AFARIKI DUNIA BAADA YA PIPI ZINAZOZANIWA KUWA ZA DAWA ZA KULEVYA KUPASUKIA TUMBONI

MNAMO TAREHE 07.11.2013 MAJIRA YA SAA11: 00 HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA.

KASSIM SAIDI MBOYA, MIAKA 36, MKAZI WA DSM ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.

MAREHEMU ALIFAHAMIKA JINA KWA MUJIBU WA HATI YAKE YA KUSAFIRIA NAMBA – AB 051010 KUTOKA DSM KUELEKEA LILONGWE NCHINI MALAWI.

MAREHEMU ALIKUWA ANASAFIRI AKIWA KATIKA BASI LA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJIRI T.319 BLZ AINA YA NISSAN KWA MUJIBU WA TIKETI YAKE ILIYOKUWA NA JINA LA KASSIM MUECK MICHAEL, AKIWA NA BEGI DOGO LENYE SURUALI MOJA AINA YA JEANS, T-SHIRT MOJA NYEUSI, RABA JOZI MOJA RANGI NYEKUNDU, MKATE MMOJA , MKOBA MDOGO WA KIUNONI, VACCINATION CARD MBILI ZA KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RANDI MBILI SARAFU ZA AFRIKA KUSINI NA MIFUKO SITA YA RAMBO RANGI NYEUSI.

AWALI BASI HILO BAADA YA KUFIKA MPAKANI KASUMULU NA ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE GARI HILO NA KUANZA KUFANYA TARATIBU ZA KUVUKA MPAKA KUINGIA NCHINI MALAWI, MAREHEMU ALIBAKI NDANI YAGARI HUKU HALI YAKE YA KIAFYA IKIZIDI KUDHOOFIKA.

WAHUSIKA WA GARI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO MAREHEMU ALICHUKULIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA KWA MATIBABU. HATA HIVYO KABLA HAJAPATA MATIBABU ALIFARIKI DUNIA.

KUFUATIA DALILI ALIZOKUWA NAZO KABLA YA KUFARIKI ILIBIDI MWILI WA MAREHEMU USAFIRISHWE HADI HOSPITALI YARUFAA MBEYA NA KUFANYIWA UPASUAJI AMBAPO ZILIPATIKANA PIPI 65 ZA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA KULEVYA ZIKIWA TUMBONI KWA MAREHEMU NAMOJA KATI YAPIPI HIZO IKIWA IMEPASUKA.

TARATIBU ZINAFANYWA ILI DAWA HIZO ZIPELEKWE OFISI YAMKEMIA MKUU WA SERIKALI KWA UCHUNGUZI WA KITAALAM IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA AINA YA DAWA.

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO.

KAMANDA WA POLISI. MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA KWANI SIO TU NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI BALI PIA NI HATARI KWA AFYA YAMTUMIAJI.

AIDHA ANATOA RAI KWA WAKAZI WA MBEYA NA TANZANIA KWA JUMLA KUFIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA AJILI YA UTAMBUZI WA MWILI WA MAREHEMU.

[DIWANI ATHUMANI- ACP]KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Source: Mbeya Yetu