka jana, kwamba wananchi wanaovunja amani wapigwe tu na vyombo vya dola.

Alisema mwaka 2013 kulikuwa na matukio ya kutisha ya mauaji kwa mfano, watu kujichukulia sheria mkononi na kuua wengine. Watu 1,669 waliuawa, ikiwa ni ongezeko la vifo 435 kutoka 1,234 mwaka 2012.


"Pia tulishuhudia aina mpya ya mauaji kama vile kumzika mtu akiwa hai kwa imani potofu za kishirikina, kuwapiga mawe na kuwachoma moto watuhumiwa... nivitendo vya kutisha katika utoaji waadhabu ambavyo vinavunja haki za binadamu. Pia kumekuwa na ugumu kwa upande wa polisi na waendesha mashtaka kufanya uchunguzi wa kina na kuwashtaki waliotekeleza vitendo hivyo."


Ripoti hiyo ya kumi na moja tangu zilipoanza kutolewa mwaka 2002, pia imebainisha kuongezeka kwa vitendo vya kuwaua watu kutokana na imani za kishirikina. Watu 765 waliuawa mwaka jana ikilinganishwa na 630 mwaka 2012.

"Kati ya hao waliouawa wanawake walikuwa 505 na wanaume 260," iliongeza ripoti hiyo ikisema mikoa iliyokumbwa zaidi na matukio hayo ni Geita, Mbeya, Shinyanga, Iringa, Tabora na Mwanza.


*JWTZ, Polisi wafafanua

Luteni Kanali Komba alisema: "Ni kweli kumekuwa na baadhi ya wanajeshi wachache kwa kipindi kilichopita, waliofanya vitendo vya uvunjifu wa amani wakiwa katika shughuli za kijamii—nje ya utekelezaji wa majukumu ya kijeshi."

Alisema waliopatikana na makosa hayo walifungwa na wengine kufukuzwa kazi na kwamba katika baadhi ya matukio hayo, wananchi wachache walikuwa chanzo na kusababisha uvunjifu wa sheria.

Alisema JWTZ ni jeshi la wananchi na litaendelea kuenzi dhana hiyo na lina taratibu na sheria mbalimbali za kumwongoza mwanajeshi... "Nidhamu ni suala la msingi kwa mwanajeshi kutokana na dhamana aliyokuwa nayo."

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu alisema katika taarifa iliyosomwa na DCI Mungulu kuwa matukio hayo ya uvunjifu wa amani hayawezi kuvumiliwa. Aliwataka wadau kushirikiana kuyatokomeza.

"Kufanya vurugu na kuwashambulia raia wengine wakati vyombo vya usalama vipo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Hivyo tukiwa na jamii isiyotii na kuheshimu sheria zilizopo ni hatari kwa amani na utulivu wa nchi yetu," alisema Mangu na kuomba kila mmoja kutimiza wajibu wake ili kulinda haki za binadamu.


Moja wa watafiti walioandaa ripoti hiyo, Pasience Mlowe alisema walikusanya taarifa kutoka katika wilaya 131 kupitia wawakilishi wao na pia kufanya mahojiano ya moja kwa moja katika wilaya 28.

MASWALI SABA YA JAJI WARIOBA KWA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadilikoya Katiba, Jaji Joseph Warioba ameuliza maswali saba ya msingi kwa wajumbe wa Bunge la Katiba wanaopinga Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume yake akitaka wawajibu wananchi ili kutuliza kiu yao.

Jaji Warioba ambaye tangu awasilishe Rasimu ya Katiba Desemba 30, mwaka jana amegeuka kuwa adui kwa watu wanaotaka muundo wa serikali mbili, aliuliza maswali hayo jana katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Taasisi ya Twaweza kuhusu mchakato wa Katiba.

Akizungumza kwa ukali, Jaji Warioba alisema: "Kwanza, jibuni kwa nini mnapinga muundo wa Muungano wakati walioupendekeza ni wananchi?


"Sheria inasema uwepo wa Muungano na mapendekezo katika rasimu hayasemi Muungano usiwepo. Kumbukeni kuwa wananchi walitakiwa kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha Muungano."


Katika swali lake la pili, Warioba alisema kwa nini Tanganyika imevaa koti la Muungano? Kwa kuwa katika ukusanyaji wa maoni wananchi walieleza kuwa Serikali yaMuungano ya sasa siyo ya Muungano, ni ya Tanganyika.


Katika swali la tatu alisema wajumbe hao wanatakiwa kujibu maelezo ya wananchi ambao waliieleza tume hiyo kuwa Katiba imevunjwa na madaraka ya rais yamechukuliwa na sasa kuna marais wawili katika nchi moja.


"Tume inapewa lawama kubwa, wajibuni wananchi hii tume ilitumwa na nani kukusanya maoni ya wananchi? Waambieni ilikusanya maoni hayo kwa kutumia sheria ipi zaidi ya ile ya Mabadiliko ya Katiba?" alisema Jaji Warioba katikaswali lake la nne.


Katika swali lake la tano, Warioba aliwataka wajumbe hao kutoa sababu za kumtuhumu kuwa amependekeza muundo wa serikalitatu kwa sababu yeye pamoja na (Joseph Butiku) walikuwa wajumbe wa Tume ya Jaji Kisanga na Jaji Nyalali ambazo nazo zilipendekeza muundo wa serikali tatu, kitu ambacho alisema si kweli na hawakuwahi kuwa mjumbe wa tume hizo.


Pia, aliwataka wajumbe hao kujibu swali la sita, kwa nini hawataki kuzungumzia yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na badala yake wanageuza rasimu hiyo kuwa imeandikwa na Tume ya Mabadilikoya Katiba.


Katika swali lake la saba, aliwataka wajumbe kujibu kwa nini wanaishutumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa imeingiza maoni yake, wakati ilikusanya maoni hayo kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?

Alisema badala ya kujadili hoja za msingi, wajumbe wa Bunge hilo wamekuwa wakitoa lugha za kejeli na matusi kwa baadhi ya watu (akiwamo na yeye), kitendo ambacho alisema si sahihi na kinaweza kuligawa taifa kwa sababu yaliyomo katika Rasimu ya Katiba yametokana na maoni ya wananchi.


*Amshukia Lukuvi

Katika maelezo yake, Jaji Warioba alieleza kushangazwa kwake na wajumbe kulitumia Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kama mfano wa kuwashawishi Watanzania kukubaliana na matakwa yao ya kutaka kupinga mfumo wa serikali tatu.

"Nchi hii imekuwa na matatizo ya rushwa na ufisadi, lakini hakuna hata siku moja mtu amesema jeshi linaweza kushika madaraka. Leo kwa sababu ya madaraka mnaingiza jeshi na mchakato wa Katiba katika makundi."

Licha ya kutomtaja mlengwa, kauli hiyo ilionekana kumlenga Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge), William Lukuvi ambaye Aprili 13, mwaka huu aliwataka wananchi kupinga muundo wa serikali tatu, akisema la sivyo jeshi linaweza kuchukua madaraka.

Akiwa katika Kanisa la Methodist, Jimbo la Dodoma alipokuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Lukuvi alisema muundo huo ukipita, nchi itatawaliwa na jeshi kwa kuwa Serikali ya Muungano itashindwa kuwalipa mishahara wanajeshi.

Kauli kama hiyo pia iliwahi kutolewa na Rais Jakaya Kikwete wakati akizindua Bunge Maalumu laKatiba mjini Dodoma.


"Msiliingize jeshi katika siasa za makundi na inakuwa mbaya zaidi kama mkienda katika makanisa na kutoa kauli za namna hii," alisema Warioba na kuongeza:

"Umoja wetu, amani na utulivu kwa kiwango kikubwa mhimili wake ni viongozi wa dini. Wamekuwa wakihubiri umoja, amani na mshikamano, hivyo tusiingize siasa za makundi kwenye makanisa na misikiti."

Jaji Warioba aliwataka wajumbe wa Bunge hilo kukumbuka wajibu wao wa kuwaunganisha wananchi na kuwataka waachane na kauli za kejeli, kuudhi na matusi kwani zinaweza kuleta mgawanyiko na mpasuko nchini.

"Nimekuwa mtumishi wa umma kwa muda mrefu lakini sijawahi kuona taasisi yenye uzalendo wa hali ya juu kama JWTZ," alisema Warioba.


Warioba ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, kuanzia mwaka 1985 hadi 1990, alisema: "Katika ziara zangu mikoani nilikuwa nikikutana na wanajeshi na kunieleza matatizo yao.

Licha ya wakati huo serikali za mataifa mengine zilikuwa zikipinduliwa na jeshi, hapa kwetu ilikuwa tofauti, walikuwa na uzalendo wa hali ya juu licha ya kuwa hali yetu kiuchumi ilikuwa mbaya," alisema.


Alisema wakati huo wanajeshi walikuwa wakivaa sare zilizochakaa na viatu vilivyopasuka, lakini hawakufikiria kuipindua Serikali.

Alisema hata katika vita dhidi ya Uganda, wanajeshi wa Tanzania walishinda kwa sababu ya uzalendo na siyo vifaa vya kisasa vya kivita... "Inashangaza kuona watu wanatoleamfano mmoja tu wa kama wanajeshi wasipolipwa; kwa nini wasiseme mawaziri au watumishi wa serikali wasipolipwa?"Alisema kauli hiyo ni sawa na kuwaeleza wananchi kuwa jeshi ni baya na kama ikipita Katiba isiyoendana na matakwa ya walio wengi jeshi litachukua nchi.

Alisema wakati Tume ya Mabadilikoya Katiba ikikusanya maoni ya wananchi, wanajeshi na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini walijikita zaidi kutoa maoni ya kuimarishwa kwa ulinzi na usalama na siyo mambo mengine.

"Tatizo ambalo walitueleza ni kuchoshwa na kitendo cha kupiga mizinga 21 kwa Amri Jeshi Mkuu wakiwa Dar es Salaam na wakiwa Zanzibar. Walisema kwa nidhamu ya jeshi, Amri Jeshi Mkuu ni mmojatu. Nadhani mngewaondolea kero hiyo na si mambo mengine," alisisitiza.


*Kigwangalla

Kwa upande wake, Dk Kigwangalla alisema kama tatizo ni Muungano ni vyema suala hilo likarejeshwa upya kwa wananchi ili watoe maoni yao kwa sababu mchakato huo sasa umehamia katika muundo wa Muungano pekee.

"Mchakato huu si wa kuifufua Tanganyika na kuvunja mkataba wa Muungano na siyo wa kubadili muundo wa utawala. Mambo haya yalihitaji mchakato unao jitegemea," alisema.

Alisema tume zote zilizotoa mapendekezo ya Serikali tatu zilikuwa na asilimia ndogo ya watu waliounga mkono kama ilivyo kwa Tume ya Jaji Warioba.

WATU 63 WAARIFIWA KUFA KATIKA AJALI YA TRENI DRC

Takriban watu 63 wamefariki baada ya treni iliyokuwa imebeba abiria kupoteza mwelekeo Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.


Msemaji wa serikali Lambert Mende alisema kuwa polisi wanahofia kuwa idadi ya watu waliofariki huenda ikaongezeka. Pia alisema kuwa polisi watafanya uchunguzi kubaini chanzo cha ajali.

Ajali hiyo ilitokea karibu na eneo la Kamina katika mkoa wenye utajiri wa madini wa Katanga.

Treni hiyo ilikuwa imebeba idadi kubwa ya watu kupindukia wengine wakiwa wameketi juu ya treni yenyewe.

Waziri wa mambo ya ndani katika mkoa huo Jean Marie Dikanga Kazadi, aliambia BBC kuwa dereva wa treni hiyo alikuwa anaiendesha kwa kasi.


Watu 80 walijeruhiwa vibaya huku wengine saba wakiwa bado wamekwama ndani ya treni vifusi.

Treni ilianguka Jumanne asubuhi lakini waokozi waliweza tu kuwasili nyakati za jioni.

Sehemu kubwa ya njia ya reli ya DRC, imesalia katika hali yake tangu enzi za ukoloni na ni nadra kufanyiwa ukarabati.

Treni hiyo ilianguka wakati dereva alipokuwa anajaribu kupunguza kasi.

JAJI WARIOBA AWATAKA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUACHA MALUMBANO

Aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba, jaji mstaafu, Joseph Warioba, ameeleza wasiwasi wake juu ya lugha zinazotumiwa na wajumbe wa bunge maalum la katiba na kwamba hazimpi matumaini kama wanaweza kufikia maridhiano, huku akiwaonya wajumbe hao kuacha malumbano badala yake watafute njia ya kushirikiana.


Jaji Warioba ametoa rai hiyo jijini Dar es salaam baada ya kuzindua ripoti maalumu iliyotolewa na taasisi ya utafiti yatwaweza kuhusu katiba, ambapo amesema ili kuepuka hali inayoendelea katika bunge hilo, ni lazima wajumbe hao wafikie maridhiano kwani katiba haiwezi kupatikana bila ya kuwapo kwa muafaka baina yao.


Akizungumzia namna tume yake ilivyoshikamana katika kukusanya maoni ya wananchi jaji warioba amesema tume ilipata maoni kutoka kwa wananchi wanaozungumzia utawala bora, wanataka kuwapo kwa miiko ya uongozi, hivyo wakaa pamoja na kuyaratibu mwisho wa siku wakaja na rasimu moja, na kuwataka wajumbe hao wajirekebishe, wafanye kile ambacho wananchi wahitaji na kilichowapeleka Dodoma.


Uzinduzi huo pia umeshirikisha baadhi ya wajumbe wa bunge maalum la katiba ambapo Dk. Hamisi Kigangwala alikuwa miongoni mwao ambaye mbali na kutokukubaliana na utafiti huo kwa madai kuwa siyo wa kisayansi amesema kujitoa kwa baadhi ya wajumbe siyo sababu ya kuvunjika kwa bunge hilo bali litavunjika lenyewe hapo baadaye iwapo safu inayotakiwa kikanuni itapungua lakini akaongeza kuwa katiba haiwezi kupatikana bila kuwapo kwa maridhiano baina ya makundi yanayohusika.


Kwa upande wake Julius Mtatiro ambaye pia ni mjumbe wa bunge hilo amesema iwapo wajumbe wanataka kujadili muundo wa serikali mbili basi iundwe tume nyingine kwa ajili ya kujadili aina hiyo ya serikali na iwapo baadhi ya wajumbe hao wanang'ang'ania serikali mbili kitakachotokea ni wananchi kuendelea na katiba ile ile iliyopo na hivyo kukosa yale waliyoyataka kuingizwa kwenye katiba mpya kwa mustakabali wao.

CHINA NA MAREKANI WALAANI MAUWAJI S.KUSINI

China na Marekani zimelaani ghasia zinazoendelea nchini Sudan, kufuatia shutuma kwamba wapiganaji waasi waliwauwa mamia ya raia katika mji wenye utajiri wa mafuta wa Bentiu.


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa China amezitaka pande zote husika kwenye mzozo huo kufanya mazungumzo ya kisiasa na kuwataka maafisa wa Sudan Kusini kulinda maslahi ya Uchina.

Uchina ni muwekezaji mkuu katika sekta ya mafuta Sudan kusini.

Ikulu ya White house imeelezea ghasia nchini Sudan kama zisizokubalika nakwamba zinakiuka imani ya raia wa Sudan Kusini waliyokua nayo kwa viongozi wao.


Kadhalika Marekani imesemakuwa imeshangazwa na mauaji ya kinyama ya mamia ya raia Sudan Kusini na kutoa wito wa kusitishwa kwa msururu wa vurugu zinazoendelea nchini humo.

Umoja wa mataifa ulisema siku ya Jumatatu kwamba waasi waliwauwa mamia ya raia katika mji wa Bentiu na wengi walikufa katika msikiti mmoja, hosipitali na kanisa ambako walikuwa wamekimbilia kutafuta usalama.


Msemaji wa ikulu ya White House, Jay Carney, amesema kuwa rais, Salva Kiir, na kiongozi wa waasi ni sharti watangaze hadharani kuwa mashambulizi dhidi ya raia haya kubaliki.

Maelfu ya watu wamefariki dunia tangu mapigano ya kikabila yazuke mwezi Disemba mwaka uliopita.

AFISA MKUU WA POLISI AUWAWA MISRI

Maafisa wa usalama nchini Misri wanasema afisa wa ngazi ya juu wa polisi nchini Misri ameuawa katika shambulio la bomu katika mji mkuu Cairo.

Polisi huyo Brigedia Generali Ahmed Zaki aliuawa katika kitongoji cha Magharibi mwa mji huo baada ya bomu lililokuwa limetegwa chini ya gari lake kulipuka.

Shambulio hilo ni la hivi karibuni katika mfululizo wa mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama tangu kung'olewa madarakani kwa aliyekuwa Rais Mohamed Morsi Mwezi Julai mwaka jana

Mjini Alexandria,afisaa mwingine mmoja aliuawa wakati wa shambulizi dhidi yakile maafisa wanasema ni maficho ya wanamgambo.

Wapiganaji wa kiisilamu wameongeza kasi ya mashambulizi dhidi ya maafisa wa usalama na kuwaua mamia tangu jehi kumwondoa mammalakani Morsi.

Mnamo siku ya Jumapili, mtu aliyekuwa amejihami kwa bunduki alimpiga risasi na kumuua afisaa mmoja wa polisi aliyekuwa anashika doria.

Shambulizi hilo lilitokea siku moja baada ya polisi mwingine kuuawa mjini Cairona kundi la wapiganaji wajulikanao kama Ajnad.

Kundi hilo linasema linashambulia polisi kwa sababu ya msako unaofanywa dhidi ya kundi la Muslim Brotherhood. Zaidi yawatu 1,300 wameuawa na wengine 16,000 kuzuiliwa.

Ghasia hizi huenda zikatishia usalama wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Mei, ambapo aliyekuwa mkuu wa majeshi Abdul Fattah al-Sisi anatarajiwa kushinda.

WALIOFARIKI KATIKA FERI WAFIKIA 113

Idadi ya watu waliofariki kutokana na ajali ya feri iliyozama wiki jana nchini Korea Kusini imefika 113.


Wapiga mbizi walipata miili zaidi hii leo ndani ya Feri hiyo. Wamekuwa wakijaribu kufikia sehemu ya mkahawa wa feri hiyo ambako wanatarajia kupata miili zaidi.

Watu 190 bado hawajapatikana , wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa shule ya sekondari iliyo karibu na mji mkuu Seol.

Wahudumu wa feri hiyo bado wanazuiliwa kwa kusababisha ajali hiyo hasa baada ya Rais wa taifa hilo kusema hapo jana kuwa kitendo chao kinatosha kuwa mauaji.

Maafisa wanasema wataanza juhudi za kuiondoa Feri hiyo kutoka majini Siku ya Alhamisi baada ya mashauriano na ndugu wa waathiriwa wa ajali hiyo.


Feri hiyo ilizama katika muda wa saa mbili wiki jana na haijulikani kilichosababisha ajali hiyo.

Wafanyakazi wa feri hiyo wanalaumiwa kwa kukosa kuwaokoa abiria wengi waliokuwa wameabiri feri hiyo.

Watano kati yao tayari wamefunguliwa mashitaka ya kuzembea katika kazi ya kuwaokoa waathirwa.

Wakati meli hiyo ilipokuwa inazama, abiria wanadai kuwa waliambiwa kusalia ndani ya ferry na kujifungia katika baadhi ya vyumba huku kukizuka hali ya wasiwasi ikiwa abiria waondoke kwenye Feri.

Inaarifiwa kilio cha kwanza cha kutaka msaada kilitoka kwa kijana mmoja akiwa na uoga na kisha kufuatiwa na simu nyingine kutoka kwa wanafunzi 20 wakitaka kusaidiwa.


Takriban abiria 174 waliokolewa kutoka kwa feri hiyo iliyokuwa imewabeba watu 476 ikiwemo wanafunzi 339 pamoja na walimu waliokuwa wanafanya ziara ya kimasomo.

WAASI WAKANA MAUAJI SUDAN KUSINI

Waasi nchini Sudan Kusini wamekanusha madai yaliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuwa waliwaua watu kwa misingi ya ukabila.

Msemaji wa waasi, Brigedia Lul Ruai Koang, ameambia BBC kuwa wanajeshi wa serikali ndio waliowaua raia walipokuwa wanaondoka mji wa Bentiu uliotekwa wiki janana waasi wanaomuunga mkono makamu wa zamani wa Rais Riek Machar.

Umoja wa Mataifa katika ripoti yake iliyotolewa Jumatatu, ulisema kuwa takriban watu miambili waliokuwa wamepewa hifadhi msikitini na wengine wengi wakiwa wanahifadhiwa hospitalini na makanisani waliuawa kwa sababu ya kabila lao.

Jeshi la Sudan Kusini linasemakuwa linakabiliana vikali na waasi hao katika majimbo matatu nchini Sudan Kusini.

Zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kuondoka makwao tangu mapigano kuanza Disemba mwaka jana.

Mgogoro huo ni kati ya Rais Salva Kir wa kabila la Dinka na Riekl Machar aliyekuwa makamu wa Rais anayetoka kabila la Nuer Pande zote mbili zinasemekana kufanya mauaji.

Lakini mauaji yaliyofanywa na waasi mjini Bentiu, Bor na Malakal, umewafanya watu kumchukia kiongozi wa waasi Riek Machar.

Mapigano huenda yakaanza tena ingawa pia mazungumzoya kusitisha vita yanatarajiwa kuanza nchini Ethiopia katika wiki chache zijazo.

Kumekuwa na taarifa za jeshi kuwalenga watu wa kabila la Nuer huku waasi wakiwalenga watu wa jamii ya Dinka.

TATOO YAMTIA SHAKANI MTALII

Mtalii mmoja muingereza amekataliwa kuingia nchini Sri Lanka baada ya kupatikana akiwa amechorwa'Tattoo' ya Budhaa kwenye mkono wake.

Naomi Michelle Coleman, alikamatwa na maafisa wakuu alipowasili katika uwanja wa ndege katika mji mkuu Colombo baada ya maafisa wakuu kuiona 'Tattoo' hiyo kwenye mkono wake wa kulia.

Budhaa alikuwa mtu mwenye busara na hekima kubwa na pia mwanzilishi wa dini hiyo ambayo mafunzo yake mengi yalijenga msingi wa dini yenyewe.

Msemaji wa polisi alisema kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37, alikamatwa kwa kosa la kuwachukiza watu wa dini ya Budhaa na pia kwa kuumiza hisia zao za kidini.

Hakimu aliamuru Bi Coleman arejeshwe nchini mwao.

Kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha wahamiaji wanaosubiri kurejeshwa makwao.

Maafisa huchukua hatua kali dhidi ya watu wanaonekana kutusi dini ya Budhaa ambayo waumini wake wengi wanatoka kabila la Sinhalese lenye idadi kubwa ya watu nchini humo.

Bi Coleman aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bandaranaike siku ya Jumatatu kutoka nchini India ambapo maafisa punde ya kuiona Tattoo hiyo ya Budhaa akiwa amekaa kwenye mauwa, walimkamata.

Mwezi Machi mtalii mwingine muingereza, alizuiwa kuingia katika uwanja huo baada ya maafisa kusema kuwa alijibu kijeuri alipohojiwa kuhusu Tattoo aliyokuwa amechorwa ambayo pia ilikuwa na Budhaa.

MADUKA YATEKETEA NA MOTO DODOMA

Maduka matatu makubwa yameteketea kwa moto na mengine yameathirika katikati ya mji wa Dodoma baada ya jengo linalodaiwa kumilikiwa na mamlaka ya uendelezaji makao mkuu-CDA kuwaka moto.


Katika maduka hayo yaliyokuwa mkabala na makao makuu ya cmm na kukuta moto mkubwa ukiendelea kuteketeza, huku vikosi vya zimamoto na jeshi la polisi vikifanya jitihada za kukabiliana na moto huo husivamie maduka mengine huku baadhi ya wamiliki wa maduka wakiondoa bidhaa zilizomo ndani ya baadhi ya maduka kwa hofu ya moto huo kuingia katika maduka yao.

Akizungumza mkuu wa wilaya ya Dodoma bwana Lify Gembe amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, na inaseemekana moto huo umeanza katika duka moja linalouza vipodozi.

Kwa upande wake mkuu wa kikosi cha zimamoto mkoa wa Dodoma Sajenti Meja Amri Issa amesema umbali wa eneo ya kuchukua maji na uchakavu wa vifaa umesababisha zoezi la kukabiliana na moto huo kuchukua muda mrefu na kuwataka wamiliki wa maduka kuhakikisha wanaweka vifaa vya kuzimia moto.

Wakizungumza baadhi ya wamiliki wamelalamikia kikosi cha zimamoto kukosa vifaa huku mipira ya maji ikionekana kutoboka hali inayosababisha maji kuvuja barabarani, huku wengine wakidai askari wanashindwa kupanda juu ya magari zimamoto ili kunusuru baadhi ya mali za watu zisiteketee.

ZAIDI YA WATU 10 WAFARIKI NA WENGINE 44 WAJERUHIWA KATIKA AJARI YA GARI

Zaidi ya watu 10 wamefariki dunia papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa baada ya basi la Luwuye express walilokuwa wamepanda likitoka Tarime kwenda Mwanza kuacha njia na kuparamia nyumba na kupinduka katika kijiji cha Itwimila wilaya ya Busega mkoani Simiyu.


ITV ilifika katika eneo la tukio mara tu baada ya ajali hiyo kutokea na kukuta umati mkubwa wa watu ambao wengine ni wakazi wa kijiji hicho cha Itwimila a, kitongoji cha Inchira, kata ya Kirureli wilaya ya Busega mkoani Simiyu na wengine ni abiria waliokuwa wakisafiri na basi hilo la Luhuye express yenye namba za usajili t.410 awq inayodaiwa kuwa ilikuwa ikitoka tarime kuelekea mwanza.


Licha ya ITV kushuhudia baadhi ya miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo huku idadi ya watu waliojeruhiwa ikionekana kubwa zaidi, baadhi ya watu wamedai basi hilo ilikuwa ikiendeshwa kwa mwendo kasi sana lakini ilipofika katika eneo hilo, ghafla tairi ya mbele ya gari hilo ilipasuka na kusababisha basi hilo kuacha njia na kupinduka mara kadhaa na kuvamia nyumba ya mkazi wa eneo hilo ambalo limejengwa pembezoni mwa barabara kuu ya kuelekea Mwanza.


Kutokana na maumivu makali, baadhi ya abiria ambao ni majeruhi walionekana wakiomba msaada kwa watu ili kukimbizwa katika hospitali mbalimbali za jirani jambo ambalo itv kwa kushirikiana na mashuhuda walifanikisha kulifanya huku gari ya polisi moja nalo likiwa limefanikiwa kufika katika eneo la tukio kutoa msaada ambapo baadhi ya majeruhi waliingizwa katika gari kwa ajili ya kukimbizwa hospitalini.


Baadhi ya watu wameonekana kupoteza maisha huku wengine wakilaliwa na tairi za gari na wengine wameonekana kuvunjika sehemu mbalimbali ya miili baada ya kuangukia nje kupitia madirisha ya busi hilo.

ITV ilizungumza na kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu SACP Charles mkumbo kwa njia simu na kithibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akidai kuwa idadi ya walipoteza maisha kwa upande wa wanawake ni wanne, wanaume walipoteza maisha ni sita na mtoto ni mmoja huku idadi ya majeruhi akidai kuwa ni 44 ambapo wanawake ni 19 na wanaume ni 25 na kwamba majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya bugando jijini mwanza na wengine katika hospirtali ya wilaya ya magu huku chanzo cha ajli hiyo akidai haijajulikana na kwamba dereva wa basi hilo hajaonekana hivyo hawana uhakika iwapo amefariki au amekimbia kwani kuna mtu alionekana akikimbia wakati wa ajali ila haijajulikana iwapo ni dereva wa basi hilo au lah.

Chanzo: ITV

MAKALIO MADOGO KIKWAZO VENEZUELA

Wanawake nchini Venezuela wanatumia kemikali haramu kuongeza ukubwa wa makalioyao na kujiletea madhara makubwa ya kiafya

Hii ni kutokana na mtindo ambao unaonekana na wengi nchini humo kwamba mwanamke mwenye makalio makubwa ndiye anayependeza zaidi

Wanawake wengi sasa wanahatarisha afya zao kwa kutaka kuwa 'warembo' Akiwa anabubujikwa na machozi , mwanamke kwa jina Denny anakumbuka vyema alivyoamka siku moja na kujipata na uvimbe sawa na ukubwa wa mpira katika sehemu ya chini ya mgongo wake.

Hangeweza kutembea wala kuinama na uchungu ukawa mwingi kupita kiasi.

Hata kabla ya kumwona daktari, Denny, mwenye umri wa miaka 35 ambaye pia ni wakili, alijua kuwa hiyo ilikuwa athari ya kudungwa kemikali ijulikanayo kama 'silicon' , ili kuongeza ukubwa wa makalio yake.

Uvimbe huo ulisonga hadi katika sehemu ya chini ya mgongo wake na kuanza kuumiza uti wake wa mgongo. Yote kwa sababu ya kutafuta urembo.

"nilishtuka sana . Singeweza kutembea na hivyo ndivyo masaibu yangu yalivyoanza, ''alisema Denny.

Sindano ambazo wanawake hujidunga ili kuongeza ukubwa wa makalio , ni moja ya mbinu ya kujiongeza urembo ambayo wanawake wengi wamebugia nchini Venezuela.

Sindano hizo zilipigwa marufuku na serikali mwaka 2012, miaka sita baada ya Denny kudungwa.

Denny alidungwa sindano ya kemikali hiyo ya Silicon mwaka 2006 na leo ndio ameanza kuhisi athari zake.


*Miaka 18-50

Hata hivyo wanawake wengi wanaendelea kujiongezea makalio. Takriban asilimia 30 ya wanawake walio kati ya umri wa miaka18 na 50 wanatumia Silicon kuongeza ukubwa wa makalio yao.

Wanawake wanavutiwa na mbinu hii ya kuongeza ukubwa wa makalio kwa sababu bei yake ni nafuu. Lakini madhara yake ni amkubwa mno.

Madaktari wanasema kuwa kemikali hii husambaa mwilini na pia inaweza kuathiri kinga ya mwili.

Utafiti unaonyesha kuwa wanawake zaidi ya kumi hufariki kila mwaka kutokana na kudungwa sindano hizo.

Kuna madaktari wawili pekee wanaoweza kumfanyia upasuaji mtu kama Danny aliyeathrika kutokana na kemikali hiyo lakini kwa Danny anahitaji kusubiri kwa mwaka mmoja kabla ya kufanyiwa upasuaji huo maana kuna wanawake wengi kwenye orodha ya wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.

Wanawake wengine wanasema kuwa wanalazimika kuongeza ukubwa wa makalio kutokana na shinikizo za wapenzi wao. Lakini madhara yanapowakuta , ni wao wanaoteseka zaidi.

Astrid de la Rosa ambaye sasa ni mwanaharakati anayepinga sindano hizo, anasema yeye hakujua kama mwanamume angeweza kumfanya akaongeze ukubwa makalio yake.

Nusura amuache Lakini madhara yalimpata walati kinga yake ya mwili ilianza kuathirika baada ya kudungwa sindano hiyo na kuwa na makali makubwa..Wanaharakati nchini Venezuela wanataka serikali ichukue hatua kali zaidi dhidi ya wanaowadunga wanawake sindano hizo za 'Biopolymer.

'Waigizaji , wanaume kwa wanawake, wanamitindo , wote hawa wanataka kupendeza na hivyo hudungwa sindano hizo nchini Venezule, lakini madaktari wanaonya kuhusu madhara yake ambayo ni makubwa mno.

KIKOSI CHA TAIFA STARS CHATANGAZWA

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza wachezaji wengine 23 watakaoingia kambini kesho (Aprili 20 mwaka huu) kuungana na 16 waliotajwa awali kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu.


Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam), Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadili Ali (Azam).

*Mabeki

Abdi Banda (Coastal Union), Aidan Michael (Ruvu Shooting), Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kelvin Yondani na Said Moradi (Azam).


Viungo

Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga), Himid Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba).


*Washambuliaji

Athanas Mdamu (Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).


Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).


Viungo

Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).


Washambuliaji

Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga) na Bayaga Athanas Fabian (Mbeya).

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach.

TUNDU LISSU ADAI HATI YA MUUNGANO ILIYOPELEKWA NI FEKI

Hata baada ya Wajumbe wa Bunge Maalumu kugawiwa nakala za Hati ya Muungano, Tundu Lissu, ameendelea kung'ang'ana kuwa haipo, ni feki.

Akizungumza kwenye Viwanja vya Bunge mjini hapa mara baada ya nakala kugawiwa bungeni, Lissu ambaye aliibua hoja hiyo alisema; "Hivi hawa wanamghiribu nani? Nasema hiyo hati haikuwahi hata kupelekwa Umoja wa Mataifa."

Alisema saini iliyo kwenye hati hiyoni tofauti na zilizo kwenye hati ya Mabadiliko ya Kwanza ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya 10 ya Juni 1965, Hati ya Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Fedha za kigeni na Sheria ya kugawa ardhi kwa Wazanzibari ambazo zote zinafanana.

Lissu alisema kwa miaka 50 haikuwahi kuonyeshwa, wala haikuwahi kuwa UN na hata Zanzibar hawana.

Alisema walishuhudia Benard Membe (Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) akisema iko UN, jambo alilosema ni kudanganyana tu.

Alisema nyaraka kama hizo, mkataba wa Uhuru zinatakiwa kuwekwa Makumbusho ya Taifa kwa kuwa ni nyaraka wazi zinazotakiwa kuona na kila anayetaka, kwa rahisi.

"Marekani ilipata uhuru zaidi ya miaka 200, lakini kila nyaraka za uhuru zinaonekana kwa rahisi siyo hapa...mambo yanafanyika chini kwa chini, utadhani biashara haramu," alisema.

Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu wamembeza Lissu kwa hoja hiyo wakisema hatua ya nakalazake kufikishwa bungeni ni sawa na kumfunga bao la kisigino na kuhoji watazungumza nini baada ya hati kupatikana.

MUGABE AWAONYA MABALOZI KUHAMASISHA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ametishia kuwafukuza kutoka nchini humo wanadiplomasia wanaopigia debe mapenzi ya jinsia moja.

Katika hotuba yake ya sherehe za kuadhimisha uhuru wa nchi hiyo, Mugabe alitumia fursa hiyo, kukaripia kile alichokiita upuuzi wa nchiza ulaya zinazohubiri ushoga

Alituhumu nchi za ulaya kwa kukosa maadili na kusisitiza kuwa ndoa inaweza kuwa tu kati ya mwanamke na mwanamume.

Sio mara ya kwanza Mugabe amekemea swala la ushoga.

Aliwahi kuwataja mashoga kuwa wabaya kuliko Mbwa na Nguruwe.

Mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Zimbabwe na mashoga hukamatwa mara kwa mara kwa kosa hilo.

MELI YA MIZIGO FB MATARA YAZAMA ZIWA VIKTORIA

Watu 10 wamenusurika kufa maji katika ziwa Victoria baada ya meli ya mizigo Fb Matara kupinduka na kuzama ikiwa na shehena ya sukari tani 280 zilizonunuliwa katika kiwanda cha sukari Kagera wakati ikitoka Bukoba kwenda jijini Mwanza.

Meli hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Mkombozi fishing and marine transport limited, imezama ikiwa na magunia 5600 ya sukari sawa na tani 280, mali ya mfanyabiashara wa jijini Mwanza aitwaye V.h. Shah, ambapo mkurugenzi wa kampuni hiyo Gitano Chacha Munanka ameeleza kwamba meli hiyo imezama ikiwa katikati ya visiwa vya Kerebe na Lukolu majira ya saa 10.30 usiku na kuongeza kwamba hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa kufuatia tukio hilo.

Imeshuhudiwa meli hiyo ikiwa imepinduka huku juhudi za wafanyakazi wa kampuni hiyo kuipundua zikiwa zinaendelea bila mafanikio, huku baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakisema chanzo cha meli hiyo kuzama ni kutokana na dhoruba kali ambapo wametoa ushauri kwa wamiliki wa vyombo vya majini kuzingatia utabiri unaotolewa na mamlaka ya hali ya hewa nchini ili kuepusha maafa.

Meli hii ilianza safari yake ya kutoka Bukoba majira ya saa 7 mchana, ikiwa inaendeshwa na kapteni Erick Lasana-mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra kanda ya ziwa, umethibitisha kuzama kwa meli hiyo yenye uwezo wa kubeba tani 280 za mizigo na abiria 100.

WASOMALI WALAANI MARUFUKU YA MIRAA NCHINI UINGEREZA

Jamii ya wasomali waishio nchini Uingereza wanaotafuna mmea wa Miraa wameelezea hasira yao baada ya serikali ya Uingereza kuthibitisha kuwa itapiga marufuku kileo hicho.
Uingereza ni mnunuzi mkuu wa mmea wa Miraa Katika mataifa ya Magharibi.
Mmea huo unaokuzwa zaidi katika eneo la Afrika mashariki , hutafunwa zaidi na wasomali waishio nchini Uingereza.

Mwandishi wa BBC wa Idhaa ya Kisomali Rage Hassan alitembelea duka linalouza miraa saa 24 kaskazini mwa mji wa London kushuhudia hali ya watafunaji wa Miraa.
Wafanyi biashara wanasema kuwa kuiharamisha Miraa itawanyima kitega uchumi chao.
Zao la miraa linategemewa sana kiuchumi na wakulima wengi katika maeneo ya Meru na Embu nchini Kenya.
Iwapo itapigwa marufuku Uingereza itakuwa taifa la pili kuharamisha mmea huo baada ya Uholanzi kupiga marufuku uingizaji na uuzaji wa Miraa.

Majina.
Miraa pia Inafahamika kama Khat na mairungi kwa walaji.
Ni jani lenye dawa ambalo likitafunwa linatoa juisi ambayo ina visisimuzi vya asili na ni maarufu kwa jamii ya wasomali.
Kuna wasiwasi kuwa dawa zinaweza kusababisha maradhi ya akili au kuchanganyikiwa.
Serikali ya Uholanzi ilisema kelele, uchafu na tishio kwa umma linalotolewa na watu wanaotafuna mirungi kama baadhi ya sababu za kupiga marufuku dawa hiyo.
Watumiaji wanajisikia wako macho, wana furaha na wanaongea sana.
Inakata hamu ya chakula.
Matumizi makubwa yanaweza kusababisha kukosa usingizi, shinikizo la damu, matatizo ya moyo na kukosa nguvu.

Athari za Miraa
*.Watumiaji wanajisikia wako macho, wana furaha na wanaongea sana.
*.Inakata hamu ya chakula.
*.Matumizi makubwa yanaweza kusababisha kukosa usingizi, shinikizo la damu, matatizo ya moyo na kukosa nguvu.
*.Inaweza kusababisha kansa ya mdomo ikiwa itatumika kwa muda mrefu.
*.Inaweza kusababisha kujikia kuwa na wasiwasi,ukorofi na kusababisha hofu na matatizo ya akili.
*.Inaweza kusababisha matatizo ya akili kuwa makubwa zaidi.
*.Inaweza kusababisha kansa ya mdomo ikiwa itatumika kwa muda mrefu.
*.Inaweza kusababisha kujiskia kuwa na wasiwasi, ukorofi na kusababisha hofu na matatizo ya akili.
*.Inaweza kusababisha matatizo ya akili kuwa makubwa zaidi.

Mumea huo kwa kiasi kikubwa unatafunwa na watu kutoka Somalia, Ethiopia, Kenya na Yemen.
Matumzi ya visisimuzi umepigwa marufuku Marekani, Canada na baadhi ya nchi nyingine za Ulaya.
Lakini bado inapatikana Uingereza ambako inauzwa kihalali katika idadi ndogo ya maduka.
Mwaka uliopita ujumbe wa serikali ya Uingereza ilitembelea Kenya kubaini na kuchunguza ukuaji na uuzaji mbali na athari za Miraa.

Wabunge wa kenya pia walitembelea uingereza kuishawishi serikali ya nchi hiyo isipige marufuku Miraa kwani ni kitega uchumi cha mamilioni ya wakulima wanaotokea mkoa wa kati wanchi hiyo ya Kenya.
Aidha kulikuwa na madai kuwa pato kubwa la mmea huo huenda linafaidi makundi ya kigaidi, hata hivyo hakukuwa na ushahidi wa kutosha kudhihirisha madai hayo.




























WAKIMBIZI WAUAWA KATIKA KAMBI S.KUSINI

Afisa mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Sudan kusini Tobby lanzer ameiambia BBC kuwa makumi ya wakimbizi wa ndani ya nchi hiyo iliyosakamawa na vita vya wenyewe kwa wenyewe wameuawa ndani ya kambi ya Umoja wamataifa iliyoko katika mji mkuu wa jimbo la Jonglei BOR.

Afisa anayesimamia shughuli za utoaji misaada ya umoja wa mataifa nchini sudan toby Lanzer amesema kuwa kundi la vijana wanaokisiwa kuwa zaidi ya mia tatu hivi walikuja katika kambi hiyo wakidai kuwa walitaka kuwasilisha malalamiko, kwa wasimamizi wa kambi hiyo. Toby alisema '' Ilikuwa mwendo wa saa nne hivi katikati ya mji mkuu wa jimbo la jonglei BOR ambapo vijana takriban 350 hivi walikusanyika na kuanza kuandamana hadi kwenye ualakambi yetu mara wakavunja lango kuu na kuingia ndani ya kambi.

Maafisa wetu walifyatua risasi ilikuwatawanya lakini wao pia wakaanza kufyatua risasi kiholela na katika tafrani iliyotokea wavamizi hao waliwashambulia wakimbizi waliokuwa wametorokea katika kambi yetu wakati wamapigano yaliyozuka desemba."

Mjini Bor Afisa huyo alilaanitukio hilo akisema ni jambo la kuhuzuzisha kwa watu waliokimbilia usalama ndani ya kambi ya umoja wa mataifa wakivamiwa humo humo na kuwa Umoja wa mataifa sasa utachukua tahadhari zaidi ilikuzuia matukio kama hayo katika siku za usoni.

''Tumeimarisha hali ya usalama katika kambi zetu ilikuwazuia wale wote wenye niya ya kutudhuru sisi na kuanzia sasa tunatoa tahadhari kwa makundi yote kuwa tutatumia nguvu kadri na uwezo wetu ilikuzuia matukio kama hayana kulinda maisha ya wale wote ambao wametorokea hapa ilikuokoa maisha yao''.

Maafisa 2 wa kulinda usalama wa umoja wa mataifa walijeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo.

Kambi ya BOR imehifadhi zaidi ya wakimbizi 5000 tangu mwezi Desemba majeshi ya serikali ya rais Salva Kiir yalipoanza makabiliano na makundi ya wapiganaji wanaomuunga mkono aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Riek Machar.

NAHODHA MKUU WAKUWEPO KATIKA USUKANI WAKATI FERRI IKIZAMA

Naibu wa tatu wa nahodha wa ferri iliyozama ''Sewol'' ndiye aliyekuwa usukani wakati feri hiyo ilipozama.

Uchunguzi wa kimsingi umebaini.

Nahodha mkuu haijabainika alikuwa wapi wakati wa tukio ila inadhaniwa feri hiyo iligonga mwamba na kupinduka kwa haraka baadaya shehena yake kuegemea upande mmoja.

Wachungizi sasa wanaelekeza juhudi zao kubaini kwanini Nahodha wa Sewol hakuwa kwenye usukani na pia kwanini baadaya tukio la kwanza abiria walikanywa wasiruke baharini ilikuokoa nafsi zao kama ilivyodesturi chombo kikigonga mwamba?

Kiongozi wa Mashtaka ya umma nchini Korea bwana Park Jae-Eok amesema kuwa nahodha mkuu Lee Joon-seok,atakuwa na swali la kujibu.

Kufikia sasa abiria 270 waliokuwa ndani ya feri hiyo hawajulikani walipo asilimia kubwa kati yao wakiwa ni wanafunzi waliokuwa wakieleka katika kisiwa cha Jeju kwa safari ya masomo.

Watu 26 pekee ndio wamedhibitishwa kufariki kufikia sasa, huku 179 wakiokolewa.

Makundi ya waokoaji wamefanikiwa kuingia ndani ya feri hiyo kwa mara ya kwanza leo asubuhi baaha yakutoboa shimo upande wa juu wa chombo hicho kilichozama.

Waokoaji walikuwa wameshindwa kuingia ndani ya feri hiyo baada ya bahari kuchafuka.

Mamia ya jamaa na marafiki ya wahasiriwa wamelalamikia ukosefu wa habari za uokaji.

Wengi wamekuwa wakivumilia hali mbaya ya hewa wakiomba kuruhusiwa kusubiri wapendwa wao ufukweni.

MH. LUKUVI AWALIPUA CUF ADAI WANASHIRIKIANA NA UAMSHO

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, amesema, si makosa raia wa Tanzania kuhofia majeshi ya ulinzi kuchukua nchi ikiwa muundo wa Muungano wa serikali mbili ukibadilishwa na kuwa serikali tatu.

Aidha, amesema pia ana hofu kuhusu mwenendo wa CUF unaoshirikiana kisiasa na Taasisi ya kidini ya Uamsho, inayotekeleza majukumu yake Zanzibar kwamba umelenga kuua Muungano na kuhatarisha amani kwa mgongo wa dini ya Kiislamu.

Lukuvi alisema hayo bungeni, alipotoa ufafanuzi wa kauli zake alizozitoa katika Kanisa la Methodist, Jimbo la Dodoma wakati waIbada ya kumsimika Mchungaji Joseph Bundala kuwa Askofu wa Kanisa hilo.

Kauli hiyo ndio iliyodaiwa na Ukawa kuwa moja ya sababu ya kutoka nje ya Bunge kususia kikao.
Madai mengine ya Ukawa yalikuwa ni ubaguzi, matusi na vitisho vinavyoendelea bungeni.
Katika ufafanuzi wake Lukuvi alisema kwamba mfumo wa serikali tatu unaweza ukasababisha nchi kupinduliwa na Jeshi na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaweza ikaongozwa na CUF kwa Sera za Kikundi cha Uamshojambo linalompa hofu ya udini na kuvunjika kwa amani.

Lukuvi ambaye jana alilazimika kukatisha safari yake ya kwenda India kwa matibabu, alisema alichoeleza katika hafla hiyo ya kumsimika Askofu ni hofu zake binafsi kuhusu muundo wa serikali tatu.

"Wote nikiwauliza hapa uamsho ni nani mtasema niCUF, kwa nini sasa nisiwe na hofu ya kidini wakati kuna chama cha siasa ambacho kinamiliki taasisi inaitwa Uamsho lakini ina ladha ya kidini, hizo ndizo sera zao, unakuwaje na chama cha siasa kinachojipanga kutawala Zanzibar lakini kinaendeshwa na sera za Uamsho?

"Wanachosema CUF ndicho wanachosema Uamsho, wakisema serikali tatu ngangari, wakisema serikaliya mkataba sawa kabisa, wapi umeona vikundi kama hivyo, ukiona chama kinajitayarisha kuchukua madaraka na kinatumia taasisi hii kueneza sera zake ni hatari kwa mustakabali wa nchi," alisema.

Akizungumzia hofu ya nchi kupinduliwa, Lukuvi alisema katika muundo wa Serikali tatu, Rais wa shirikisho hawezi kuwa Amiri Jeshi Mkuu, kutokana na kutokuwa na vyanzo vya mapato hivyo haiwezi kuendesha vyombo vya dola kama Jeshi na Polisi ambao mara nyingi bajeti zao ni kubwa na hazijawahi kutosha hata katika serikali mbili za sasa.

"Kwa mfumo huu wa serikali tatu, tusiwatafutie sababu wanajeshi wetu, mimi nilishasema sitashiriki kutafuta vyanzo kwa serikali ya tatu badala yake naukataa muundo huu," alisema Lukuvi na kuongeza kuwa katika ukosefu mkubwa wa mapato, majeshi yahawezi kuvumilialazima kutokee uasi na hiyondio hofu yake.








RAIS KIKWETE ATEUWA MABALOZI WATATU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Mabalozi ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi na Mabalozi wastaafu kwa mujibu wa sheria.
Mabalozi wateule na aliyehamishwa kituo ni kama ifuatavyo:

1. Balozi Dora Mmari Msechu; ameteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Stockholm, Sweden. Hadi uteuzi huu unafanyika Balozi Dora Mmari Msechu ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Anachukua nafasi ya Balozi Mohamed M .H. Mzale ambaye amestaafu.

2. Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba, ameteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Moscow, Urusi. Hadi uteuzi huu unafanyika, Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba alikuwa Mkuu wa Utendaji Kivita na Mafunzo, Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Anachukua nafasi ya Balozi Jaka Mwambi.

3. Kadhalika, Mheshimiwa Rais amemteua Ndugu Joseph Edward Sokoine kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Kabla ya uteuzi huu, Bw. Sokoine alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania, Ottawa, Canada.


UKAWA WATISHIA KUANDAMANA

Umoja wa viongozi wa katiba ya wananchi (UKAWA) umetishia kuanzisha maandamano makubwa hadi ikulu, endapo Rais nchini na Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha daftari la wapiga kura, hawatafanya marekebisho kabla ya chaguzi zijazo.

Hayo yamesemwa na makatibu wakuu wa vyama vya upinzani nchini, kikiwemo chama cha CHADEMA, CUF na NCCR, ambapo wamesema watanzania milioni tano na laki nane hawana vitambulisho vya kupigia kura.

Vyama hivyo vimewataka viongozi husika, kufanya jitihada za kurekebisha daftari hilo, ili chaguzi zijazo ziwe za huru na haki

USHAHIDI WA MTAALAMU WAZUA UTATA KESI YA PISTORIUS

Mtaalamu wa uchunguzi wa mauaji anahojiwa vikali na mwendesha mkuu wa mashitaka katika kesi ya mauaji dhidi ya mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius.

Picha za risasi zilizomuua Reeva Steenkamp alizopiga Roger Dixon zilikinzana na zilie zilizopigwa na polisi na mtaalamu mwingine wa mauaji waliokuwa mashahidi wa upande wa mashitaka.

Pistorius alikana kumuua mpenzi wake Reeva kwa makusudi mwezi Februari mwaka jana.
Aliambia mahakama kuwa alifyatua risasi baada ya kuhisi kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande wa mashitaka unasema kuwa Pistorius alimuua mpenzi wake aliyekuwa na miaka 29 baadaya wawili hao kuzozana
Huenda Oscar akafungwa jelamiaka 25 au kifungo cha maisha ikiwa atapatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake kwa makusudi.
Kesi hiyo inatarajiwa kuahirishwa hadi tarehe 5 mwezi Mei.
Roger Dixon, ni shahidi wa upande wa utetezi, na katika ushahidi wake alisema kuwa Steenkamp alikuwa anasimama karibu na mlangona risasi zote nne zilimgonga hadi akaanguka sakafuni kinyume na ushahidi wa upande wa mashitaka ulivyosema nkuwa Pistorius aligeuka katika sehemu alipokuwa na kuendelea kumpiga risasi Steenkamp.

Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani anasema kuwa ushahidi wa bwana Dixon unakinzana na ule wa upandewa mashitaka unaosema kuwa Steenkamp alikuwa na muda wa kupiga mayowe baada ya kupigwa risasi ya kwanza na kisha Pistorius akaendelea kumpiga risasi.