DALADALA YAGONGA TRENI NA KUUWA WAWILI

Watu watatu wamekufa na wengine sita kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti zilizohusisha daladala aina ya Toyota DCM lenye namba za usajili T474 AST, kuligonga treni na lingine likipinduka.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Ilala, Marieta Minangi alisema tukio hilo la basi kuligonga treni lilitokea Novemba 18 saa, 3 usiku eneo la Karume, karibu na Machinga Complex.

Ajali hiyo ilitokea makutano ya Barabara ya Kawawa na Reli. Basi hilo liliigonga treni na kusababisha vifo vya watu wawili, ambao ni Bakari Sajina (25) na Suleimani Adili (38).

Treni ilikuwa ikitoka Ubungo na DCM ikitoka Chang'ombe.

Wakati huohuo ajali nyingine ilitokea eneo la Pugu Kanisani baada ya Toyota DCM kumshinda dereva wake kabla ya kupinduka nakusababisha kifo chake.