WATUPWA JELA MIAKA 70 KWA KUKAMATWA NA MENO YA TEMBO

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imewahukumu watu watatu kutumikia kifungo cha jumla ya miaka sabini jela bada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na meno ya tembo manne yenye thamaniya shilingi milioni 45.

Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya kulidhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka na upande wa utetezi.

Waliohukumiwa kifungo hicho ni Gwabi Mayala (39) mkazi wa kijiji cha Majimoto Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi ambae alikuwa mshitakiwa wa kwanza amehukumiwa kifungo cha miaka 30 na kulipa fidia ya shilingi milioni 45 Washitakiwa wengine waliohukumiwa ni Mashaka Mabanga (33) Mkazi wa Sumbawanga Mkoa wa Rukwa na Adamu Kalinzi (30)Mkazi wa Kijiji cha majimoto Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wamehukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka ishirini jela.

Awali katika kesi hiyo ilidaiwana mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Fadhili Mwandoloma kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo hapo Oktoba 10 mwaka huu majira ya saa nne usiku katika Kijiji cha Majimoto Wilayani Mlele Wanadaiwa siku hiyo ya tukio washitakiwa walikamatwa wakiwa na meno manne ya Tembo yenye uzito wa kilo kumi na sita yenye thamani ya shilingi milioni 45 wakiwa katika harakati ya kuyauza.


Mwanasheria huyo wa Serikali aliiambia mahakama kuwa Mshitakiwa wa kwanza Gwabi Mayala ndiye aliyekuwa mwenye meno hayo ya Tembo na aliwashirikisha wenzake hao wawili kwa ajiri ya kumtafutia wateja ambao wangeyanunua meno hayo ya Tembo Aliiambia mahakama baada ya washitakiwa hao kukamatwa na Askari wa Hifadhi ya wanyama pori ya Katavi walioshirikiana na polisi washitakiwa walipofikishwa polisi mshitakiwa wa pili na watatu walikiri kuhusika na meno hayo ya tembo na kudai kuwa meno hayo ni ya mshitakiwa wa kwanza Gwabi Mayala.


Hakimu mkazi mfawidhi Chiganga baada ya kusikiliza mwenendo mzima wa kesi hiyo aliiambi mahakama kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo wa pande mbili za mashitaka na utetezi mahakama imewaona washitakiwa wote watatu wanahatia hivyo kabla ya mahakama haijatowa adhabu inatowa nafasi kwa washitakiwa kujitetea Katika utetezi washitakiwa Mashaka na Adamu walikiri kukamatwa na meno hayo ya Tembo lakini walidaikuwa meno hayo ya Tembo yalikuwa ni ya mshitakiwa wakwanza Gwabi Mayala ambae alikuwa amewaomba wamtafutie wateja wa kuyanunua kwa upande wake mshitakiwa Gwabi aliiomba mahakama isikubaliane na maelezo ya washitakiwa wenzake kuwa meno hayo yalikuwa sio ya kwake.


Hakimu Chiganga alieleza mahakama kuwa washitakiwa wamevunja sheria ya kifungunamba 86 (1) (2) cha sheria ya huifadhi ya mwaka 2009 na kifungu namba 57 na 60 ya sheria ya kuhujumu uchumi sura ya 200 ya mwaka 2002 hivyo mahakama imetowa adhabu kwa mshitakiwa wa kwanza Gwabi Mayala kutumikia kifungo cha miaka 30 jela la kulipa fidia ya shilingi milioni 45 ambayo ni thamani ya meno hayo ya TemboPia washitakiwa Mashaka Mabanga na Adamu Kalinzi wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kushirikiana na mshitakiwa wa kwanza katika biashara ya kumtafutia wateja wa kununua meno ya Tembo.

Kwa hisani ya: Katavi yetu blog