Zitto ametoa kauli hiyo jana Dar esSalaam, alipokutana na waandishi wa habari kufafanua hatua ya Kamati Kuu ya chama hicho ya Ijumaa iliyopita, kutangaza kumvua madaraka yote aliyokuwa nayo ndani ya chama hicho.
Katika mkutano huo, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Dk Kitilya Mkumbo, alimsafisha Zitto, akidai kwamba hakuhusika katika makakati wa kung'oa uongozi uliopo madarakaniwa Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa.
Aidha Mwanasheria wa wanasiasa hao, Diwani wa Mabogini Moshi Vijijini, Albert Msando (Chadema), ambaye amewahi pia kuwa Mwanasheria wa Mbowe katika kesi zake Arusha, alielezea kumkabili Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, kwa madai ya kukiuka Katiba ya chama hicho, wakati wa kutangaza kumvuamadaraka Zitto.
Usafi wa Zitto, Dk Mkumbo alirudia kukiri kwamba yeye ndiye aliyeandaa na kuhariri mkakati wa kung'oa madarakani viongozi wa sasa wa juu wa Chadema, akishirikiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa ChademaMkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na kiongozi mmoja aliye na nafasi za juu katika chama hicho, ambaye alisema muda ukifika atajitaja mwenyewe.
"Zitto Zuberi Kabwe hajafukuzwa kwa sababu ya waraka huu yeye hakuhusika kwa namna yoyote kuandaa," alisema Dk Mkumbo huku Zitto akikiri kuwa hakufahamu mkakati wala waraka huo na kwamba kwa mara ya kwanza aliuona katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichomvua madaraka.
Kukabiliana na MboweAlipoulizwa kama yeye anakubali maudhui ya waraka huo, ambayo yalikuwa yamemuandalia mkakati awe Mwenyekiti wa Taifa Chademana mbinu za kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi ujao, Zitto alisema swali hilo ni gumu lakini angefurahi kama angepata nafasi ya kuuona waraka huo mapema, iliaufanyie kazi.Alipotakiwa kufafanua wazi kama yuko tayari kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Zitto ambaye alisisitiza angependa kuona waraka wa kumweka madarakani mapema ili aufanyie kazi, alijibu kwamba hataki kuthibitisha kama atagombea nafasi hiyo au la, kwa kuwa hataki kukiuka utaratibu wa chama ila muda ukifika wakati wagombea wakiruhusiwa kujitangaza, atazungumza.
Mbali na hapo, aliwatuliza mashabiki wake pale alipozungumzia kinachoendelea ndani ya Chadema, kwamba ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa za majitaka.
Lisu avunjaKatiba Wakili Msando ambaye katika mkutano wa jana, alizungumza kama Wakili wa Zitto na Dk Mkumbo na wakati huo huo, mshereheshaji, alisema Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Lisu amekiuka Katiba ya chama wakati wa kutangaza kuwaadhibu Zitto na Dk Mkumbo.Kwa mujibu wa Msando, Katiba ya Chadema inataka kabla ya kumvua kiongozi madaraka au kutangaza adhabu yoyote, anapaswa kupelekewa mashitaka yake kwa maandishi na kupewa siku 14 kujibu kwa maandishi.
Baada ya kujibu kwa utaratibu huo,mshitakiwa ataitwa katika kikao kinachohusika na kutakiwa kujitetea kwa mdomo na baada ya hapo kikao kitatafakari hatua ikiwemo adhabu kwa muhusika, ambayo nayo itapelekwa kwake kwa maandishi.
Wakili Msando alisema pamoja na Lisu kuwa wakili mzoefu, lakini amekiuka utaratibu wa Katiba yao kwa kuwa mpaka sasa si Zitto, walaDk Mkumbo aliyepokea hati ya mashitaka yanayowakabili, zaidi ya kuambiwa kwamba wamevuliwa madaraka.
Akifafanua zaidi ukiukwaji huo wa Katiba, pamoja na kukubali adhabualiyopewa, Dk Kitila alisema Kamati Kuu haina uwezo wa kumvua nafasi yake moja kwa moja kwa kuwa mamlaka yake ya uteuzi, yenye mamlaka ya kumuadhibu ni Baraza Kuu."Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema, Sura ya Sita, Ibara ya 6.3.6 (b), inasomeka hivi. 'Kiongozi aliyeteuliwa na vikao vya uongozi, ataweza kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao kilichomteua," alinukuu Katiba Dk Mkumbo na kuongeza; "Mimi nilichaguliwa na Baraza Kuu na ni kikao hiki pekee chenye uwezo wa kunivua nafasi niliyokuwa nayo.
"Usanii wa akina SlaaKatika kile alichoelezea kuwa ni usanii, Zitto alisema sababu za kuvuliwa madaraka zilizotangazwa katika mkutano na waandishi wa habari Ijumaa iliyopita, ni tofauti na alizoambiwa katika Kamati Kuu."Ukweli ni kwamba waraka uliotajwa si sababu ya mimi kuvuliwa nafasi zangu za uongozi kama ilivyojadiliwa katika kikao chaKamati Kuu, sababu za kufukuzwa kwangu kama zilivyojadiliwa katika kikao hicho ni tuhuma lukuki ambazo si mara yangu ya kwanza kuzisikia zikijadiliwa ndani na nje ya vikao vya chama," alisema.
Alisema hitimisho la tuhuma hizo ni yeye kuitwa msaliti wa chama kwa kutumika na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Usalama wa Taifa.
Alibainisha tuhuma hizo kuwa ni pamoja na madai kuwa hakushiriki kumpigia kampeni mgombea uraiswa chama hicho, Dk Willibrod Slaa katika uchaguzi wa mwaka 2010 na madai kuwa katika Mkoa wa Kigoma alishindwa kuwapigia kampeni wagombea wa chama hicho na hivyo kushinda mwenyewe.
Tuhuma nyingine ni pamoja na kushiriki kuwashawishi wagombea wa Chadema katika baadhi ya majimbo kujitoa katika uchaguzi wa mwaka 2010, ili kuwapisha wagombea wa CCM wapite bila kupingwa kwa njia ya rushwa na madai kuwa amekuwa hashiriki katika operesheni mbalimbali za chama hicho.
Aidha Zitto alitaja tuhuma nyingine, ambayo ilichukua muda mrefu kujadiliwa kuwa ni madai kwamba amedhalilisha chama kwa tamko la Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) kwamba hesabu za vyama hazijakaguliwa naMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ikiwa ni pamoja na kuitwa mnafiki kwa kukataa kuchukua posho ya vikao.
Ajibu tuhuma Akijibu tuhuma hizo,Zitto alisema kati ya viongozi wa chama hicho waliofanya ziara nyingi katika mikoa na majimbo katika kampeni za 2010 yeye anaongoza.
Alisema alifanya kampeni katika mikoa na majimbo 16, huku Mkoa wake wa Kigoma ukiongoza kwa kuipatia kura za urais Chadema iliyopata asilimia 45 na kufuatiwa na Kilimanjaro uliyoipatia kura asilimia 37.
Kuhusu kuwa ushindi pekee wa ubunge mkoani Kigoma na wagombea wengine wa chama hicho kukosa, alisema hana uwezo na suala hilo kwa kuwa uamuzi ni wa Wanakigoma na cha msingi ni kuangalia wapi walikosea na kujirekebisha ili isijirudie 2015.
Kuhusu kushawishi wagombea wa chama hicho kukacha nafasi zao kupisha wagombea wa CCM, Zitto alitaja majimbo anayotuhumiwa kufanya hivyo kuwa ni kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Musoma Vijijini kwa Nimroad Mkono na Singida Mjini kwa Mohammed Dewji.
"Kama nilivyokwisha kueleza katikavikao mbalimbali vya chama jambohili si la kweli na hakuna popote ambapo watoa tuhuma hizi wamewahi kutoa ushahidi kwamba nilifanya jambo hili. Nipo tayari kwa uchunguzi ndani ya chama na watoa tuhuma waje na ushahidi bayana wa jambo hili," alifafanua.
Kuhusu tamko la PAC ambalo yeye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto alisema anachofahamu na kuamini kuhusu suala hilo ni kwamba utawala bora hautaki kiongozi kama yeye, kutumia nafasi yake ya uenyekiti wa PAC kulinda chama chake.
Alidai akifanya hivyo na kuonea vyama vingine atakuwa akiendeleza tabia ambazo chama hicho inapinga vikali. Kuhusu suala la posho ya vikao Zitto alisisitiza kuwa hapokei posho yoyote ya vikao ndani na nje ya Bunge tangu 2011, hiyo ikiwa ni pamoja na posho za vikao vyote katika Kamatiza Bunge anazohudhuria na huo ni msimamo wake wa kutekeleza kwavitendo mwito wa Chadema kupinga posho za vikao.