AUWAWA KWA KUKATWA NA PANGA KICHWANI

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mele Seni (60) Mkazi wa Kijiji cha Kapalala Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ameuwawa kwa kukatwa na panga kichwani na mgongoni na watu wasio fahamika wakati akiw nyumbani kwake akiota moto.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari tukio hilo la mauwaji ya kinyama yalitokea hapo jana majira ya saa moja na nusu usiku nyumbani kwa marehemu huyo kijijini hapo.

Alisema siku hiyo ya tukio marehemu akiwa nyumbani kwake amejipumzisha akiota moto ghafla walitokea watu wasiofahamika na kupiga hodi nyumbani kwa marehemu ambae nae aliwakaribisha watu hao kwa kujua ni watu wema.

Alieleza ndipo watu hao walipoanza kumshambulia marehemu kwa kumkata kwa panga kwenye kichwa na mgongoni huku marehemu akiwa anapiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani zake.

Kidavashari alisema licha ya marehemu kupiga moyowe majirani zake hawakuweza kujitokeza mapema kuweza kumpatia msaada na ndipo watu hao walipoona Mele Seni amefariki dunia walitokomea kusiko julikana.

Majirani waliweza kufika nyumbani kwa marehemu baadaya muda mrefu wa kutokea kwa tukio hilo ambapo walimkuta marehemu akiwa ameisha fariki dunia huku mwili wake ukiwa na majeraha ya panga kichwani na mgongoni na kisha walitowa taarifa kwa uongozi wa serikali ya kijiji ambao nao walitowa taarifa kwa jeshi la polisi.

Kamanda Kidavashari alieleza kabla ya tukio hilo marehemu alikuwa akilalamikiwa na majirani zake na wanakijiji hichokuwa amekuwa akijihusisha na vitendo vya kishirikina kwa kuwaroga watu kijijini hapo.

Hivyo uchunguzi wa awali uliofanywa na jeshi la Polisi umebaini kifo hicho kametokanana imani ya ushirikina ulisababisha wanakijiji hicho kumjengea chuki marehemu huyo.

Mpaka sasa hakuna mtu au watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hili na jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ili kuwakamata na kuwafikisha mahakamani waliohusika katika tukio hili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi ametowa wito kwa wananchi kutojichukilia sheria mkononi kutokana na kuwahusisha watu na imani za kishirikina na matokeo yake wamekuwa wakiua watu pasipo sababu.


Source:Katavi Yetu Blog