JESHI LA POLISI LAMTAJA ALIYE NA LAPTOP YA DR. MVUNGI

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemtaja mkazi wa Vingunguti, kuwa ndiye aliye na kompyuta mpakato ya aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, marehemu Dk Sengondo Mvungi.

Hata hivyo Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova amesema mkazi huyo Abdul ThabitChief (20) anaendelea kusakwa sambamba na wahusika wengine walioshiriki kusababisha kifo cha Dk Mvungi.

kushambuliwa na watu wasiojulikana ambapo viliibwa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kompyuta, fedha na bastola. Kamanda Kova alisema jana kuwa mpaka sasa watuhumiwa 10 wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

"Jeshi la Polisi linaendelea na jitihada kubwa kwa lengo la kuipatakompyuta hiyo baina ya HD hiyo na simu ya marehemu. Kwa sasa tumegundua kuwa Abdul anamiliki kompyuta hiyo isivyo halali.

"Kuna dalili kuwa mtuhumiwa amegundua anatafutwa, hivyo anakwepa kukamatwa na anajifichamaeneo tofauti ya Jiji ikiwa ni pamoja na kusafiri sehemu kadhaanchini kukwepa mkono wa sheria," alisema Kova.Alisema upatikanaji wa kompyuta hiyo ni muhimu katika kukamilishaupelelezi wa shauri hilo na taratibuza kipolisi.

"Katika mazingira ya sasa katika suala la upelelezi la watu wanaotafutwa, mtu huyo ameingia katika sifa ya wanaotafutwa bila kificho," alisema. Kova aliongeza:"Ni busara kwa mtuhumiwa kujisalimisha kwani kasi ya kumkamata itaongezeka na itamhusu kila raia mwema kutokana na urahisi uliopo kupitia mitandao ya habari.

"Kova aliomba raia wema kutosita kutoa taarifa zitakazosaidia kumkamata mtuhumiwa huyu kwani tukio la kuuawa kwa Dk Mvungi limeleta huzuni kubwa kwawapenda amani na Watanzania wote. Hivi karibuni katika msako wa Polisi, bastola ya Dk Mvungi iliyoporwa nyumbani kwake pia, ilikutwa nyumbani kwa mkazi wa Kiwalani, Dar es Salaam.

Bastola Sambamba na bastola hiyo,vifaa vya kutengenezea milipuko navyo vilikutwa nyumbani kwa mkazi huyo, John Mayunga 'Ngosha'(56) kwa mujibu wa Kamanda Kova.

Ngosha anashikiliwa na Polisi Kanda Maalumu kwa tuhuma za kukutwa na silaha na vifaa hivyo.

Kamanda Kova alisema kumbukumbu za nyuma zinaonesha kwamba Mayunga ni mhalifu mzoefu na hivi karibuni alimaliza kifungo cha miaka saba jela kwa makosa ya ujambazi.

Alisema polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema ya kuwapomhusika wa tukio hilo na alipokamatwa na kuhojiwa alikiri kuhusika na kuongozana na askari hadi nyumbani kwake Kiwalani, Migombani.

Kamanda alisema upekuzi ulifanyika na katika moja ya vyumba vyake, ilikutwa silaha hiyo ambayo ni bastola aina ya Revolvernamba BDN 6111 na risasi 21 za bastola hiyo. Aidha, alisema katika chumba hicho vilipatikana vifaa vyamilipuko ya baruti vyenye muundowa soseji, tambi mbili ambazo ni viwashio vya baruti na milipuko minne ambayo imeunganishwa na tambi tayari kutumika.

Milipuko hiyo hutumika kulipulia miamba migodini.

Simu Akizungumza na wanahabari Novemba 11 Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, alisema Polisi imekamata watu tisa wakituhumiwa kuvamia nyumbani kwa Dk Mvungi na baadhi yao kukutwa na simu iliyoporwa nyumbani kwa marehemu.


Pia alisema baada ya mahojiano yakina walikiri kushiriki tukio hilo na walitoa ushirikiano wa kutosha hadi kupatikana kwa mapanga yaliyotumika kwenye uvamizi huo pamoja na kigoda. Kova alimtaja Chibango Magozi kuwa ndiye alikamatwa na simu hiyo. Wengine wanaoshikiliwa ni Ahmed Ali, Zakaria Msesa, Manda Saluwa, PaulJailos, Juma Khamis wote wakazi wa Vingunguti.

Longishu Semariki muuza ugoro katika eneo la Msimbazi na Msunga Makenza mwendesha bodaboda wa Kitunda na Msigwa Mpopera ambaye ni mlinzi nyumbani kwa Dk Mvungi.