Baadhi ya waandamanji walipura mawe na kuchoma magurudumu ya magari na kufunga mabarabara ya miji wakidai serikali haikuzingatia matakwa ya wananchi kama vile elimu sekta ya afya na muundo msingi.
Katika tukio linaloibua hofu ya kuwepo kwa usalama wafanyakazi wa umma na walimu walijiunga na waandamanaji katika miji yote mikuu ikiwemo mji mkuuwa Brasil.
Wengi wao waliahidi kurejea mabarabarani kadri mchuanohuo unavyosongea.
Mwaka uliopita takriban watumilioni moja walishiriki maandamano wakilalamikia ufisadi ubadhirifu wa mali ya umma na ongezeko la gharama ya uandalizi wa kipute hicho cha fainali ya dimba la dunia.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 12 June.
Waandamanaji walianzia Sao Paulo,karibu na uwanja wa Corinthians Itaquera karibu na mtaa wa Itaquera.
Uwanja huo wa Corithians ndio utakaoandaa mechi ya ufunguzi wa kombe la dunia mwaka huu tarehe 12 juni.
Kwa mujibu wa shirika moja la kijamii linaloandaa maandamano hayo HomelessWorkers Movement waandamanji wanaitaka serikali kutumia fedha katika ujenzi wa nyumba.
Kulingana naye hangependa viwanja vilivyogharimu mabilioni ya dola viharibiwe ila wafanyikazi wanaojenga viwanja hivyo wajengewe nyumba kuambatana na ubora wa shirikisho la soka duniani FIFA.
Serikali imepinga uhisano wowote kati ya maandamano haya na kombe la dunia.
Waziri wa michezo Aldo rebelo amenukuliwa akisemakuwa ameona matakwa ya waandamanaji na ikampa matumaini maandamano hayo hayataathiri ujio wa takriban watalii milioni tatu na wageni laki sita wanaotarajiwa kuzuru miji itakayoandaa mechi za kombe la dunia.
Hata hivyo maandamano haya yanawadia wakati ambapo serikali inakabiliwa na mgomo wa wafanyikazi wa umma na hata polisi katika jimbo la Pernambuco