WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE WATATU KUJERUHIWA KWA RISASI JIJINI DAR

Watu wawili wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi na kijana aliyetambulika kwa jina la Gabriel Munisi mfanyabiashara wa jijini Mwanza ambaye naye alijiua baadaya kufanya mauaji hayo.

Mkasa huo unaodaiwa kusababishwa na wivu wa kimapenzi umetokea Jumanne hii majira ya saa 2 asubuhi katika eneo la Ilala Sharifu shamba Jijini Dar es Salaam.

Ni nyumba iliyopo karibu klabu ya Wazee Ilala Dar es Salaam yalipofanyika mauaji hayo ambapo baadhi ya wakazi walioshuhudia wamesema walisikia milio ya risasi na kisha majeruhi walikimbizwa hosptali ya Amana na baadaye ya Taifa Muhimbili kutokana na hali zao kuwa mbaya.

Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Ilala amezungumza na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akimtaja mwingine aliyefariki dunia kuwa ni Christina Alfred.

Kamanda Minangi akatoa wito kwa jamii kuacha kuchukua maamuzi ambayo yanaweza kusababisha kutoelewana miongoni mwa jamii na kushangazwa kujitokeza kwa vitendo hivyo