WATU 20 WANAOCHOCHEA MAUAJI AFRIKA YA KATI

Shirika la kupigania haki za kibinadamu lenye makao yake mjini Washington Marekani Amnesty International limewataja watu 20 inayowatuhumu kwa kuendeleza mauaji ya kimbari katika jamhuri ya Afrika ya kati CAR.


Viongozi wa kadhaa wa makundi ya waasi pamoja na marais wawili wa zamani wamo katika Orodha hiyo ambayo Amnesty International inasema ndio wanaochochea kufadhili na kuendeleza mauaji ya halaiki nchini humo.

Aliyekuwa rais wa taifa hilo Francois Bozize aliyeng'olewamadarakani na kundi la wapiganaji wa Seleka chini yauongozi wake Michel Djotodia, mwezi Marchi mwaka uliopita pamoja na Djotodia mwenyewe wametajwa.


Djotodia aliyeongoza makundi ya waislamu wachache(Seleka) alishurutishwa kunga'atuka madarakani na viongozi wa mataifa jirani mapema mwaka huu, lakini kuondoka kwake kukaibua changamoto nyengine kwani sasa makundiya wapiganaji wafahamikao kama Anti-Balaka walianza kuwavamia na kuwauwa Waislamu ambao walidaiwa kuwaunga mkono wapiganaji wa Seleka.


Robo ya idadi ya wananchi wa taifa hilo milioni 4.6 walilazimika kutoroka makwao kuepuka mapigano

Katika Ripoti hiyo yenye kichwa '' Time for Accountability'' Amnesty inasema kuwa viongozi hao wanaoongoza mauaji hayo hawana uwoga wowote kuwahuenda wakachukuliwa hatuana mtu yeyote kwa serikali yataifa hilo ni hafifu sana kwa sasa.


Aidha kuweko kwa zaidi ya maafisa elfu 7 wa kulinda amani nchini humo hakujasaidia chochote kwani kwa sasa vita vimekuwa kuuwa na kulipiza kisasi.

Kwa mujibu wa Christian Mukosa jumuiya ya mataifa inapaswa kuwachukulia hatu kali wale waliotajwa kwani nawao pia wamewanyika amani watu wa jamhuri ya Afrika ya kati.


Amnesty imemtaja kiongozi wa kijeshi wa kundi la Seleka Nourredine Adamkuwa mtuhumiwa mkuu wa visa vya mauaji,ubakaji na mauaji ya halaiki yaliyotokea kati ya Desemba mwaka wa 2012 hadi Januari mwaka huu.Kundi hilo bado linadhibiti kaskazini mwa taifa hilo ambako Amnesty inetrnational inadai visa vya ukiukaji wa haki za kibinadamu vinaendelea kwa kulipiza kisasi dhidi ya watu wasiokuwa wakislamu.


Kwa Upande wa Anti Balaka, Amnesty International imeonya kuwa kundi hilo silo lile lililodhaniwa kuwa ni kundila vijana bali sasa limegeuka na kuwa kundi lenye uwezo mkubwa kijeshi na kuwa linajumuisha wanajeshi aliokuwa wakihudumu wakatiwa enzi za uatawala wake aliyekuwa rais wa taifa hilo Francois Bozize.

Aidha Anti Balaka imewalazimisha waislamu wengi kutoroka mji mkuu wa Bangui ambapo wengi waliuawa.


Kwa sasa Amnesty International inasema kuwa shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia maslahi ya wakimbizi linaendelea kuwahamisha waislamu kutoka maeneo chini ya Anti-Balaka na kuwapelekea maeneo chini ya utawala wa Kundi la Seleka ambapo wanakubalika.


Vilevile Kidole cha lawama kimewaelekea wanajeshi wa kulinda amani kutoka Chad ambapo Amnesty inasema kuwa waliwauawa wakaazi wa mji wa Bangui mwezi Machi.

Rais wa serikali ya mpwito Catherine Samba-Panza, ameiomba mahakama ya jinai ICC kuchunguza tukio hilo.