DIAMOND NDANI YA BET AWARDS

Msanii kutoka Tanzania Diamond Platnumz ameipa tena heshima kubwa bendera ya Tanzania kwa kuwa kwenye kipengele cha msanii bora wa Kimataifa (Best International Act) Hii ni hatua kubwa kwa Diamond baada ya siku chache tu nyuma alitangazwa kwenye tuzo za MTV Base (Mama Awards).

Diamond Platnumz kwenye kipengele hiki cha tuzo kubwa za Television ya burudani Marekani ya BET yupo kama Best International Act Africa naanawania tuzo hii na wasanii Davido kutoka Nigeria, Mafikizolo kutoka South Africa,Tiwa Savage kutoka Nigeria, Toofan na Sarkodie kutoka Ghana.

BET imetumia twitter kutoa hii taarifa kama kuthibitisha uchaguzi wa Diamond na kuumpa hongera kama msanii peke Africa Mashariki