RAIA WA ITALIA ISHIE BURUNDI AKAMATWA NA MAFUVU YA BINADAMU

Polisi nchini Burundi wanasema zaidi ya mafuvu 40 ya binadam yamepatikana katika makao ya raia mmoja wa Italia anayefanya kazi nchini humo.

Giussepe Favaro alikamatwa mwezi uliopita baada ya mafuvu mawili yaliyonuiwa kusafirishwa kwa ndegekunaswa katika uwanja wa ndege nchini Burundi.

Kwa mujibu wa polisi mafuvu hayo yalinuiwa kusafirishwa hadi nchini Thailand.

Polisi hata hivyo hawajatoa taarifa zaidi na mwandishi wa BBC nchini Burundi anasema watu wana shaukuya kutaka kujua mafuvu hayo yalitoka wapi na yalikua yatumike kivipi.

Kumekuwepo ripoti za sehemu za miili ya binadam kutumika katika ushirikina hasa katika nchi jirani ya Tanzania, lakini haifahamiki kwanini mafuvu yaliyopatikana hapo awali yalikua yakipelekwa Thailand.

Bwana Favaro amekua akiishi nchini Burundi kwa miaka kadhaa.