Marekani imeanzisha mfululizo wa
mashambulizi mapya ya anga huko Syria kwa ushirikiano na nchi tano za
Kiaraab zinazounga mkono mapambano dhidi kundi la IS.
Taarifa zinasema kuwa mashambulizi hayo yanalenga mji wa Raqqa ambako ni makao makuu ya wapiganaji hao.
Uingereza imesema kuwa baadhi ya wapiganaji wa kundi hilo wameuawa. Hata hivyo mashambulizi yamelenga mtandao wa Al Qaeda ambao unadaiwa kushirikiana na wapiganaji wa kundi la kiislam ambalo limekuwa likiwalenga raia wa Mgahribi.