MWALIMU ALA NJAMA ZA KUMLAWITI MWANAFUNZI

Katika hali isiyo ya kawaida, mwalimu wa Shule ya Sekondari Nyerere iliyopo wilayani hapa mkoani Kilimanjaro anatuhumiwa kuwakodi vijana watatu wamlawiti mwanafunzi wa kidato cha tatu na kumsababishia maumivu makali huku mwalimu huyo akidaiwa kupiga picha unyamahuo.

Akizungumza na gazeti hili mwanafunzi aliyefanyiwa unyama huo alidai, bila kujua njama za mwalimu wake alikubali kuitika wito na alipomfuata walitokea waendesha bodaboda na kumteka na kumpeleka katika moja ya nyumba zao, ambapo walimpiga na shoti ya umeme, baadaye alipokuwa hajielewi walimwingiza karoti na baadaye kumlawiti kwa zamu.

Mwanafunzi huyo amesema hajui kosa lake na anasikitika kwa unyama huo na kuiomba Serikali ichukue hatua stahiki kwa wahusika.

Kwa sasa mwanafunzi huyo anaendelea vizuri na matibabu.

Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa alisema, mwanafunzi huyo amekutwa na balaa hilo kufuatia mwalimu anayetuhumiwa kurudi nyumbani na kukuta mtoto wake wa kike wa miaka mitatu akiwa chumbani kwa mwalimu mwenzake anayeishi na mwanafunzi huyo. "Alipomwita mtoto wake alidai alichelewa kutoka na akahisi huenda mwanae amefanyiwa kitendo kibaya lakini alipompeleka hospitali kwa vipimo hakukutwa na dalili ya kubakwa," alisema mwalimu huyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz alithibitisha kutokea kwa tukio hilo Novemba 3, mwaka huu saa 12 jioni katika maeneo ya Lembeni wilayani hapa.

Alisema mwalimu na wanaume waliomfanyia kitendo hicho mwanafunzi huyo wanashikiliwa na kwamba watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma.


Kutoka:Mwananchi