USA KUONGEZA VIKOSI 200 IRAQ

Rais Barak Obama ametangaza kuwa anatuma vikosi 200 zaidi , na pia helikopta zisizoKuwa na ruban nchini Iraq.


Katika barua yake wa baraza la Cogress rais Obama amesema kuwa vikosi hivyo vitatoa msaada wa nyongeza na usala kwa ubalozi mjini Baghdad.


Rais Obama amesema vikosi hivyo vya ziada vimepewa mafunzo kabambe ya kijeshi na majukumu yao makuu yatakuwa kuwalinda raia wa Marekani na mali zao huko Iraq.


Wataungana na wanajeshi wengine wa Marekani walioko Badghad wanaolinda ubalozi wa Marekani.


Katika barua yake kwa bunge la Congress, Obama amaesema amepeleka pia helicopters, na ndege zisizo na rubani kuimarisha ulinzi huo.


Tayari Marekani washapeleka washauri wakijeshi wapatao 180 kufanya kazi na jeshi la Iraq.


Obama kupeleka pia ndege za kivita zisizo na rubani 'drones' huko Baghdad

Hata hivyo idadi ya jumla ya wanajeshi wa Marekani nchini Iraq ni kama 750 pekee.


Huku mapigano yakiendelea kuchacha huko Iraq rais Obama amesisitiza hatapeleka majeshi ya ardhini nchini lakini hatua ya kufanya mashambulizi ya angani dhidi ya kundi la wapiganaji wa ISIS huenda ikachukuliwa.


Wakati huohuo Balozi wa Saudi Arabia katika umoja wamataifa amekana madai ya Waziri mkuu wa Iraq , Nouri Maliki kwamba nchi yake inatoa usidizi wowote kwa kundi la ISIS na pia kupinga nadharia kuwa usaidizi wa Saudia kwa waasi wa Syriaumechangia kuliinua kundi hilo la ISIS.


Tangazo la kundi hilo la ISIS hapo jana kwamba wataunganisha ardhi walizoziteka huko Iraq na Syria ndio waunde eneo mojawanalolitaja kama 'Islamic Caliphate' litakalotawaliwa na sheria kali za kiislamu, liwawatia tumbo joto mataifa mengi ya mashariki ya kati namataifa ya kizungu hasa Marekani.


Kwa kipindi cha mda mfupi ISIS imeweza kushambulia na kuyateka maeneo makubwa kwa kasi iliyowashangaza wengi huku serikali za nchi husika zikishindwa kukabiliana nao.


Kuzuka kwa kundi hili kunaleta tisho jipya katika mashariki ya kati ambayo tayari inayumbishwa na vita na vizozo mbalimbali ya kisiasa.