MTANDAO MPYA MPINZANI WA FACEBOOK WAANZA KUSHIKA KASI

Mtandao wa kijamii wa Ello unapokea maombi 31,000 ya watumiaji wanaotaka kujiunga kila saa moja hali ambayo inaibua ushindani mkubwa kwa mtandao wa Facebook.

Muanzilishi wa mtandao huo Paul Budnitz ameiambia BBC kuwa wakati mtandao huo unaazishwa ulilenga watu kuhudumia marafiki 90 tu.

Mtandao huu kwa mjibu wa muanzilishi umeanzishwa August mwaka huu ukiwa ambapo hauna gharama yoyote kwa mtumiaji iwe matangazo ama kulipia data.

Hata hivyo baadhi ya watumiaji wameubatiza kwa jina la Anti-Facebook mtandao huo, wakimaanisha kwamba ndiye mpinzani mkubwa wa Facebook.

Baadhi ya wataalam wa masuala ya kimitandao wamekosoa mfumo wa Ello kutotoza gharama yoyote wakidai kuwa katika siku za usoni huenda mtandao wa Ello utalazimika kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa watumiaji wake.

Paul Budnitz mtengenezajiwa baiskel za kampuni ya Vermont ameiambia BBC kuwa wapo imara katika ushindani wa kimitandao na kujigamba kuwa ana wataalamu wa kutosha kukabiliana na makampuni pinzania.

Hata hivyo kuhusiana na baadhi ya watu kuuiita kwa jinala bandia la anti-Facebook mtandao huo yeye amesema wanajiendesha kama mtandao wenye mtazamo wake binafsi na si kutegemea mtazamo wa mtandao wa Facebook.

RAILA ODINGA ACHARAZWA BAKORA

Hali ya taharuki iliibuka katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kwale nchini Kenya, baadaya mwanamume mmoja kwenda ukumbini na kuanza kutandika bakora kiongozi wa upinzani Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine.

Raila alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake waliokuwa wanacheza densi ya kitamaduni kuwatumbuiza wageni, pamoja na gavana wa jimbo la Kwale Pwani ya Kenya Salim Mvuruya katika mkutanmo wa kisiasa.

Walikuwa wameambatana na viongozi wengine, wakiwemo, Seneta Juma Boy, Hassan Omar, Agnes Zani, James Orengo, Johnstone Muthama na wengineo.

Mwanamume huyo alimshambulia Odinga ambaye ni waziri mkuu wazamani na kumchapa mara mbili kabla ya kumgeukia gavana wa jimbo hilo na pia kumchapa mara mbili.

Hata hivyo mwanamume huyo alishindwa nguvu na walinzi wa Raila Odinga.

Polisi walithibitisha kuwa walimkamata mwanamume huyo na kumwachilia baada ya kugundua kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili.

Haijulikani kwa nini mwanammume huyo alimshambulia Raila ila baadhi wanasema ni kwa sababu alighadhabishwa pale waziri mkuu alipocheza densi na mwanamke aliyesemekana kuwa mke wake ambaye alikuwa katika kikundi cha wanawake waliokuwa wanawatumbuiza wageni waheshimiwa.

Viongozi waliofika walilazimika kusitisha densi hiyo kabla ya mwanamume huyo kushindwa nguvu.

OBAMA: TULIKOSEA KUKADILIA NGUVU YA IS

Rais Obama amekiri katika televishen ya kitaifa kuwa Mashirika ya Marekani yalikosea katika kukadiria hatari ya wapiganaji wa dola ya kiislam, Islamic State nchini Iraq na Syria.

Amesema kuwa wapiganaji hao wenye uhusiano na Al Qaeda walitumia fursa ya kutokuwepo serikali thabiti nchini Syria na kuongezewa nguvu zaidi na vijana waliojiunga kupigania jihadi kutoka mataifa mengine.

Hata hivyo Obama amesema wapiganaji hao waliwahi kuvurumishwa huko Iraq na majeshi ya nchi yake yakishirikiana na kabila la Sunni.

Obama amekiri vyombo vya Ujasusi vya Marekani zilikadiria vibaya uwezo wa majeshi ya Iraq kupambana na wapiganajiwa kiislamu ambao wameteka maeneo mengi nchini humo.

MWANAMKE APIGWA MAWE HADI KUFA

Mwanamke mmoja ameuawa kwa kupigwa mawe nchini Somalia na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab.

Ripoti zinasema kuwa takriban watu 200 akiwemo gavana wa eneo hilo walishuhudia watu wakimpiga mawe mwanamke huyo kwenye mji wa Barowe.

Mwanamke huyo wa umri wa miaka 30 alikuwa ameshutumiwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa.

Wadadisi wanasema kuwa mauaji hayo ni ishara ya ushawishi wa kundi la Al shabaab hata baada ya kushambuliwa na serikali ya Somalia pamoja na vikosi vya muungano wa Afrika.

Mji wa Barowe ambao ukoumbali wa kiomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu umekuwa ngome ya Al Shabaab.

WHO: WALIOFARIKI NA EBOLA WAFIKA 3000

Shirika la afya duniani limesema kuwa zaidi ya watu elfu tatu sasa wamedaiwa kufariki kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola katika eneo la Afrika Magharibi kati ya visa elfu sita vya ugonjwa huo vilivyoripotiwa.

Liberia imeathiriwa vibayana ugonjwa huo huku WHO ikisema kuwa kumekuwa na vifo 150 vilivyotokea katika kipindi cha siku mbili pekee.

Idadi hiyo inaweza kupuuzwa kwa kuwa watu wengi wanaogopa kwenda hospitalini.

Hazina ya Fedha duniani IMF imeahidi dola millioni130 kama msaada wa dharura kwa mataifa ya Liberia, Guinea na Sierra Leone.

UINGEREZA KUJIUNGA KUISHAMBULIA IS

Uingereza itajiunga na kampeni ya mashambulizi nchini Iraq baada ya wabunge wengi wa taifa hilo kupiga kura za kuunga mkono mashambulizi ya angani dhidi ya wapiganaji wa Jihad kutoka kwa kundi la Islamic state.

Ndege za kijeshi za Uingereza huenda zikajiunga na kampeni hiyo ya mashambulizi wikendi hii.

Wakati wa mjadala huo wadharura katika bunge,waziri mkuu wa UingerezaDavid Cameron alisema kuwa Uingereza ilifaa kuonyesha subra na uvumilivu badala ya mshtuko na hofu katika kukabiliana na tishio linalosababishwa na wapiganaji wa Islamic State.

Bado hakuna uamuzi wa kuongeza mshambulizi ya kijeshi dhidi ya kundi hilo nchini Syria,lakini muhariri wa BBC anayesimamia maswala yakisiasa amesema kuwa Cameron ameonyesha kuwa yuko tayari kuunga mkono hatua kama hiyo.

WABUNGE WATISHIWA, WAAMBIWA WATAJUTA

JESHI la Polisi mkoani Dodoma linawasaka watu wanaosambaza vipeperushi vya vitisho dhidi ya Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba, watakaoingia bungeni leo ambapo pia watu hao walichora ukuta wa Jengo la Makao Makuu Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Vipeperushi hivyo ambavyo vimesambazwa katika maeneo mengi ya mji, ikiwemo CCM Makao Makuu, maeneo ya Bunge na Uwanja wa Jamhuri, vilikuwa vikisomeka , 'Onyo – Dodoma si mahali pa kufuja wezi wa fedha za umma, utakayeingia bungeni kuanzia kesho (leo), yatakayokupata utajuta.

"Pia, katika Jengo la CCM makao makuu na kwenye ukuta wa Uwanja wa Jamhuri, kuliandikwa maneno kwa rangi nyekundu yaliyokuwa yakisomeka `No Katiba Ufisadi'.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alisema jana alfajiri viliokotwa vipeperushi maeneo mbalimbali mjini Dodoma vyenye ujumbe wa kutishia kuvunjika kwa amani.

Alisema wanaendelea kupokea taarifa za watu wanaodaiwa kuandaa vipeperushi hivyo na wanafanyia kazi ili waweze kuwakamata na kushtakiwa, kulingana na kosa walilolitenda hasa la kutoa vitisho na kuhamasisha uvunjifu wa amani.

"Kila mmoja ajiepushe kujiingiza kwenye kuhamasisha uvunjifu wa amani, kujiingiza katika mikusanyiko isiyo halali na maandamano ambayo yameshapigwa marufuku na Jeshi la Polisi. Atakayekiuka na kujiingiza katika vitendo hivyo vya kiuhalifu atashurutishwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria za Nchi na kwa mamlaka iliyopewa Jeshi la Polisi," alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Dunga Omary alisema ni jambo la ajabu kuona kuwa jengo la CCM linaandikwa maneno kama yale wakati Katiba ni ya Watanzania wote.

"Kwa nini CCM wamelengwa kwani Katiba ni ya watanzania hatupaswi kulaumiwa kwa sababu ya Katiba," alisema na kuongeza kuwa, ushahidi wa mazingira ya kawaida utaona kuwa wale walioshindwa kuandamana wameamua kufanya hivyo na huko ni kufilisika kisiasa.

Kuvamia Polisi Mkoani Mwanza, uongozi wa chama hicho umesema utahakikisha watu wao waliokamatwa na jeshi la polisi, wanatolewa bila masharti, la sivyo watahamasisha wananchi kuvamia kituoni.

Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Chadema mkoani humo, John Nzwalile wakati akizungumzia kujipanga kwao kufanya maandamano nchi nzima.

Alisema maandamano na migomo isiyo na ukomo itaendelea kufanyika ili waweze kufikisha ujumbe wao na kuongeza kuwa, watatumia akili na kudai kuwa maandamano yao yamefanikiwa kwani polisi wameandamana zaidi yao.

Tangu jana asubuhi askari polisi wamekuwa wakionekana katika maeneo mbalimbali na jiji la Mwanza ili kukabiliana na wafuasi wa chama hicho ambao wangeandama katika maeneo mbalimbali na kuishia kwa mkuu wa mkoa.

Hata hivyo, hakukuwa na maandamano huku kwenye lango kuu la kuingia katika ofisi ya mkuu wa mkoa ulinzi ukiwa umeimarishwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana aliliambia gazeti hili kuwa hadi jana majira ya saa 5.30, hakukuwa na kiongozi yeyote wa Chadema aliyekuwa anashikiliwa na jeshi hilo.


Chanzo:Habari lem

HOTEL YA BLUE PEARL YAFUNGWA, YADAIWA TSH MIL 639

KAMPUNI ya Udalali ya Majembe Auction Mart, imeifunga Hoteli ya Blue Pearl ya jijini Dar es Salaam na kutoa vitu vyote nje kwa madai kwamba mmiliki wake anadaiwa kodi Dola za Marekani 380,000 ambazo ni  sawa na Sh milioni 635.9.

Tukio  hilo, limetokea jana ambapo wafanyakazi wa Majembe waliingia hotelini hapo wakiwa na gari la fuso lenye namba za usajili T389 AGG kwa ajili ya kubeba vifaa vyote.

Baadhi ya Wafanyakazi wa majembe Auction Mart wakichukua viti Hoteli ya Blue Pearl
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Saalam jana, Mkurugenzi wa Bule Pearl Hoteli, Rustam Meran alisema ameendesha hoteli hiyo kwa miaka 15, lakini kwa miaka saba aliweza kulipa kodi pango kwa mmiliki wa jengo hilo ambaye ni Ubungo Plaza Investment kwa wakati.

Meran alipewa ruhusa ya kuzungumzia sakata hilo na Wakili wa Hoteli ya Blue Pearl, Joseph Tadayo ambaye aliombwa awali kulizungumzia hilo akasema hawezi kusema wakati mteja wake yupo anaweza kufanya hivyo.

“Miaka saba ya mwanzo nililipa pango kwa wakati,  miaka saba ya mwisho niliomba baadhi ya vyumba ambavyo havijamalizika vimaliziwe kwani vimenisababishia hasara ya Dola za Marekani milioni 3.5.

“Hatukuweza kukubaliana, nilipeleka suala hilo katika Baraza la Usuluhishi, baada ya kusikilizwa nikatakiwa kulipwa kiasi hiki cha fedha, sikuweza kulipwa, kwani Blue Pearl Investment walikata rufaa Mahakama Kuu wakidai kwamba mmoja wa wasuluhishi alikuwa ni mpangaji wangu.

“Uamuzi ule ulibatilishwa, nilibakia na fedha zao kwa sababu sisi tunadai Dola za Marekani milioni 3.5, hata hivyo kabla hatujachukua hatua zozote za kukata rufaa wamekuja kutuondoa bila ya kuwa hata na amri ya mahakama.

“Mpaka sasa tumeshalipa Dola za Marekani 120,000 na tuko tayari kuendelea kuwalipa, huu uharibifu wanaofanya Blue Pearl Investment wanajiharibia mali zao wenyewe,”alidai.


Chanzo: Mtanzania

ASAMOAH GYAN AKANUSHA KUMTOA KAFARA RAFIKI YAKE


Asamoah Gyan
Nahodha wa timu ya taifa ya Ghana, Asamoah Gyan, amekanusha madai kuwa alimtoa kafara rafiki yake ambaye pia alikuwa mwanamuziki mashuhuri nchini Ghana Castro.

Gyan amesema tetesi hizo ni za kushangaza sana wala hazina msingi.

Mwanamuziki huyo aliyekuwa anaiimba nyimbo za mtindo wa Afrobeats, ambaye jina lake halisi ni Theophilus Tagoe, alitoweka pamoja na rafiki yake Janet Bandu, mnamo mwezi Julai.
Wawili hao walitoweka wakati walipokuwa wamekwenda likizo na Gyan ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Sunderland, katika mji wa Ada.

Madai katika vyombo vya habari nchini Ghana yanasema kuwa kutoweka kwa rafiki ya Gyan kumezua wasiwasi baadhi wakidai kuwa huenda alimtoa kafara mwanamuziki huyo.
Castro na rafiki yake Bandu, walionekana kwa mara ya mwisho wakielekea baharini na baadaye iliarifiwa kuwa walizama.

Miili ya wawili hao haikuwahi kupatikana na madai yaliendelea kusambazwa mwezi huu wakati ambapo kakake Gyan, Baffour Gyan alidaiwa kuwa mmoja wa genge la vijana waliowashambulia wandishi wa habari waliohoji maswali kuhusu madai hayo.

Hata hivyo baadaye aliachiliwa na polisi waliokuwa wamemkata kwa lengo la kumfungulia mashitaka.

Tetesi hizo zilimfanya Gyan kuitisha mkutano na wandishi wa habari kuzungumzia madai hayo.
Wakili wake Kissi Agbyabeng alitoa taarifa akisema kuwa familia ya Gyan imeshangazwa sana na madai hayo na iliamua kutosema chochote ili polisi waendelee na uchunguzi wao.

Taarifa hiyo ilisema: " Tumekuwa kimya huku madai na tetesi zikienezwa kila upande katika vyombo vya habari. Tumekuwa kimya sio eti kwa sababu tunaficha ukweli, bali kwa sababu hatuoni umuhimu wa kusema kilichojiri mjini Ada. Tumekuwa kimya kwa sababu tunataka polisi wafanye kazi yao bila kuingiliwa.''

WAFUASI WA BOKO HARAM WAJISALIMISHA

Jeshi nchini Nigeria limesema zaidi ya wafuasi 260 wa Boko Haram wamejisalimisha Kaskazini mwa nchi hiyo.

Jeshi hilo limesema katika mapambano limemuua mtu mmoja ambaye huwa anaonekana kwenye picha za video za propaganda za Boko haram akijidai kuwa Kiongozi wa wa kundi hilo, Abubakar Shekau.

Jeshi lilisema kuwa wapiganaji 135 walijisalimisha wakiwa na silaha zao katika eneo la Biu , jimbo la Borno siku ya Jumanne. Liliongeza kuwa wengine 133 walijisalimisha Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Hata hivyo mwandishi wa BBC mjini Lagos Will Ross anasema kuwa ni vigumu kuthibitisha madai hayo ya jeshi.

Mwaka jana jeshi lilisema kuwa Shekau huenda aliuawa , lakini halikutoa thibitisho lolote.
Hata hivyo ikiwa ni kweli kuwa wapiganaji hao wamejisalisha basi huenda ni ushindi kwa jeshi la Nigeria katika vita vyake dhidi ya Boko Haram.

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kuwa majuma ya hivi karibuni Boko Haram imeshindwa kwa kiasi kikubwa wakati walipokuwa wakipambana kudhibiti eneo karibu na mji wa Maiduguri ambalo ni ngome yake.

Jeshi limesema wafuasi 135 wa Boko Haram wamejisalimisha wakiwa na silaha zao katika majimbo ya Biu na Borno,halikadhalika wafuasi wengine 133 wanahojiwa.

Kwingineko , Rais wa Nigeria,Goodluck Jonathan amesema kuwa zaidi ya watu 13,000 waliuawa katika miaka mitano ya kwanza ya harakati za Boko Haram nchini humo.
Rais Jonathan alisema hayo katika hotuba yake katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York siku ya Jumatano.

Rais Jonathan pia alisisitiza kuwa juhudi zinafanywa kuwaokoa wasichana wa Chibok.

MKE WA OSAMA BIN LADEN AFUNGWA MAISHA

Mkwe wa aliyekuwa kiongozi wa al-Qaeda , Osama bin-Laden amehukumiwa kifungo cha maisha na mahakama moja mjini New York. Alikuwa anakabiliwa na mashitaka ya ugaidi.

Jaji wa mahakama hiyo amemwambia Suleiman Abu Ghaith kuwa alionekana kuwa na nia na tayari kutekeleza ajenda ya mauaji kwa niaba ya al-Qaeda'Suleiman Abu Ghaith mwenye umri wa miaka 48, alifanywa kuwa msemaji wa Al Qaeeda baada ya shambulizi la 9/11 na anasemekana kuwa afisaa wa ngazi ya juu wa Al Qaeeda kufikishwa mahakamani Marekani tangu kutokea kwa mashambulizi hayo.

Alikamatwa nchini Jordan mwaka jana na kupelekwa Marekani alikokabiliwa na mashitaka hayo.

Pia alitetea kazi yake akisemani jukumu lake la kudini kuwaambia waisilamu wapambane na maadui wao

Mnamo mwezi Machi, jopola majaji wa kiraia lilimpata na hatia ya njama ya kuwaua wamarekani pamoja na kulisaidia kundi la al-Qaeda.

Kanda za video zinazomuonyesha Abu Ghaith akitoa vitisho dhidiya Marekani akisema analenga kuangamiza Marekani kwa kutumia ndege zilionyeshwa kwa majaji hao.

Abu Ghaith alisema kuwa jukumu lake ni la kidini kwani alikuwa akiwaaasa waisilamu kupambana na maadui wanao wakandamiza.

IFM YATOA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGUWA KUJIUNGA NA NAFASI SHAHADA(DEGREE) KWA MWAKA 2014/2015

Bofya hapa chini kuangalia majina ya wanafunzi waliochaguliwa.

Bofya Hapa kuangalia Majina ya waliochaguliwa

Chuo cha usimamizi wa fedha(IFM) Kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shahada(Bachelor degree) katika kozi tofauti zinazotolewa na chuo hicho, Kwa wanafunzi watakao ona majina yao wanatakiwa kufika chuo kwa ajili ya usajili na na orientation  kuanza tarehe 6 mpaka 10 October ra taribaya masomo kuanza 13 oktoba. Hivo wanatakiwa kuwahi kufanya usajili.

AMCHINJA MKEWE MBELE YA WANAE

POLISI mkoani Katavi wanamsaka mkazi wa kijiji cha Urwila wilayani Mlele, Mohamedi Katyukuru (49) kwa kumuua mkewe kwa kumchinja.

Inadaiwa mwanaume huyo alifanyamauaji hayo Septemba 14 mwaka huu wakati watoto wao wawili, wenye umri wa kati ya miaka 11 na14, wakishuhudia.

Inadaiwa baada ya mauaji hayo, alitoroka pamoja na watoto hao na kujificha kusikojulikana.

Alifunga mlango kwa nje na kufanya majirani wachukulie kwamba ametoka kwenda kwenye shughuli zake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alimtaja aliyeuawa kuwa ni Bernadeta Mwetel (38), ambaye mumewe alikuwa akimtuhumu kuwa na uhusiano na mwanamume mwingine.


Chanzo: Habari leo

BUNGE LAPITISHA UPIGAJI KUWA KWA FAX, EMAIL

Bunge la Katiba limeingia katika historia baada ya kupitisha kanuni zinazoruhusu wajumbe wake watakaokuwa nje ya nchi kupiga kura kwa njia ya nukushi (fax) na baruapepe (email).

Uamuzi huo ulifikiwa bungeni Mjini Dodoma, baada ya wajumbe wa Bunge hilo kupitisha azimio la kuzifanyia marekebisho kanuni ya 30, 36 na 38 za Bunge hilo za mwaka 2014.
Hata hivyo, wajumbe watatu kati ya 15 waliochangia azimio hilo, walipinga vikali marekebisho hayo, lakini yalipitishwa kwa wingi wa kura baada ya Mwenyekiti, Samuel Sitta kulihoji Bunge.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa raia wa Tanzania kupiga kura akiwa nje ya nchi, uamuzi ambao Sitta aliutetea akisema wanaoupinga wanachanganya kati ya kura ya uamuzi na kura ya uchaguzi.
Mwakilishi wa walimu, Ezekiah Oluoch alisema Kifungu cha 16 (6) cha Kanuni za Bunge kinamtaka mwenyekiti kuendesha Bunge kwa mujibu wa sheria walizonazo, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na sheria nyingine za nchi.
“Hoja ya walioko nje ya Bunge hili kupiga kura, siiungi mkono na wengi mkiunga mkono mtakuwa mmekiuka sheria ... kila raia ana haki ya kupiga, Katiba yetu inaeleza, ilimradi atimize miaka 18 lakini haki hiyo imewekewa pia utaratibu wa kisheria,” alisema.
Alisema kwa taratibu zilizowekwa nchini, hakuna unaomruhusu mtu aliyeko nje ya eneo la kupiga kura kufanya hivyo.
Hata hivyo, Sitta aliingilia kati akisema mjumbe anasema uongo, akimtaka aeleze ni kura ipi anayoizungumzia na kifungu gani kimesema hilo, naye akajibu kura anazozungumzia ni zote ikiwamo ya kufanya uamuzi ndani ya Bunge.
“Unasema uongo mtupu wewe ... sheria ya uchaguzi, tunamchagua nani hapa?” alihamaki Sitta na hali kama hiyo aliionyesha pia kwa wajumbe wengine waliokuwa wakipinga marekebisho hayo.
Oluoch alisema anachoona ni kuwa si halali kwa mjumbe ambaye hayuko ndani ya Bunge kupiga kura na kutaka Bunge lisifanye mambo kwa sababu linataka kutimiza mambo ambayo si msingi wa sheria.
“Uamuzi wowote huo tunaotaka kufanya kwa lengo la kupata utashi wa kisiasa, mimi nitasimama peke yangu kukataa na itaingia kwenye hansard (kumbukumbu za Bunge) kwamba nilikataa jambo hili,” alisema.
Kwa upande wake, Said Arfi alisema hakubaliani na azimio hilo kwa sababu Kanuni ya 38 ilikuwa imeshaweka utaratibu na haoni kuwapo haja ya kufanya marekebisho.

“Jambo hili tunalofanya ni kubwa sana, kuandika Katiba ya Taifa letu ni lazima tuwe na nia zilizokuwa njema ili kulipatia Taifa Katiba ambayo itaridhiwa na Watanzania. Sioni sababu zozote za msingi kwa wajumbe ambao hawapo humu ndani kupiga kura.”
Arfi alisema uzoefu wa mabunge mengi duniani wanaopiga kura ni watu waliomo ndani ya ukumbi wa Bunge tu... “Sasa hii ya kwenda kuwatafuta watu huko waliko hauna uhakika anayepiga kura ndiye, ni shaka tupu. Kwa kweli mheshimiwa mwenyekiti Watanzania watatutazama juu ya nia zetu na dhamira zetu juu ya kulipatia Taifa Katiba maridhawa,” alisema.
Alisema kura ni hiari na mjumbe anaweza kuwapo ndani ya Ukumbi wa Bunge na kuacha kupiga kura na kuonya kuwa kuwalazimisha na kuwatafuta watu ili wapige kura si jambo la kidemokrasia.
Wakati akiendelea, Sitta aliingilia kati na kumhoji nani anayelazimisha mtu kupiga kura? Arfi akamjibu;
“Unapotuingilia katika michango yetu Watanzania wanakupima. Watanzania wanakuheshimu mwenyekiti.”
Kwa upande wake, Ali Omary Juma alisema Katiba ni maridhiano ya nchi mbili huru na si busara kuharakisha kupiga kura kwa watu ambao hawamo ndani ya Bunge.
Alisema kama hilo litaruhusiwa itakuwa ni mgongano mkubwa wa kisheria ambao utaleta ufa mkubwa kama uliojitokeza baina yao na Ukawa … “Nashauri suala la kura tulisitishe ili kutoa fursa pana ya mashauriano na kutoa muda ili wajumbe wote tuhudhurie.”
Mjumbe Paul Makonda aliunga mkono hoja hiyo akisema wajumbe zaidi 600 kuwa mahali pamoja si jambo rahisi:
“Nakumbuka tukiwa kwenye kamati yetu siku moja mtu alilazimika kutoka hospitalini. Ni mgonjwa lakini afanyeje, lakini kama kuna uhuru wa kupiga kura pale alipolala ni jambo la heri.
“Hatutafuti kura mpya. Hapa tunatafuta kupiga kura kwa wale watu ambao walishajadili jambo hili, haina maana tunatafuta kuokotaokota kama tumepungukiwa, hatujapungukiwa hata kidogo.”
Baadaye Sitta alisimama na kusema ipo dhana inayojengeka kwamba utaratibu huo unalenga kulazimisha kila mjumbe kupiga kura ili tu theluthi mbili ipatikane, hivyo akataka wajumbe waache kupoteza muda ... “Hii ni dhana ya ajabu na ina nia mbaya ndani yake. Mmoja wa watu ambao ameomba apige kura yuko hospitali India, nina mamlaka gani ya kumkatalia?”
“Tumempigia Balozi atamwapisha atapiga kura ya siri italetwa na itafunguliwa humu. Zote hizo zitafunguliwa humuhumu ndani ya ukumbi na majina yatasomwa,” alisema Sitta.


Chanzo: Mwananchi

WASIRA: URAIS SI MAMA MKWE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wasira amesema hana sababu ya kuona haya kutangaza kuutaka urais kwa kuwa urais si ukwe ila anasubiri wakati mwafaka.
Wasira alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipokuwa akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili mjini Dodoma.

“Watakaposema ruksa, nitasema na wala kugombea urais si suala la kuonea haya.
Ni kutoa huduma kwa Watanzania. Unalionea haya la nini? Kwani kugombea urais ni ukwe?” alihoji Wasira na kuendelea;
“Urais ni mama mkwe wako, hapana. Wakati ukifika nitasema tu. Na mradi kuna wananchi wanasemasema na wananitia moyo, ukifika wakati nitasema.”
Hata hivyo, waziri huyo ameonya kuwa endapo urais utachezewa kwa kuingia mtu ambaye si mwadilifu, biashara atakayoifanya Ikulu itakuwa ni kuuza haki za watu.

Alisema hawezi kufahamu nani atashinda katika kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani, lakini lazima rais awe mtu mwenye sifa za kushika nafasi hiyo.

“Mimi siwezi kufahamu ni nani ataongoza Tanzania, lakini ninaweza kusema sifa.”
Alisema Wassira na kutaja sifa hizo kuwa ni pamoja na kuwa Mtanzania kwa sababu haiwezekani kuagiza mtu kutoka nje ya nchi kuja kuwania nafasi hiyo.

Aliongeza; “Rais pia anatakiwa kuwa mzalendo anayeipenda nchi yake na adhihirishe mapenzi yake, awe na uwezo wa kuongoza na pia ame-prove (amedhihirisha) uwezo wake huo wa kuongoza.”
Sifa nyingine ya urais, aliitaja kuwa ni mgombea kuwa mtu aliyewahi kuongoza taasisi nyingine na kuwaridhisha Watanzania kuwa aliongoza vizuri.

“Lakini pia rais lazima awe mwadilifu maana unalinda haki za watu. Baba wa Taifa aliwahi kusema Ikulu kuna biashara gani, lakini kuna biashara ya nguvu tu.
Unaweza kuuza haki za hao watu,” alisema na kuongeza;

“Maana chakuuza pale hakuna. Mimi nafanya pale. Mimi naona watu wanamwagilia maua tu lakini kuna power (nguvu), kama wewe unapenda hela zaidi kuliko watu waliokuweka pale basi wewe utakuwa kazi yako ni kuuza haki zao.”

Alisema sifa hizo ni za msingi na wala si ngumu na kama mtu hana, hana tu.
Alipoulizwa katika sifa hizo anazozielewa yeye anajipimaje, alijibu, “Mimi siwezi kujipima. Nitajipimaje? Mimi nitapimwa na watu wengine”.

“Lakini kama wananitaja habari ya urais, wananisema na mimi nawashukuru wanaonisema. Kumbe na mimi ninaweza kupimwa na Watanzania,” alisema.

Waziri huyo ambaye pia ni mbunge wa Bunda alisema kwa sababu Watanzania wanasema na yeye ni miongoni mwa watu wenye nia ya kuwania urais, labda wanapima kwa sifa hizo.
Alisema chama chake kina utaratibu wa kufuata endapo mwanachama anataka kuwania nafasi ya uongozi.


Chanzo: Mwananchi.

MSIKITI WA MASHOGA WAFUNGWA CAPE TOWN

Taj Hargey amekataa kwenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu.
Muasisi wa msikiti wa Open Mosque, Taj Hargey ambaye amekataa kwenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu.

Msikiti wa kwanza wa mashoga wa nchini Afrika Kusini, ambao unaruhusu wanawake wkuongoza ibada, umefungwa kwa muda usiojulikana, afisa wa hapo aliiambia BBC.


Diwani wa Mji wa Cape Town amesema msikiti huo mpya unaoitwa Open Mosque umevunja sheria za manispaa kwa kutokuwa na sehemu za kuegesha magari.

Msikiti huo ulifungua milango yake rasmi siku ya Ijumaa pamoja na ukosoaji kutoka kwa wanachama wa jumuiya ya Waislamu wa eneo hilo.

Muasisi Taj Hargey aliseme msikiti huo ungesaidia kupambana na imani kali ya kimapinduzi.
“Tunafungua msikiti huu kwa watu wenye mawazo huru, na sio waliofungwa mawazo,” alisema wakati wa ufunguzi.

Diwani wa Jiji Ganief Hendricks alikataa kuwa kufungwa kwa msikiti ni sehemu ya kuwanyanyasa watu wenye mawazo yanayopingana na wengi.

MASHAMBULIZI ZIDI DHIDI YA IS


Marekani imeanzisha mfululizo wa mashambulizi mapya ya anga huko Syria kwa ushirikiano na nchi tano za Kiaraab zinazounga mkono mapambano dhidi kundi la IS.

Kamanda wa Marekani anasema tayari wamefanikiwa kuangamiza kituo cha mafunzo cha wapiganaji wa dola ya Kiislam,vifaa na magari yao huko kaskazini na Mashariki mwa Syria.

Taarifa zinasema kuwa mashambulizi hayo yanalenga mji wa Raqqa ambako ni makao makuu ya wapiganaji hao.

Uingereza imesema kuwa baadhi ya wapiganaji wa kundi hilo wameuawa. Hata hivyo mashambulizi yamelenga mtandao wa Al Qaeda ambao unadaiwa kushirikiana na wapiganaji wa kundi la kiislam ambalo limekuwa likiwalenga raia wa Mgahribi.

PSI YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA WANAOSAMBAZA KONDOMU MKOA KATAVI


Na khalfani Zozi:

Mwenyekiti wa wafanya biashara Mkoa wa Katavi akifungua kikao.
Jamii wilayani Mpanda mkoani Katavi imetakiwa kuwa na mazoea ya kutumia kondomu ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi,mimba zisizotarajiwa sanjari na magonjwa mengine ya zinaa.
Mhamasishaji mkuu wa shirika la PSI Tanzania Kanda ya nyanda za juu kusini Elia Jackson Ndutila.
Mhamasishaji mkuu wa shirika la PSI Tanzania Kanda ya nyanda za juu kusini Elia Jackson Ndutila.
Kauli hiyo imetolewa na muhamasishaji mkuu wa kampuni ya PSI kanda ya nyanda za kusini Jackson Ndutila wakati akizungumza na wasambazaji na wauzaji wa kondomu Mkoani Katavi.

Aidha amesema kuwa jamii isitishike na kuwepo kwa aina nyingi za kondomu kwani zote zina ubora sawa.
Meneja wa Shirika la PSI Tanzania Kanda ya Mbeya,Rukwa na Katavi Bw.Edgar Mchaki.
Naye meneja wa PSI Mbeya, Rukwa na Katavi Edgar Mchaki ameongeza kuwa wananchi mkoani humu wanatakiwa kutumia kondomu ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI ambapo imefikia asilimia 5.9 ukilinganisha na asilimia 5.1 kitaifa.
Mganga Mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Mpanda Dk.Leonce L.K. Mutajwaha.
Mganga Mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Mpanda Dk.Leonce L.K. Mutajwaha.
Kwa upande wake mganga mkuu wa Halimashauri ya mji wa Mpanda Dokta Leonce Mutajwaha amesema kuwa ni wakati wa kila mmoja kuwa mwaminifu kwa mwenza wake ili  kupunguza maambukizi holela ya VVU.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauli ya Mji wa Mpanda Bw.Brian Severe akisoma Risala kwa niaba ya mgeni Rasimi mbele ya wadau wa PSI.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauli ya Mji wa Mpanda Bw.Brian Severe alisema kuwa mchango wa PSI Tanzania umejidhihirisha wazi kutokana na wigo mpana walionao wa usambazaji wa bidhaa za kiafya kwa ajili ya huduma za uzazi wa mpango, kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI, kujikinga na malaria, kujikinga na magonjwa yanayosababishwa na maji ambayo si salama kwa matumizi ya binadamu, na bidhaa za uzazi wa mpango na uzazi salama kwa akina mama.

Aidha amezitaja bidhaa hizo ikiwa ni pamoja na kondomu za kiume(salama na dume kondomu) water guard, kondomu za wanawake(lady pepeta), vidonge vya uzazi wa mpango, vipandikizi, pamoja na lupu au vitanzi.

Mratibu wa UKIMWI Halmashauli ya Mji wa Mpanda Bi.Mary Byaro akitoa ufafanuzi juu ya kondomu za kike.


Wadau wa bidhaa zinazo sambazwa na PSI Tanzania wakiuliza maswali juu ya matumizi ya kondomu.

Wadau wa bidhaa zinazo sambazwa na PSI Tanzania wakiuliza maswali juu ya matumizi ya kondomu.

Wakala Mkuu wa bidhaa zinazosambazwa na PSI Tanzania akitoa shukulani kwa wadau na wageni waalikwa.

ANUSURIKA MIAKA 30 JELA, AHUKUMIWA VIBOKO

KIJANA wa kiume mwenye umri wa miaka 17, mkazi wa Kijiji cha Karundi wilayani Nkasi katika Mkoawa Rukwa, amenusurika kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka nakumpatia ujauzito msichana mwenye umri wa miaka 16.

Msichana huyo aliyekuwa akisoma darasa la saba alishindwa kufanya mtihani wa Taifa wa kumaliza elimu ya msingi uliofanyika Septemba 10 na 11, mwaka huu.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Nkasi, Ramadhani Rugemalira alisema mshitakiwa mwenyewe baada ya kukiri kutenda kosa hilo, Mahakama hiyo imemtia hatiani chini ya kifungu cha 130 (1) na (2)(e) na 131 (1) cha kanuni ya adhabu Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Rugemalira aliieleza mahakama hiyo kuwa katika kosa la kwanza la kulawiti, mshitakiwa amehukumiwa kucharazwa viboko 12, na kwa kosa la pili la kumpa ujauzito mwanafunzi huyo atachapwa viboko vinane.

Awali Mwendesha Mashitaka, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Hamimu Gwelo alidai mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mwaka huu.

Alisema baada ya mwanafunzi huyo kukutwa na ujauzito, mshitakiwa alikamatwa na kufikishwa katika mahakama hiyo kwa kuvunja sheria chini ya kifungucha 130 (1) na (2) (e) na 131 (1) chakanuni ya adhabu Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Aliiomba mahakama hiyo iweze kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo hasa baada ya vitendo hivyo vya ubakaji na kumsababishia ujauzito mwanafunzi ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kufanya vitendo hivyo viovu.

Chanzo: Habari Leo

POLISI KUCHUNGUZA LUGHA ZA KIBAGUZI DHIDI YA BALOTELLI

(Picha: Tweets za kibaguzi dhidi ya Balotelli)

Mario Balotelli alipokea ujumbe wa kibaguzi baada ya kutuma ujumbe kwenye Twitter kwenye mechi ya Man United iliyofungwa 5-3 na Leicester siku ya Jumapili.
Raia huyo wa Italia alipokea udhalilishaji huo baada ya kutuma ujumbe 'Man Utd…LOL'wakati wa kipigo cha kushtukiza kutoka Leicester siku ya Jumapili.
Nyota huyo, 24, alijibiwa zaidi ya mara 150,000 na kukutana na mfululizo wa wabaguzi na jumbe za matusi.
Baadhi ya akaunti zilizotuma jumbe za matusi zimeshafungiwa.
Polisi wanasema kwanza watahitaji kumjua nani alituma jumbe hizo na kujua alitoka wapi.
Kundi linalopambana na ubaguzi la Kick It Out lilisema watumiaji wa mitandao ya kijamii walitahadharisha hili kwa jumbe ya kibaguzi iliyotumwa kwa mchezaji wa zamani wa Manchester City.
"Tunaendelea kutoa msaada wetu kwa Mario Balotelli baadaya udhalilishaji wa kibaguzi kuelekezwa kwake," alisema msemaji.





WAHUKUMIWA VIBOKO 91 KWA KUCHEZA WIMBO WA PHARREL 'HAPPY'

Watu sita nchini Iran waliokamatwa baada ya kuonekana kwenye kanda ya video iliyokuwa inaiga wimbo wa 'Happy' wake mwanamuziki mashuhuri Pharrell William, wamehukumiwa kifungo cha hadi mwaka mmoja jela kila mmoja pamoja na adhabu ya kuchapwa mijeledi 91.

Wakili wa sita hao amesema kuwa hukumu hiyo itaahirishwa kwa miezi sita ikmaanisha kuwa watafungwa tu jela ikiwa watarejelea kosa hilo.

Kanda hiyo inaonyesha wanaume watatu na wanawake watatu ambao hawajafunika vichwa vyao wakicheza densi kwenye barabara na katika paa za nyumba mjini Tehran.

Kanda hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, imetazamwa na zaidi ya watu milioni moja.

Wengi wa waliohusika kuitengeza kanda hiyo, walifungwa kwa miezi sita, huku mmoja wao akifungwa kwa mwaka mmoja, alinukuliwa akisema wakili wao Farshid Rofugaran.

Mmoja wa watu waliokamatwa kwa kucheza densiKanda hiyo kwa jina,"Happy we are from Tehran" ilifikishwa kwa maafisa wakuu nchini Iran mwezi Mei baada ya kutazamwa na watu 150,000 kwenye You Tube.

Waliohusika pia walikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kukiuka sheria za kiisilamu ambazo zinawazuia wanaume kucheza densi na wanawake na pia wanawake kutoka nje bila hijab.

Baadaye washukiwa walionekana kwenye televisheni wakijitetea kwamba wao ni waigizaji walihadaiwa kushiriki katika kanda hiyo Kukamatwa kwa vijana hao kulizia ghadhabu kutoka anga za kimataifa huku watetezi wa haki za binadamu wakianzisha kampeinii kwenye mitandao ya kijamii kutaka waachiliwe.

Mwanamuziki Pharrel Williams mwenyewe, ambaye wimbo wake huo, uliteuliwa kwa tuzo la Oscar, pia alieleza kukerwa na kukamatwa kwa watu hao.

"Inachukiza kwamba vijana waliokuwa tu wakijaribu kujifurahisha wanakamatwa,'' aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

POLISI WATEMBEZA KICHAPO KWA WAANDISHI WA HABARI


Siku moja baada ya makamu wa rais dkt mohamed ghalib bila kuhimiza mahusiano mema wakati wa utendaji kazi baina ya vyombo vya ulinzi na usalama na vyombo vya habari jeshi la polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa limekiuka kauli hiyo kwa kuwapiga na kuwajeruhi baadhi ya waandishi wa habari na kuwazuia kutekeleza wajibu wao wakati mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema alipowasili katika makao makuu ya jeshi hilo kwa mahojiano.
Kauli hiyo ya makamu wa rais imeshindwa kutekelezwa kutokana na tukio lililotokea majira ya saa 5 na dk 15 asubuhi wkati mwenyekiti wa chadema taifa Mhe. Freeman Mbowe alipowasili makao makuu na askari wa polisi kutaka kuzuia gari alilopanda kuingia ndani ya lango kuu pamoja na waandishi wa habari na watu wengine kuamriwa kuondoka katika eneo hilo agizo lililopingwa na waandishi wa habari na baadhi ya wanasheria wa Chadema.Kufuatia na kutolewa kwa ilani hiyo jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia-FFU- kilianza kupiga waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wananchi huku wengine wakikimbia kuhofu vipigo toka kwa askari hao ambapo baaadhi ya waandishi walioumizwa sehemu mbalimbali ya mihili yao.Akiwatangazia wafuasi waliokuwa wakikataa kuondoka katika maeneo hayo mwanasheria wa chadema mhe. Tundu lissu licha ya kuwahakikishia kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa Mhe. Freeman Mbowe yuko salama amewataka kuondoka katika eneo hilo na kurudi majumbani ili kuepusha vurugu na misongamano ambayo ingeweza kusababisha matatizo zaidi.Aidha imeshuhudia mwenyekiti wa Chadema taifa Mhe Freeman Mbowe akitoka makao makuu ya jeshi la polisi akisindikizwa na ulizni mkali wa jeshi la polisi kuelekea katika ofisi za makao makuu ya chama hicho baada ya kukamilika kwa taratibu za kipolisi.



MAJAMBAZI WAMPORA KADINALI JIJINI RIO

Watu waliokuwa wamejihami wamemuibia Askofu mkuu wa Rio de Janeiro nchini Brazil msalaba wake na pete Kadinali, Dom Orani Tempesta, alikuwa njiani kuelekea kuhudhuria mkutano mjini alipovamiwa na majambazi hao.

Mmoja wa majambazi aliyekuwa na bunduki katika kanisa, alimfahamu kadinali huyo na kumuomba msamaha.

Hata hivyo, hilo halikushutua genge hilo ambalo liliendleea kumpora kadinali huyo, na hata nusura wampore gari lake.

Vitu vilivyoibwa vilipatikana baadaye.

Hakuna aliyejeruhiwa kwenye tukio hilo, ambalo lilifanyiika Jumatatu jioni katika mtaa wa Santa Teresa.

Mwandishi wa BBC Gary Duffy, anasema kuwa visa vya wizi hutokea mara kwa mara katika mtaa huo wenye shughuli nyingi za kitalii na kwamba visa hivyo vimekuwa vikiongezeka sana mwaka huu.

Mwanafunzi wa dini pamoja na mpiga picha mmoja waliokuwa kwenye gari na kadinali huyo pia waliporwa.

Licha ya tukio hilo, kadinali aliendelea na shughuli zake huku mwanafunzi na mpiga picha wakienda kuripoti kwa polisi.

Pete ya kadinali na msalaba, vilipatikana pamoja na simu yake ya mkononi Hata hivyo, vifaa vya mpiga picha havijapatikana.

Dom Orani Tempesta alitawazwa kama kadinalina Papa Francis mapema mwaka huu.

HATMA YA SCOTLAND KUJULIKANA LEO

Wapiga kura wamekuwa wakielekea kwa vituo vya kupigia kura katika maeneo mbali mbali nchini Scotland, ambapo watu wanaamua leo ikiwa wataendela kuwa sehemu ya uingereza au wawe taifa huru kwa mara ya kwanza kabisa tangu zaidi ya miaka 300 iliyopita.

Mwandishi wa bbc anasema kuwa siku ya leo inatarajiwa kuwa ya shughuli nyingi katika historia ya kupiga kura eneo la Scotland ikiwa asilimai 97 ya watu wamejisajili kupiga kura.

Kumekuwa na kampeni kali katika saa 24 zilizopita huku ikidhihirika matokeo yanaweza kwenda upande wowote.

Kiongozi wa chama cha Scotish National Party, Alex Salmond, ametaja kampeni ya kuitisha Uhuru wa Scotland kutoka kwa Uingereza kama tukio muhimu zaidila kidemokrasia kuwahi kutendeka nchini humo.

Kadhalika amesema tayari limebadilisha mfumo wa maisha eneo la Scotland.

Idadi kubwa ya wapiga kura wamesajiliwa na kwa mara ya kwanza vijana wenye umri wa miaka 16 na 17 wataruhusiwa kupiga kura.

POLISI WA DORIA WAPIGWA BOMU

SIKU chache baada ya majambazi kuvamia Kituo Kikuu cha Polisi wilayani Bukombe mkoani Geita, kuua askari wawili na kuiba silaha za moto, watu wasiofahamika wamewajeruhi askari watatu waliokuwa doria kwa kuwarushia kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu.

Askari hao kwa sasa wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea wakitibiwa majeraha.

Tukio hilo limeripotiwa kutokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa moja na nusu jioni katika kata ya Msufini karibu na daraja la Matarawe, wilayani Songea.

Mkurugenzi wa Upepelezi na Makosa ya Jinai (DCI), Issaya Mngulu amethibitisha kwa njia ya simu kutokea kwa tukio hilo, ingawa alishindwa kuingia kwa undani akisema alikuwa njiani kwenda eneo la tukio akitokea mkoani Mbeya.

Hata hivyo, gazeti hili limeweza kubaini waliojeruhiwa kuwa ni WP. 10399 PC Felista aliyejeruhiwa mguu wa kulia kwenye unyayo na pajani, G 7351 PC Ramadhani aliyejeruhiwa mguu wa kulia karibu na goti na tumboni upande wa kulia na G. 5515 PC John aliyepata majeraha katika mguu wakulia chini ya goti na jeraha dogo tumboni.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk Daniel Malekela, akizungumzia tuki hilo alikiri kupokea majeruhi na kueleza kuwa ametoa vipande vya bati na misumari katika majeraha ya askari hao na mpaka sasa wanaendelea na matibabu.

Habari zaidi zinasema jeshi la polisi mkoani humo kwa kushirikiana na maofisa wengine kutoka makao makuu ya jeshi, wanaendelea na uchunguzi ikiwa nipamoja na kujua chanzo cha tukio hilo.

Bomu hilo la kutupwa kwa mkono inasadikiwa limetengenezwa kienyeji.

Kutokana na tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Saidi Mwambungu ameelezea kusikitishwa na kitendo hicho cha wahalifu kujeruhi askari kwa makusudi na amesema Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi nausalama itahakikisha wanawasaka na kuwakamata.


Chanzo: Habari leo

AUWAWA NA MWILI KUTUPWA KISIMANI

MWANAKIJIJI cha Itenka Tarafa ya Nsimbo wilayani Mlele Katavi, Mary Magese (39) ameuwawa na mwili wake kutupwa katika kisima cha maji.

Mauaji hayo yalifanyika Septemba 14 mwaka huu saa mbili usiku kijijini hapo baada ya marehemu kumaliza kula chakula cha usiku akiwa na mume wake Lazaro Maziku (40).

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema wanandoa hao walipomaliza kula mume alikwenda bafuni kuoga.

Aliporudi hakumkuta mkewe hivyo alianza kumtafuta bila mafanikio ndipo alipokwenda kwa majirani na ndugu zake pia hakumpata.

Alisema siku iliyofuata saa mbili asubuhi zililizagaa taarifa ya kuwpeo kwa maiti kisimani ndipo uongozi wa kijiji ulipokwenda na kuukuta mwili wa mke wa Maziku Kidavashari alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kati ya Maziku na Shija Joseph aliyetuhumiwa kuwa hawara wa marehemu kwa muda mrefu.

Alisema jeshi la polisi linamshikilia mume wa marehemu kuhusiana na kifo hicho kwa mahijiano zaidi na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kumekamilika.

Chanzo:Tz Daima

WANANCHI MPANDA WAGOMA KUPANDA BUS

KITUO Kikuu cha Mabasi mjini Mpanda, mkoani Katavi kilikumbwa na tafrani jana baada ya abiria kugoma kusafiri na mabasi mawili baada ya kubaini matairi yake yamechakaa.

Abiria hao waligomea kusafiri kwa mabasi ya abiria mali ya Kampuni ya AM Drama, yenye namba za usajili T740 AQD na T 468 AGC na kushinikiza warudishiwe fedha zao za nauli.

Kamanda wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani mkoa wa Katavi , Joseph Shilinde alilazimika kuingilia kati sakata hilo kwa kuagiza magari hayo mawili kusitisha safari zake hadi hapo yatakapowekewa tairi mpya.

Pia, aliagiza mmiliki wa mabasi hayo, kurejesha fedha za nauli zilizotolewa na abiria hao watafute usafiri mwingine.

Mabasi hayo yalikuwa yafanye safari kutoka mjini Mpanda mkoani Katavi kwenda Tabora kupitia mjini Inyonga Wilaya ya Mlele.

"Matairi ya magari haya yamechakaa, hayafai, ni vipara vitupu hatuko tayari kusafiri nayo…ukizingatia kuwa hayawezi kamwe kumudu kusafiri katika barabara za vumbi. Kutoka hapa hadi Tabora barabara ni ya vumbi ," alisema John Kikwala.

POLISI, WABUNGE WAMSHUTUMU MBOWE

KAULI ya Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe ya kuagiza yafanyike maandamano na migomo nchi nzima bila kikomo, ikiwezekana hata bila ya kibali cha Polisi, imelichefua Jeshi la Polisi.
Jeshi hilo limeonya kuwa halitasita kumchukulia hatua kali, kwa kuwa anavuka mipaka ya kisiasa na kugeukia makosa ya jinai.

Aidha, limemtaka kuacha mara moja kuihamasisha jamii, kutofuata sheria na taratibu za nchi, kwani nao atakuwa anawaingiza matatani. Kauli hiyo yaJeshi la Polisi ilitolewa jana na Kamishna wa Jeshi hilo anayeshughulikia Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya jeshi hilo, jijini Dar es Salaam.

Alisema endapo Mbowe na wafuasiwake, watafanya migomo na maandamano bila ya kufuata sheria, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake, kwa kuwa tayari alishapewa onyo mara ya kwanza kufuatia kauli hiyo.

Alisema Mbowe anatakiwa kufuata taratibu na sheria kuhusu kufanya maandamano, kwani taratibu zote zipo, hivyo kwa kauli zake hizo, anavunja sheria na kuvuka mipaka iliyowekwa kugeuka kuwa jinai na siyo siasa.

''Kauli iliyotolewa na Mbowe Septemba 14 (juzi) inaashiria uvunjifu wa amani na inahamasisha jamii kutotii sheria na taratibu za nchi. Tunaonya kwamba Mbowe anatakiwa kufuta kauli yake na kwamba taratibu zote zilizowekwa zifuatwe,'' alisema Chagonja.

Awali, alisema kwamba siasa zina mipaka yake, hivyo mtu atakayetumia mwavuli wa siasa kutaka kuvuruga amani na utulivu uliopo, jeshi hilo halitamvumilia na halitasita kumchukulia hatua kali kama mhalifu mwingine.

''Masuala ya Bunge yana sheria na taratibu zake, hivyo kuna masuala mengine ya ndani ambayo hayatakiwi kutolewa nje bila ya kufuata taratibu zilizowekwa na bunge hilo, haikumpasa kusema kwamba atashinikiza wafuasi wake na wananchi kufanya maandamano yasiyofuata sheria,'' aliongeza.

Aidha, aliwaonya wananchi wote kuzingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa katika kutekeleza jambo lolote, pia kuepuka kauli zitakazowashawishi kuvunja sheria hizo.

Alisisitiza kuwa ili kuimarisha amani na utulivu uliopo, wananchi wanatakiwa kutoshiriki katika masuala ya uvunjifu wa amani kwa namna yoyote, badala yake kushiriki katika shughuli zao za kulijenga taifa na kuleta maendeleo.

Wabunge wacharuka Wakati Jeshi la Polisi likionya kuhusu kauli zinazotajwa kuwa za kichochezi za Mbowe, Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba nao jana waliibuka na kulishutumu kundi la wajumbe wa bunge hilo wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa kuhamasisha watu kuandamana barabarani, kupinga kuwepo kwa Bunge hilo huku viongozi wa kundi hilo wakionesha kuwa mstari wa mbele.

Wajumbe hao pia wameshutumu kitendo cha Ukawa, kumwandama Mwenyekiti wa Bunge hilo, SamuelSitta kwa kufafanua kwamba Bungehilo, sio mali ya Sitta, bali linafanyika kwa mujibu wa sheria za nchi.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye ameshutumiwa kuwandiye chanzo cha vurugu na chokochoko, zinazoendelea kufanywa na UKAWA, kutokana na kauli zake, ambazo amekuwa akizitoa kuwa Bunge hilo limepoteza uhalali wa kisiasa.

Akizungumza wakati wa majadiliano bungeni, George Simbachawene alisema Ukawa wamekuwa wanafanya upotoshaji mkubwa kwa kuutangazia umma kuwa uwepo wa bunge hilo sio halali. Alionya kuwa wananchi sasa wanapaswa kupima uzalendo wa viongozi wa kundi hilo kupitia kaulizao.

Alisema Bunge hilo, sio mali ya Sitta ambaye ni Mwenyekiti na kuwa kiongozi huyo na hata Rais, hana mamlaka ya kulisitisha, kwani linaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Alisema kwa wingi wa wajumbe walioko bungeni, hawawezi kuwa wendawazimu kuendelea na jambo ambalo sio halali.

Alisema kuwa wale ambao waliamua kutoka nje ya Bunge hilo, ndio ambao wamevunja sheria.
Simbachawene alisisitiza kuwa wanachofanya wajumbe hao ni kupinga Katiba inayopendekezwa.

Alihoji; "Hivi kuingia barabarani kuandamana ndio kutunga Katiba ya wananchi? Halafu hao Ukawa ndio wanataka tuwape nchi, kwa kweli naomba wananchi wawaone kwamba watu hawa ni wabaya".

Aliwahadharisha wananchi wasiende kuandamana, badala yake wasubiri wapige kura ya kuikubali au kuikataa Katiba hiyo na sio kwenda kuandamana.

Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alikiri kuwa bunge hilo limewakosa walio nje kwa sababu waliwahitaji ili wachangie mawazo mbadala, lakini wamekosa uzalendo kwa kukataa kurejea bungeni.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya aliwashangaa Ukawa kuwachochea vijana waandamane nchi nzima wakati viongozi wao hawashiriki maandamano hayo.

Alisema Chadema na washirika wake wa Ukawa, wasiwapeleke vijana ambao ni tumaini la taifa hili kwenye maandamano, kwani kufanya hivyo ni hatari kwa maishaya vijana hao ambao ni nguvukazi ya taifa.

Kapteni John Komba, yeye katika mchango wake alitumia muda wake mwingi, kumshutumu Jaji Warioba, kuwa ndiye aliyesababisha vurugu zote zinazoendelea nchini juu ya mchakato wa Katiba.

Alisema Jaji Warioba aliheshimiwa na Rais Jakaya Kikwete na wananchi walimheshimu, ndio maana alikabidhiwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa ajili ya kukusanya na kuandika mabadiliko ya Katiba na wakati huo Watanzania walikuwa kimya.

Alisema yeye baada ya kumaliza kazi yake, kazi hiyo sasa ni ya Bunge Maalumu la Katiba, lakini kila kinachofanywa na bunge hilo Jaji Warioba anawakosoa na alimwomba Mwenyekiti wa Bunge hilo, atoe tamko la kumkemea mwanasheria huyo.

Komba ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Magharibi, alishauri Jaji Warioba akae kimya katika kipindi hiki ambacho bunge hilo linamalizia kazi yake ya kuandika katiba hiyo.

Komba pia alimshutumu Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa kujigeuza kuwa Amiri Jeshi kwa kutangaza vita na kuwataka wafuasi wake waingie barabarani nchi nzima katika maandamano ambayo hayana kikomo.

"Si mlimsikia akisema 'mko tayari kwa vita?' Wakamjibu 'tuko tayari'…akaendelea, 'lakini mjue kuna risasi mko tayari' na wafuasi wake wakajibu 'ndio tuko tayari'… hivi hii ni amani gani wanayoitangaza huko nje, hii ni hatari kwa nchi," alisema Komba."

Amos Makalla, mjumbe na Mbunge wa Mvomero ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, aliungana na wajumbe wengine, kuwashambulia Ukawa bungeni. Alisema kuwa umoja wao huo, maana yake ni umoja wa katiba ya wachache na sio ya wananchi, kama wanavyojitangaza.

Alisema kama ingekuwa ni umoja wa katiba ya wananchi walio wengi,kundi hilo lingebaki ndani ili waandike na kushiriki kwenye mambo yanayogusa wananchi wao;na sio kutoka nje ya Bunge.

Alimtaka Sitta asitishike na kauli zaUkawa, badala yake awe imara ili kazi iliyobaki ya kuandika Katiba yanchi imalizike.

Mwenyekiti wa Chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa aliliambia bunge hilo kuwa wenzake hao wa upinzani, wanamsakama Sitta kwa kuwa ndiye alikuwa chaguo lao wakati wa mchakato wa kumtafuta mwenyekiti wa bunge hilo.

Alisema wakati wa mchakato wa kumchagua mwenyekiti, vyama vyote vya upinzani venye wabunge ambavyo vinaunda Ukawa, walimuunga mkono Sitta kwa mategemeo kuwa angelinda maslahi yao.

Mwanasiasa huyo ambaye mara nyingi amekuwa anatofautiana na misimamo ya Ukawa tangu bunge hilo kuanza, alisema waliamini kuwa Sitta angewaunga mkono katika hoja zao za ovyo, ambazo alidai hazina faida kwa nchi, ndio maana wanamshambulia kila kukicha.

Mohammed Misanga alimtaka Sitta asitetereke kwa kuitwa king'ang'anizi, kwani wananchi walio wengi wanaliunga mkono bunge hilo, kutokana na mambo mengi yanayojadiliwa kuwahusu wao.

"Nimeongea na wananchi kwenye jimbo langu na kule Dar es Salaam wanawashangaa hawa Ukawa, maana haya mambo tunayozungumzia hapa ni ya wananchi wenyewe," alisema Misanga ambaye pia ni Mbunge wa Singida Magharibi.

Chanzo: Habari Leo

POLISI 6 WAUAWA KATIKA MLIPUKO

Askari polisi 6 wameuawa katika mlipuko katika rasi ya Sinai Misri wizara ya maswala ya ndani ya Misri imetangaza.

Polisi hao waliuawa bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara ilipolipuka msafara wa polisi ukipita.

Maafisa wawili zaidi walijeruhiwa vibaya katika tukio hilo.

Wanamgambo katika rasi ya Sinai wameendeleza mashambulizi zaidi haswa baada ya kung'olewa mamlakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi mwaka uliopita.

Shambulizi hili la leo lilitokea katika barabara ya kutoka mji wa rafah Kuelekea mpaka wa Palestina wa Gaza.

Kundi la wapiganji wa Ansar Beit al-Maqdis wanaohusishwa na Al Qaeda ndio waliodai kutekeleza shambulizi hilo.

Kundi hilo linadai kulipiza kisasi mauaji ya maelfu ya waislamu waliouawa katika mapinduzi ya Morsi.

MAMIA YA WAHAMIAJI WAFA MAJI

Mamia ya wahamiaji wamekufa maji wakati wakijaribu kuelekea nchini Italia kupitia Bahari ya Meditarian ambapo boti yao ilizama karibu na kisiwa cha Malta wakati wakijaribu kuelekea nchini Italia.

Manusura wawili raia wa Palestinian wamelieleza shirika la kimataifa la uhamiaji la IOM jinsi ajalihiyo ilivyotokea na kwamba ilisababishwa navurugu kati ya abiria hao na wafanya biashara za magendo..

Msemaji wa shirika la IOM Leonard Doyle ameiambia BBC kuwa watu wawili walionusurika katika ajalihiyo wamesema mazingira ya kuzama kwaboti yao ilitokea pale walipolazimishwa kuhamia katika chombo kingine na walipokataa vurugu ikaanza.

Doyle anasema kuwa watu hao wamesema kuwa walianza safari hiyokatika bandari ya Damietta nchini Misri Septemba wakiwa 500.

Shirika la umoja wa mataifa linasema wahamiaji wapatao 130,000 wamefanikiwa kuingia Ulaya kupitia bahari ya Mediteranian ambapo kwa mwaka huu pekee wahamiaji 80,000 wamepitia njia hiyo.

Kwa mjibu wa ripoti ya umoja wa mataifa Italia imepokea wahamiaji 118,000.

MNARA MREFU ZAIDI KUJENGWA AMAZON

Nchi ya Brazil imeanza rasmi ujenzi wa mnara mrefu zaidi duniani huko Manaus mjini Amazon.

Mnara huo kwa jina Amazon observation Tower, unatazamiwa kutumika katika utafiti wamapana wa hali ya anga.

Utakuwa na vifaa maalum venye uwezo mkubwa wa kukusanya data kuhusu gesi chafu iliyo hewani, chembe chembe za erosoli na haliya anga ya kila uchao katika msitu wa Amazon.

Eneo hilo la Amazon ndilo linalinaloshuhudia mvua kubwa zaidi kila msimu.

Wanasayansi wa Brazil na Ujerumani wanatumai kuutumia mnara huu katika uchunguzi wao wa vyanzo vya gesi chafu na mabadiliko ya hali ya anga.

Kutokana urefu wake, mnara huu utawezesha wanasayansi kuelewa mabadiliko ya mwelekeo wa upepo kwa kitalifa cha zaidi ya kilomita mia moja katika msitu wa Amazon.

Msitu wa Amazon ni kati ya misitu mikubwa zaidi duniani inayoathiri mazingira kwani inahusika pakubwa katika kuongeza na kupunguza kiwango cha hewa aina ya (carbon) angani.

Kulingana na bw. Paulo Artaxo, mwelekezi wa mradi huo kutoka chuo kikuu cha Sao Paulo, amesema mnara huo utasaidia pakubwa katika juhudi za kutafuta majibu ya maswali mengi kuhusu mabadiliko ya hali ya anga duniani.

Aidha, mnara huu unatarajiwa kutumiwa pamoja na minara mingine midogo ambayo tayari imejengwa nchini humo.

Kulingana na wajenzi, mnara huu utafanana na ule uliojengwa Siberia ya kati katika mwaka wa 2006.

NASA YASHINDWA KUBAINI VIMONDO

Shirika la safari za anga la juu nchini Marekani NASA,imeoneshwa ukinzani kutokana na kushindwa kung'amua vitu vya hatari angani.

Shirika hilo linajaribu kubainisha vimondo na vitu vingine ambavyo hupita katika umbali wa kilomita milioni arobaini na tano katika uso wa dunia ili kujaribu kuilinda kutokana na hatari inayoweza kutokea.

Lakini mpaka sasa NASA imegundua asilimia kumiya makisio yake na haidhaniwi kua malengo iliyojiwekea mpaka kufikia mwaka 2020 endapo yatafikiwa na huku muda wa mwisho wa kutoa ripoti kuhusiana na masuala yaanga ukifikia tamati.

Vimondo na vitu vingine husambaratishwa angani kabla havijaufikia uso wa dunia lakini vingine si rahisi.

Mwaka wa jana kimondo kimoja kiliripuka huko Urusi katika mji wa Chelyabinsk kikiwa na kasi kuwa wakati kikishuka mjini humo kasi ambayo ni mara thelathini zaidi ya bomu la atomic lililotupwa Hiroshima.

MUINGEREZA ACHINJWA KAMA KUKU NA IS

Serikali ya Uingereza imesema kuwa inachukua hatua za dharura ili kubaini ukweliwa kanda ya video inayoonyesha mateka wa Uingereza David Haines aliyetekwa nyara na kundi la himaya ya kiislamu akikatwa kichwa.

Mfanyakazi huyo wa misaada aliyekamatwa nchini Syria mnamo mwezi Machi mwaka jana ameonyeshwa akipiga magoti katika jangwa, kando yake akiwa ni mtu aliyeficha uso wake ambaye amebeba kisu.

Atakuwa mateka wa tatu wa magharibi kukatwa kichwa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Katika kanda hiyo ya Video mtu aliyeshika kisu anaonekana akishtumu mataifa yanayounga mkono Marekani, naye Haines ambaye anaonekana kuwa chini ya shinikizo anaonekana akimlaumu waziri mkuu nchini Uingereza David Cameron kwa hatma yake.

Mwisho wa kanda hiyo mateka wa pili wa Uingereza anaonyeshwa na kutishiwa.

David Cameron Wakati huohuo Waziri mkuu nchini Uingereza David Cameron ameshtumu kukatwa kichwa kwa David Haines kama kitendo cha kishetani.

Amesema kuwa wauaji watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria ata iwapo itachukua mda mrefu.

Katika taarifa yake rais Obama pia ameshtumu mauaji ya kikatili ya David Haines.

Amesema Marekani inaomboleza na Uingereza kifo cha mateka huyo na kungezea kuwa itashirikiana na muungano mkubwa wa kimataifa ili kuwakamata washukiwa mbali na kuharibu tishio hilo kwa ulimwengu.

Wanahabari wawili Steven Sotlof na james Foley waliuawa na wapiganaji hao mwezi uliopita.

OSCAR PISTORIUS ALIMUUA BILA KUKUSUDIA MPENZI WAKE

Jaji anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius, amesema upande wa mashitaka umekosa kuthibitishia kikamilifu shitaka kuu la kwanza dhidi ya Pistorius kuwa alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Hata hivyo jaji huyo Thokozile Masipa amepinga ushahidi wa upande wa utetezi kwamba mwanariadha huyo hakunuia kutenda uhalifu alipomuua mpenzi wake Reeva.

Pistorius alikiri kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwaka jana lakini amekana kumuua kwa maksudi , akisema alidhani kuwa mwizi alikuwa amevamia nyumba yake.

Upande wa mshitaka unasisitiza kuwa Pistorius alimuua Reeva kwa maksudi, baada ya wapenzi hao wawili kutofautiana.

Mandishi wa BBC anasema kuwa jaji Thokozile Masipa heunda akachukua hadi Ijumaa kumaliza uamuzi wake.

Pia atakuwa anaangalia kwa makini ukweli wa mashahidi waliotoa ushaidi wao katika kesi hiyo akiwemo Pistorius mwenyewe.

Pistorius huenda akafungwa jela miaka 25 ikiwa atapatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake.

Oscar Pistorius amekana mashitaka ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao ya Valentine mwaka jana.

Mwendesha mashitaka anasisitiza kuwa Pestorius alimpiga risasi aliyekuwa mpenziwe Reeva baaya ya ugomvi baina yao lakini amejitetea akisema alimpiga risasi kimakosa akidhani mwizi amevamia nyumba yake.

WATU WAWILI WAFARIKI BAADA YA KIFARU KUGONGA NYUMBA

WATU wawili wamekufa baada ya gari la Kijeshi (Kifaru cha Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ) kupoteza mwelekeo na kuparamia makazi ya watu mkoani Lindi na kupelekea watu wengine saba kujeruhiwa vibaya.

Taarifa zilizoifikia FikraPevu leo na kuthibitishwa na Jeshi la Polisi mkoani humo zinaeleza kuwa ajali hiyo imetokea saa 05:30 asubuhi katika eneo la Mnonela barabara ya Mingoyo-Mtwara na kuwa ajali hiyo ilihusisha gari namba 018 APC mali ya JWTZ kikosi namba 83 Reget.

Gari hilo lilikuwa likitokea mkoani Mtwara kuelekea katika wilaya ya Nachingwe mkoani Lindi kikazi ambapo lilikuwa likiendeshwa na Askari mwenye namba MT 99241 Priv. Shadhil Nandonde pia haijawekwa wazi kuwa ni kazi gani lilikuwa linaenda kufanya shughuli gani.

Imeelezwa kuwa watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni Askari mwenye namba MT 10728 Pr Pascal Komba na mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Somoe Kamtaule (75), mkulima wa eneo hilo aliyekuwa ndani ya nyumba.

"Lilipoteza mwelekeo na kuingia kwenye nyumba mbili na katika nyumba moja ilisababisha kifo cha mtu mmoja (mwanamke) na kwenye gari hilo Mwanajeshi mmoja alikufa pamoja na majeruhi saba kujeruhiwa vibaya".

Aidha, majeruhi katika ajali hiyo ni Askari mwenye namba MT 10744 Pr. Simon Edward, Askari namba MT 106842 Pr.Feruz Haji, Askari mwenye namba MT 1077263 Pr.Omary Makao pamoja na Askari mwenye namba MT 99018 Pr.Mbaruk Duchi.

Wengine ni Askari mwenye namba MT 107442 Pr. Simon Masele, Askari mwenye namba MT 107218 Pr.Ndekenya R na Askari mwenye namba MT 99241 Pr.Shadhil Nandonde ambaye alikuwa dereva.

Kwa mujibu wa Polisi mkoani humo, chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa na majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mtwara ya Ligula kwa ajili ya matibabu.

Wakati huo huo, watu 2 wameripotiwa kufa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa, baada ya basi la Kampuni ya Super Feo kupinduka katika eneo la Sanangula nje kidogo ya mji wa Songea likitokea mkoani Ruvuma kwelekea mkoani Mbeya.

Majeruhi wa ajali hiyo wanatibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma, huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa bado hakijafahamika.

Chanzo: Fikra Pevu

RAIS JK AWATIMUA MAKADA WALIOENDA KUMPOKEA

Rais Jakaya Kikwete jana aliwafukuza makada wa CCM waliokuwa wakimsubiri kwenye kituo cha dharura cha ebola alipo kitembelea kwa kushtukiza katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Makada hao ambao baadhi yao walivalia sare za CCM, kinyume na matarajio yao, kiongozi huyo alipofika hospitalini hapo alionyesha kuwashangaa kabla ya kuwataka waondoke kwa kuwa hakuhitaji kuzungumza nao, bali wasimamizi wa kituo hicho.

“Hawa watu wote wanafanya nini hapa! Sijajakuhutubia hapa mimi. Ndugu zangu hawa waliowaita wamewasumbua bure, nawashukuruni sana kwa kuja, endeleeni na shughuli zenu,” alisema Rais Kikwete ambaye aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki.

Hatua hiyo ilionekana kuwanyong’onyeza makadahao ambao hawakuwa na jinsi isipokuwa kuondoka taratibu kwenye eneo hilo na kumwacha Rais Kikwete na viongozi wa kituo hicho.

Ukaguzi wa kituo

Katika ukaguzi wa kituo hicho, Rais Kikwete alielezakutoridhishwa na maandalizi na akaagiza ukarabati mkubwa ufanywe haraka ili kiwe na hadhi inayostahili.

Alionyesha kushangazwa na miundombinu duni ikiwamo vyoo vibovu na ukosefu wa maji katika kituo hicho na kuagiza kufanyika marekebisho ya haraka.

“Hivi hii ni kweli? Hakuna maji, vyoo vibovu, kituo chenyewe kikuukuu! Kwa taarifa za awali, kituo hiki kilikuwa ni kwa ajili ya ugonjwa wa kipindupindu, hakiendani kabisa na hitajila sasa la kuwa hudumia wagonjwa wa ebola iwapo watabainika kuingia nchini,” alisema Rais Kikwete.

Alisema katika hali ya kawaida, kituo hicho kinatakiwa kuwa cha kisasana chenye mazingira yanayowezesha kutoa huduma kwa wagonjwa hao kwa usalama.

Alisema ameamua kufanyaziara hiyo Temeke na ukaguzi wa namna Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuona ukweli wa taarifa alizopewana kuzizungumza katika mkutano na wazee wa Mkoa wa Dodoma wiki iliyopita.

“Hii ndiyo fursa ya hii dharura ambayo mnatakiwa kuitumia vyemana kupata kituo cha kisasa na kwa wakati huu. Kama kuna matatizo ya fedha tuelezane tutajua namna ya kufanya,” alisema Rais Kikwete.

Alisema ni vyema kuhakikisha kunakuwa na kituo maalumu cha kuwapokea na kuwahifadhi waathirika wa magonjwa ya mlipuko ambacho ni cha kipekee na cha aina yake nchini.

KATIBA YA SASA KUREKEBISHWA, MGOMBEA BINAFSI RUKSA UCHAGUZI UJAO

MCHAKATO wa kuandika Katiba mpya kabla ya Uchaguzi Mkuu ujaoumekwama, baada ya viongozi wa vyama vya siasa vyenye wabunge na Rais Jakaya Kikwete, kukubaliana kusitisha mchakato huo. Badala yake viongozi hao wa vyama vya siasa wamekubaliana kwamba Katiba ya sasa ya mwaka 1977, ipelekwe bungeni kufanyiwa marekebisho, ili kutoa fursa Uchaguzi Mkuu ujao ufanyike mwakani kisha mchakato wa Katiba mpya, uendelee baada ya uchaguzi huo.

Mambo ambayo vyama vya siasa wamekubaliana, ni kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi itakayosimamia uchaguzi wa mwaka 2015; mshindi wa uchaguzi wa Rais apate zaidi ya asilimia 50 ya kura zote, matokeo ya uchaguzi wa rais yaruhusiwe kupingwa mahakamani na kuruhusu mgombea binafsi katika uchaguzi.

Pia vyama vingine vya siasa ambavyo vinataka kupendekeza mambo mengine ya kurekebisha katika Katiba ya mwaka 1977, vimeombwa kufanya hivyo mapema kwa kuwa muda uliopo wa kufanya mabadiliko ni mdogo.

Kutokana na mabadiliko hayo, TCD kupitia vikao vyake, itaratibu na kujadili mapendekezo hayo na kupeleka serikalini kwa hatua zingine za kuingiza mapendekezo hayo kwenye marekebisho ya Katiba.

"Muda tulio nao ni kwa mabadiliko yanayopendekezwa kujadiliwa katika Bunge la Novemba na wakichelewa Bunge la Februari 2015," alisema John Cheyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.

Kwa makubaliano hayo, kazi inayofanywa na Bunge Maalumu la Katiba (BMK) ya kuandika Katiba mpya itakoma Oktoba 4 mwaka huu, siku ambayo Bunge hilo litakuwa halijakamilisha uandikaji wa Katiba, ambao unafanywa na kamati ya uandishi iliyo chini ya Andrew Chenge.

Alipoulizwa kama Rais atakayekuja asipoona Katiba kama kipaumbele itakuwaje, Cheyo alisema yeye na viongozi wenzake wanaamini kuwa kiongozi huyo atashauriana na wenzake ili kukamilisha mchakato huo.

"Rais ana uhuru wake, tusimwekee masharti Rais ajaye," alisema Cheyo.

Hata hivyo hakuweka bayana kama mchato huo utaanzia pale ulipomalizikia au utaanza upya.

Uamuzi huo unakidhi baadhi ya madai ya kundi la Umoja wa Katibaya Wananchi (Ukawa) ambao ni wajumbe waliokuwa ndani ya Bunge Maalumu la Katiba, lakini walijiondoa kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa Bunge hilo.

Kutokana na msimamo wao wa kutorejea bungeni hata baada ya kuombwa kufanya hivyo na viongozi mbalimbali, kundi hilo lilitia ngumu badala yake wakataka kukutana na Rais Kikwete.

Miongoni mwa madai yao waliyokuwa wanayataka ya kusitisha Bunge hilo hayakufanikiwa kwani litaenda hadi mwisho kwa kuwa lipo kisheria.

Ratiba ya Bunge inaonesha kuwa majadiliano ya wabunge ambayo yalianza jana, yangekuchukua siku 15 na yangekamilika Septemba 29.

Septemba 30 hadi Oktoba 6 Kamati ya Uandishi ilitengewa siku tano kwa ajili ya kuandika Katiba inayopendekezwa na Bunge Maalumu.

Oktoba 9 Kamati ya Uandishi ilikuwa iwasilishe Katiba hiyo bungeni na Oktoba 10 hadi Oktoba 21 ingekuwa siku saba kwa ajili ya kupiga kura. Baada ya hapo Bunge lilijipangia kuwa baada ya upigaji kura, wajumbe wangepewa siku tano kwa ajili ya kujadili na kupitisha masharti ya mpito.

Ratiba hiyo ya Bunge pia inaoneshakuwa Oktoba 29 na 30, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu alikuwa awasilishe kwa Rais Katiba inayopendekezwa na Bunge lake.

Sababu za maafikiano Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia (TCD) Cheyo alitaja sababu saba zilizowaongoza kuafikiana mambo hayo; moja ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, inayotaka mwisho wa mchakato wa kupata Katiba mpya, uwe kura ya maoni iliyotarajiwa kufanyika Aprili 2015.

Cheyo alisema kama itabidi kura kurudiwa kwa mujibu wa sheria iliyotajwa, ilitarajiwa kufanyika hivyo Julai 2015, muda ambao Bunge la Muungano linatakiwa liwe limevunjwa kwa ajili ya kupisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.

Alisema ili Katiba mpya itumike katika uchaguzi mkuu utakaokuja, ilionekana kuwa itabidi uhai wa Bunge na Serikali uongezwe zaidi ya 2015, jambo ambalo alisema viongozi wa vyama vya siasa hawaliungi mkono jambo hilo.

Alitaja sababu ya pili ni kwamba Bunge Maalumu la Katiba kwa sasa linafanya kazi kwa mujibu wa tangazo la Serikali namba 254 lililotolewa na Rais Kikwete Agosti mosi mwaka huu.

Tangazo hilo litatumika hadi Oktoba 4, mwaka huu ambapo Katiba inayopendekezwa ilitarajiwa kupatikana.

Alisema wajumbe walikubaliana hatua hiyo iachwe iendelee hadi ifikie mwisho, kama tangazo linavyoelekeza kuwa mwisho itakuwa Oktoba 4.
Cheyo alisema pia kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, baada ya Bunge Maalumu la Katiba kumaliza kutunga Katiba, ingefuata hatua ya kura ya maoni kuthibitisha Katiba.

Alisema kwa kutambua kuwa hatua ya kura ya maoni italazimisha Uchaguzi Mkuu 2015 kuahirishwa hivyo hatua hiyo lazima iahirishwe.

Cheyo alisema sababu nyingine ni mchakato wa Katiba uendelee baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Hivyo viongozi hao wamekubaliana Katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho haraka, ili kusaidia kufanyika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa haraka iwezekanavyo.

Katika eneo hilo viongozi hao wametaka Serikali kuchukua hatua za kisheria, ili uchaguzi huo ufanyike mapema mwakani.

Vyama vilivyoshiriki kwenye mazungumzo hayo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) NCCR Mageuzi, Tanzania Labour Party (TLP), United Democratic Party (UDP) na chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP).

Chanzo: Habari Leo

MWALIMU ATEKWA NA KUTESWA MSITUNI

(Picha: Asutsa katikati akiwa na mkewe)

Mwalimu wa kanisa Katoliki, Magharibi ya Kenya alijikuta taabani baada ya kutekwa nyara na majambazi waliomtesa pamoja na kumpiga msumari kwenye mti msituni, umbali wa kilomita mia mbili kutoka nyumbani kwake.

Peter Asutsa alikaa msituni kwa saa 16 mkono wake ukiwa unaning'inia kwenye mti kabla ya kuokolewa na polisi.

Inaarifiwa Peter alipigwa msumari kwenye kwenye mkono wake mmoja baada ya majambazi hao kukosa kumpata na pesa zaidi walizokuwa wakitaka.

Inaarifiwa Asutsa aliizimasimu yake na kuificha ndani ya nguo zake za ndani ambapo majambazi hao wasingeweza kuipata.

Baada ya majambazi hao kumtelekeza, alimpigia simu mkewe ambaye aliwaarifu polisi waliokuja kumuokoa.

Masaibu ya Asutsa yalianza pale alipokwenda dukani kumnunulia mkewe mgonjwa dawa katika duka la dawa mjini Kitale Magharibi ya Kenya.

Abiria mmoja aliyekuwa ndani ya gari alimokuwa anasafiria Asutsa aliamrisha dereva kusimamisha gari. Kisha akawafungia ndani akiwana abiria wengine wawili.

Alitekwa nyara na majambazi waliofika katika sehemu hiyo kwa gari jingine na kumuingiza ndani ya gari hilo na hapo ndipo alipogundua kuwa alikuwa ametekwa nyara.

Walimpora dola 24 na kumtaka asalimu simu yake , lakini akataa.

Baadaye walimpeleka ndani ya msitu na kumpigia msumari mtini kupitia kwenye mkono wake mmoja na kumuacha ndani ya msitu wa Kaptagat.

Alilazimika kuwatisha na kuwafukuza Fisi na Mbweha waliokuwa wakitishia kumvamia usiku.

MABAKI YA MIFUPA YA DINOSAR YAPATIKANA BONDE LA RUKWA

(Picha: Maktaba)


Aina mpya ya dinosaria imetambuliwa kufuatia kupatikana kwa mifupa nchini Tanzania.

Mabaki hayo ya dinosaria yaliyopewa jina la - Rukwatitan Bisepultus - yalipatikana katika korongo moja kwenye eneo la Rukwa(Bonde la Rukwa), kusini magharibi mwa nchi hii.

Inadhaniwa mnyama huyo aliyekuwa akiishi kwa kula majani, aliishi karibu miaka mia moja iliyopita, na alikuwa na uzito sawa na tembo kadhaa na alikuwa na miguu ya mbele yenye urefu wa mita mbili.

Mnyama huyo ni aina ya titanosaurus -- ambao ni wakubwa, na wanao kula nyasi.

Mabaki ya wanyama aina hiyo mpaka sasa yamepatikana katika maeneo ya Amerika ya Kusini, bara ambalo lilijitenga kutoka Afrika katika kipindi cha Cretaceous, (kipindi ambacho miamba ya chaki iliumbika) takriban miaka milioni mia moja na arobaini iliyopita.

WACHINA WA 'SAMAKI WA MAGUFULI' WADAI MELI YAO

RAIA wa China waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya kuvua samaki kinyume cha sheria, wamewasilisha barua kwa Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, kutaka warudishiwe Meli ya Tawariq 1 na samaki waliopokewa mahakamani kama vielelezo.

Barua hiyo iliwasilishwa na kampuni ya uwakili ya M and B iliyokuwa ikiwawakilisha Wachina hao na kusaini na mshirika wa kampuni hiyo, Ibrahim Bendera.

Katika barua hiyo, raia hao wanaiomba mahakama iwarudishiemeli hiyo pamoja na tani 296.3 za samaki zenye thamani ya Sh bilioni 2.074 ambazo zilipokelewa mahakamani hapo kama vielelezo katika kesi namba 38/2009 iliyokuwa inawakabili.

Hatua hiyo inatokana na amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyotolewa na Hakimu Mfawidhi Isaya Arufani Agosti 23, mwaka huu wakati akiwaachia huru washitakiwa wawili; nahodha wa meli hiyo, Hsu Chin Tai na wakala wa meli, Zhao Hanquing.

Awali watu 35 kutoka mataifa mbalimbali walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutuna baadaye kesi hiyo ilihamishiwa katika Mahakama Kuu mbele ya JajiRazia Sheikh ambaye alipokea vielelezo hivyo.

Kesi hiyo ilihamishiwa kwa Jaji Augustino Mwarija, ambaye aliwaachia huru washitakiwa 31 na kuwahukumu Tai na Hanquing kifungo cha miaka 30 jela au kulipafaini ya Sh bilioni 22.

Hata hivyo mmoja wa washitakiwa alifariki dunia wakati kesi hiyo ikiendelea.

Washitakiwa hao walikata rufaa kupinga adhabu hiyo.

Machi 28, mwaka huu, Mahakama ya Rufani iliwaachia huru kabla ya kukamatwa tena na kufunguliwa upya mashitaka hayo.

Wakati kesi hiyo ikiendelea, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), aliwasilisha hati ya kutokuwa na niaya kuendelea kuwashitaki.

Aliwaachia huru na Mahakama kuamuru warudishiwe mali zao.

Washitakiwa walikamatwa wakati Dk John Magufuli akiwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, hali iliyochangia samaki waliokamatwa kuitwa wa 'Magufuli' hasa baada ya serikali kuamua kutaifisha meli na pia kugawa samaki kwa wananchi, vyuo na taasisi nyingine za umma.

Kutoka: Habari Leo

WATOTO WATATU WA FAMILIA MOJA WAFARIKI BAADA YA NYUMBA YAO KUCHOMWA

Watoto watatu wa familia moja mkoani Geita, wamefariki dunia usiku wa kuamkia jana baada ya nyumba yao kuteketezwa kwa moto uliowashwa kwa mafuta ya petroli na mtu asiyefahamika.

Dada mkubwa wa marehemu hao ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili Sekondari Mwatulole na wazazi wao, walijeruhiwa vibaya katika tukio hilo ambalo chanzo chake ni ugomvi wa ardhi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya hiyo, Dkt. Adam Sijaona, alisema miili ya watoto hao imehifadhiwa hospitalini hapo.

Aliwataja marehemu hao kuwa ni Reginald Robert (9), mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Nyankumbu Mkombozi, Sophia Robert (6) aliyekuwa akisoma darasa la kwanza shuleni hapo na Remijius Robert (4).

Majeruhi ni Scholastica Robert (15), ambaye amejeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake ambapo hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.

Wazazi wa watoto hao ambao pia walijeruhiwa katika tukio hilo ni Bi. Angelina Gaspa (36), ambaye amelazwa hospitalini hapo akiwa na majeraha katika mkono wake wa kulia, mgongoni, begani pamoja na Bw.Robert Remijius (45) aliyejeruhiwa kichwani.

Akizungumza kwa tabu akiwa wodini, Bi. Gaspa alisema siku ya tukio walikuwa wamelala watoto wakiwa chumbani kwao ambapo ghafla alisikia watoto wakipiga kelele na kusema 'mama tunakufa' na alipokwenda kuwaangalia, akakuta nyumba inateketea kwa moto.

"Nilikuta nyumba nzima ikiwaka moto, tulipiga kelele za kuomba msaada kutoka kwa majirani ambao walifika na kuanza kuvunja milango pamoja na ukuta ili waweze kutuokoa.

"Mimi na mume wangu tulijitahidi kuvunja tofali japo tupate sehemu ya kupita na majirani walipofanikiwa kuvunja nyumba, tayari watoto wangu watatu walikuwa wameteketea kwa moto,"alisema.

Aliongeza kuwa, anaamini chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa ardhi uliokuwepo kati yao na mkazi mmoja wa eneo hilo (jina limehifadhiwa) ambaye alifika na kuchimba kisima katika eneo ambalo wao walilinunua kisheria lakini alidai ni lake.

"Tunaishi vizuri na majirani zetu, yote tunamuachia Mungu kwani hata tulipotaka kumlipa ili aondoke katika eneo letu alikataa na mgogoro huu umedumu kwa mwaka mmoja,"alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. Manzie Mangochie, alisema kitendo hicho cha kikatili hakitavumilika na aliyefanya tukio hilo lazima asakwe kwa nguvu zote ili aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria mara moja.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kalangalala, Bw. Hamad Hussein, alisema watu waliofanya ukatili huo walitumia mafuta ya petroli kuyamwaga mlangoni mwa nyumba hiyo na kusambaa vyumbani ukianzi katika chumba walicholala watoto hao.

"Katika eneo la tukio, tumekuta ndoo ya plastiki yenye ujazo wa lita tano iliyotumika kuhifadhia mafuta hayo, tunaomba ushirikiano kwa wananchi ili tuwatie mbaroni wote waliohusika,"alisema.


CHANZO:Majira

MBOWE AWEKEWA PINGAMIZI

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amewekewa pingamizi la kutogombea nafasi hiyo katika uchaguzi unaotarajia kufanyika wiki hii kwa madai kuwa, amekosa sifa.

Pingamizi hilo limewekwa na mgombea mwingine wa nafasiya uenyekiti wa Chadema Taifa, Kansa Mbaruku, ambapo ameliwakisha kwa viongozi wachama hicho jana.

Akizungumza baada ya kuwasilisha pingamizi hilo la kumtaka Mbowe kutogembea uenyekiti, Mbarouk alisema amefikia amuzi huo kwa madai kuwa, Mbowe hana sifa za kugombea kwa mujibu wa Katiba ya Chadema.

"Katiba ya chama chetu, inamruhusu mtu kugombea nafasi moja katika vipindi viwili na baada ya muda huo kuisha, anatakiwa kugombea nafasi nyingine tofauti na hiyo. Hivyo, Mbowe ametimiza awamu mbili katika nafasi hiyo, hivyo anapoteza sifa," alisema Mbarouk.

Alisema kuwa, yeye alikuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Tabora kwa vipindi viwili na alipomaliza muda huo, alitangaza kutogombea tena nafasi hiyo ya mkoa kwa kuwa katiba haimruhusu.

"Hivyo, nilitarajia Mbowe naye aache nafasi hiyo na asigombee tena ili kuiheshimu katiba ya chama chetu," alisisitiza.

Alifafanua Juni mwaka huu, baadhi ya wanachama waliandamana hadi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu hilo hilo la Katiba ambalo linaweka wazi ukomo wa vipindi viwili na aliwaambia viongozi kama wanataka kugombea, wabadili kipengele hicho vinginevyo wakigombea bila kufanya marekebisho, hatawatambua.

Sababu nyingine za kumwekea pingamizi, alisema inatokana na kuona Katiba ya Chadema ikivunjwa mara kwa mara na Mbowe, huku akiongeza tabia hiyo ya kutoheshimu katiba ilisababisha Novemba mwaka jana kubariki kuwavua madaraka aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na Dk. Kitila Mkumbo, jambo ambalo ni kinyume cha katiba.

Alisema katiba ya chama hicho inatamka kuwa,  kiongozi wa ngazi ya Taifa anavuliwa madaraka na mkutano mkuu na wala si watu wachache.

"Kuna mwanachama mwingine Mecky Mziray alifukuzwa chama hicho bila kupewa muda wa kujieleza, kitendo ambacho ni kinyume cha katiba ya chama chetu," alisisitiza.

Kuhusu uchaguzi huo, alisema sura ya 7 ya katiba inasema uchaguzi unatakiwa kusimamiwa na wazee wastaafu wa chama, lakini hana uhakika hadi sasa kama yapo hayo mazingira ya kuwepo wazee hao.

Pamoja na hayo, Chadema leo itakutana na waandishi wa habari ili kuzungumzia uchaguzi huo ngazi ya Taifa. Hiyo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho, Benson Kigaila.

WASHIKILIWA NA POLISI BAADA YA KUKUTWA WAKILIMA UCHI

POLISI mkoani Simiyu inawashikilia watu wanne wa familia moja kwa tuhuma za kukutwa wakilima katika shamba lafamilia yao, huku wakiwa watupu kama walivyozaliwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Venance Kimario alisema ofisini kwake jana kuwa wanafamilia hao wamekamatwa wakihusishwa kushiriki katika imani za kishirikina.

Alisema polisi walipata taarifa za siri kutoka kwa raia wema kuhusu wanafamilia hao, kulima shamba huku wakiwa watupu na kuamua kufuatilia, na walipofika eneo la tukio saa 12 za asubuhi, walikuta wanafamilia hao wakilima huku wakiwa uchi wa mnyama.

Alitaja waliokamatwa kuwa ni baba wa familia hiyo, Makoye Gamoge (42) na mke wake Neema Kigela (31), watoto wao wawili (majina yamehifadhiwa).

Kamanda Kimario alidai familia hiyo inatuhumiwa kwamba wamekuwa wakilima huku wakiwa uchi, kutokana na imani za kishirikina kuwa kwa kufanya hivyo, wataongeza tija na mazao yataongezeka maradufu na hivyo kuwakwamua kiuchumi.

“Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na baba wa familia hiyo kwenye kituo cha Polisi, kulima kwa mtindo huo kunalenga kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo cha jembe la mkono,” alisema Kamanda Kimario.

Makoye anadaiwa kusema mbinu hiyo mpya na ya aina yake ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya ndugu yao ambaye ni mganga wa jadi, aliyefariki mwaka jana kwa maradhi ambayo hata hivyo hawayafahamu.

Kwa sasa watuhumiwa hao wanashikiliwa Polisi na baada ya uchunguzi kukamilika, watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili.

UVUMI WA KUACHIWA BABU SEYA WAKANUSHWA NA JESHI LA MAGEREZA

Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani.

Wafungwa hao wanaotajwa ni Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la Papii Kocha).

Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.

Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa kisheria.

Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.

Imetolewa na;Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,

Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM.
Septemba 8, 2014.

PIKIPIKI ZOTE KUSAJILIWA UPYA

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza kuanza kwa mfumo mpya wa usajili wa pikipiki zote nchini.

Usajili huo utakwenda sambamba na kubadilishwa kwa namba za pikipiki unaoanza na namba MC 101 AAA badala ya namba zinazotumika sasa.

Kwa mujibu wa taarifa ya TRA kwa umma, usajili wa mfumo mpya ambao uko kwa mujibu wa sheria, unatarajiwa kuanza Oktoba mosi, mwaka huu.

"Kwa mantiki hiyo, wamiliki wote wa pikipiki za magurudumu mawilina matatu wanajulishwa kuwa namba zote zitabadilishwa kuanzia Oktoba mosi mwaka huu, hivyo wamiliki wa vyombo hivyo wanatakiwa kufika katika ofisi za TRA kwa ajili ya utaratibu huo ," inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Hata hivyo, wamiliki wa pikipiki wametakiwa kulipia Sh 10,000 kama gharama za kubadilisha namba na kupewa kadi mpya ya umiliki wa chombo. Imeelezwa kazi ya kubadilisha namba kwa pikipiki zilizokwisha andikiwa itafanywa kwa miezi sita kuanzia Oktoba mosi na kwamba baada ya muda huo, ubadilishwaji utakwenda sambamba na adhabu.

WALIOIBA NMB WAHUKUMIWA MIAKA 37 JELA NA VIBOKO 24

WATU watano wamehukumiwa kifungo cha miaka 37 jela na kuchapwa viboko 24 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kuvamia na kupora fedha benki ya NMB tawi la Maswa kwa kutumia silaha.

Hukumu hiyo ilitolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga na kusikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Neema Gasabile ambapo alitoa hukumu hiyo.

Aliwahukumu kifungo cha miaka 37 na viboko 24 kila mmoja viboko 12 wakati wa kuingia na 12 wakati wa kutoka baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashitaka kuwa kwa pamoja walitenda kosa hilo kinyume cha sheria.

Washitakiwa hao ni Kapama Hamis Ramadhan (37), Mussa Athuman Buberwa (38), Amos Mathayo, LucasVincent Mabela (40) na Zainabu Mchau (60) wote kwa pamoja walipatikana na hatia ya makosa tisaya jinai.

Mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Mwendesha Mashitaka Mwanasheria wa Serikali Edith Tuka aliieleza mahakama hiyo kuwa washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo majira ya saa 6:00 mchana Julai 5, mwaka 2010 mjini Maswa.

ANAYEDAI KUBAKWA NA MBASHA ATOA USHAHIDI

SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya ubakaji inayomkabili mume wa mwimbaji wa muziki wa injili, FloraMbasha, Emmanuel Mbasha (32) ameieleza mahakama jinsi alivyobakwa akiwa kwenye gari na nyumbani kwao.
Shahidi huyo mwenye umri wa miaka 17 (jina limehifadhiwa) ambaye pia ni shemeji wa Mbasha, alidai mbele ya Hakimu Wilberforce Luhwago kuwa Mei 23 mwaka huu, Mbasha alimbaka kwa mara ya kwanza wakati mkewe Flora akiwa hayupo.

Alidai siku hiyo, Flora na mumewe walitoka kwenda kufuatilia CD za video zao za nyimbo huku mtoto wao (jina tunalo) akiwa shuleni.

Alidai alishangaa kuona ghafla Mbasha alirudi nyumbani peke yake na kumlazimisha kufanya mapenzi kisha alimtukana na kumtishia kumdhuru endapo atatoa siri.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, shahidi huyo aliendelea kudai kwamba Mei 25 mwaka huu, siku ya Jumapili walikwenda kanisani na waliporudi Mbasha alilalamika kuwa ana njaa hivyo alimpa fedha kununua chipsi.

Alidai baada ya kula, Mbasha alimwambia waondoke nyumbani kwenda kumtafuta Flora ambaye hakuwepo nyumbani siku hiyo.

"Tulipanda gari aina ya Toyota Ipsum, wakati tupo njiani aliniambia nikae kiti cha mbele pamoja naye kwani nilikuwa nimekaa kiti cha nyuma. Nilikubali kukaa katika kiti hicho ndipo aliniambia kuwa ananipenda hivyo tufanye mapenzi kwani nimeshazoea," alidai shahidi.

Aliendelea kuieleza mahakama kuwa baada ya kukubali kukaa katika kiti cha mbele, Mbasha alipandisha vioo vya gari na kulaza kiti alichokuwa amekalia mtoto huyo na kuanza kumvua sketi yake na nguo za ndani.

Pamoja na hayo alimkaba shingo na kumziba mdomo kwa khanga ili asipige kelele na kumbaka kwa mara nyingine.

Shahidi huyo alieleza kwamba baada ya kitendo hicho kuisha, Mbasha alishuka kwenye gari na kumuacha dada huyo akiwa ndani ya gari na aliporudi alimtaka waendelee kufanya mapenzi kitendo ambacho mtoto huyo alikataa.

Hata hivyo, alidai baadaye alimtafuta Flora kwa simu na alipopokea hakumwambia kilichotokea hadi alipofika Sinza kwa dada zake ambako walimweleza Flora kwa njia ya simu kitendo alichofanyiwa na mumewe, huku akiwa haamini kilichotokea.

Alidai walitoka pamoja na dada zake kwenda kuripoti katika kituo cha Polisi cha Sinza na polisi waliokuwepo kituoni hapo waliwaamuru kutoa taarifa hizo katika kituo cha polisi ambacho tukio la ubakaji limetokea.

Hivyo walirudi hadi kituo cha Polisicha Tabata na kutoa taarifa.

Kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kifungu cha 186, kifungu kidogo cha tatu cha sheria za mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 kinaeleza kuwa mashauri yote ya ubakaji yanatakiwa kusikilizwa katika mahakama ya siri.

Wakili Katuga aliiomba mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo katika mahakama ya siri kwa kuwa mtoto huyo yupo chini ya miaka 18 na hairuhusiwi mtu yeyote asiyehusika kusikiliza mashauri hayo.

Kesi imeahirishwa hadi Septemba 12 mwaka huu.

Mbasha anashitakiwa kwa mashitaka mawili ambayo Mei 23 mwaka huu, maeneo ya Tabata Kimanga Wilaya ya Ilala, alimbaka mtoto wa miaka 17 nyumbani kwake. Pia alidaiwa Mei 25 mwaka huu, alimbaka tena mtoto huyo ndani ya gari kinyume na sheria.

IDADI YA WATU WANAOJIUA YAONGEZEKA DUNIANI

Shirika la afya ulimwenguni WHO limetowa ripoti yake inayosema kwamba idadi ya watu wanaojiua duniani imeongezeka na kufikia kiwango cha kutishaRipoti inasema kwamba katika kila sekunde 40 mtu mmoja anajiua.

Shirika hilo limelitaja tatizo hilo kama la kiafya ambalo linahitaji kushughulikiwa baada ya kufanya utafiti wake katika nchi 172 duniani.

Barani Afrika nchi zilizotajwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaojiua ni Msumbiji,Tanzania,Burundi Sudan Kusini na Uganda.

Tanzania iko katika nafasi ya pili barani Afrika ikiwa na asilimia 24.9 ya vifo hivyo vya kukusudia.

AJALI MBAYA YA BUS YAUA WATU 36 PAPO HAPO

Watu 36 wamefariki dunia papohapo na wengine 79 kujerihiwa vibaya katika ajali mbaya ambayo imetokea saa tano leo asbuhi katika kijiji cha sabasaba nje kidogo ya mji wa musoma wilaya ya butiama mkoani mara kwa kuhusisha mabasi mawili ya abiria na gari dogo aina ya Nissani Tellono yenye namba za usajili T332 AKK.

Mbali na gari hilo kugongwa na kutumbukia ndani ya mto mmoja katika daraja hilo kwenye barabara kuu ya Musoma-Mwanza pia mabasi mawili ambayo yamehusika katika ajali mbaya ni j4 express yenye namba za usali T677 CYC liyokuwa ikitokea jijini Mwanza kwenda sirari wilayani tarime ambalo limegongano uso kwa uso na basi la Mwanza coach yenye namba T736 AWJ lilokuwa likitokea Musoma kwenda jijini Mwanza.

Baada ya taarifa za ajali kusambaa katika manipaa ya musoma vilio na simanzi vimetawala katika mji huo wa Musoma mkoani Mara baada majeruhi na miili ya marehemu wa ajali hiyo kuanza kufikishwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara mjini Musoma.

Wakizungumza wakati wakipatiwa matibabu baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamesema kuwa ajali hiyo imesababishwa na mwendo kasi wa mabasi hayo hatua ambayo ilisababisha kushindwa kupishana katika daraja hilo hivyo kugongana uso kwa uso.

Akizungumza kwa niaba ya mganga mkuu wa mkoa wa Mara Dk Martin Khan,amesema kuwa wamepokea maiti na idadi kubwa ya majeruhi na wengi wao hali zao si za kuridhisha.

Hata hivyo Dk Khan ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kujitolea damu kwani amesema kuwa hospital hiyo ya rufaa ya mkoa wa mara inakabiliwa na upungufu mkubwa wa damu katika kuhudimia wagonjwa wakiwemo majeruhi wa ajali.

kamanda wa polisi mkoa wa Mara ACP Alex Kalangi, akizungumza kwa njia ya simu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba taarifa rasmi za jeshi la polisi zitatolewa baada ya kupata taarifa kutoka kwa madaktari na kwamba ametoa wito kwa wananchi kujitokea katika hospitali ya mkoa kwa ajili ya kutambua miili ya marehemu.