WANAUME NA WAVULANA WATOROSHWA PWANI YA KENYA

Idadi kubwa ya watu wameanza kuhama mji wa Hindi, karibu na eneo la Lamu, Pwani ya Kenya.

Mji huo ulishambuliwa na wapiganaji wa Al Shabaab na kuwaua watu 29.


Mashambulizi hayo yametokea chini ya mwezi mmoja tangu mashambulizi mengine kutokea eneo jirani la Mpeketoni ambako zaidi yawatu sitini waliuawa.


Inaarifiwa wakaazi wanawatorosha wavulana na wanaume kwa sababu ya hofu kuwa wao ndio wanalengwa kwa mashambulizi washambuliaji wanapofika kutekeleza mashambulizi.

Wakaazi wanahamia maeneoya Mpeketoni na Malindi kutafuta hifadhi.


Wamelalamikia serikali kwa kukosa kuwapa ulinzi wa kutosha kwani siku moja kabla ya mashambulizi walikuwa wamehakikishiwa usalama wao ingawa kesho yake mashambulizi yakawakuta.


Hata hivyo mkuu wa kaunti ya Lamu, Miiri Njiri, ameiomba serikali kupeleka wanajeshi wa KDF pamoja na polisi wa kupambana na ghasia katike eneo zima la Lamu ili kulinda usalama wa wananchi.


Naibu Rais William Ruto, ametoa makataa ya saa 48 kwa maafisa wakuu wa usalama katika pwani ya Kenya kuwakamata washambuliaji waliofanya mauaji mwishoni mwa wiki Polisi wanalaumu kundi la MRC linalotaka eneo la Pwani kujitenga na Kenya licha ya AlShabaab kukiri kufanya mashambulizi hayo.


Mashambulizi ya Jumamosi yalitokea karibu na eneo la Mpeketoni ambako watu 65 waliuawa mwezi jana , katika mauaji ambayo kundi la Al Shabaab pia lilikiri kuyatekeleza.


Serikali hata hivyo ilidai kuwa mashambulizi hayo yalichochewa kisiasa wala hayakutekelezwa na kundi la Al Shabaab.


Mashambulizi ya mara kwa mara na kudorora kwa hali yausalama katika eneo la Pwanini changamoto kubwa kwa sekta ya utalii ambayo imepata pigo kubwa