ARSENE WENGER AONGEZA MKATABA KUBAKI ARSENAL KWA MIAKA MITATU

Arsene Wenger ametia saini mkataba wa miaka miwili kama meneja wa klabu hiyo hadi mwaka 2017.

Wenger, 64, ameongoza Arsenal na kufanikisha ushindi wa mataji 8 tangu kujiunga na klabu hiyo Septemba mwaka 1996.

Msimu huu aliweza kuongoza timu hiyo hadi kufuzu kwa mara ya 17 kwa kombe la klabu bingwa ulaya na kupata ushindi aliosubiri kwa hamu kwa miaka tisa dhidi ya Hull City katika fainali ya kombe laFA Cup.

Wenger alikuwa anafika ukingoni mwa mkataba wake mwaka huu

Arsenal ilikuwa haijawahi kushinda taji la nyumbani tangu mwaka 2005 ingawa walifika fainali ya kombe la mabingwa wa Ulaya mwaka 2006.


*Rekodi ya Wenger

Ligi ya Premier:1998, 2002, 2004

Kombe la FA:1998, 2002, 2003, 2005, 2014

Kombe la Community Shield:1998, 1999, 2002, 2004

Kombe ya ligi ya klabu bingwa nafasi ya 2:2006

Nafasi ya pili kombe la Uefa Cup:2000

Nafasi ya pili Kombe la League:2007, 2011


Wenger, ambaye sasa ni meneja mkongwe zaidi katikaligi ya Ulaya baada ya Sir Alex Ferguson kustaafu, mwezi Mei mwaka 2013, anasifika kwa kuleta mawazo mapya kuhusu michezo na lishe bora katika soka Uingereza.

''Huyu ndiye mtu anayefanya kazi mwa saa 24 kila siku,'' alisema mlinda lango wa zamani wa Arsenal Bob Wilson.

"Anachukia sana kushindwa. Alileta mageuzi makubwa, katika kila sekta ya mchezo huo nchini Uingereza. Watu wanadhani kuwa ana mamlaka sana lakini mtu ambaye anajitolea sana kwa mchezo huu ni mtu anayethaminiwa sana.''

Ushindi mkubwa wa Wenger ulikuwa wakati ambapo alishinda kombe la ligi ya Premier kati ya mwaka 2003-04 alipokuwa na wachezaji kama vile Thierry Henry na Patrick Vieira.


Wenger alimsajili Mesut Ozil kwa kima cha dola milioni 42.4 kwa msimu ambao umekamilika.

Lakini licha ya hali ya suitofahamu kuhusu mustakabali wa Wenger mwezi Januari, mkurugenzi mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis, alitabiri kuwa Wenger huenda akaongezewa muda Arsenal.

MCHAWI KUTOKA TANZANIA AHUKUMIWA MIAKA 3 KENYA

Mchawi kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu nchini Kenya kwa kumlaghai mwanamke mfanyabiashara mkenya na kumuibia shilingi milioni tisa.


Mchawi huyo alimhadaa mama huyo kuwa kwa kupitia njia za kichawi angeweza kuzifanya pesa hizo kuwa maradufu yaani milioni 18.

Bwana Amos Chipeta pia ataongezwa kifungo cha miezi tatu kwa kupatikana na vifaa vinavyoumiwa kufanya uchawi kama vile chupa, visu na ngozi ya Paka.


Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation, Chipeta alihukumiwa pamoja na mwenzake bwana Peter Christopher aliyepatikana na hirizi zinazotumika kufanyia uchawi.


Bwana Chipeta alimlaghai Bi Catherine Njeri hela zake tarehe tofauti tofauti kati ya mwezi wa Agosti na Decemba 2012 baada ya mwanamke huyo kuwaendea na kumwomba wazifanye pesa hizo ziwe maradufu


Walijitetea kwa kusema kuwa mwanamke huyo aliwatendea ili wampe nguvu za kichawi aweze kuwashinda wapinzani wake wa kisiasa


Maafisa wa polisi walipata hirizi hizo na vifaa walivyotumia kwa uchawi mwezi Februari 1, 2014 katika nyumba ya kukodisha iliyo kando ya barabara ya Juja viungani mwa mji mkuu Nairobi.


Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo alisema kuwa wanaume hao waliona mwanamke huyo kuwa mjinga na basi kumnafiki kwa urahisi na kuwa hawana majuto au toba.

UNAFIKI WA WABUNGE WA CHADEMA LISSU, MSIGWA, LEMA WAJULIKANA WAPOKEA HONGO TOKA KWA MUHONGO

KASHFA KUBWA YA RUSHWA WABUNGE WA CHADEMA MUHONGO AWAHONGA MAMILLIONI ILI KUPITISHA HOTUBA YAKE LISSU, MSIGWA NA LEMA WACHUKUA MAMILIONI HAYO, WAMTOSA SUGU SUGU AGOMA KUSOMA SHUTUMA DHIDI YA ZITTO KWA SABABU YA KUNYIMWA GANJI.

Hali inayoendelea hivi sasa ni hatarikwa ustawi wa Upinzani wa kweli na uhakika hapa nchini kiasi cha wabunge wenzangu CHADEMA kukubali kupokea Rushwa ili waweze kumkashifu na kumchafua mbunge mwenzao Zitto Zuberi Kabwe. Hali hii imejitokeza rasmi kwa kipindi cha wiki nzima sasa hasakuelekea kupitishwa kwa bajeti ya wizara ya nishati na madini. Mkakati mzima upo kama ifuatavyo na kwa sasa ninaufichua kwa siri lakini muda si mrefu nitausema hadharani ili kila mtu ajue hasa nini kinaendelea.

MKAKATI ULIVYO

Juzi Jumaatatu usiku Wabunge wa CHADEMA ikiwa ni pamoja na MIMI,TUNDU LISSU PETER MSIGWA na GODBLESS LEMA tulikutana na katibu mkuu wa wizara ya nishati namadini ndugu ELIAKIM MASWI , na waziri wake PROF. MUHONGO kwa nyakati tofauti tofauti zaidi ya mara moja na kila mmoja kwa wakati wake.

Katika makutano hayo MASWI na MUHONGO wametuomba sisi WABUNGE WA CHADEMA kuhakikisha tunawafunga midomo wabunge wote makini ili waweze kupitisha kwa urahisi bajeti yao.

Katika mikutano huo uliofanyika katika hotel za ST. GASPER, Dodoma Hotel na Royal Village, kwa pamoja tulikubaliana kuhakikisha tunamshambulia ZITTO KABWE hasakwa madai makuu mawili 1. Kwamba yeye ndio kiongozi mkuu wa kujidai anatetea maslahi ya wanyonge na kwamba anawatumia wabunge kina KAFULILA na wengine kwenye sakata la IPTL ambalo linaonyesha kuinyima usingizi WIZARA kutokana na UFISADI wa zaidi ya BILLIONI 200. 2. Kwamba wamepata documents zinazomuhusisha zitto na matumizi mabaya ya madaraka. Ndio maana wanaanza nae na kwamba yeye si msafi kama anavyojifanya.


MAKUBALIANO

Tumeahidiwa kila mmoja kupewa MILLIONI 10 kama suala hili litakamilika ipasavyo, na Tayari tumeshachukua kila mmoja shilingi MILLIONI 5 . nitakapochangia BUNGENI NITAWEKA WAZI KILA KITU


SUGU AWAKATALIA

Mbunge mwenzetu JOSEPH MBILINYI-SUGU mbaye ni Waziri Kivuli wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo ameingizwa Mkenge kwa kujikuta akishindwa kuzisoma PARAGRAPH zilizoingizwa kinyemela na wenzake hao waliokula mlungula na Badala yake kuziruka.

Ilikuwa hivi, mchungaji msigwa alimfuata SUGU na kumuambia akasome kipengele kinachomuonyesha zitto kabwe kutumia vibaya madaraka yake, SUGU akakubali, lakini baadae alipogundua kama wenzake wameramba mlungula akawagomea, kwa kuwa aliyeiandaa hotuba ya SUGU ni LISSU, basi akaiandika kwa siri, lakini SUGU alipokuwa anasoma akagundua kwamba imepenezwa tena, SUGU AKAAMUA KURUKA KIPENHELE HICHO. NDIO MAANA SUGU HAKUONEKANA AKISOMA SEHEMU HIYO. LAKINI KWA KUWA KINA LISSU WALISHAKULA HELA ZA MOTO IKABIDI WACHUKUE SEHEMUYA HANSARD NA KUISAMBAZA MITANDAONI KWAMBA SUGU AMLIPUA ZITTO KABWE, ILI WASIONEKANA WAONGO. KWA KINA MASWI NA MUHONGO.

MBUNGE DAVID SILINDE yeye alikataa kabisa kuwa sehemu ya UNAFIKI HUU WA KISIASA.


KAZI INAYOFUATA,.

Kuanzia tarehe 30.5.2014, wabunge MSIGWA, LEMA na LISSU wataanza kuchangia kwa kumshambulia ZITTO KABWE katika kile wanachokiita kumshuhulikia, lakini hii ni kwamba watakuwa wanatii Makubaliano yao na MUHONGO NA MASWI.

MSIGWA ATAMSHAMBULIA ZITTO KABWE LISSU AYAMSHAMBULIA ZITTO KABWE LEMA ATAMSHAMBULIA Na Tumeagizwa KURUDISHA Hongo Hizo ikiwa hawatawashambulia..


UZOEFU UKOJE

Kila kinapofika kipindi cha WIZARA YA NISHATI NA MADINI kusoma BAJETI YAKE huzushwa shutuma kalidhidi ya WABUNGE MAKINI WENYE KUHOJI MASWALA YA MSINGI KWA TAIFA. 1. MWAKA 2012 LISSU, MSIGWA, LEMA na NASSARY walimshutumu ZITTO KABWE kuhongwa na MKURUGENZI WA TANESCO, lakini ilipoundwa Tume Kuchunguza wakagundulika kuwa walitumika KISIASA kumchafua ZITTO na kwamba habari zile hazikuwa sahihi. 2. MWAKA huu wanafanya mchezo ule ule.

Nitaendelea kutoa ushirikiano kwa WAZALENDO wenzangu kwa kadri itakavyohitajika.

Na ninampongeza KAMANDA SUGU kwa kitendo chakecha kishujaa cha kukataa kumezeshwa maneno asiyoyaamini yaliyotokana na Rushwa iliyotolewa kwetu mimi, MSIGWA, LEMA na LISSU.

Pakua hapa -----> http://ubuntuone.com/3Yvcq8P9kqiHBUtIcCzFB5

ZITTO AJIBU TUHUMA ZA WAPINZANI

Maelezo yangu kuhusu kazi za Kigoma AllStars/LEKADUTIGITE kwa NSSF na TANAPA.

Leo tarehe 29 Mei, 2014 Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni amenituhumu kuhusika na kinachoitwa ufisadi katika Shirika la TANAPA na NSSF.

Nasikitika kwamba katika hali niliyonayo ya kumwuguza mama yangu naingizwa kwenye siasa za majitaka. Kwa sasa nitatoa maelezo kwa ufupi ili kuondoa upotoshaji.

Kampuni ya LekaDutigite inamilikiwa na wasanii 15 ambapo kila mmoja ana hisa 5% ambazo niliwalipia ili waweze kushirikiana katika kazi zao. Hisa 25% zilizobakia zinamilikiwa na kampuni ya Gombe Advisors ambayo ni kampuni isiyofanya faida (Company limited by guarantee) na haina maslahi yeyote ya kibiashara (not for profit company). Hivyo Mimi binafsi sina maslahi yeyote ya kifedha zaidi ya kuwasaidia wasanii hawa katika kazi zao mbalimbali.

Wasanii wa Kigoma AllStars wamefanya kazi na TANAPA na NSSF, kazi ambazo zinajulikana na zipo. Kwa upande wa TANAPA wasanii hawa waliandaa kazi ya kuitangaza Hifadhi ya Saadani na walilipwa. Kwa upande wa NSSF wasanii hao walitunga wimbo na video yake ( http://m.youtube.com/watch?v=sMl8T-RkIdM ) na wimbo huo unatumika katika Shirika hilo.
Vile vile walifanya matamasha mbalimbali ya kuhamasisha watu kujiunga na NSSF. Wasanii wa Kigoma All Stars wote ni wanachama wa Mfuko huo.

Katika kazi zote hizi Mimi binafsi sijafaidika kwa namna yeyote ile kifedha. Kauli yeyote ya kujaribu kuonyesha kazi hizi za wasanii ni ufisadi ni kauli za kusikitisha na kukatisha tamaa kwa mtu ambaye anajaribu kusaidia wasanii kufaidika na kazi zao za sanaa.

Toka mwaka 2012 nilipoanza kujitokeza kusemea wasanii watu kadhaa wenye maslahi na tasnia hii wamekuwa wakinikatisha tamaa na hata wengine kuona nimewaingilia kazi zao.
Hivi sasa wasanii wa Kigoma AllStars ni wanahisa katika kampuni ya PERA Africa limited ili kufaidika na biashara ya miito ya simu. Yote haya nilifanya kwa uchungu nilionao kwa vijana wetu na sio kwa kutaka kufaidika kifedha. Nimeumizwa sana na tuhuma hizi za kuokoteza okoteza.

Inaniumiza zaidi kutokana na ukweli kwamba ninamwuguza mama yangu mzazi, kipindi ninachohitaji kutiwa moyo na kuombewa hata na maadui zangu kisiasa. Kipindi ambacho mama yangu yupo mahututi, tena mjumbe wa kamati kuu ya chama ambacho watoa tuhuma wanatoka, pole ninayopewa ndio hiyo. Hakuna namna ya kukosa ubinaadamu zaidi ya hivi.

Najua wajibu wangu ni kusimamia Mashirika ya Umma na nikiwa mpigania uwajibikaji nipo makini sana kuhakikisha sina mgongano wa maslahi katika mambo yangu. Ndio maana sina biashara yeyote ile ili kuhakikisha natimiza wajibu wangu kwa uadilifu mkubwa. Napata 'moral authority' ya kutaka uwajibikaji kwa sababu nafanya kazi zangu kwa misingi hiyo 'at arms length'.

Hivyo ninataka mara moja CAG afanye ukaguzi wa kazi za wasanii hao kwenye NSSF na TANAPA. Pia achunguze kama Gombe Advisors ( company limited by guarantee) ina maslahi yeyote ya kifedha katika kazi hizo za wasanii.

Nataka pia Shirika la NSSF na TANAPA waweke wazi mchakato wa kazi zao na wasanii hawa kupitia LEKADUTIGITE Limited.

Zitto Kabwe
Mei 29, 2014
Dar Es Salaam.

WASICHANA WAWILI WABAKWA KISHA KUNYONGWA INDIA

Wasichana wawili wa kihindi waliopatikana wakiwa wananing'inia kwenye mti katika jimbo la Uttar Pradesh, walikuwa wamebakwa kisha wakanyongwa.

Polisi wanasema kuwa mwanamume mmoja amekamatwa kuhusiana na mauaji hayo huku polisi watatu wakiachishwa kazi kwa kutosajili kesi hiyo iliporipotiwa kuwa wasichana hao walikuwa wametoweka, kabla ya kupatikana wakiwa wameuawa.

Wasichana hao walipatikana katika wilaya ya Badaun na wanadhaniwa kuwa na umri mdogo kuanzia 13 hadi 15 Ubaguzi dhidi ya wanawake umekita mizizi katika jamii nyingi nchini India.

Visa vya dhuluma za kingono vimeendelea kukithiri nchini India tangu mwaka 2012 ambapo msichana mmoja alibakwa na genge la vijana hadi kufa

Serikali ililazimika kuweka sheria kali kwa wanaopatikana na hatia ya kutenda vitendo vya dhulumaza kingono baada ya maandamano kufanyika kote nchini kufuatia shambulizi hilo.

Polisi mmoja aliambia BBC kuwa wasichana hao walikuwa na uhusiano wa kifamilia na walipatwa wakiwa wananing'inia kwenye mti kijiji cha Badaun mnamo siku ya Jumatano.

Alisema kuwa polisi wanawasaka wanmaume wawili waliowabaka wasichana hao na kisha kuwanyonga.

Wasichana hao walichomwa kuambatana na tamaduni za maziko ya kihindi Jumatano.

Polisi wanasema wanachunguza ambavyo wasichana hao walipotea, kubakwa na kisha kuwekwa kwenye mti

ABDEL-FATTAH AL-SISI RAIS MPYA MISRI

Rais mpya wa Misri Al Sisi
Aliyekuwa mkuu wa jeshi nchini Misri , Abdel-Fattah al-Sisi, ndiye Rais mpya wa Misri baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika wiki hii.
Vyombo vya habari vya kitaifa nchini Misri vinasema matokeo ya mapema yanaonyesha kwamba amejinyakulia zaidi ya asilimia 96 ya kura hizo.
Muslim Brotherhood na makundi mengine yaliususia uchaguzi huo na idadi ya waliojitokeza kupiga kura inakadiriwa kuwa chini ya asilimia 45.
Hii ni licha ya kuongezwa siku ya kupiga kura, kutangazwa siku ya kitaifa ya mapumziko na hata pia kutolewa usafiri wa bure kuwapeleka wananchi kupiga kura.
Sisi alimng'oa mamlakani aliyekuwa Rais Mohammed Morsi ambaye alikuwa Rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Misri.
Sherehe za baada ya kutangzwa ushindi wa Al Sisi

'Vita dhidi ya Brotherhood'
Aliongoza vita dhidi ya vuguvugu la Muslim Brotherhood, lake Mohammed Morsi ambapo wanachama zaidi ya 1,400 waliuawa na wengine 16,000 kuzuiliwa.
Vuguvugu la Brotherhood lilisusia uchaguzi huo,kama walivyofanya wanaharakati wa makundi mengine ya kisiasa.
Hamdeen Sabahi, mgombea mwengine wa pekee katika uchaguzi huo,alisema hapo awali kuwa chama chake kilishuhudia ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa uchaguzi.
Hata hivyo alikatalia mbali wito kutoka kwa wafuasi wake kujiondoa katika uchaguzi akisema kuwa jambao kama hilo lingekiuka matakwa ya wamisri.
Sabahi alipata kura 760,000 kati ya kura milioni 24.7 zilizohesabiwa , na kushindwa katika maeneo mengi ya nchi ambako kura nyingi zilizopigwa zilikuwa na makosa.
Shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea

Mamia ya wafuasi wa Sisi walisherehekea ushindi wake mjini Cairo nyakati za asubuhi na mapema, wakipeperusha bendera za Misri huku wakipiga honi kwa fujo.
Maafisa wa uchaguzi waliongeza muda wa kupiga kura kwa siku nyingine moja na ya tatu kwa matumaini kuwa wangepata idadi kubwa ya wapiga kura.
Licha ya hilo vituo vingi vya kupigia kura viliripotiwa kutokuwa na watu Jumatano.

TUME YA UCHAGUZI KUTANGAZA MATOKEO KESHO

Hatimaye tume ya uchaguzi nchini Malawi imesema itatangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kesho ijumaa.

Uamuzi huo unakuja baada ya mivutano na mapingamizi kadhaa kwenye mahakama kuu nchini humo.

Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza ameeleza kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Lilongwe kuwa sasa wananchi wa Malawi wameondolewa hofu ya kusubiri kwa muda mrefu matokeo ya kura za uchaguzi walioufanya juma lililopita.

Taarifa fupi iliyotolewa na tume ya uchaguzi jana usiku mjini Blantyre, imesema wameamua kutangaza matokeo hayo kwa kuzingatia sheria inayoibana kufanya hivyo ndani ya siku zisizozidi nane na ikiwa ni baada ya saa 48 tangu kumaliza hesabu ya kura.

Kwa siku mbili sasa kumekuwa na tuhuma za kuokotwa kwa baadhi ya masanduku ya kura, huku baadhi ya magari ya yakipatikana na masanduku ya kura na hata katika baadhiya maeneo ambako ilielezwa kuwa kura zimehifadhiwa, usalama wake umesemwa kuwa mdogo.

Tume ya uchaguzi ya Malawi imesema itatangaza matokeo ya uchaguzi ijumaa.

Tangu jumatatu tume hiyo imekuwa ikisubiri uamuzi wa mahakama kuu mjini Blantyre wa kuiongeza muda wa angalau siku 30 kukamilisha jukumu ililopewa, hata hivyo mahakama yenyewe bado ina mashauri mengine iliyopokea kuhusu uchaguzi huu

Mmoja kati ya wananchi wa nchi hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Malani Nyirenda, alielezea hisia zake alipozungumza na BBC mjini Lilongwe kutokana na suala la kuchelewa kutolewa matokeo na mpango wa kuhesabu upya kura za baadhi ya maeneo.

Tume hiyo imesema hadi kufikia sasa imepokea malalamiko 275 na imekwisha yafanyia kazi malalamiko 170 tu.

MOTO WAZUKA HOSPITALI NA KUUWA WATU 21

Moto Uliozuka Hospitalini wauwa watu 21 Nchini Korea Kusini. Wagonjwa wapatao 20pamoja muuguzi wameuawawa baada ya moto mkubwa kuwaka hospitalini katika jimbo la Janseong nchini Korea Kusini, huku wengine 6 wakiwa hali mahututi baada ya moto huo katika hospitali ya Hyosarang iliyoko kilomita 300 kusini mwa Seoul.

Wengi wa walioaga dunia wanafikiriwa kuwa wazee wenye umri wa kati ya miaka 70 na 80 na wasioweza kutembea. Maafisa walisema kuwa wengi waliokufa walikosa hewa kutokana na gesi zenye sumu.

Moto huo ulizimwa kwa takribani nusu saa. Moto huo ulianza muda mfupi tu baada ya saa sita usiku katika hilo jumba lenye orofa tatu.

Vyombo vya habari vinaarifu kuwa wengi wa wagonjwa waliokuwa katika orofa ya juuya jumba hilo walishindwa kujiokoa kwa sababu vyuba vyao vilikuwa vimejaa moshi uliotokana na moto huo.Muuguzi huyo aliyekufa alikuwa akijaribu kuzima moto kwa kutumia kizima moto kulingana na shirika la Agence-France Presse. Ripoti ya shirika la Yonhap ilisema kuwa polisi walisema kuwa jumba hilo lilikuwa limefanyiwa uchunguzi wa kiusalama majuzi.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo Lee Hyung Seok aliomba msamaha na kuwaambia wanahabari kuwa alikuwa ametenda dhambi kubwa, na kuwa hangetoa visababu wakati watu wameaga dunia.

Tukio hili limekuja wakati wananchi wa Korea kusini wakiendelea kuomboleza vifovya zaidi ya watu 300 waliofariki katika ajali ya feri iliyotokea mwezi uliopita.

Rais wa taifa hilo Park Geung-Hye ameliomba taifa radhi kirasmi kwa ajali hiyo ya feri, huku akiahidi kuimarisha viwango vya usalama.

Waziri mkuu Chung Hong-won wakati huo alijiuzulu kwa madai ya jinsi serikali ilivyokuwa ikikabiliana na majanga.

Ajali hiyo ya hospitali pia imetokea siku moja tu baada ya watu 7 kuuwawa na wengine 20 kujeruhiwa katika mkasa wa moto uliozuka katika kituo cha mabasi jijini Goyang.

BIBI ALIYEKAMATWA NA UNGA APANDISHWA KIZIMBANI

Hatimaye 'Bibi wa unga' raia wa Nigeria, Olabis IbidunCole (65), amepandishwa kizimbanina kusomewa shtaka linalomkabili kwa lugha ya Kiingereza.

Juzi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliahirisha kesi hiyo hadi jana kwa kile kilichoelezwa kuwa mtuhumiwa hafahamu lugha ya Kiingereza baada ya kusema anafahamu lugha ya Kiyoruba tu.

Hata hivyo, ilielezwa kuwa baada yauchunguzi, ilibainika kuwa alipokamatwa Uwanja wa Ndege waJulius Nyerere, alihojiwa kwa Kiingereza hivyo Mahakama ikamlazimisha kuendelea na lugha hiyo.

"Uchunguzi ulifanywa na mahakam aumebaini kuwa mshtakiwa unafahamu vizuri lugha ya Kiingereza hivyo, kutokana na hili tunakusomea hati yako ya mashtaka kwa lugha ya Kiingereza,"Hakimu wa Mahakama hiyo, Frank Moshi alisema.

Bibi huyo ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Lagos,Nigeria, alikubali kusomewa hati hiyo kwa lugha ya Kiingereza.

Akisoma hati ya mashtaka, Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Jackson Chidunda alidai kuwa Cole alikutwa na gramu 831 za dawa za kulevya aina ya heroini zenye thamani ya Sh37 milioni Mei 19, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa tisa jioni.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Hakimu Moshi alimwambia mshtakiwa kuwa hatakiwi kujibu chochote mahakamani hapo kutokana shtaka linalomkabili kutokuwa na dhamana na aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 10, mwaka huu itakapotajwa tena.

Mshtakiwa ambaye anayeshikilia rekodi ya kuwa mtuhumiwa wa dawa za kulevya mwanamke mwenye umri mkubwa kukamatwa kwenye uwanja huo alinaswa alipokuwa akijiandaa kwenda Paris, Ufaransa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.


Chanzo: Mwananchi

MBUNGE WA NKASI ANUSURIKA KIPIGO

Kelele, kukunjana na kunyoosheana vidole jana mchana vilitawala nje ya ukumbi wa Bunge wakati wabunge wa CUF kutoka Zanzibar walipotaka 'kumkanya' Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy.

Sakata hilo la aina yake lililodumu kwa takriban dakika 15 lilitokea saa 7:05 mchana baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuahirisha kikao cha Bunge.

Wabunge hao Mussa Haji Kombo (Chakechake), Kombo Khamis Kombo (Magogoni) na Muhammad Ibrahim Sanya (Mji Mkongwe), walitaka 'kumkanya' Keissy kutokana na kile alichosema alipokuwa akichangia Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mwaka 2014/15 na kusema Zanzibar haichangii katika Muungano, hivyo haina haki ya kuhoji mambo ya upande wa pili.

Kauli hiyo licha ya kulalamikiwa na wabunge wote wa CUF kutoka Zanzibar kiasi cha kufikia hatua ya kusimama na kuomba mwongozo wa Spika, Keissy alizidi kuwashambulia na kusema kuwa majimbo ya Zanzibar watu wake wanaweza kukusanywa sehemu moja kwa kupigiwa filimbi tu.

"Nyie Zanzibar idadi yenu ya watu ni asilimia 2.8 ya watu wote wa Tanzania. Sasa mnataka kupata kila kitu sawa ili iweje! Mnataka ajira asilimia 21 na Watanganyika wakafanye kazi wapi?" alisema Keissy.

Baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho na wabunge kuanza kutoka nje, wabunge hao wa CUF walikwenda kumsubiri Keissy karibu na jengo la kantini.

Mbunge wa kwanza kumvaa Keissy alikuwa Khamis Kombo ambaye kabla ya kumfikia alizuiwa na Mbunge wa Mpanda Kaskazini (CCM), Moshi Selemani Kakoso.

Wakati Keissy akishangaa alitokea Haji Kombo ambaye naye alizuiwa na Mbunge wa Mikumi (CCM), Abdulsalaam Selemani Amer.

"Mimi sitaki kupigana bwana ninachokijua ni kwamba nilikuwa nikichangia mjadala wa bajeti na nilichokisema ni ukweli mtupu," alisema Keissy huku akiwa amenyanyua mikono yake juu na kuondoka eneo hilo."Wewe (Keissy) sijui una nini wewe.

Unapenda kutufuata fuata sana watu wa Zanzibar. Hivi una nini wewe? Hivi hujui kuwa Tanzania ni Muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar?" alisikika akisema Khamis Kombo.

Kwa upande wake, Sanya hata baada ya wenzake kutawanyika eneo hilo, aliendelea kumlaumu Keissy na kuwataka wabunge wa CCM kumuonya.

"Anapenda sana kutoa kauli mbaya dhidi ya Zanzibar. Jamani mkanyenimwenzenu haiwezekani kila siku awe yeye tu anayetukashifu bungeni," alisema Sanya huku akitulizwa na mbunge wa Kibiti (CCM), Abdul Jabiri Marombwa.

WALIO MUUA DEREVA BODABODA SAMWELI KUFIKISHWA MAHAKAMANI(Tunaomba Radhi kwa muonekano wa picha)

(Picha ni majambazi waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo).

Jeshi la Polisi Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kumuuwa Bodaboda mmoja aitwaye Frenk Joseph (25)mkazi wa mtaa wa Nsemlwa Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi kwa kumchinjashigo na kisha kumpola pikipiki yake aina ya SANLG yenye namba za usajiri T 704 CDQ Kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi
Kamishina msaidizi mwandamizi Dhahiri Kidavashari aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Charles Kidaha(29),Madia Mtema (40) na Buyenza Jendesha (40) wote wakazi waTarafa ya Mwese Wilayani Mpanda.

Kidavashari alisema watuhumiwa hao walimuuwa bodaboda huyo hapo Aprili 26 mwaka huu majira ya saa saa kumi na moja jioni huko katika eneo la Kijiji cha Mpembe Tarafa ya Mwese Wilayani Mpanda.

Siku hiyo ya tukio marehemu Samwel alikuwa kwenye kijiwe chake cha Bodaboda kilichoko kwenye hospitali ya Wilaya ya Mpanda akiwa na pikipiki yake aina ya Sunlg yenye Namba za usajiri T704CDQ aAlisema wakati akiwa kwenye kituo hicho cha Bodaboda alitokea mtu asiye fahamika na kumkodisha marehemu ambapo waliondoka nae huku marehemu akiwa aja waaga bodaboda na kuwafahamisha mahari alikokuwa wakielekea na mteja wake huyo.

Alifafanua kuwa ndipo siku iliyofuata ya tarehe 27 Aprili mwili wa marehemu bodaboda huyo ulipoonekana ukiwa umetelekezwa porini katika kijiji cha Mpembe huku akiwa amechinjwa na kitu chenye ncha kali na pikipiki yake haikuonekana katika eneo hilo.

Kamanda Kidavashari alieleza kuwa baada ya tukiola mauwaji hayo polisi waliendelea kufutilia tukio hilokwa kushirikiana na raia wema na ndipo hapo mei 22 majira ya saa kumi na moja jioni huko katika kijiji cha Kasekese Kata ya Simbwesa Wilaya ya Mpanda raia wemawalitowa taarifa kwa jeshi la polisi kuwa wanamashaka na watuhumiwa hao kwani waliwasili kijijni hapo wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki moja.

Alisema baada ya taarifa hizo jeshi la polisi liliweza kufanikiwa kufika kijijini hapo mara tuu baada ya muda mfupi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wote watatu wakiwa na pikipiki hiyo ya marehemu Samweli waliompola baada ya kumuuwa.

Katika maojiano ya awali bainiya jeshi la polisi na watuhumiwa hao watatu imeonyesha kuwa watuhumiwa hao ndio waliohusika na mauwaji ya bodaboda huyo.

Kamanda Kidavashari ameleza watuhumiwa hao wote watatu wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamiliki.
Picha jinsi alivyochinjwa)





AHUKUMIWA JELA MIAKA 30 KWA UBAKAJI

Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu Philipo Emanuel (35) Mkazi wa Mtaa wa Mpanda Hotel mjini Mpanda kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na kosa la kumbaka shemeji yake msichana (13) mdogo wa mke wake mdogo.

Hukumu hiyo imetolewa hapo juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya mahakama kulidhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na pambe zote mbili za upande wa mashitaka na utetezi

Mshitakiwa alidaiwa kutenda kosa hilo la kumbaka mdgo wa mke wake hapo Septemba 24 mwaka jana majira ya saa moja na nusu usiku huko katika eneo la mtaa wa Nsemulwa mjini Mpanda.

Awali katika kesi hiyo mwendesha mashitaka Godfrey Ruzabila aliiambia mahakama kuwa siku hiyo ya tukio msichana huyo aliyebakwa alikuwa ametumwa dukani na dada yake kwenda kununua mafuta ya kupikia mlo wa jioni.

Alieleza wakati msichana huyo akiwa anaelekea dukani ndipo alikutana na mshitakiwa ambae alimwita msichana huyo na kisha alimwomba amsindikize dukani alikokuwa anakwenda kununua mafuta ya kula aliyokuwa ametumwa na dada yake.

Mwendesha mashitaka alidai baada ya kuwa wamefika dukani msichana huyo alinunua mafuta na kisha mshitakiwa alimweleza shemeji yake kuwa anataka kumnunulia zawadi dukani hapo hivyo achague kitu gani anachokihitaji ndipo msichana huyo alipomweleza shemeji yake kuwa yeye anahitaji Biscut na Pipi bomu

Mshitakiwa baada ya kumnunulia shemeji yake zawadi hizo alimtaka amsindikize alikokuwa akienda ombi ambalo msichana huyo alilikubali kwani hakuwa na mashaka yoyote ya kusindikizwa na shemeji yake.

Mwendesha mashitaka alieleza wakati wakiwa njiani mshitakiwa Philipo Emanuel alimwingiza msichana huyo kwenye pagara na kisha alipiga ngwala na kuanza kumbaka huku msichana akijaribu kupiga mayowe ya kuomba msaada lakini alishindwa kutokana na mshitakiwa muda wote kuwa amembana mdomo.

Alieleza baada ya kuwa amemaliza kumfanyia unyama huo alipatia mtoto huyo shilingi elfu moja kama malipo yake na shilingi elfu tano alimpatia ili amfikishie dada yake na alimkaza asimwambie mtu yoyote yule kuwa amefanyiwa kitendo hicho na mshitakiwa.

Ruzabila alisema baada ya msichana kufika nyumbani kwao dada yake alimuuliza kwanini amechelewa kurudi ndipo binti huyo alimweleza dada yake njisi ambavyo shemeji yake alivyomfanyia hari ambayo ilmshitua dada yake na kumfanya achukue uamuzi wa kumvua nguo na kumkagua katika sehemu zake za siri na kukuta anatokwa na damu hari ambayo ilimfanya ashituke na kupelekea kuamua kutoa taarifa kwa wapangaji wenzake.

Alieleza dada wa binti na majirani walimtaka msichana huyo awapeleke kwenye eneo alilofanyiwa unyama huo na walipofika kwenye eneo la tukio waliingia ndani ya pagala na kukuta Paketi ya Biscuti aliyokuwa amenunuliwa na shemeji yake huku pembeni kukiwa na mafuta ya kula yaliyomwagika na ndipo walipo amua kwenda kituo cha polisi cha mpanda na kutoa taarifa.

Katika kesi hiyo upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi wanne akiwemo Daktari ambae alithibitisha kuwa msichana huyo alifanyiwa kitendo cha ubakwaji baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kidakitari na kukutwa na mbegu za kiume na upande wa utetezi ulikuwa na mashahidi wanne.

Hakimu mkazi Chiganga Ntengwa baada ya kusikiliza mwenendo mzima wa kesi aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa Philipo Emanuel amepatikana na hatia ya kosa la kifungu namba 130 (1)(2) hivyo mahakama inampa nafasi mshitakiwa kabla ya kutolea kwa adhabu kama anayo sababu ya msingi ya kuishawishi mahakama impunguzie adhabu.

Katika utetezi wake mshitaki aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwaanafamilia ya wake wawili ambao wanamtegemea pamoja na watoto ombi ambalo lilipingwa na mwendesha mashitaka.

Baada ya utetezi huo hakimu Chiganga alisoma hukumu kwa kueleza kuwa kutokana na mshitakiwa Emanuel Philipo kupatikana na kosa hilo mahakama imemuhukumu kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kuanzia mei 26 mwaka huu.

Chanzo: Katavi yetu

WATU SABA WAKAMATWA MAUAJI YA POLISI WAWILI

WATU saba wamekamatwa na Polisi mkoani Tabora wakituhumiwa kuhusika katika mauaji ya askari Polisi wawili na unyang'anyi wa kutumia silaha, yaliyofanyika mwezi uliopita.

Matukio hayo ya unyang'anyi na mauaji yalifanyika Aprili 28, mwaka huu katika Tarafa ya Usoke Wilaya ya Urambo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Suzan Kaganda alisema askari waliouawa, walikuwa katika harakati za kutekeleza majukumu yao katika eneo hilo la Usoke.

Askari hao ni F.5179 Konstebo Jumanne na G.3388 Konstebo Shaaban.

Kuhusu waliokamatwa, waki tuhumiwa kwa mauaji ya askari hao, kamanda aliwataja ni Silvester Mussa maarufu kama Kingwendu (31), mkazi wa Mkuyuni Tambukareli, Mwanza.

Watuhumiwa wengine ni Sadiki Rushikamwa ambaye anajulikana pia kama Sadiki Milambo au White (28), mkazi wa Mihogoni Tabora na Abel Benedicto maarufu kama Mwendo wa saa (23), ambaye ni mkazi wa Muungano Wilaya ya Urambo.

Wengine waliokamatwa ni Francis Kashinje maarufu Masanja (38) mkazi wa Nansio, Ukerewe, Haji Athanas (50) mkazi wa Usoke, Mussa Khatibu Ally (49) ambaye ni mfanyabiashara wa nafaka na mkazi wa Mwanza Road.

Mtuhumiwa mwingine ni Ramadhan Mkunya, mkazi wa Tabora.

Kwa mujibu wa Kamanda, baada ya mahojiano na polisi, watuhumiwa walikiri kushiriki matukio mbalimbali ya unyang'anyiwa kutumia silaha pamoja na mauaji ya askari Polisi wawili.

Alisema baada ya upekuzi, walikutwa na silaha aina ya Pistol Glock 17, yenye namba za usajili TZ Car 91968, ikiwa na magazini yenye risasi tano.

M23 NI RAIA WA RWANDA

Tanzania kwa mara ya Kwanza imesema inayo uhakika kuwa waasi wa M23 walioondolewa nchini Jamuhuri ya Kongo ni ni raia Rwanda.

Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Benard Membe ameliambia Bunge la Tanzania kuwa anao uhakika kuwa waasi M23 walitokea nchini Rwanda.

Hii ni Mara kwanza kwa Tanzania kukiri hadharani kuwa inao uhakika kuwa waasi hao ni raia wa Rwanda.

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimepeleka majeshi Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo kwa kushirikiana na yale ya umoja wa Mataifa yaliwaondoa waasi hao DRC Benard Membe Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania

Matamshi hayo ya Waziri huyo aliyatoa wakati alipokuwa akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara yake ambapo pia alikiri kuwa bado uhusiano wa Tanzania na Rwanda sio mzuri.

Hata hivyo upande wa Upinzani mlishambulia Waziri huyo wa Mambo ya nje Benard Membe wakidai kwamba Waziri huyo anachochea kuvurugika kwa uhusiano wa Watanzania na Rwanda kwa kuhisi kuwa M23ni Wanyarwanda nahata kutaka achukuliwe adhabu kali.

Mbali na tuhuma hizo Waziri Membe alizidi kusisitiza kuwawaasi wa M23 ni raia wa Rwanda akisema hiyo ni ripoti ya Umoja wa Mataifa.

Mbali na waziri baadhi ya wabunge wanamuunga mkono waziri Membe kuwa waasi wa M23 ni raia wa Rwanda wao.

Matamshi haya Waziri wa Tanzania kuhusu M23 bado haijulikana ni kwa namna gani utaathiri uhusiano wa Tanzania na Rwanda kama utakuwepo huenda ukajulikana hapo baadae.

MKUU WA MAJESHI ANUSURIKA KIFO SOMALIA

Mkuu wa jeshi la Somalia ameponea chupuchupu kuuawa mjini Mogadishu.

Hili ndilo shambulio la punde zaidi katika msururu wa mashambulio dhidi ya viongozi wa serikali na rasilimali za serikali nchini humo.

Gari lake Jenerali Dahir Aden Elmim lilirushiwa bomu katikabarabara kuu karibu na afisi za wizara ya ulinzi mjini Mogadishu.

Aliponea kwa sababu yeye huendesha mojawepo ya magari machache yaliyo na uwezo wa kudhibiti shambulio la risasi, ambayo yametengewa viongozi wakuu wa serikali hiyo.

Hakuna yeyote aliyedai kuhusika na shambulio hilo kufikia sasa japo inafahamika kuwa kundi la Al shabaab limekuwa likifanya mashambulio ya mara kwa mara mjini Mogadishu.

Mwishoni mwa juma, watu 15waliuawa katika shambulio lililolenga jengo la bunge la Somalia.

Wengine wengi walijeruhiwa wakiwemo wabunge 3.

BABA AMUUA MWANAE WA KIKE KWA MAWE

Mwanamke mmoja nchini Pakistan amepigwa mawe na familia yake wakiwemo babake na ndugu zake wa kiume hadi kufariki. Aliuawa nje ya jengo la mahakama mjini Lahore.

Mwanamke huyo aliuawa kwa kuolewa na mtu ambaye alikuwa chaguo lake mwenyewe.

Farzana Bibi, mwenye umri wa miaka 31, aliolewa na Muhammad Iqbal miezi michache iliyopita bila ya idhini ya familia yake.

Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo alishambuliwa na familia yake.

Kaka zake na binamu yake mmoja walimshika alipokuwaakiingia mahakamani na kuanza kumpiga kwa mawe. Alifariki papo hapo.

Waliomuua walikimbia kabla ya polisi kufika katika eneo hilo.

Babake msichana huyo amekamatwa ingawa washukiwa wengine wangali hawajulikani waliko.

Kwa wanawake wanaoolewa na wapenzi ambao ni chaguo lao wenyewe, ni kitendo kisichokubalika kitamaduni katika baadhi ya maeneo ya Pakistan.

Mamia ya wasichana huuawakwa kisingizio cha kuolewa nawatu wasiokubalika na familia zao kila mwaka

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wanaaminikuwa kwa kuwa mauaji hayo hufanywa na familia zenyewe, huwa ni vigumu kufikisha kesi hizo kortini.

MAMA NA MWANAE WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI

Mwanamke ajulikanaye kwa jina la Milembe Masanja na mtoto wake aitwaye Kulwa Madirisha wakazi wa kijiji cha Nyabusalu wilayani Kahama, wameuwawa kwa kupigwa risasi saa 2 usiku, wakati wakiandaa chakula.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangalla amesea Milembea aliuwawa kwa kupigwa risasi kwenye kwapa la kushoto huku mwanaye Kulwa akipigwa risasikidevuni na tumboni, hali iliyosababisha vifo vyao papo hapo.

Hadi sasa chanzo cha tukio kinachunguzwa na hakuna mtu anayeshikiliwa.

Kamanda Mangalla pia amesema bunduki ni aina ya gobore kutokana na majeraha waliyokutwa nayo marehemu.

MISRI WAANZA KUPIGA KURA KUMCHAGUA RAIS

Raia wa Misri watapiga kura kwa muda wa siku mbili kumchagua rais mpya chini ya ulinzi mkali kuhakikisha mchakato wa upigaji kura unafanyika kwa usalama. Karibu maafisa wa usalama laki mbili wameshika doria kote nchini Misri serikali ikionya dhidi ya hatari za usalama zinazoweza kusababishwa na itikadi kali za kiislam.

Adbel Fatah al-Sisi Kiongozi wa kijeshi wa zamani aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya rais wa awali Mohammed Morsi anatarajiwa kupata ushindi kwa u rahisi.

Oparesheni kubwa ya usalama inayoendelea nchini Misri ni ushahidi kamili kuwa utawala wa sasa unaoungwa mkono na jeshi unatambua kuwa ugaidi unaoungwa mkono na Waislamu wenye itikadi kali upo na unaweza kuteguliwa wakati wo wote.

Mbinu ya kukabiliana na ugaidi huo ya Abdel Fatah al-Sisi haijabadilika ila tu ni magwanda yake ya kijeshi ya field Mashel yaliyojaa medali yaliyobadilishwa na nguo za kiraia.

Ametangaza katika kampeni yake kuwa anaunga mkono kuangamizwa kabisa kwa kundi la Muslim Brotherhood ambalo limeshuhudia maelfu ya wanachama wake wakizuiliwa na mamia wakihukumiwa vifo.

Bwana Sisi ametoa wito kwa watu wanaotakia Misri amanina utangamano baada ya miaka kadhaa ya mapinduzi na ghasia na ameheshimiwa kiwango cha kusujudiwa na wengine hivi kwamba unaweza kununua peremende au chokoleti dukani iliyopachikwa picha yake.

Mpinzani wake mwenye mrengo wa kushoto, Hamdeen Sabbahi, anatajwa katika vyombo vya habari ambavyo vinaoenekana kuamua tayari kuwa yeye atashindwa katika Uchaguzi unaoanza leo.

Ingawa wapiga kura wana mazoea ya kubadilika dakika za mwisho kabla ya uchaguzi lakini wengi nchini Misri watashangaa iwapo Bwana Sisi hashindi uchaguzi huu, natena kwa urahisi.

STARS KUMENYANA NA MALAWI TENA

TIMU ya soka ya taifa, Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi ya kimataifa ya kirafiki na Malawi (Flames) keshokutwa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwenye vyombo vya habari jana, mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuanzia saa 11 jioni.

Stars ilishacheza mechi ya kirafiki na Malawi kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya mwezi uliopita na kutoka suluhu.

Mechi hiyo itakuwa ya mwisho kwa Stars kujipima kabla ya kucheza mechi ya marudiano ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya Zimbawe mjini Harare Juni mosi mwaka huu.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Stars ilishinda bao 1-0, matokeo ambayo yana ilazimisha kufanya jitihada ama kulinda bao hilo ama kuongeza ili kusonga mbele.

Mshindi wa mechi hiyo atacheza na mshindi wa mechi kati ya Msumbiji na Sudan Kusini ambapo katika mechi ya kwanza Msumbiji ilishinda mabao 5-0.

Stars ipo kambini Tukuyu mkoani Mbeya chini ya Kocha wake Mart Nooij kujiandaa kwa mechi hizo.

Malawi iliwasili jana mchana na msafara wa watu 27 Flames inayofundishwa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Malawi, Young Chidmozi inatarajia kufanya mazoezi leo jioni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

Baada ya mechi hiyo, Malawi itakwenda moja kwa moja nchini Chad kwa ajili ya mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika itakayochezwa Mei 30 mwaka huu jijini Ndjamena.

WATU SITA WAKAMATWA WADAIWA KUWA VIONGOZI WA MBWA MWITU

JESHI la Polisi limewakamata watu 6, wanaosadikiwa kuwa ni vinara wa vikundi hatari vya `Mbwa Mwitu', `Watoto wa Mbwa' au `Panya Road'. Vikundi hivyo vinajihusisha na matukio ya kihalifu jijini Dar es Salaam.

Vijana wanaounda makundi hayo, wengi wakiwa wenye umri wa kati ya miaka 16 na 20, hutembea kwa makundi na kufanya uhalifu kwa kutumia silaha, kama mapanga, visu, nondo na marungu.

Hayo yalisemwa na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleman Kova wakati akizungumza na waandishi wa habari jana.

Alitaja waliokamatwa wakihusishwa na vikundi hivyo kuwa ni Athuman Said (20), mkazi wa Kigogo, Joseph Ponela ambaye ni dereva bodaboda, Clement Peter (25) fundiseremala, Roman Vitus (18) mfanyabiashara, Mwinshehe Adam (37) mkazi wa Temeke na Daniel Peter (25) mkazi wa Yombo.

Alisema Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limefanya msako katika maeneo mbalimbali ya Jiji ili kudhibiti makundi ya uhalifu na vijana wahuni wasio na kazi. Aliongeza kuwa maeneo ambayo yameonekana kuwa na vijana hao niKigogo, Magomeni, Tabata, Manzesena Mbagala.

"Askari wa kutosha wa doria wamepangwa kufanya doria ili kuthibiti milipuko yoyote ya vitendo vya kihuni vinavyoleta hofu kwa wananchi," alisema Kova.

Aidha, alisema kumekuwa na mtindo wa watu ambao hawafahamiki jijini hutuma ujumbe mfupi wa simu za mkononi, wakieneza uvumi kwamba maeneo yao yamevamiwa na makundi ya Mbwa Mwitu au Panya Road.

Alisema uvumi huo, ulianza Mei 18 na 20 mwaka huu baada ya vibaka wawili wa kundi hilo, kuuawa na hofu ilikuja baada ya mazishi ya vijana hao, kwani wangeweza kulipiza kisasi.

"Jeshi la Polisi linatoa onyo kali mtindo huu ukome, kwani watu haowanasababisha hofu kwa wananchi,"aliongeza Kova. Alisema Jeshi la Polisi limejiimarisha kiulinzi na vijana hao, hawana uwezo wa kufanya watakavyo, kama uvumi unavyoenezwa kimakosa.

Jeshi la Polisi limeamua kufanya msako huo baada ya kundi la Panya Road, kuibuka wiki hii na kusababisha hofu kwa wananchi wengi, ikiwa ni pamoja na kufanya uporaji na kujeruhi kwa kutumia silaha za jadi, kama marungu, mapanga, visu na nondo katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

JOYCE BANDA HOI UCHAGUZI MALAWI KWA MATOKEO YA AWALI

Hatimaye Tume ya uchaguzi nchini Malawi imeanza kutoa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo jumanne iliyopita.

Matokeo hayo ambayo ni asilimia 30 tu ya kura ambazo zimehesabiwa hadi sasa yanaonyesha kuwa mgombeawa chama kikuu cha upinzani Democratic Progressive Party-DPP Profesa Peter Mutharika anaongoza kwa kura 683,621 akifuatiwa na Dr Joyce Banda wa Peoples Party kwa kura 372,101

Mgombea Urais wa chama kikongwe cha kisiasa nchini humo, Malawi Congress Party MCP Mchungaji Dr Lazarus Chakwera anashika nafasi ya tatu kwa kujipatia kura 289,145 huku Atupele Muluzi wa United Democratic Front- UDF akikusanya kura za wamalawi 269,250

Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza ambaye anafuatilia uchaguzi huo nchini humo, amesema mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mackson Mbendera aliwaambia waandishi wa habari mjini Blantyre usiku wa kuamkia leo kuwa tume yake kwa pamoja na wawakilishi wa vyama vya siasa wamethibitisha matokeo hayo.

*Udanganyifu

Katika mkutano huo Jaji Mbendera amesema tume yake imegundua kuwa kulikuwa na udanganyifu katika baadhi ya maeneo ambapo wamekuta idadi ya kura zilizopigwa ni zaidi ya watu walioandikishwa kupiga kura, na kwamba wamezuia matokeo hayo hadi watakapopata ufumbuzi na ukweli wa hali ilivyokuwa.

Wakati huo huo Mahakama nchini humo imezuia uamuzi wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la utangazaji la Malawi MBC kumlazimisha Mkurugenzi Mkuu Dr Benson Tembo kwenda likizo ya lazima na haraka.

Uamuzi huo umefuatia baadhi ya wanasheria kutoka kamisheni ya wanasheria wa Lilongwe kuweka zuwio mahakamani kupinga uamuziwa bodi ya shirika hilo.

Itakumbukwa kuwa ijumaa asubuhi Dr Tembo alipewa barua ya kumtaka aende likizo ya lazima kutokana na madai kuwa ameshindwa kufuata maelekezo ya mwajiri wake ambaye ni serikali.

Miongoni mwa madai hayo nipamoja na vyombo vya shirika hilo ikiwemo televisionna radio za taifa kuendelea kutoa matokeo ya uchaguzi ambayo hayajathibitishwa na Tume ya uchaguzi.

Pia MBC ilishindwa kurusha moja kwa moja matangazo yamkutano wa Rais Joyce Bandana waandishi wa habari mjini Lilongwe siku ya alhamis, ambapo Dr Banda alikuwa akitoa maelekezo kwa tume ya uchaguzi kuanza kuhesabukura kwa kutumia mikono na kuzuia kutoa matokeo kutokana na udanganyifu uliojitokeza.

MBWA MWITU, WATOTO WA MBWA NA PANYA ROAD KUTOKOMEZWA

JESHI la Polisi nchini limewaagiza Makamanda wa Polisi wa Mikoa, kuhakikisha wanavidhibiti na kuvitokomeza vikundi vyote vinavyojihusisha na vitendo vya uhalifu, ikiwemo uporaji, unyang'anyi na kujeruhi watu katika maeneo mbalimbali.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Nchini(DIGP), Abdulrahman Kaniki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, hatua hiyo imetokana na kushamiri kwa matukio ya uhalifu na yanayojenga hofu miongoni mwa jamii, ikiwa ni pamoja na vikundi vinavyozidi kuibuka na kutishia amani katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Vikundi hivyo ni pamoja na vile vilivyojipachika majina ya mbwa mwitu, watoto wa mbwa au panya road, ambavyo vimekuwa vikifanya uporaji, unyang'anyi wa kutumia nguvu na kuwajeruhi watu katika maeneo mbalimbali.

Makamanda hao wametakiwa kuhakikisha wanavitafuta vikundi hivyo popote vilipo na kuwakamata kisha kuwafisha katika vyombo vya sheria.

"Naibu IGP amekemea vikali vikundi hivyo na kuvitaka kuacha tabia hiyo mara moja, kwani vitendo hivyo ni vya kihalifu na vinatakiwa kukemewa na kila mtu katika jamii," ilieleza taarifa hiyo ya Senso.

Aidha, iliwataka wananchi kuondoa hofu na badala yake watoe ushirikiano kwa kutoa taarifa za vikundi hivyo katika vituo vya Polisi ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.

MUSWADA WA VYOMBO YA HABARI KUFIKISHWA BUNGENI

MUSWADA wa Sheria ya Kusimamia Vyombo vya Habari umekamilika baada ya kupitia hatua zote muhimu na unatarajia kufikishwa bungeni wakati wowote mwaka huu.

Aidha, Muswada wa Haki ya Kupata Habari, utafiti wake umekamilika na unaandaliwa na wizara ya katibana sheria na baada ya maamuzi utafikishwa bungeni kujadiliwa na kuwa sheria.

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia aliliambia bunge jana wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya (CCM) aliyetaka kujua ni lini serikali itapeleka miswada hiyo miwili na kujadiliwa kisha kuwa sheria.

Alisema ni kweli mwaka 2007, serikali iliitikia mwito wa wadau mbalimbali wa habari, waliotaka kuwepo na tofauti za sheria ya huduma ya vyombo vya habari na uhuru wa kupata habari.

"Serikali imepokea mapendekezo kutoka kwa wadau, nafurahi kulijulisha bunge lako tukufu kuwa muswada wa sheria ya kusimamia vyombo vya habari, umekamilika baada ya kupitia hatua zote muhimu za kuandaa muswada na taratibu za kuletwa bungeni zinaandaliwa," alisema.

Katika swali la nyongeza, mbunge wa Nchinga, Saidi Mtanda(CCM) alitaka kujua ni lini muswada utaletwa bungeni baada ya kuombwa kwa miaka 17 na kusababisha mazingira ya uhuru wakupata habari kuwa na changamoto.

Akimjibu, Nkamia alisema muswada huo utapelekwa wakati wowote kuanzia sasa, kwa kuzingatia kalenda za bunge la bajeti na wakati wa muswada.

Mtanda aliungwa mkono na mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR -Mageuzi) na Mbunge wa Viti Maalumu, Zainabu Vullu (CCM) waliotaka kujua muda maalumu wa muswada huo kufikishwa bungeni na kuhoji vyombo vya habari vinapokosea wanashtakiwa kwa sheria gani na hakuna sheria.

Nkamia alisema akiwa mdau wa habari, atahakikisha kuona waandishi wa habari wanapata haki zao hivyo utapelekwa bungeni lakini kila jambo lina utaratibu wake.

ANASWA AKIBANIKA MIKONO YA MTOTO

WAKATI jamii ya Watanzania ikipigwa butwaa na ukatili wa kutisha aliofanyiwa mtoto wa miaka minne kwa kufungiwa ndani ya boksi kwa miaka mitatu mjini Morogoro, ukatili mwingine wa kutisha dhidi ya watoto umeripotiwa mkoani Kagera. Katika mkoa huo, mganga wa kienyeji ametiwa mbaroni, akituhumiwa kumuua kwa kumnyonga, kumkata mikono na kumzika katika nyumba yake.

Mganga huyo, Mujingwa John (20) amekiri mbele ya jeshi la polisi kuhusika na mauaji ya mtoto Fausta Geofrey (8), mwanafunzi wadarasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kitunga kata ya Muhutwe, wilayani Muleba.

Anatuhumiwa kwamba, alimkamata kwa nguvu akienda shule na wenzake, akamuua, kumkata mikono, nyama ya mgongo, masikio na sehemu za siri kwa lengo la kuibanika na kutengeneza 'uchawi' wake, kisha akachimba shimo na kuzika mwili ndani ya nyumba.

Tukio hilo lilithibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, George Mayunga aliyesema mganga huyo alikamatwa na polisi kwa kushirikiana na wananchi, ambapo alikutwa akibanika viungo alivyovikata kutoka kwa mtoto huyo.

Aidha, akiwa polisi, mganga huyo alipewa fursa ya kueleza kilichotokea mbele ya waandishi wa habari, ambapo alidai alifikia uamuzi wa kumuua mtoto huyo, kutokana na hali ngumu ya umaskini inayomkabili.

Alisema baada ya kumkamata mtoto huyo, alimkaba shingo na kumvuta hadi katika nyumba aliyokuwa akiishi, akamnyonga hadi kufa na baada ya kufa, alimkata ngozi ya mgongoni, mikono akianzia na mkono wa kushoto aliodai una bahati, sehemu za siri na masikio.

"Nilimkamata mtoto na kumuua, maana niliona nikikamata mtu mzima atanizidi nguvu na kupiga kelele," alidai.

Alidai kuwa, "Nilipomaliza kumuua nilichimba shimo chini ya kitanda changu nikamzika na kutandaza nyasi juu yake ili isigundulike kamaeneo hilo kuna shimo".

Mganga huyo aliyejitambulisha kuwa ni Msukuma, alidai viungo hivyo ambavyo hadi polisi wanafika, alikuwa bado akivikausha, angevichanganya na dawa ambayo angewapatia wateja wake ili iwasaidie kufanikisha mambo yao, ikiwamo kupata bahati na utajiri na alitarajia kuuza kwa Sh 500 kwa kila ujazo wa kijiko kimoja cha dawa yake.

Alisema hiyo ni mara yake ya kwanza kufanya tukio la aina hiyo na kwamba alihamia Muleba mkoani Kagera miaka miwili iliyopita akitokea Nyanguge wilaya ya Magu mkoani Mwanza. Alisema alirithi uganga huo kutoka kwa babu yake mzaa mama na kuwa alianza uganga akiwa na umri wa miaka minane na hakuwahi kwenda shule.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bisole katika Kata hiyo wilayani Muleba, Khamis Hassan, akizungumzia tukiohilo baada ya mauaji hayo, alidai muuaji alimkata mtoto huyo mikono yake miwili kabla ya kumzika.

Hassan alisema kuwa tukio hilo ni la Mei 21 mwaka huu asubuhi katika kijiji hicho, wakati mtoto huyo akiwa na wenzake wakielekea shuleni, ambapo inadaiwa aliitwa na kukamatwa na mganga huyo, aliyetambulika kwa jina la Mujingwa John (20).

Alisema kuwa baada ya taarifa za mtoto huyo kutoonekana kuzagaa, wanakijiji walikusanyana na kuanza msako, ambapo walikamata kundi la watu waliokuwa wakiwahofia kuhusika, hasa vijana.

Alisema baada ya kuwakamata watu hao, waliwaweka sehemu moja na kuwaita wanafunzi waliokuwa na marehemu, ambapo walimtambua mganga huyo kuwa ndiye aliyemwita na kumkamata mtoto huyo.

Mtendaji huyo alidai baada ya mganga huyo kutambuliwa, wananchi na polisi waliofika eneo hilo, walikwenda naye hadi katika nyumba anayoishi na kumtaka awaonyeshe alipo mtoto huyo. Alidai baada ya kumbana, aliwaonesha sehemu alikomzika, ambapo walichukua jembe na kuanza kufukua mwili wa mtoto huyo, uliokuwa umezikwa ndani ya nyumba aliyoishi mganga huyo.

Alidai baada ya mganga huyo kumuua mtoto huyo, alimkata mikono yake miwili na kisha kuchimba shimo ndani ya nyumba, ambapo baada ya kumzika alifukia shimo akatandaza nyasi juu yake na kisha kuweka kitanda chenye godoro alilokuwa akilala.

Alisema kuwa alipohojiwa ili kujua nani kamtuma kutekeleza unyama huo, mganga huyo alidai ilitokana na yeye kuoteshwa na mizimu yake, iliyomtaka kumuua mtoto ili amkate viungo vyake kwa ajili ya kuchanganya na dawa.

Alisema mikono hiyo alitaka kuibanika kwenye moto ili aichanganye na dawa, ambayo angewapatia watu wanaohitaji kupata utajiri.

Tukio hilo limekuja siku chache wakati Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, likiendelea na uchunguzi wa kilichotokea mpaka mtoto mmoja mkoani hapa (jina limehifadhiwa), akateswa na mamamlezi kwa kuwekwa katika boksi tangu akiwa na miezi tisa, mpaka alipotimiza miaka minne.


Chanzo: Habari leo

BOKO HARAM WAWEKEWA VIKWAZO

Baraza la usalama la umoja wa mataifa hatimaye limeidhinisha kuwekewa vikwazo kundi la Boko Haram baada ya utekaji nyara wa takriban wasichana 300 wa shule katika eneo la Chibok Nigeria.

Kundi hilo limeshutumiwa kuwaua maelfu ya watu nchini Nigeria katika miaka michache iliyopita.

Nigeria ni mwanachama wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwa kipindi cha miaka miwili. Kwa nafasi hii imeweza kushinikiza baraza hilo kuimulikia tochi.


*Vikwazo na adhabu

Hatua ya baraza hilo kuiorodhesha Boko Haram miongoni mwa magaidi wa kimataifa, wakipishana au hata kuhusishwa moja kwa moja na AL Qaeda, huenda isionekane kama hatua kubwa. Lakini hii ina maana kuwa sasa jamii ya kimataifa italichukulia kwa uzito mkubwa zaidi kundi hilo.Baraza hilo limeidhinisha pia vikwazo kuwekewa kundi hilo, viongozi wake na yeyote anayehusishwa nalo. Hii ina maana kuwa hata mali zao zitazuiliwa na akaunti zao zote zinazojulikana kufungwa.


*Jamii ya kimataifa

Mjumbe wa Marekani katika Umoja wa mataifa Samantha Power amepongeza hatua hiyo akisema kuwa itaimarisha vita vya serikali ya Nigeria dhidi ya Kundi hilo, ambalo limetikisa jamii ya kimataifa mwezi uliopita kwa kuwateka zaidi ya wasichana mia mbili wa shule.

Kwa upande wake mjumbe wa Australia katika baraza hilo balozi Gary Quinlan amesema kuwa wanao ushahidi wa kutosha kuwa Boko Haram wamepewa mafunzo na kundi la Al Qaeda hasa namna ya kujitengenezea mabomu, mtindo ambao umekuwa mbinu mpya zaidi ya ugaidi.

Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau amenukuliwa katika mtandaoakitoa matamshi ya kuunga mkono AL Qaeda nchiuni Afghanistan, Yemen na Somalia.


*Magaidi wanaojulikana

Kabla ya kujumuishwa Boko Haram katika orodha ya Al Qaeda, kulikuweko makundi 62 kote duniani waliowekewa vikwazo kuhusika na Ugaidi, na watu binafsi 162, ambao wamewekewa vikwazo vya usafiri na mali zao kutwaliwa.


*Wamesababisha maafa

Shughuli za Boko Haram katika miaka 5 iliyopita zimesababisha vifo vya maelfu ya waislamu na wakristu wakiwemo watu 1500 waliouawa mwaka huu pekee.

Jina la Boko Haram lina maanisha masomo ya magharibi ni Haram na kundi hilo limetumia nembo hiyo kuendeleza mashambulio yao na chuki dhidi ya chochote kinacho husishwa na nchi za magharibi.

URUSI NA CHINA YAPIGA KURA YA TURUFU KUZUIA JARIBIO YA KUIFIKISHA SYRIA ICC

Uchina na Urusi zimepigia kura ya turufu, kuzuia jaribio la baraza la usalama, la kutaka kuifikisha Syria katika mahakama ya kimataifa ya jinai, ICC, kwa mashtaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Hili ni azimio la nne dhidi ya Syria, ambalo nchi hizi mbili zimelizuia.

Azimio hilo lingezielekeza Serikali na vikosi vya waasi nchini Syria katika mahakam hiyo ili zichunguzwe kutokanana ushahidi uliokusanywa na tume moja ya haki za kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.

Ufaransa ilitoa rasimu ya azimio hilo baada ya kushindwa kwa mchakato wa kisiasa ulioidhinishwa na Umoja wa Mataifa na pia wakati kukiendela kushuhudiwa maovu yanayotekelezwa na pande zote mbili, ingawa zaidi na serikali.

Balozi wa Ufaransa alisema kuwa maadili yanapaswa kutumika kukabiliana na migawanyiko ya muda mrefu kuhusu Syria katika baraza hilo.

Lakini Urusi tayari imetangaza kwamba hatua hiyo ni ya kutafuta umaarifu na kwamba itaharibu jitihada za kutafuta amani na kwa pamoja na China ikapiga kurahiyo ya turufu kulipinga azimio hilo.

WATU WAWILI WAJERUHIWA KATIKA MLIPUKO WA BOMU

Watu wawili wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea mjini Mombasa pwani ya Kenya.

Miongoni mwa wawili hao ni afisa wa polisi aliyekimbizwa katika hospitali ya mkoa kupokea matibabu.

Shambulio hilo lilitokea wakati maafisa wa polisi walimkamata mshukiwa wa ugaidi, na hapo pakatokea mtu wa pili aliyewarushia guruneti katika jitihada ya kumuokoa mshukiwa aliyekamatwa.

Mbunge wa Mvita kutoka eneo hilo, Abdulswamad Sharrif ambaye ni miongoni mwa viongozi waliofika katikaeneo hilo punde baada ya mlipuko huo, amelaumu udhaifu katika idara ya ujasusi Kenya kwa kutoweza kutambua mipango ya mashambulio kama hayo kabla ya yafanyike, ili kuweza kuyatibua.

Akizungumza na BBC Abdulswamad amesema, 'Ni lazima tuweze kukubali kasoro iko wapi, ili tuweze kujua suluhisho litakuja vipi'.

Shabulio hilo limetokea wakati usalama umeimarishwa nchini Kenya kutokana na tisho la kutokea shambulio la kigaidi dhidi ya maeneo ya umma.

Katika siku za hivi karibuni Kenya imekuwa ikikabiliwa na mashambulio kadhaa katika maeneo mbali mbali nchini ukiwemo mji huo wa Mombasa na Nairobi, yaliosababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wengi kujeruhiwa.

Ni hivi juzi tu watu 10 waliuawa huku zaidi ya hamsini walijeruhiwa katika milipuko miwili iliotokea katika Soko kubwa la nguo la Gikomba katika mji mkuu Nairobi.

INTER MILAN KUKIPIGA DHIDI YA KENYA

Kwa mara ya kwanza klabu mashuhuri duniani Inter Milan ya Italia inazuru bara laAfrika.

Inter inatarajiwa kuwasili nchini Kenya kesho kwa mechi yao ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa Harambee Stars Jumapili, kama anavyotueleza mwaspoti wa BBC John Nene.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa shirikisho la kandanda nchini Kenya Sam Nyamweya klabu hiyo ya Italia Inter Milan inawasili Nairobi siku ya Ijumaa na kisha ipambanena Harambee Stars Jumapili kwenye mechi ya kimataifa ya kirafiki kuanzia saa kumi za afrika mashariki.

Ziara ya Inter inatokana na ushirikiano mpya kati ya shirikisho la kandanda nchini Kenya na lile la Italia.

Wengine ambao wamechangia kwa ziara hiyo ni wizara ya michezo, bodi ya utalii nchini Kenya na wasimamizi wakuu wa uwanja wa Kasarani.

Shirikisho la kandanda la Kenya hatahivyo halijataja kikosi cha Inter kwa ziara hii lakini wamesema mabingwa hao wa ligi ia Italia serie A mara 18 watakua na wachezaji wake wa kutegemewa.

Tayari mmoja wa nyota ya Inter MacDonald Mariga wa Kenya yuko Nairobi akijiandaa kwa mechi hiyo.

Mariga aliiwakilisha Harambee Stars wikendi iliyopita kwenye mechi yao yakufuzu kwa finali ya mechi za kombe la Afrika dhidi ya Comoros katika uwanja wa taifa wa Nyayo..

Inter ina mchezaji mmoja tu kwenye kikosi cha timu ya Italia cha kombe la dunia nchini Brazil, naye ni mlinzi Andrea Ranocchia aliye kwenye idadi ya wachezaji 30 ambao watapunguzwa hadi 24..


Haijulikani kama mshambuliaji matata wa Inter Diego Milito yuko kwenye ziara ya Kenya kwani tayari anaondoka Inter baadaya kukitumikia klabu hicho kwa miaka mitano.

Mashabiki wengi hawatamsahau Milito alipofunga mabao mawili yaliyoiwezesha Inter kuicharaza Bayern Munich mabao 2-0 katika mechi ya fainali ya kombe la mabingwa wa ligi ya ulaya mwaka 2010.

Msimu uliopita Milito, mwenye umri wa miaka 34, hakuonyesha mchezo mzuri kutokana na majeraha ambayo yamemsumbua kwa miaka ya hivi karibuni.

Miongoni mwa wachezaji wengine wanaoondoka ambao Milito alikua nao wakishinda Bayern ni Javier Zanetti, Esteban Cambiasso na Walter Samuel..

Inter pamoja na Manchester United ndizo timu mbili ambazo zimeshinda kombe la mabingwa wa ligi ya ulaya mara tatu.

MAMA YAKE ZITTO ALAZWA ICU

Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania, (Chawata), Shida Salum, yuko katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Ami, Masaki, Dar es Salaam akisumbuliwa na maradhi ya saratani.

Shida ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amelazwa tangu juzi. Alianza kusumbuliwa na maradhi hayo mapema Agosti mwaka jana lakini hali yake ilibadilika mapema mwaka huu akiwa mjini Dodoma akisubiri kuapishwa pamoja na wajumbe wengine wa Bunge Maalumu la Katiba.

Akizungumza hospitalini hapo jana, Zitto alisema baada ya hali ya mama yake kuwa mbaya alishindwa kuendelea kukaa Dodoma kusubiri kuapishwa na alipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),ambako aligundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi na kupatiwa tiba kwa mwezi mmoja kabla ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi.

Alisema kabla ya kupelekwa hospitalini hapo, alikuwa akiendelea kupata matibabu akiwa nyumbani, lakini hali yake ilibadilika juzi.

Zitto alisema hali ya mama yake haijatengemaa tangu aanze kusumbuliwa na maradhi hayo. Alisema kutokana na maradhi hayo ya mama yake, ameshindwa kuhudhuria Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma.

"Hali ya mama kwa kweli siyo nzuri,lakini nina imani itakuwa nzuri na kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa kama zamani," alisema Kabwe.

Tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti, Zitto alionekana Dodoma mara moja tu, siku ilipowasilishwa Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

MTOTO AFICHWA KWENYE BOKSI KWA MIAKA MINNE

Mwanamke aliyetambuliwa kuwa ni Mariamu Said mkazi wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro juzi alishushiwa kipigo nawananchi kutokana na kumficha mtoto wa marehemu mdogo wake kwenye boksi kwa miaka minne.

Tukio hilo lilitokea juzi saa nne asubuhi baada ya majirani zake kutoa taarifa kwa Ofisa Mtendaji waKata ya Kiwanja cha Ndege, Dia Zongo kuhusu mtoto huyo, Nasra Rashid, kufichwa ndani ya boksi tangu akiwa na umri wa miezi tisa.

Zongo alisema majirani hao walimweleza pia kuwa jirani yao huyo hamfanyii usafi mtoto huyo wala kumtoa nje.

Baada ya kupata taarifa hizo, Zongo alimtafuta Mwenyekiti wa Mtaa huo, Tatu Mgagala na kuongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo na kumhoji mwanamke huyo ambaye alikuwa akijibu kwa kubabaika.

Moja ya maswali aliyoulizwa ni idadi ya watoto wake na akajibu kuwa ana wawili lakini wakati akiendelea kujibu maswali, ghafla mtoto huyo alipiga chafya na kuanza kukohoa, hivyo kuwapa wasiwasi na kuamua kuingia chumbani kwa mwanamke huyo kwa nguvu na kumkuta mtoto Nasra akiwa ndani ya boksi.

Ofisa mtendaji huyo alisema wakati wakimtoa mtoto huyo ndani ya nyumba, kundi kubwa la watu waliokuwa na fimbo na mawe walianza kumshambulia mwanamke huyo na kumlazimu mtendaji kutoa taarifa polisi.

Alisema muda mfupi baadaye, polisi waliwasili na kumkamata Mariam na kumpeleka katika ofisi ya kata ambako aliwekwa chini ya ulinzi.

Baadaye aliwekwa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi, Morogoro namtoto alipelekwa Ofisi za Ustawi wa Jamii.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alisema wanaendelea kukusanya taarifa za tukio hilo ikiwamo matokeo ya vipimo vya madaktari kuhusu afya ya mtoto huyo kabla ya kuchukua hatua zaidi.

Kamanda Paulo alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwakosa la kumfanyiwa mtoto vitendo vya kikatili.

Hata hivyo, kamanda huyo alisema polisi wanakadiria kwamba mtoto huyo alianza kufichwa kwenye boksihilo akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu.


*Utetezi wa Mariam

Akijibu maswali ya polisi, mwanamke huyo alikiri kuanza kumlea mtoto huyo tangu akiwa na umri wa miezi tisa baada ya mama wa mtoto huyo kufariki dunia mwaka 2010.

Pia mtuhumiwa alikiri kwamba mtoto huyo hajawahi kupewa chanjo yoyote wala kupelekwa kliniki.

Alikuwa akitoa maelezo hayo huku akiwa amemshikilia mtoto huyo aliyetapakaa uchafu ikiwamo haja kubwa na ndogo alizokuwa akitoa ndani ya boksi na kusema kwamba mara ya mwisho alimwogesha Julai mwaka jana.

Pia alisema alikuwa akimwekea chakula na maji ndani ya boksi lililokuwa nyuma ya mlango wa chumba.

Mume wa mwanamke huyo, Mtonga Ramadhani anayefanya biashara katika Soko la Mawenzi, Morogoro ambaye pia anashikiliwa na polisi, alidai kuwa hakuona sababu ya kutoa taarifa za kufichwa kwa mtoto huyo kwa sababu hamhusu na wajibu wake ni kutafuta chakula.


*Alivyonaswa

Baadhi ya majirani wa mwanamke huyo ambao hawakutaka kutajwa majina, walisema Mariam alihamia katika nyumba hiyo mwaka 2010 na hawajawahi kumwona mtoto huyo akitolewa nje wala kufanyiwa usafi.

Walisema mtoto huyo alibainika baada ya kusikika akikohoa na kulia nyakati za usiku, jambo lililozua wasiwasi kuwa huenda mtuhumiwa alikuwa mshirikina anayefuga misukule.


*Baba wa mtoto

Baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid Mvungi alisema hakujua kama mwanaye alikuwa analelewa katika mazingira hatarishi.

Akihojiwa na Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu, Mvungi alisema alimzaa mtoto huyo nje ya ndoa na amekuwa akituma fedha za matumizi kwa mama yake mkubwa.

Mvungi ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, alisema baada ya mzazi mwenzake kufariki dunia alishindwa kumchukua mtoto wake kwa sababu tayari alishakuwa na mke.


Chanzo: Mwananchi

BAADA YA KIKOMBE CHA BABU DHAHABU YAIBUKA SAMUNGE

Maelfu ya watu wamemiminika tena katika eneo la Samunge, Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha, safari hii siyo kunywa Kikombe cha Babu Mchungaji Ambilikile Mwasapile, bali kupata dhahabu inayodaiwa kugundulika katika eneo hilo.


Habari kutoka katika eneo hilo zinasema kuwa watu wanazidi kumiminika katika kujipatia madini hayo yaliyobainika katika mashamba ya watu na maeneo ya kingo za Mto katika Kijiji cha Mgongo kilichopo jirani na Kwa Babu.

Diwani wa Samunge, Jackson Sandea alisema maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali nchini wamefurika katika kijiji ambacho kuna mto na madini ya dhahabu yanapatikana hapo.


"Hadi sasa kuna watu zaidi ya 4,000na bado wanaongezeka, hii inawezakuwa ni zaidi ya kipindi kile cha Babu wa Kikombe. Dhahabu hii inapatikana mtoni tu, watu wanakusanya michanga na kupata dhahabu, hakuna mtu ambaye anachimba," alisema Sandea.

Alisema tofauti na maeneo mengine, dhahabu ya Samunge inaonekana ni ya Watanzania wote kwani ipo eneo la mto ambao unamilikiwa na Serikali na ndiyo sababu watu wanaingia kwa wingi.

"Kuna wengine wanapata hata mashambani lakini mtoni ndipo inapatikana kwa wingi zaidi," alisema.


*Ulinzi waimarishwa

Diwani huyo alisema ulinzi umeanza kuimarishwa katika eneo hilo akisema hali ikiachwa kama ilivyo, kunaweza kutokea vurugu kubwa na hata mauaji.

"Sisi kama viongozi, tumeweka utaratibu mzuri wa kuchimba madini kiusalama na hata wale ambao wameanza kuuza mashambayao, tunawawekea utaratibu mzuri," alisema.


*Maofisa madini kutua Samunge

Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Alex Magayane alisema jana kwamba baada ya kupokea taarifa za kugundulika kwa dhahabu katika eneo la Samunge, maofisa wake wanajiandaa kwenda kijijini hapo.

Alisema taarifa za kitaalamu kuhusu akiba ya madini hayo iliyopo Samunge itatolewa baada yamaofisa hao kufika katika eneo hilona kufanya utafiti.


*Ahadi ya Babu

Kugundulika dhahabu katika eneo hilo kunahusishwa na ahadi ya Mchungaji Mwasapila kuwa mamilioni ya watu watafika tena Samunge baada ya kupungua ikilinganishwa na miezi ya mwanzo baada ya kuanza kutoa tiba ya kikombe cha dawa iliyodaiwa kutibu magonjwa sugu.


Tiba yake hiyo ambayo ilizua utata kitaalamu na ikielezwa kuwa waliotibiwa waliugua tena na wengine kupoteza maisha, aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akisema watu kutoka mataifa yote watakwenda tena Samunge siyo kupata kikombe pekee, bali huduma nyingine.

Licha ya wengi kuitilia shaka kauli yake hiyo, aliendelea kuisisitiza na akikata miti na kujenga kituo kikubwa cha kutolea huduma ya kikombe.


Chanzo: Mwananchi

WAWAKILISHI MARUFUKU KUJADILI KATIBA

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho amepiga marufuku mijadala ya Bunge la Katiba, kuzungumzwa katika vikao vya Baraza la Wawakilishi.


Alisema hayo kutokana na kujitokeza kwa hoja mbali mbali zawajumbe, zinazozungumzia Bunge la Katiba, kiasi ya kuibua mijadala yenye muelekeo wa chuki na uhasama.

"Mimi ni mdau mkubwa wa umoja na mshikamano wa wananchi wa Zanzibar, sitaki kusikia lugha zenyekuashiria chuki na uhasama na kuwagawa wananchi wanaoishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alisema.

Swali lililoibua hisia za Bunge la Katiba, liliulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Saleh Nassor Juma aliyesema kwamba hotuba ya Rais Jakaya Kikwete katika Bunge la Katiba, ndiyo chanzo cha kuvurugika kwa bunge hilo.


Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud, alisema katika hotuba yake Rais Kikwete alitoa tahadhari kwa Watanzania kuhusu hatari ya kugawanyika kwa taifa hili, kama Muungano utavunjika.

Akifafanua, Aboud alisema kauli zawajumbe wa pande mbili, ndiyo zilizozusha mijadala, ambayo iliegemea matusi na baada kupelekea wajumbe wa vyama vya siasa vya upinzani kugomea vikao.


Mapema, Kificho alisema kuanzia sasa swali la mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, litakaloelekea masuala ya Bunge la Katiba, litazuiliwa na halitosomwa.

Aliwataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, kuchangia na kutoa maoni ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa maslahiya wananchi wa pande mbili huku wakiyapatia ufumbzi matatizo ya wananchi.

PPFT WAMVAA ASKOFU KAKOBE

USHIRIKA wa wachungaji wa Kipentekoste nchini (PPFT) umemtaka Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zakaria Kakobe, kuacha tabia ya kutumia mwavuli wa dini kuhubiri chuki na uchochezi kwa wananchi.

Akizungumza juzi wakati wa kufunga semina ya viongozi wa diniwa Mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika katika ukumbi wa Umoja Hostel, Mwenyekiti wa Ushirika wa Wachungaji nchini, Askofu Ikongo alisema kauli za Askofu Kakobe zimekuwa za hatari na zinaweza kuliingiza Taifa kwenye machafuko ya kidini.


"Nchi yetu imekuwa na dalili za viashiria vya kutoweka kwa amani na utulivu, kutokana na baadhi ya viongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa na kuanza kutoa kauli za kuashiria uchochezi na kupandikizachuki kwa waumini…sasa umefika wakati sisi viongozi wa dini hatuwezi kunyamaza kwani tutaonekana na matamko yanayotolewa kiholela kwa kutumia mwamvuli wa upentekoste," alisema Askofu Ikongo.


Alisema Askofu Kakobe amekiuka uadilifu wake, kwani Aprili 20 mwaka huu katika kanisa lake la Mwenge, alitoa kauli kuwa atapambana hadi Tanganyika irudi hata kwa kukatwa kichwa, kauli ambayo inadhihirisha ugaidi.

Askofu Ikongo alisema kauli kama hiyo haistahili kutolewa na mtumishi yeyote wa Mungu, kwanimtu mwenye uwezo wa kusema hata akatwe kichwa sio wa kawaida bali ni mtu aliye na mafunzo ya kujitoa mhanga kama gaidi.


"Tunasikitishwa na kauli za Askofu Kakobe ambazo zinaweza kuliletea Taifa machafuko ya kidini…siku ya Pasaka Aprili 20 mwaka huu aligeuza mimbari kuwa jukwaa la siasa, kwa kuhubiri uchochezi kwa kudai; kila mtu anayepigania kurudi kwa Tanganyika, ana Mungu ndani yake," alisema.

Kwa mujibu wa Askofu Ikongo, kauli hizo za Kakobe ni za kigaidi na zina nia ya kuvuruga amani ya Watanzania na kuliingiza taifa kwenye machafuko, ambayo yataharibu tunu iliyoachwa na Babawa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.


Alisema ni vyema viongozi wa dini wajikumbushe wajibu wao wa kuliombea Taifa, na kuwaongoza waumini wao kufuata yaliyo mema badala ya kugeuka sehemu ya kutumiwa na wanasiasa.

Akifunga semina hiyo Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Makiluli aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Leonidas Gama, alisema inasikitisha kuona viongozi wa dini kutumiwa na wanasiasa, kwa kutoa kauli zinazowafanya wananchi kuhoji kama viongozi hao hawatumii dini kutekeleza malengo ambayo sio mema.


Alisema Serikali bado ina imani na viongozi wa dini, kwa wale wanaozingatia maadili na utume wao wa kuhakikisha amani iliyodumu kwa miaka mingi inadumishwa.

Aliwataka waumini kutowaunga mkono wanaotumia mimbari kuwa jukwaa la siasa kwa kutoa maneno makali yanayohatarisha amani na kupandikiza chuki miongoni mwa waumini na wananchi.

WIZARA ZAASI SERIKALI

Wizara ya maswala ya ndani ya Libya imetoa taarifa ikisema kuwa inaunga mkono kampeini dhidi ya serikali inayoongozwa na jenerali wa zamani wa jeshi la taifa aliyeasi serikali tawala.


Hata hivyo waziri husika Salihal-Mazig baadaye alikanusha kumuunga mkono jenerali muasi Khalifa Haftar, aliyeanzisha operesheni ijumaa iliyopita.

Jenerali Haftar amezindua kampeini ya kivita inayolenga kuing'oa mamlakani utawala uliomrithi aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Maummar Gaddafi kuanzia kwa bunge lililoshambuliwa siku ya jumapili.

Jenerali huyo aliongoza wapiganaji wake kuvamia mjiwa Benghazi katika kampeini anayoiita "Libya's Dignity".


Jenerali huyo anailaumu serikali kwa kuwatepetevu dhidi ya wapiganaji waasi.Wizara ya maswala ya ndani tayari imemuunga mkono katika mtandao wake wa kijamii wa Facebook.

Jumatatu hii kiongozi wa jeshi la wanahewa la Libya Jenerali Guma al-Abany, alitoa ujumbe wa kumuunga mkono Jenerali huyo aliyestaafu akisema hatua yake ni jambo la kupigiwa mfano kwa walibya wazalendo.

Kiongozi wa jeshi la wanamaji Brigadia jenerali Hassan Abu-Shannaq, alinusurika jaribio la mauaji muda mchache tu baada ya kutangaza kumuunga mkono jenerali huyo aliyezindua vita dhidi ya wapiganaji wakiislamu ambao wanalumiwa kwa utovu wa usalama nchini Libya.


Serikali imempuzilia mbali jenerali Khalifa Haftar na ikasema kuwa haita jiuzulu.

Takriban watu 100 wameripotiwa kuuawa tangu mapigano hayo kuzuka ijumaa iliyopita na kuilazimisha serikali kuitisha uchaguzi wa haraka tarehe 25 mwezi juni.

Iwapo uchaguzi huu utaendelea mbele basi utakuwa ni uchaguzi wa pili tangu aliyekuwa rais Muammar Gaddafi kungolewa madarakani mwaka wa 2011.

Hadi kufikia sasa Libya imekuwa na mawaziri wakuu watatu tangu mwezi Machi mwaka huu.

WATU 46 WAUAWA KATIKA MILIPUKO KATIKA MJI WA JOS

Takriban watu 46 wameaga dunia na wengine wengi kujeruhiwa baada ya milipuko miwili mikubwa kutokea nchini Nigeria katika mji wa Jos.Milipuko hiyo imetokea katika soko lenye shughuli nyingi .
Mwandishi wa BBC aliyeko huko anasema kuwa amehesabu miili 40 ikipelekwakatika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali moja iliyoko JOS.




Mwandishi wa BBC Ishaq Khalid aliye mjini humo anasema kuwa kuna hofu ya watu wengi kujeruhiwa hasa kwa kuwa soko hilo lilikuwa na idadi kubwa ya watu.

Aidha anaarifu kuwa taharuki ietanda katika eneo hilo baada ya vijana waliopandwa na hasira kufunga mabarabara ya kuingia na kutoka mjini humo na kuzua hofu ya makabiliano.
Mji wa Jos itakumbukwa iliwahi kushuhudia mapigano mabaya zaidi baina ya makundi ya vijana Waislamu na wale Wakristu iliyosababisha maafa mengi.
Mabomu hayo yanasemekana kuwa yalikuwa yametegwa moja katika lori na lingine katika gari la uchukuzi wa abiria na yakalipuka kwa mpigo moja katika soko la lingine karibu na hospitali.
Hakuna aliyekiri kutekeleza mashambulizi hayo ijapokuwa jimbo hilo limewahi kushambuliwa na kundi la Boko Haram zaidi ya miaka miwili iliyopita.


Jimbo la Platue liko mpakani kati ya waislamu wanaoishi Kaskazini mwa Nigeria na Wakrstu ambao wanaishi Kusini .
Jimbo hili limewahi kushudia mapigano baina ya wakulima wakristu wa tabaka la Berom na waislamu wafugaji wa kuhamhama wa tabaka la Fulani.
Mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kituo cha basi kilishambuliwa kwa bomu na awali mwaka wa 2012, Boko Haram walifanya shambulio baya zaidi lililowaua zaidi ya watu 150 katika msururu wa milipuko.
Kundi hilo bado linawazuilia wasichana zaidi ya 200 wa shule, lililowateka kutoka kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa Nigeria mwezi mmoja uliopita.
Nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Ufaransa na Marekani wameahidi kutuma wanajeshi kusaidia kuwakomboa wasichana hao.
Nao viongozi wa Afrika wanaokutana mjini Paris wametangaza 'vita' dhidi ya Boko Haram na kuahidi kushirikiana ki-intelijensia na kijeshi, kupambana na Boko Haram.

WANAWAKE WATAKA MAPADRE WARUHUSIWE KUOA

Kundi moja la wanawake walio na hisia za kimapenzi na mapadre wa kikatoliki wamemuandikia barua kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ya kumtaka kubadilisha sheria za kanisa hilo zinazowazuia viongozi hao wa dini kuoa.

Wanawake hao 26 kutoka Italy na maeneo mengine wanasema kwamba wamekuwa wakishiriki ama wanataka kushiriki katika uhusiano wa kimapenzi na mapadre na kwamba wametoa ombi hilo kwa niaba ya wanawake wengine ambao wako katika hali kamahiyo.

Barua hiyo inazungumzia kuhusu uchungu wa kushindwa kuishi maisha yao kikamilifu mbali na kutaka kukutana na papa Francis.

Papa Francis amekuwa akiunga mkono utamaduni wa useja, lakini mwaka 2010 aliandika akisema kuwa huenda msimamo wake ukabadilika.

Papa francis amekuwa akimtembelea mjane wa aliyekuwa kasisi Jeronimo Podesta ambaye alijiuzulu katika utumishi wake na kuoa, zaidi ya miaka 40 iliopita.

WATU 12 WAUAWA MPAKANI MWA KENYA NA SOMALIA

Maafisa wa Kenya wamethibitisha kuwa watu 12 wameuawa katika mpaka wa nchi hiyo na Somalia, katika shambulio linaloshukiwa kufanywa na wanamgambo wa Al shabaab.

Watu wengine 7 raia wa Kenya hawajulikani waliko. Shambulio hilo la Jumatatu limetokea siku moja baada yajeshi la anga la Kenya kuvamia kwa makombora maeneo yanayoshukiwa kuwa ngome za wapiganaji hao wa kiislamu, upande wa Somalia.

Bado Kundi hilo halijatoa taarifa yoyote kukana au kukiri kuhusika katika shambulio hilo.


*Washambuliaji

Akizungumza na BBC, Seneta wa kaunti ya Mandera iliyoko mpaka wa Kenya na Somalia Billow Kerrow, amethibitisha kuwa washambuliaji hao walitoka upande wa Somalia.

Amesema kuwa inashukiwa kuwa walikuja kuiba miraa kutoka kwa wafanyibiashara wa zao hilo upande wa Kenya, na walipofumaniwa na askari wa Kenya ndipo waliwafyatulia risasi.

Seneta Kerrow amekanusha madai kuwa huenda shambulio hilo linahusika na uhasama wa kikabila na kiukoo ulioko kati ya jamii zinazoishi katika mpaka huo.

Shabulio hilo limetokea wakati usalama umeimarishwa nchini Kenya kutokana na tisho la kutokea shambulio la kigaidi dhidi ya maeneo ya umma.


*Usalama

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umepunguza wafanyikazi wake na kuongeza ulinzi, huku Uingereza ikiimarisha usalama katika ubalozi wake na hata kuwaondoa baadhi ya raia wake waliokuwa nchini Kenya kwa usalama wao.

Wanamgambo wa Al shabaab wamezidisha mashambulio nchini Kenya tangu nchi hiyo iingize wanajeshi wake ndani ya Somalia kuwasaka wapiganaji hao haramu mwaka wa 2011

BOSI WA EWURA AKUTWA AMEFARIKI HOTELINI

Meneja Biashara wa Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) amekutwa amekufa hotelini katika mazingira ya kutatanisha muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam akitoka Dodoma ambako alihojiwa na Kamati ya Bunge ya Bajeti.

Meneja huyo, Julius Gashaza, ambaye alikuwa na jukumu la kupanga bei za mafuta za kila mwezi, alihudhuria kikao hicho mjini Dodoma kwa siku mbili; Ijumaa na Jumamosi iliyopita kuhusu mambo mbalimbali, yakiwamo kiwango cha mafuta kinachoingizwa nchini, mgawo wa fedha unaotolewa na Ewura kwenda kuhudumia umeme vijijini (Rea) na fedha za mfuko wa barabara.

Jeshi la Polisi, Mkoa wa Temeke limethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa meneja huyo alikutwa amejinyonga kwa kutumia tai kwenye hoteli ya Mwanga Lodge iliyopo Yombo Vituka wilayani Temeke.

Nyumbani kwa meneja huyo wa Ewura, kulikuwa na waombolezaji waliokuwa kwenye vikundi na kikao cha maandalizi ya mazishi kilifanyika ndani ya nyumba ya marehemu iliyopo Yombo Vituka na baadaye kuhamia nyumba ya jirani.

Kamati ya Bunge ya Bajeti, inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, ilikutana na maofisa wa Ewura, akiwamo Gashaza na wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kugundua kuwapo kwa tofauti katika takwimu za kiwango cha mafuta kilichostahili kutozwa kodi.

Gashaza alikwenda Dodoma kutoa ripoti ya Ewura kwenye kamati hiyo ya Bunge akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kamati hiyo, takwimu za Ewura ziliashiria kuwa fedha zilizopatikana ni nyingi zaidi ya zile zilizoelezwa na TRA, lakini Wizara ya Fedha ilisisitiza zifuatwe takwimu za mamlaka ya mapato.

Habari hizo, zinasema baada ya kurejea Dar es Salaam juzi majira ya saa tatu usiku, Gashaza hakwenda nyumbani kwake na badala yake alikwenda kwenye hoteli iliyo karibu na nyumbani ambako mkewe na ndugu yake mmoja walimfuata na akawaeleza kuwa anahisi kutishiwa maisha yake.

Baadaye walifanya maombi maalumu kabla ya kuachana naye.

Inadaiwa kuwa marehemu aliomba akalale hotelini kwa sababu hakuona kama ana amani kulala nyumbani kwake na ilipofika asubuhi alikutwa ‘amejinyonga’ ndani ya chumba alicholala hotelini humo.

Nyumbani kwa marehemu waombolezaji walikusanyika katika makundi, lakini baada ya kukaa katika kikao cha familia walitoka na kauli moja kuwa hawatasema chochote na kwamba jukumu hilo libaki mikononi kwa polisi.

Kamanda wa polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Seleiman Kova hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo akidai kuwa anayetakiwa kulizungumzia ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Engbert Kiondo.

Alipotafutwa, Kamanda Kiondo alisema kulingana na taarifa zilizopo Gashaza aliitwa bungeni Mei 14 na akarejea Dar es Salaam Mei 17. Alisema aliporejea, Gashaza aliaga nyumbani kwake kuwa hajisikii vizuri na kuelekea Hoteli ya Mwanga Lodge iliyopo Yombo ambako alichukua chumba Namba 113.

Kamanda Kiondo alisema akiwa hotelini, Gashaza alimpigia simu rafiki yake mmoja anayejulikana kwa moja la Silipwango akimweleza kuwa yupo hotelini hapo kujipumzisha kwa sababu bungeni aliulizwa mambo ambayo hayakumpendeza na kwamba alihitaji kupumzika.

Rafiki huyo, kwa mujibu wa Kiondo, alimpigia simu mkewe anayeitwa Judith akamweleza alivyoelezwa na mumewe na baadaye kwa pamoja wakamfuata hotelini ambako baada ya kuzungumza nao kwa muda mfupi, aliwaomba wamuache apumzike na ndipo walipoondoka.

Asubuhi, Silipwango alipigiwa simu na mkewe kumueleza kuwa Gashaza hakurudi nyumbani na akaamua kupitia kwenye hoteli waliyomuacha na alipofika akakuta watu wamejaa. Alipouliza akaelezwa kuwa kuna mtu amejinyonga chumbani.

Kamanda Kiondo alisema Gashaza alijinyonga kwa kutumia tai aliyoifunga kwenye bomba la maji ambalo pia lilikatika na hivyo kuukuta mwili wake ukiwa sakafuni.

Kilichojiri kamati ya bajeti

“Kisheria kodi ya mafuta ni Sh263 kwa lita inakwenda mfuko mkuu Hazina na Sh50 inakwenda kwa Wakala wa Umeme Vijijini (Rea), lakini takwimu za mafuta yaliyouzwa inayostahili kutozwa kodi kati ya TRA na Ewura zinatofautiana,” alisema mmoja wa wajumbe.

“Kwa hiyo Kamati ya Bajeti iliwaita wote (Ewura na TRA) na kwa kweli wajumbe wa kamati tulikuwa wakali sana, hatutaki mchezo tulitaka kujua nani anasema ukweli,” alidokeza mjumbe huyo.

“Uko ugomvi mkubwa tu kati ya TRA na Ewura kuhusu nani hasa mwenye takwimu halisi,” alisema mjumbe huyo na kudokeza kuwa meneja huyo alisema kila kitu kwa uwazi.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zimeeleza kuwa baada ya vuta nikuvute ndani ya kamati hiyo, iliamuliwa watendaji wa vyombo hivyo viwili wakafanye ulinganisho na kupeleka jibu kwa kamati hiyo. Ewura waliwasilisha takwimu zao Jumamosi.

“Tension (mvutano) ni kubwa kwa sababu kuna watu wizarani hawazitaki takwimu za Ewura na wanataka za TRA ambazo sisi kama wajumbe tunaziona hazina uhalisia kunaweza kukawa na ufisadi,” alisisitiza mjumbe mwingine.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge alipoulizwa jana, alikiri kufanyika kwa kikao kilichomuhusisha meneja huyo na kwamba taarifa alizotoa zilionekana tofauti na zile za TRA.

“TRA ni chombo cha Serikali na Ewura ni chombo cha Serikali, kwanini wawe na takwimu zinazotofautiana? Hilo tu ndio tumewaagiza wakae pamoja watuambie zipi ni takwimu halisi,” alisema Chenge.

Alipoelezwa kuwa mmoja kati ya maofisa wa Ewura waliofika mbele ya kamati yake amejinyonga, Chenge alionyesha kushtushwa na kuhoji kama taarifa hizo zina ukweli.

“Una uhakika kwamba amejinyonga? lini? Kama ni kweli basi ni jambo la kusikitisha sana, lakini hiyo sasa ni kazi ya polisi. Mimi nisingependa sana kuzungumza, tuwaachie wao wachunguze sababu za kifo chake,” alisema Chenge.

Serikali inaelezwa kuwa katika hali mbaya kifedha na kamati hiyo ya Bajeti imekuwa ikifanya kila linalowezekana kuinusuru kwa kukutana karibu kila siku na Hazina na wadau wengine wanaochangia fedha katika mfuko wake.

Kwa bajeti ya mwaka 2013/2014 iliyopitishwa na Bunge, Serikali imejikuta ikiwa na upungufu wa Sh1.8 trilioni hali ambayo kamati ya bajeti inatafuta kila njia ikiwamo kushauri vyanzo vipya vya mapato ili kunusuru bajeti ya mwaka huu wa 2014/2015.

Bajeti ambazo zinaelezwa kuiumiza kichwa Serikali ni ya Maji, Miundombinu na Nishati na Madini ambazo zinaelezwa kupata mgawo kidogo mwaka jana na kuzifanya zishindwe kutekeleza miradi mbalimbali.

Mkurugenzi wa Petroli wa Ewura, Godwin Samwel alisema alipata taarifa jana saa 3:00 asubuhi.

Alithibitisha kuwa marehemu alikuwa Dodoma kikazi kwenye vikao na kamati ya Bunge tangu Alhamisi iliyopita.

Baada ya kumaliza kazi ndiyo ndiyo jana (juzi) alichelewa sana kurudi ndipo alipoamua kujipumzisha kwenye nyumba ya wageni (iliyopo karibu na nyumbani kwake) ambako alikutwa amefariki,” alisema Samwel.

Alisema marehemu alikuwa mwadilifu, mchapa kazi na asiye na tatizo lolote kazini na kuondoka kwake kumeacha pengo kubwa.

Fc_Rapper AACHIA NGOMA NYINGINE KALI


WANACCM WASIKITISHWA NA VIJEMBE VYA BUNGENI

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamesema wanasikitishwa na tabia za viongoziwa CCM badala ya kujadili matatizoya wananchi bungeni wanaanza kutupiana vijembe na wapinzani.


Akisoma risala katika uzinduzi wa shina la Pamba Road, mwanachama wa CCM, Exavery Rugina alisema kwa kufanya malumbano badala ya kujadili matatizo ya wananchi inawafanya waonekane hawajui watanzania wanahitaji nini wakati mategemeo ya Watanzania ni wabunge wa CCM.


Aidha, alisema ni vema kuachana na viongozi wasiojua wajibu wao kwa watanzania kwa sababu wanataka chama kiwatumikie wao na si wao kukitumikia chama.


Mgeni rasmi katika ufunguzi wa shina hilo, Katibu Mwenezi wa kataya Kivukoni, Hasan Malocho akiwataka wanachama wa CCM kuepuka watu wanaoponda muungano.

DOKTA ASAHAU KITAMBAA TUMBONI KWA MGONJWA

MKAZI wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Mwamini Adamu ametolewa mfuko wa kizazi na kukatwa sehemu ya utumbo baada ya mganga wa idara ya upasuaji katika wilaya hiyo kusahau kitambaa tumboni kwa mwanamama huyo wakati akijifungua.

Kutokana na kumsababishia ulemavu huo kwa uzembe, Mwamini ameifikisha Halmashauri ya wilaya ya Urambo kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Magharibi akidai fidia ya Sh milioni 500.

Mwamini ambaye anadai kuwa alipwe kiasi hicho cha fedha kutokana na uzembe wa uliofanywa na Dk Jacob Kamanda aliyemfanyia upasuaji wakati wa kujifungua na kumsababishia aondolewe mfuko wa kizazi pamoja na kukatwa utumbo.

Mwamini pamoja na mumewe Idrisa Jafari katika madai yao wametaka walipwe fedha hizo kutokana na makosa ya uzembe uliofanywa na wataalamu wa upasuaji kwa kuacha kitambaa tumboni mwa mama huyo.

Akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji Amir Mruma jana, mama huyo alidai kuwa Januari 6 mwaka 2011 alijifungua kwa upasuaji baada ya hapo hali yake ilizidi kuwa mbaya huku akitokwa usaha ukeni na sehemu ya tumbo kwenye mshono.

Huku akiongozwa na wakili wa kujitegemea Mussa Kwikima, mamahuyo aliiambia mahakama kuwa halihiyo ilifanya apelekwe hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete bila mafanikio ndipo ikamlazimu kwenda Itigi kwa matibabu zaidi.

Katika uchunguzi wa kitaalamu uliofanywa na madaktari bingwa, Haile Sales ambaye ni raia wa Italia pamoja na Anatole Lukonge wa hospitali hiyo ya Itigi, waligundua kuwa kuna kitu tumboni kama uvimbe hivyo wakalazimika kumfanyia upasuaji mwingine.

Baada ya upasuaji huo walikuta kitambaa cha rangi ya kijani ambacho kilikuwa kimeozesha mfuko wa uzazi pamoja na utumbo kugandana na kitambaa hicho ikabidi kitambaa hicho kutolewa na kusababisha kupasuka kwa utumbo ili kumnusuru maisha yake.

Naye daktari bingwa wa magonjwa ya akinamama na ambaye ni mganga mkuu wa hospitali ya Itigi, Anatory Lukonge katika ushahidi wake ameiambia mahakama hiyo kuwa alimpokea mlalamikaji akiwa anatokwa na usaha ukeni na sehemu iliyoshonwa.

Dk Lukonge amebainisha kwamba walipomfanyia upasuaji mama huyo, walikuta utumbo umeshikana na mfuko wa uzazi huku kukiwa na kitambaa kimeng'ang'ania juu yake.

Alisema wakati walipojaribu kukiondoa kitambaa hicho kibofu cha mkojo kilipasuka wakalazimika kumuwekea mpira ili uweze kumsaidia kutolea uchafu.

Kesi hiyo ya madai namba 13/2011 imeahirishwa hadi Agosti tatu mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa kwa upande wa utetezi kuleta mashahidi wake.

MAKINDA AMUONYA NYALANDU

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda amemuonya Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kuwa kitu kimoja na watendaji wake vinginevyo, Wizara itamshinda.


Ushauri huo aliutoa baada ya Bunge kupitisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/15; bila upinzani mkubwa tofauti na ilivyozoeleka. Katika mwaka wa fedha 2013/14, Wizara ya Maliasili na Utalii iliidhinishiwa na Bunge Sh bilioni 83.1.Kati ya hizo, Sh bilioni 68.9 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh bilioni 14.1 kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Makinda alisema tangu ameingia bungeni, wizara hiyo ni tete.

"Tangu nimeingia Bunge wizara hii ni tete. Mimi nilitegemea Nyalandu utafanya mabadiliko na nategemea utafanikiwa," alisema.

"Nendeni mkafanye kazi kwa mujibu wa sheria na sisi tunategemea utalii ni sehemu yetuambayo nchi inaweza kuishi vizuri zaidi bila kuleta vineno neno," aliwaambia watendaji wa wizara hiyo wazidi kushirikiana kwani suala hilo ni la kitaifa si suala la mtu binafsi.

Wakati wa kujadili bajeti ya wizara baadhi ya wabunge, ikiwemo Kambi Rasmi ya Upinzani, walieleza kusikitishwa na kile walichosema ni mvutano baina ya Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ya Maliasili na Utalii."

Hali hiyo inaonesha kuwa kuna mgongano aidha wa kimaslahi…

Waziri na Katibu Mkuu wa wizara moja wanafanya kazi bila kushirikiana na kila mmoja akionekana kumvizia mwenzake hadharani, badala ya kukaa kwa pamoja kutekeleza maazimio ya Bunge," alisema Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa wizara hiyo, Mchungaji Peter Msigwa.

WEREMA AOMBA RADHI

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, jana aliomba radhi Bunge baada ya kutoa kauli, iliyoonesha ubaguzi kwa wabunge kutoka Zanzibar. Kabla ya kuomba radhi, kauli hiyo ilisababisha wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), kutoka nje ya Bunge kuonesha kukerwa na kauli hiyo.

Muda mfupi baadaye, wabunge hao waliungwa mkono na wabunge kutoka Bara, ambao wanatoka Chadema na NCCR Mageuzi, ambaonao walitoka na kuwaacha wabungewa CCM na mbunge wa UDP, John Cheyo.


Awali kabla ya kutoka nje, Mbunge wa Ole, Rajabu Mbarouk (CUF), aliomba muongozo wa Spika akilalamikia kauli ya Werema wakati akimjibu Mbunge wa Mkanyageni, Habibu Mnyaa (CUF).

Werema alimwambia Mnyaa kuwa mambo mengine akaulize Zanzibar na sio katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwa sio kila kitu kitaulizwa ndani ya bunge hilo.

Hoja ilianzia kwa Mnyaa, wakati akiomba Kamati ya Matumizi ya Bunge iliyokaa kupitisha vifungu vya hotuba Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka 2014/15.


Mbunge huyo aliituhumu Wizara ya Katiba na Sheria kuwa ni moja ya Wizara muhimu lakini imekuwa ikivunja sheria na haki za binadamu. Baada ya hoja hiyo, Werema alijibu:

"Alichokizungumza Mnyaa ni sahihilakini hapa sio mahali pake, namshauri kuwa akaulize huko Zanzibar kwenye vikao vyao hapa sisi hatuna majibu."

Mara baada ya Bunge kurejea, Mbunge wa Ole, Rajabu Mbarouk (CUF), aliomba mwongozo wa Spikaakitaka ufafanuzi wa kauli hiyo kwamba ilikuwa ya ubaguzi.


"Mheshimiwa Spika, wakati wa majadiliano na wakati ambapo Mheshimiwa Mnyaa anaongea na kutaka ufafanuzi wa haki za binadamu, huu ni ubaguzi na haupaswi kufanywa na mtu msomi kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali," alisema Mbarouk. Hata hivyo Spika alipinga na kusema;

"hakuna mwongozo wowote kwa kuwa hata wewe umevunja sheria kwani hata nilipokuambia kaa chini, umeendelea kuzungumza, tunaendelea Katibu."

Baada ya kauli ya Spika, wabunge wa Zanzibar walihamasishana na kuamua kutoka nje wote kwa wakati mmoja na kuwaacha wabunge wenzao wa upinzani wakiendelea kuitana na kutafakari cha kufanya.


Spika alifafanua kuwa Mbarouk alikosea kumshutumu Spika hadharani, kwa kuwa kanuni zinaelekeza kama amekosea, malalamiko yapelekwe katika Kamati ya Kanuni.

WATALII TOKA UINGEREZA WATOROKA MOMBASA

Mamia ya watalii kutoka Uingereza waliokuwa kisiwani Mombasa Kenya wamelazimishwa kurejea makwao baada ya serikali ya nchi hiyo kutoa tahadhari ya tishio la mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya.

Kampuni zinazopanga safari za watalii kutoka Uingereza Thomson na First Choice zilifutilia mbali safari zote zilizokuwa zimepangwa kuwaleta watalii Mjini Mombasa hadi mwezi Oktoba zikihofia usalama wao.


Gazeti la The Telegraph linasema kuwa takriban watalii 500 kutoka Uingereza wataathirika na kauli hiyo.

Tahadhari hiyo kutoka kwa serikali ya Uingereza imesema kuwa wanamgambo wa kiislamu kutoka nchi jirani ya Somalia al-Shabab huenda wakafanya mashambulizi nchini Kenya.

Ilani hiyo iliwaonya raiya wote wa Uingereza ambao wako nchini Kenya kwa shughuli ambazo si za dharura waondoke takriban kilomita 60 kutoka kwenye mpaka kati ya kenya na Somalia.

Kampuni ya utalii ya Thomson imewarejesha nyumbani kundi la kwanza la watalii huku waliosalia wakiratibiwa kuondoshwa ijumaa.

Watalii walishauriwa wasizuru kisiwa cha Mombasa huku wakishauriwa kuwa Diani beach na Uwanja wa ndege wa Moi Mombasa ni salama kwao.


Al Shabab

Al-Shabab imeimarisha mashambulizi katika eneo hilo katika siku za hivi punde kundi hilo likisisitiza kuwa linalipiza kisasi vitendo vya majeshi ya Kenya nchini Somalia.

Ilani hiyo ilionya kuwa kuna uwezekano mkubwa wa matukio ya ugaidi na utekaji nyara.

Huku wakionywa kuwa waepuke maeneo ya hadhara ambayo yamejaa watu.

Ndege zinazowarejesha nyumbani watalii hao zimekodishwa na serikali ya Uingereza.


Marekani ,Ufaransa na Australia pia zimeagiza raiya wao walioko pwani ya Kenya kuondoka mara moja.

Mtalii moja Augustine Conall ameiambia shirika la habari la Reuters kuwa jamaa na familia zao wamekuwa wakihofia usalama wao na kuwashauri kurejea Uingereza.


Mwengine Matilda Evanalisema kuwa hamini siku zake 6 za kujivinjari zimekatizwa na makataa hiyoya kuondoka Mombasa.

Mapema mwezi huu watu watatu waliuuawa katika mlipuko uliotokea katika kituocha mabasi ya umma mjini humo.


Mlipuko mwingine umetokea katika mtaa wa kifahari wa Nyali.

Miezi miwili iliyopita polisi mjini humo waliwakamata watu wawili waliokuwa wakiendesha gari lililokuwa limebeba mabomu mawili ya kujitengenezea yenye uwezo wa kubomoa jengo lenye gorofa Kumi.


Polisi walisema kuwa watu hao wawili - mmoja Mkenya na mwingine mwenye asili ya Kisomali - walikuwa wakilenga eneo fulani mjini mhumo.

Hata hivyo hali ya usalama nchini Kenya imekuwa katika hali ya tahadhari tangu kufanywe mashambulizi katika maduka ya Westgate Jijini Nairobi Septemba, mwaka uliopita, ambapo zaidiya watu 67 walifariki.


Kundi la wapiganaji wa Alshabab walidai kuhusika nawakaahidi kuendelea na mashambulizi nchini Kenya hadi pale majeshi ya Kenya itakapoondoka Somalia.

Mwezi februari zaidi ya watu 100 walifikishwa mahakamani mjini Mombasa na kushtakiwa kwa kuwa wanachama wa Al Shabaab baada ya maafisa wa usalama kufanya operesheni katika msikiti mmoja hapo mjini mombasa.