Mama mmoja amekiri kuwaua watoto wake watatu kwa sababu ya ulemavu wao.
Tania Clarence, mwenye umri wa miaka arobaini na miwili alikiri kosa hilo la kuwaua watoto wake watatu wakiwemo vijana pacha wa miaka mitatu na msichana mmoja mwenye umri wa miaka minne kwa misingi kuwa wanawe walikuwa walemavu mno.
Baba ya watoto hao alikuwa ameenda Afrika Kusini wakatiwa mauaji hayo.
Mama huyo ambaye ametoka eneo la New Malden kusini Magharibi mwa London,alikana kufanya mauaji hayo. Watoto hao ambao walikuwa na ugonjwa wa uti wa mgongo,walipatikana nyumbani kwao tarehe 22 Aprili mwaka huu.
Ugonjwa huo wa kimaumbile husababisha watoto kuwa na uwezo mdogo sana wa kusongesha mwili na pia huwa hawaishi kwa mda mrefu.
Mwanamke huyo alitibiwa kwa majereha aliyoyapata kwa kujikata na baadaye kushitakiwa tarehe ishirini na nne Aprili.
Alizuiliwa katika hospitali ya matibabu ya akili na tarehe ya kesi kupangwa siku ya ishirini na tatu Februari mwaka ujao katika korti iyo hiyo.