HOUSE GIRL AMUUA BOSS WAKE KWA KISU

Binti wa kazi za ndani (house girl) anayejulikana kwa jina la Valetina Kerenge (17) amemchoma kisu Bosi wake cha sehemu ya juu ya titi la kulia kwa madai ya kunyanyashwa na tajiri yake huyo.


Kamanda wa polisi Mkoani Singida (SACP) Geofrey Kamwela alisema tukio hilo limetokea jana eneo la Sabasaba Kata ya Utemini Manispaa ya Singida saa 4 asubuhi.


Kamanda Kamwela alimtaja marehemu kuwa ni Asha Juma (24) ambaye ni Karani wa Mahakama ya Wilaya ya Singida.


Baada ya marehemu kuchomwa kisu na msichana wake huyo, alifanikiwa kutoka nje ya nyumba na kukimbilia kwa majirani kwa ajili ya kuomba msaada, lakini wakati majirani wakiwa katika harakatiza kumpeleka hospitali, alianguka chini na kufa papo hapo."Alisema Kamanda Kamwela