ANYONGWA KWA CHANDARUA NA WEZI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Goerge Mayunga Mzee Furgensi Batura (72), Mkazi wa Kijiji cha Nyamiyaga Kata ya Bugomora Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ameuawa kwa kunyongwa kwa chandarua na wezi nyumbani kwake na kumuibia kahawa.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Goerge Mayunga alisema kuwa mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia jana baada ya wezi hao kuvamianyumbani kwake na kumkuta nje ya nyumba yake akilinda kahawa na mjukuu wake, Shukuru John (16).


Mayunga alisema baada ya wezi hao kuvamia nyumbani hapo, walimfunga mzee huyo na mjukuu wake kwa chandarua shingoni.


Alisema mzee huyo alikufa baada ya chandarua hicho kumnyonga shingoni na mjukuu wake kunusurika nawezi hao kuiba magunia saba ya kahawa yenye thamani ya Sh. 700,000.


Alisema polisi wanawashikilia Wakazi wawili wa Bugomora na kuendelea kuwasaka wegine kwa tuhuma za mauaji hayo na wizi wa magunia hayo ya kahawa.


Mayunga alisema Spelius Lukokerwa aliyekutwa na kahawa hiyo inayodaiwa kuibwa nyumbani kwake alikufa baada ya kufikishwa kituo cha afya Murongo kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa wananchi.

Chanzo: NIPASHE