KESI YA UAMSHO KUSIKILIZWA JANUARY

Kesi inayowakabili viongozi 10 wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiisalam Zanzibar(Jumiki), inatarajiwa kuanzakusikilizwa Januari mwakani.

Hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa rufaa mbili zilizokuwa zimefunguliwa na upande wa mashtaka na utetezi katika kesi hiyo ambayo ni ya nne ya mwaka 2012.

Habari zilizopatikana zinasema kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa naJaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu.

Kesi hiyo jana ilitajwa mbele ya Naibu Mrajisi wa Mahakama Kuu Zanzibar, Ali Ameir na kupangwa tarehe hiyo.

Mrajisi Amir alisema mahakama imelazimika kupanga siku hiyo kwa sababu siku za katikati kutakuwa na Sikukuu za Krismasi, Mwaka Mpya na likizo ya mahakama.

Alisema kuanzia wiki ijayo, Mahakama ya Rufaa Tanzania, itaanza vikao vya kusikiliza kesi za Zanzibar na Kuutaka upande wa utetezi kukubaliana muda mwafakawa kutajwa kesi kabla ya kuanza kusikilizwa hapo mwakani.

Kesi hiyo inayohusu uharibifu wa mali na kuhatarisha Usalama wa Taifa inawahusu washtakiwa kumi akiwamo Sheikh Farid Hadiy Ahmed.

Watu hao wanatuhumiwa kuharibu miundombinu na mali zenye thamani ya Sh500 milioni kutokanana vurugu zilizotokea visiwani Zanzibar, mwaka jana Hata hivyo, upande wa mashtaka katika kesi hiyo umeeleza kwamba jalada la kesi ya msingi bado halijarejeshwa Zanzibar kutoka Mahakama ya Rufaa Tanzania.