Kundi la Hamas limesema kuwa wapiganaji wake sita waliuawa katika shambulizi moja karibu na eneo la Rafah Kusini mwa nchi hio.
Mashambulizi hayo yanajiri baada ya kurushwa kwa roketi kutoka ukanda wa Gaza kwenda Kusini mwa Israel ambapo wanajeshi watatu waliuawa.
Kundi la wanamgambo la Hamas linasema kuwa wapiganaji wake sita waliuawa wakati wa mashambuzi hayo na wengine watatu kuuawa eneo tofauti.
Hamas wanasema kuwa watalipiza kisasi mauaji hayo.
Hali ya wasi wasi imetanda tangu kuuawa kwa kijana mpalestina Mohammed Abu Khdeir.
Mnamo siku ya Jumapili, polisi waliwakamata washukiwa sita wa kiyahudi kufuatia mauaji ya kijana huyo wakisema kuwa walimuua kwa sababu ya uraia wake.
Taarifa zaidi bado hazijatolewa kwa sababu kesihiyo imebanwa kuzungumziwa.
Mauaji ya Abu Khdair yalitokea kufuatia mauaji ya vijana watatu wa kiyahudi katika eneo la West Bank. Miili yao ilipatikana wiki moja iliyopita.
Israel inasema kuwa wapiganaji wawili wa kipalestina waliwateka nyara vijana hao kisha kuwaua, ingawa Hamas imekanusha kuhusika na mauaji hayo.