SAMATTA BECOME FIRST TANZANIAN TO SCORE AT CAF FINAL

Mbwana Samatta is the best player of a time in Tanzania who plays soccer in DR of Congo.

No Tanzanian who had scored a goal in any CAF final match until Mbwana did today against Club Sportif Sfaxien of Tunisia.

Mbwana is currently a TPMazembe Englebert striker who get transferred from Simba Sports Club of Tanzania few years ago.

KILI STARS YAANZA CHALENJI KWA DROO

TANZANIA Bara 'Kilimanjaro Stars' jana ilianza kwa sare baada ya kufungana bao 1-1 na Zambia katika mchezo wa kwanza wa michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya.

Kilimanjaro Stars katika kipindi cha kwanza ilionekana kuutawala zaidi mchezo huo huku ikifanikiwa kuingia hadi katika eneo la hatari la Zambia, lakini walishindwa kutumia vema fursa hizo.

Zambia ndio ilikuwa ya kwanza kuziona nyavu za Bara kwa bao la Ronald Kampambe katika dakika ya41.

Bao hilo la kichwa lilitokana na pasisafi kutoka kwa kiungo Felix Katongo. Dakika tatu baadaye Zambia, mabingwa wa Afrika mwaka 2012 na timu mwalikwa katika michuano hiyo, ilifanya shambulio la kushtukiza golini mwa Bara, lakini kipa Ivo Mapunda aliondoa hatari hiyo.

Baada ya mapumziko, dakika ya 51, Kilimanjaro Stars ilisawazisha bao hilo lililofungwa na beki Said Morad kwa kichwa, kutokana na krosi ya Salum Abubakar na kumkuta Morad aliyechupa na kupiga kichwa.

Iwapo Bara ingetumia vema nafasi ilizozipata, ingeweza kutoka na mabao mengi katika mchezo huo wa kwanza kwa timu zote katika Kundi B.

Mshambuliaji Mrisho Ngasa alikosabao la wazi akiwa amebakia peke yake na kipa wa Zambia, naye Haruna Chanongo iwapo angetumia vema nafasi aliyoipata ya kuwatoka mabeki wa Zambia na kubaki na kipa, basi Kilimanjaro Stars ingeweza kutoka na mabao zaidi ya mawili.Kipa Ivo alionekana kuibeba zaidi Kilimanjaro Stars baada ya kuokoa mipira ya hatari mingi. Hata hivyo,Kocha wa Kilimanjaro Stars, Kim Paulsen alikiri kuwa kipindi cha mwanzo wachezaji wake walishindwa kucheza vema, na pia kulalamikia umakini wa kutofunga akimtolea mfano Ngasa.

Kim alisema katika kipindi cha kwanza, kila timu iilionekana kucheza kwa umakini huku timu yake ikiwa imetengeneza mazingira mazuri zaidi ya kushinda.

"Naona kuwa wachezaji wangu walishindwa kumalizia tu ila kipindicha kwanza wamecheza vema na pia wameonesha kuusoma mchezona kucheza vizuri zaidi kipindi cha pili," alisema Kim.

Naye kiungo Salum Abubakar anayechezea Azam FC, aliibuka mchezaji bora wa mchezo huo, alisema ulikuwa mchezo wenye changamoto kubwa hasa uwanja kuwa na tope kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jana kwenye Uwanja wa Machakos.

Alisema kuwa wachezaji wenzake walijitahidi kuonesha mchezo safi na kutoka na sare hiyo.

Awali, Burundi iliishinda Somalia kwa mabao 2-0, hivyo kuongoza katika Kundi hilo la B ikiwa na pointi tatu, wakati Bara na Zambia zimegawana pointi moja. Bara itashuka tena dimbani keshokutwa kuivaa Somalia wakati Burundi itaikabili Zambia.

KESI YA UAMSHO KUSIKILIZWA JANUARY

Kesi inayowakabili viongozi 10 wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiisalam Zanzibar(Jumiki), inatarajiwa kuanzakusikilizwa Januari mwakani.

Hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa rufaa mbili zilizokuwa zimefunguliwa na upande wa mashtaka na utetezi katika kesi hiyo ambayo ni ya nne ya mwaka 2012.

Habari zilizopatikana zinasema kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa naJaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu.

Kesi hiyo jana ilitajwa mbele ya Naibu Mrajisi wa Mahakama Kuu Zanzibar, Ali Ameir na kupangwa tarehe hiyo.

Mrajisi Amir alisema mahakama imelazimika kupanga siku hiyo kwa sababu siku za katikati kutakuwa na Sikukuu za Krismasi, Mwaka Mpya na likizo ya mahakama.

Alisema kuanzia wiki ijayo, Mahakama ya Rufaa Tanzania, itaanza vikao vya kusikiliza kesi za Zanzibar na Kuutaka upande wa utetezi kukubaliana muda mwafakawa kutajwa kesi kabla ya kuanza kusikilizwa hapo mwakani.

Kesi hiyo inayohusu uharibifu wa mali na kuhatarisha Usalama wa Taifa inawahusu washtakiwa kumi akiwamo Sheikh Farid Hadiy Ahmed.

Watu hao wanatuhumiwa kuharibu miundombinu na mali zenye thamani ya Sh500 milioni kutokanana vurugu zilizotokea visiwani Zanzibar, mwaka jana Hata hivyo, upande wa mashtaka katika kesi hiyo umeeleza kwamba jalada la kesi ya msingi bado halijarejeshwa Zanzibar kutoka Mahakama ya Rufaa Tanzania.

WATOTO ZAIDI YA 60 WATEKWA JIJINI DAR

Zaidi ya watoto 60 wanadaiwa kutekwa na kufichwa katika handaki lililopo kwenye msitu wa Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni ,Dar es Salaam, ambalo ndani yake kuna jengo kubwa lenye vyumba.
Utekaji huo unadaiwa kufanywa na raia wa kigeni (Wazungu), wakishirikiana na Watanzania ambapo watoto hao hufungiwa katika vyumba hivyo, kuteswa, kulawitiwa na kubakwa.

Mtoto Emmanuel Robert (11) anayesoma darasa la tano Shule ya Msingi Maendeleo iliyopo Tabata, Segerea, Dar es Salaam na mdogo wake Godianus Robert (8), anayesoma darasa la tatu shuleni hapo, ndio waliofichua ukatili huo mwishoni mwa wiki.

Watoto hao walitekwa na Wazungu wawili asubuhi ya Septemba 2 mwaka huu, wakati wakienda shuleni.

Wakiwa wamechoka na afya zao kuzorota katika Kituo kidogo cha Polisi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani, watoto hao walisema ndani ya jengo hilo kuna watoto wengi wa kike na kiume.

Walisema watoto hao wanafanyishwa kazi na kuteswa kwa kutandikwa fimbo, kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme hasa wanapo waulizia wazazi wao ambapo baadhi yao hubakwa na kulawitiwa.

"Jumba hili limejengwa ndani ya handaki, tulikuwa tukifanyishwa kazi ngumu na nzito, usiku tunajaza maji katika mapipa mengi na kubebeshwa ndoo kupanda na kushuka kilima.


"Tunapigwa fimbo, wasichana wanafungiwa kwenye vyumba, wanabakwa na kulawitiwa kwa zamu na Wazungu, tunachomwa moto (alionesha mguu wake uliochomwa) na kupigwa shoti ya umeme tunapowaulizia wazazi wetu,"alisema Emmanuel kwa uchungu akitokwa na machozi.


Aliongeza kuwa, asubuhi ya Novemba 23 mwaka huu, katika jengo hilo kulitokea kutokuelewana kati ya Wazungu na Waswahili ambapo mswahili mmoja aliwatisha wazungu kwa kuwaambia polisi wanakuja hivyo walikimbia na kuacha mlango wazi.

"Hali hiyo iliniwezesha mimi, mdogo wangu na watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu kufanikiwa kutoroka, nilimshika mkono mdogo wangu ambaye alionekana kuchoka nikamvuta.

"Watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu nao wakatoka, wengi hawakuweza kutoka kutokana na kukosa nguvu, wanaumwa, wana vidonda vikubwa mwilini kutokana na kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme, wasichana hawakuweza kabisa kutoka kwa kuwa wamefungiwa ndani ya vyumba,"alisema Emmanuel
Aliongeza kuwa, alijikokota taratibu na mdogo wake mbali ya maumivu makali waliyonayo akatokea Mswahili mmoja ambaye alikuwa na gari nyeusi akawaambia wapande ili awatoroshe.

"Tulipanda gari hilo akatushusha darajani mpakani mwa Manispaa ya Kinondoni na Wilaya ya Kibaha, jirani na mzani eneo ambalo sisi hatukuwa tukilifahamu...dereva huyo alituambia gari limeishiwa mafuta hivyo alitutaka tumsubiri aende kuyanunua.

"Tulitembea kidogo tukiwa hatujui tunakokwenda... tulikaa kando ya barabara kutokana na uchovu pamoja na njaa kali kwani katika jengo hilo mbali na kazi nzito tulizokuwa tukizifanya na mateso mengi, mlo ulikuwa mmoja tu kwa siku.

"Tulikula saa 10 jioni, wali na maharage...tukiwa kando ya barabara, nilisikia sauti ya baba yangu wa kufikia, dereva wa magari makubwa yanayobeba kokoto ikiniita.

"Nilidhani naota kumbe ilikuwa kweli, alikuja akatukumbatia akalia kwa uchungu kwa namna tulivyokuwa tumechoka na afya kuzorota, akatupeleka polisi ambapo tulipatiwa maji tukaoga na kupewa chakula kizuri na kitamu, tukala na kupata nguvu za kuzungumza vizuri,"alisema Emmanuel.

Akizungumza na Majira, Emmanuel alisema baada ya kutekwa yeye na mdogo wake, walifungwa na vitambaa vyeusi usoni hadi walipofikishwa ndani ya jumba hilo la mateso.

Aliiomba Serikali kufanya jitihada za hali na mali ili kuwaokoa watoto wengine waliopo katika jengo hilo.

Mama mzazi wa watoto hao, Martha Godianus (29), ambaye anafanya shughuli za mama lishe, njia panda y a Ba r a k u d a , Ta b a t a Manispaa ya Ilala, alisema amehangaika zaidi ya miezi mitatu kuwatafuta watoto hao bila mafanikio.

"Nimepoteza fedha nyingi kwa kuwatafuta na kutapeliwa mara kadhaa katika kuhangaika,"alisema Godianus huku akitokwa na machozi ya furaha katika Kituo kidogo cha Polisi Maili Moja.

Alisema zaidi ya watoto saba walipotea katika mtaa wao, wawili wakapatikana baada ya wiki mbili, wengine wakiwemo wanaye wakawa hawajapatikana na kuomba Serikali ilichukulie kwa uzito suala hilo ili kubaini kundi linalowateka watoto na kuwatesa.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuanza kulifanyia kazi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam.

Alisema makachero wa polisi wamewahoji watoto hao ili kupata maelekezo ya kufika katika andaki hilo na kuwataka watu wote wenye taarifa za eneo hilo watoe ushirikiano.


Chanzo: Majira

ZITTO ASEMA HATO TOKA CHADEMA

ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto, amesisitizakwamba hatoki katika chama hicho,huku akitoa ishara kwamba 'atamkabili' Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe, katika uchaguzi mkuu wa chama hicho mwakani.

Zitto ametoa kauli hiyo jana Dar esSalaam, alipokutana na waandishi wa habari kufafanua hatua ya Kamati Kuu ya chama hicho ya Ijumaa iliyopita, kutangaza kumvua madaraka yote aliyokuwa nayo ndani ya chama hicho.

Katika mkutano huo, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Dk Kitilya Mkumbo, alimsafisha Zitto, akidai kwamba hakuhusika katika makakati wa kung'oa uongozi uliopo madarakaniwa Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa.

Aidha Mwanasheria wa wanasiasa hao, Diwani wa Mabogini Moshi Vijijini, Albert Msando (Chadema), ambaye amewahi pia kuwa Mwanasheria wa Mbowe katika kesi zake Arusha, alielezea kumkabili Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, kwa madai ya kukiuka Katiba ya chama hicho, wakati wa kutangaza kumvuamadaraka Zitto.

Usafi wa Zitto, Dk Mkumbo alirudia kukiri kwamba yeye ndiye aliyeandaa na kuhariri mkakati wa kung'oa madarakani viongozi wa sasa wa juu wa Chadema, akishirikiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa ChademaMkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na kiongozi mmoja aliye na nafasi za juu katika chama hicho, ambaye alisema muda ukifika atajitaja mwenyewe.

"Zitto Zuberi Kabwe hajafukuzwa kwa sababu ya waraka huu yeye hakuhusika kwa namna yoyote kuandaa," alisema Dk Mkumbo huku Zitto akikiri kuwa hakufahamu mkakati wala waraka huo na kwamba kwa mara ya kwanza aliuona katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichomvua madaraka.

Kukabiliana na MboweAlipoulizwa kama yeye anakubali maudhui ya waraka huo, ambayo yalikuwa yamemuandalia mkakati awe Mwenyekiti wa Taifa Chademana mbinu za kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi ujao, Zitto alisema swali hilo ni gumu lakini angefurahi kama angepata nafasi ya kuuona waraka huo mapema, iliaufanyie kazi.Alipotakiwa kufafanua wazi kama yuko tayari kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Zitto ambaye alisisitiza angependa kuona waraka wa kumweka madarakani mapema ili aufanyie kazi, alijibu kwamba hataki kuthibitisha kama atagombea nafasi hiyo au la, kwa kuwa hataki kukiuka utaratibu wa chama ila muda ukifika wakati wagombea wakiruhusiwa kujitangaza, atazungumza.

Mbali na hapo, aliwatuliza mashabiki wake pale alipozungumzia kinachoendelea ndani ya Chadema, kwamba ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa za majitaka.

Lisu avunjaKatiba Wakili Msando ambaye katika mkutano wa jana, alizungumza kama Wakili wa Zitto na Dk Mkumbo na wakati huo huo, mshereheshaji, alisema Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Lisu amekiuka Katiba ya chama wakati wa kutangaza kuwaadhibu Zitto na Dk Mkumbo.Kwa mujibu wa Msando, Katiba ya Chadema inataka kabla ya kumvua kiongozi madaraka au kutangaza adhabu yoyote, anapaswa kupelekewa mashitaka yake kwa maandishi na kupewa siku 14 kujibu kwa maandishi.

Baada ya kujibu kwa utaratibu huo,mshitakiwa ataitwa katika kikao kinachohusika na kutakiwa kujitetea kwa mdomo na baada ya hapo kikao kitatafakari hatua ikiwemo adhabu kwa muhusika, ambayo nayo itapelekwa kwake kwa maandishi.

Wakili Msando alisema pamoja na Lisu kuwa wakili mzoefu, lakini amekiuka utaratibu wa Katiba yao kwa kuwa mpaka sasa si Zitto, walaDk Mkumbo aliyepokea hati ya mashitaka yanayowakabili, zaidi ya kuambiwa kwamba wamevuliwa madaraka.

Akifafanua zaidi ukiukwaji huo wa Katiba, pamoja na kukubali adhabualiyopewa, Dk Kitila alisema Kamati Kuu haina uwezo wa kumvua nafasi yake moja kwa moja kwa kuwa mamlaka yake ya uteuzi, yenye mamlaka ya kumuadhibu ni Baraza Kuu."Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema, Sura ya Sita, Ibara ya 6.3.6 (b), inasomeka hivi. 'Kiongozi aliyeteuliwa na vikao vya uongozi, ataweza kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao kilichomteua," alinukuu Katiba Dk Mkumbo na kuongeza; "Mimi nilichaguliwa na Baraza Kuu na ni kikao hiki pekee chenye uwezo wa kunivua nafasi niliyokuwa nayo.

"Usanii wa akina SlaaKatika kile alichoelezea kuwa ni usanii, Zitto alisema sababu za kuvuliwa madaraka zilizotangazwa katika mkutano na waandishi wa habari Ijumaa iliyopita, ni tofauti na alizoambiwa katika Kamati Kuu."Ukweli ni kwamba waraka uliotajwa si sababu ya mimi kuvuliwa nafasi zangu za uongozi kama ilivyojadiliwa katika kikao chaKamati Kuu, sababu za kufukuzwa kwangu kama zilivyojadiliwa katika kikao hicho ni tuhuma lukuki ambazo si mara yangu ya kwanza kuzisikia zikijadiliwa ndani na nje ya vikao vya chama," alisema.

Alisema hitimisho la tuhuma hizo ni yeye kuitwa msaliti wa chama kwa kutumika na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Usalama wa Taifa.

Alibainisha tuhuma hizo kuwa ni pamoja na madai kuwa hakushiriki kumpigia kampeni mgombea uraiswa chama hicho, Dk Willibrod Slaa katika uchaguzi wa mwaka 2010 na madai kuwa katika Mkoa wa Kigoma alishindwa kuwapigia kampeni wagombea wa chama hicho na hivyo kushinda mwenyewe.

Tuhuma nyingine ni pamoja na kushiriki kuwashawishi wagombea wa Chadema katika baadhi ya majimbo kujitoa katika uchaguzi wa mwaka 2010, ili kuwapisha wagombea wa CCM wapite bila kupingwa kwa njia ya rushwa na madai kuwa amekuwa hashiriki katika operesheni mbalimbali za chama hicho.

Aidha Zitto alitaja tuhuma nyingine, ambayo ilichukua muda mrefu kujadiliwa kuwa ni madai kwamba amedhalilisha chama kwa tamko la Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) kwamba hesabu za vyama hazijakaguliwa naMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ikiwa ni pamoja na kuitwa mnafiki kwa kukataa kuchukua posho ya vikao.

Ajibu tuhuma Akijibu tuhuma hizo,Zitto alisema kati ya viongozi wa chama hicho waliofanya ziara nyingi katika mikoa na majimbo katika kampeni za 2010 yeye anaongoza.

Alisema alifanya kampeni katika mikoa na majimbo 16, huku Mkoa wake wa Kigoma ukiongoza kwa kuipatia kura za urais Chadema iliyopata asilimia 45 na kufuatiwa na Kilimanjaro uliyoipatia kura asilimia 37.

Kuhusu kuwa ushindi pekee wa ubunge mkoani Kigoma na wagombea wengine wa chama hicho kukosa, alisema hana uwezo na suala hilo kwa kuwa uamuzi ni wa Wanakigoma na cha msingi ni kuangalia wapi walikosea na kujirekebisha ili isijirudie 2015.

Kuhusu kushawishi wagombea wa chama hicho kukacha nafasi zao kupisha wagombea wa CCM, Zitto alitaja majimbo anayotuhumiwa kufanya hivyo kuwa ni kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Musoma Vijijini kwa Nimroad Mkono na Singida Mjini kwa Mohammed Dewji.

"Kama nilivyokwisha kueleza katikavikao mbalimbali vya chama jambohili si la kweli na hakuna popote ambapo watoa tuhuma hizi wamewahi kutoa ushahidi kwamba nilifanya jambo hili. Nipo tayari kwa uchunguzi ndani ya chama na watoa tuhuma waje na ushahidi bayana wa jambo hili," alifafanua.

Kuhusu tamko la PAC ambalo yeye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto alisema anachofahamu na kuamini kuhusu suala hilo ni kwamba utawala bora hautaki kiongozi kama yeye, kutumia nafasi yake ya uenyekiti wa PAC kulinda chama chake.

Alidai akifanya hivyo na kuonea vyama vingine atakuwa akiendeleza tabia ambazo chama hicho inapinga vikali. Kuhusu suala la posho ya vikao Zitto alisisitiza kuwa hapokei posho yoyote ya vikao ndani na nje ya Bunge tangu 2011, hiyo ikiwa ni pamoja na posho za vikao vyote katika Kamatiza Bunge anazohudhuria na huo ni msimamo wake wa kutekeleza kwavitendo mwito wa Chadema kupinga posho za vikao.

ARSENAL WAZIDI KUJITANUA KILELENI, SPURS WAANGUKIA PUA, MAN U NA LIVERPOOL WABANWA

Ligi Kuu ya England imeingia raundiya 12 kwa matokeo mchanganyiko, Arsenal wakipata ushindi na kuongoza kwa tofauti ya pointi nne.

Liverpool walibanwa na Everton katika pambano la watani wa jadi kaskazini mwa England, ambapo walipata bao la kusawazisha dakika za mwishoni na kunusuru pointi moja.

Katika mechi mbili za Jumapili hii, Manchester City walionesha umahiri wa ajabu kwa kuwafyatua wakali wenza wa London Kaskazini, Tottenham Hotspur kwa mabao 6-0 wakati Manchester United wakibanwa kwa sare nchini Wales mbele ya Cardif.

Olivier Giroud alifunga mabao mawili ya Arsenal dhidi ya Southampton Jumamosi hii na kuwahakikishia Washika Bunduki waLondon ushindi muhimu dhidi ya timu inayokuja juu sana kwa uimara, chini ya kocha Mwargentina, Mauricio Pochettino.

Arsenal waling'ara huku mchezaji wake muhimu wa siku nyingi, Theo Walcott akirejea uwanjani baada ya kuwa nje kwa majeraha kwa miezi miwili, ambapo aliingia kipindi cha pili.Kwa matokeo hayo, Arsenal hawajafungwa nyumbani katika mechi za EPL tangu walipopoteza katika mechi ya kwanza kabisa dhidiya Aston Villa.

Kocha Arsenal Wenger alifurahi kupata ushindi muhimu na mgumu, baada ya kuwa wamepoteza mechi iliyopita dhdi ya Man United katika dimba la Old Trafford na Jumanne hii wanajiandaa kuwakaribisha Marseille ya Ufaransa katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.


LIVERPOOL WABAKI NAFASI YA PILI
Liverpool wanaowafukuzia Arsenal walishindwa kwenda na kasi inayotakiwa, kwani walitoka sare ya 3-3 na wenzao wa Mercyside, Everton ambapo wenyeji walishadhani wangeibuka washindi kwa mabao ya akina Kevin Mirallas na Romelu Lukaku aliye kwa mkopokutoka Chelsea ambaye alifunga mabao mawili.

Liverpool walipata mabao yao kupitia kwa Coutinho, Luis Suárez na Daniel Sturridge aliyewanusuru na kichapo katika dakika ya 89 ya mechi hiyo ya kusisimua kwenye dimba la Goodison Park.

Kwa matokeo hayo, Liverpool wanashika nafasi ya pili kwa pointi 24, zikiwa ni nne nyuma ya Arsenal wakiwa wamelingana kimichezo.

Suarez alirejea Liverpool kwa ndege binafsi ya mmiliki wa Liverpool, John Henry baada ya kushiriki mechi ya kuwapeleka Uruguay kwenye fainali za Kombe la Dunia Brazil 2014 Alhamisi. Everton wanashika nafasi ya saba kwa sare hiyo, jambo ambalo bado ni faraja kwa kocha Roberto Martinez.


CHELSEA NA MOURINHO KWA RAHA ZAO
Chelsea waliokuwa wageni wa West Ham Jumamosi hii walifanikiwa kupata pointi tatu na mabao matatumuhimu katika mechi ambayo WestHam hawakupata bao lolote.

Mabao ya Chelsea yalifungwa na Frank Lampard aliyepachika mawili,moja kwa penati na jingine lilifungwa na Mbrazili Oscar.

West Ham ni klabu ya zamani ya Lampard aliyoanza kuchezea katika ligi kuu lakini hakuwa na huruma kuwakabili kwa nguvu. Kocha Jose Mourinho alionekana mwenye furaha na katika sura mpya, wakati mwenzake Sam Allardyce aliishia kusikitikia matokeo.

Kwa ushindi huo Chelsea wanashika nafasi ya tatu kwa pointi 24 sawa naLiverpool.


KARAMU MAN CITY DHIDI YA SPURSKocha wa Tottenham Hotspurs, Andre Villas-Boas aliondoka katika dimba la Etihad akiwa hana raha, akisema kila kitu kilikuwa kibaya kwao, baada ya vijana wake kupoteza kwa mabao 6-0 dhidi ya Manchester City.

Jamaa hao wa Eastlands walikuwa katika morali kubwa tangu mwanzo, ambapo Jesus Navas ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa saba katika EPL kufunga bao mapema zaidi, ikiwa ni sekunde ya 14 tu ya mchezo.

Mhispania huyo alifunga bao kutokana na kosa la kipa Hugo Lloris aliyepatiwa mpira na kuupiga mguuni mwa Sergio Aguero, lakini mbali kidogo na goli naye akasogea na kujaribu kufunga, Lloris akautema na kuusukuma mpira uliomfikia Navas aliyefunga bao zuri na katika kona ya ajabu.

Mabao mengine yalipachikwa na Sandro wa Spurs aliyejifunga, Aguero mawili, Alvaro Negredo na Navas kupigilia msumari wa mwisho dakika ya 90. Kocha ManuelPellegrini alisema vijana wake hawangeweza kucheza vizuri zaidi ya hapo.

Hii ni mara ya kwanza tangu 1992 kwa Spurs kufungwa vibaya jinsi hiyo, na inashangaza kwa sababu walikuwa wakiutawala mchezo zaidi ya wenyeji wao na hata walijaribu kufanya mabadiliko ya wachezaji bila mafanikio yoyote.

Kwa kichapo hicho, Man City wanashika nafasi ya nne kwa pointi 22 wakati wakiwaacha Spurs wakiugulia katika nafasi ya tisa, jambo ambalo si kawaida katika miaka ya karibuni.


MAN UNITED WABANWA NA CARDIF
Manchester United walijaribu kila hali kujihakikishia ushindi mwingine muhimu kwenye ligi lakini walihangaishwa na baadaye kutulizwa na Cardiff kwenye mechi ya Jumapili hii.

United walitangulia kufunga katika dakika ya 15 kupitia kwa Wayne Rooney ambaye nusura apewe kadi nyekundu kwa rafu mbaya na ya makusudi katika dakika za kwanza dhidi ya Jordon Mutch Cardiff katikauwanja wa Cardiff City nchini Wales.

Hata hivyo bao hilo lilisawazishwa na Frazier Campbell dakika ya 33 kabla ya Patrice Evra kufunga kwa kichwa kona ya Rooney muda mfupo tu kabla ya mapumziko.

Wakati kocha wa Man U, David Moyes akidhani kwamba wangeondoka wakiwa washindi, mchezaji Kim Bo-Kyung aliyetokea benchi alifunga bao katika dakika zamwisho na kuwapa raha wenyeji na washabiki waliofurika uwanjani.

Matokeo hayo yanawafikisha Manchester United katika nafasi ya sita.


MATOKEO MENGINE YA EPLKwenye mechi nyingine wikiendi hii, Fulham waliendelea na hali mbaya baada ya kufungwa wakiwa nyumbani na Swansea kwa bao 2-1.

Hull walipotea mechi kwa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace, Newcastle wakawaadhibu Norwich 2-1 wakati Stoke wakiwafunga Sunderland bao 2-0.

Matokeo ya mechi hizo yanawafanya Newcastle kushina nafasi ya nane kwa pointi zao 20 wakifuatiwa na Spurs wenye pointi sawa nao, Swansea ni wa 10 kwa pointi 15 wakati West Bromwich Albion wanaopepetana na Aston Villa Jumatatu hii wanashika nafasi ya 11 kwa kujikusayia pointi 14.

Nafasi ya 12 inashikwa na Villa wenye pointi 14 sawa na Hull huku wakifuatiwa na Stoke na Cardiff waliokikusanyia pointi 13 kila moja.

Norwich wana pointi 11 katika nafasi ya 16 wakati West Ham itabidi wajiulize kulikoni kwa sababu wapo nafasi ya 17 wakiwa napointi 10.

Hao wapo sawa na Fulham walio katika eneo la hatari la zile timu tatu mbovu kwa pointi hizo hizo 10 wakati Crystal Palace na Sunderlandwanafungana kwa pointi saba kwenye nafasi mbili za mwisho.

MBUNGE WA MPANDA KATI NA MAKAMU MWENYEKITI CHADEMA AJIUZULU WADHIFA WAKE

Salaam, Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama.

Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki.

Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wana Mpanda kwenu imekua ni tatizo lakini hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki wa kupindukia.

Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu
Nawasilisha.

Said A Arfi (Mb)

JESHI LA POLISI LAMTAJA ALIYE NA LAPTOP YA DR. MVUNGI

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemtaja mkazi wa Vingunguti, kuwa ndiye aliye na kompyuta mpakato ya aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, marehemu Dk Sengondo Mvungi.

Hata hivyo Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova amesema mkazi huyo Abdul ThabitChief (20) anaendelea kusakwa sambamba na wahusika wengine walioshiriki kusababisha kifo cha Dk Mvungi.

kushambuliwa na watu wasiojulikana ambapo viliibwa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kompyuta, fedha na bastola. Kamanda Kova alisema jana kuwa mpaka sasa watuhumiwa 10 wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

"Jeshi la Polisi linaendelea na jitihada kubwa kwa lengo la kuipatakompyuta hiyo baina ya HD hiyo na simu ya marehemu. Kwa sasa tumegundua kuwa Abdul anamiliki kompyuta hiyo isivyo halali.

"Kuna dalili kuwa mtuhumiwa amegundua anatafutwa, hivyo anakwepa kukamatwa na anajifichamaeneo tofauti ya Jiji ikiwa ni pamoja na kusafiri sehemu kadhaanchini kukwepa mkono wa sheria," alisema Kova.Alisema upatikanaji wa kompyuta hiyo ni muhimu katika kukamilishaupelelezi wa shauri hilo na taratibuza kipolisi.

"Katika mazingira ya sasa katika suala la upelelezi la watu wanaotafutwa, mtu huyo ameingia katika sifa ya wanaotafutwa bila kificho," alisema. Kova aliongeza:"Ni busara kwa mtuhumiwa kujisalimisha kwani kasi ya kumkamata itaongezeka na itamhusu kila raia mwema kutokana na urahisi uliopo kupitia mitandao ya habari.

"Kova aliomba raia wema kutosita kutoa taarifa zitakazosaidia kumkamata mtuhumiwa huyu kwani tukio la kuuawa kwa Dk Mvungi limeleta huzuni kubwa kwawapenda amani na Watanzania wote. Hivi karibuni katika msako wa Polisi, bastola ya Dk Mvungi iliyoporwa nyumbani kwake pia, ilikutwa nyumbani kwa mkazi wa Kiwalani, Dar es Salaam.

Bastola Sambamba na bastola hiyo,vifaa vya kutengenezea milipuko navyo vilikutwa nyumbani kwa mkazi huyo, John Mayunga 'Ngosha'(56) kwa mujibu wa Kamanda Kova.

Ngosha anashikiliwa na Polisi Kanda Maalumu kwa tuhuma za kukutwa na silaha na vifaa hivyo.

Kamanda Kova alisema kumbukumbu za nyuma zinaonesha kwamba Mayunga ni mhalifu mzoefu na hivi karibuni alimaliza kifungo cha miaka saba jela kwa makosa ya ujambazi.

Alisema polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema ya kuwapomhusika wa tukio hilo na alipokamatwa na kuhojiwa alikiri kuhusika na kuongozana na askari hadi nyumbani kwake Kiwalani, Migombani.

Kamanda alisema upekuzi ulifanyika na katika moja ya vyumba vyake, ilikutwa silaha hiyo ambayo ni bastola aina ya Revolvernamba BDN 6111 na risasi 21 za bastola hiyo. Aidha, alisema katika chumba hicho vilipatikana vifaa vyamilipuko ya baruti vyenye muundowa soseji, tambi mbili ambazo ni viwashio vya baruti na milipuko minne ambayo imeunganishwa na tambi tayari kutumika.

Milipuko hiyo hutumika kulipulia miamba migodini.

Simu Akizungumza na wanahabari Novemba 11 Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, alisema Polisi imekamata watu tisa wakituhumiwa kuvamia nyumbani kwa Dk Mvungi na baadhi yao kukutwa na simu iliyoporwa nyumbani kwa marehemu.


Pia alisema baada ya mahojiano yakina walikiri kushiriki tukio hilo na walitoa ushirikiano wa kutosha hadi kupatikana kwa mapanga yaliyotumika kwenye uvamizi huo pamoja na kigoda. Kova alimtaja Chibango Magozi kuwa ndiye alikamatwa na simu hiyo. Wengine wanaoshikiliwa ni Ahmed Ali, Zakaria Msesa, Manda Saluwa, PaulJailos, Juma Khamis wote wakazi wa Vingunguti.

Longishu Semariki muuza ugoro katika eneo la Msimbazi na Msunga Makenza mwendesha bodaboda wa Kitunda na Msigwa Mpopera ambaye ni mlinzi nyumbani kwa Dk Mvungi.

KIONGOZI WA LRA ATAKA KUJISALIMISHA KWA JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI

Maafisa wakuu nchini Marekani wameelezea shaka kuhusu taarifa za kiongozi wa waasi wa LRA nchini Uganda kufanya mazungumzo na serikali ya Jamuhuri ya Afrika ya kati kuhusu kutaka kujisalimisha.

Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati ambako Kony amejificha na waasi wake amesema kua Kony, anayesakwa kwa tuhuma za uhalifu wa kivita na mahakama ya jinai ICC, amefanya mazungumzo na serikali yake.

Afisa kutoka katika wizara ya mambo ya ndani nchini Marekani, ameambia BBC kuwa waasi kadhaa walishauriana na serikali ya CAR wala sio Kony mwenyewe.

Marekani iliahidi kutoa zawadi ya dola milioni 3.3 kwa mtu yeyote mwenye taarifaambayo ingepelekea kukamatwa kwa Kony.

Kony alianzisha kundi la waasi la LRA, kaskazini mwa Uganda, zaidi ya miaka 20 iliyopita, na waasi wake wanasifika kwa kuwateka nyara watoto na kuwaingiza katika kundi lao la waasi kama wapiganaji pamoja na kuwa watumwa wa ngono.

Maafisa hao walielezea kuwa Kony amewahi kutumia mbinu zote kama hizi kupumzika, kujikusanya upya na waasi wake na hata kujihami upya na kisha kuanza kuteka nyara, kuua na kusababisha watu kutoroka makwao.

Waasi wa LRA walilazimika kutoroka Uganda mwaka 2005 na tangu hapo wamekuwa wakifanya vurugu katika CAR, Sudan Kusini na katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Nusura Joseph Kony atie saini mkataba wa Amani mwaka 2008 lakini akasisitiza kuwa mahakama ya ICC mwanzo itupilie mbali kibali cha kumkamata , ingawa mahakama hiyo ilikataa kufanya hivyo.

BABU SEYA NA PAPI KUENDELEA KUKAA JELA RUFAA YAO YATUPILIWA MBALI

Mahakama, nchini Tanzania imetupilia mbali ombi la kusikilizwa upya kwa kesi dhidi ya muimbaji Nguza Viking, anayejulikana kama Babu Seya pamoja na mwanawe, ambao walihukumiwa maisha jela, kwa kosa la ubakaji.

Majaji walisema kua kuna thibitisho tosha kuwa wawili hao waliwabaka watoto 10 wa shule ya msingi mwaka 2013.

Katika kesi yao ya kwanza ya rufaa miaka mitatu iliyopita, watoto wengine wawili wa muimbaji huyo, ambao pia walipatikana na hatia ya kosa hilo mwaka 2004, waliachiliwa.

Kesi hiyo imewashtua mashabiki waViking katika nchi hiyo iliyo katika kanda nzima ya Afrika Mashariki.

Mwanamuziki huyo mwenye kuimba nyimbo za Rhumba, ambaye ni mzaliwa wa DRC, ameishi Tanzania kwa miaka mingi na kuwa na ufuasi mkubwa huko.

Viking na kijana wake Johnson Nguza ambaye pia ni mwanamuziki,walifika mahakamani kwa uamuzi huo.

Walionekana kuwa watulivu wakati majaji walipotupilia mbali ombi lao kutaka hukumu yao kubatilishwa.

Walihukumiwa kwa kuwabaka wasichana 10 wa shule ya msingi waliokuwa kati ya umri wa miaka sita na nane wote waliokuwa katika shule ya msingi ya Mashujaa mtaaniKinondoni mjini Dar es Salaam.

Wakili wa muimbaji huyo alisema kua muimbaji huyo hana matumaini tena ya kupewa rufaa kwani hili ndio lilikuwa ombi lake la mwisho.

23 WAITWA KILI STARS KWA AJILI YA MASHINDANO YA CHALENJI

Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27 mwaka huu.

Kilimanjaro Stars iliyotwaa kombe hilo mara ya mwisho mwaka 2010 chini ya Kocha Jan Poulsen, na ambayo imepangwa kundi B katika michuano ya mwaka huu itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.

Wachezaji wanaounda kikosi hicho cha Tanzania Bara ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam).

Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius(Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).

Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar),Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

Kilimanjaro Stars inatarajia kuondoka Jumatatu (Novemba 25 mwaka huu) kwenda Nairobi kushiriki michuano hiyo itakayoanzaNovemba 27 mwaka huu na kumalizika Desemba 13 mwaka huu.

SAMATTA AJIVUNIA KUWA MMOJA WA WATAKAOGOMBANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA

Baada ya hivi karibuni kuteuliwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2013 wanaochezea klabu za ndani za Afrika, Mbwana Samatta amesema kuwa hatua hiyo ni jambo la kujivunia kwa kila Mtanzania.

Jumamosi iliyopita Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilimtangaza Samatta anayecheza soka la kulipwakatika klabu ya TP Mazembe ya DR Congo kuwa miongoni mwa wachezaji 21 watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika anayechezea timu za ndani ya bara hili.

Mshindi wa tuzo hiyo pamoja na ileya mchezaji bora wa Afrika wanatarajiwa kutangazwa Januari 9, mwakani Lagos, Nigeria.

Akizungumza jijini Dares Salaam jana, Samatta alisema anajivunia kuteuliwa kuwania tuzo hiyo lakini pia Wanatazania wanapaswa kujivunia hali hiyo kwa sababu yeye ndiye mchezaji pekee kutoka Afrika Mashariki kuingia katika kinyang'anyiro hicho ukimwondoa Victor Wanyama raia wa Kenya anayechezea Southampton ya England ambaye anawania tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika inayohusisha wachezaji 25 wanaocheza soka nje na ndani ya Afrika.

Alisema kujituma kwake na kuzingatia maadili ndiyo siri ya mafanikio ambayo ameyapata na kuwafanya viongozi wa CAF kuona kuwa anastahili kuwania tuzo huyo.

KENYA, UGANDA NA RWANDA ZAKURUZWA KORTIN

Serikali za Rwanda, Uganda,Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, zimefunguliwa kesi katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki, zikidaiwa kukiuka mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.

Hatua hiyo inatokana na Serikali hizo kufanya vikao vitatu mfululizo na kuzitenga nchi za Tanzania na Burundi.


Walalamikaji katika kesi hiyo, ni Ally Msangi, David Makata na , John Adam, ambao ni Watanzania, wanaotetewa na wakili Mwandamizi, Jimm Obedi wa jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, walalamikaji wamewaomba majaji katika mahakama hiyo, kutoa tamko la kusitisha utekelezaji wa maazimio yote ya vikao vya wakuu wa nchi hizo tatu.

Pia wameomba majaji watoe tamkola kukomesha kurejewa kwa vikao kama hivyo kinyume cha mkataba wa jumuiya hiyo.

Kesi hiyo ya aina yake, ilifunguliwa jana katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki na kupokewa na Ofisa Masijala i katika mahakama hiyo, Boniface Ogoti.

Kufunguliwa kwa kesi hiyo, kunakuja siku kadhaa baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzilalamikia nchi hizo, kuhusu kuitenga Tanzania kwakufanya mikutano mbalimbali ya maendeleo ya nchi zao. Nchi nyingine iliyotengwa ni Burundi.

Kikao cha kwanza cha pamoja kilifanyika Aprili mjini Arusha kablaviongozi hao kukutana Juni 25 na 26 jijini Entebbe nchini Uganda, walidai kuwa na nia moja ya kurahisha mawasiliano katika nchi hizo.

Mkutano mwilingine ulifanyika mjini Kigali Rwanda Oktoba 28 ukiwajumuisha Rais Yoweri Museven wa Uganda, Uhuru Kenyatta (Kenya), Salva Kiir (Sudan Kusini) na Paul Kagame.

Wakili wa walalamikaji Obedi, alisema katika kesi ya msingi, wanawashtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Rwanda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Uganda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.


Chanzo:Mwananchi

DALADALA YAGONGA TRENI NA KUUWA WAWILI

Watu watatu wamekufa na wengine sita kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti zilizohusisha daladala aina ya Toyota DCM lenye namba za usajili T474 AST, kuligonga treni na lingine likipinduka.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Ilala, Marieta Minangi alisema tukio hilo la basi kuligonga treni lilitokea Novemba 18 saa, 3 usiku eneo la Karume, karibu na Machinga Complex.

Ajali hiyo ilitokea makutano ya Barabara ya Kawawa na Reli. Basi hilo liliigonga treni na kusababisha vifo vya watu wawili, ambao ni Bakari Sajina (25) na Suleimani Adili (38).

Treni ilikuwa ikitoka Ubungo na DCM ikitoka Chang'ombe.

Wakati huohuo ajali nyingine ilitokea eneo la Pugu Kanisani baada ya Toyota DCM kumshinda dereva wake kabla ya kupinduka nakusababisha kifo chake.

AFARIKI AKICHEZA NGOMA ZA MATAMBIKO

MKAZI wa Kijiji cha Ifukutwa wilayani Mpanda , mkoani Katavi, Zainabu Mbaruku (70) amekufa ghafla huku akiwa anacheza ngoma ya matambiko na vikongwe wenzake wa kike kijijini humo.

Akithibitisha kutokea kwa mkasa huo Kamanda wa Polisi wa Mkoa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema ulitokea jana saa 12 jioni kijijini Ifukutwa , Kata ya Mpandandogo wilayani hapa ambapo kikongwe huyo alikuwa miongoni mwa vikongwe wengine waliolikwa na kikongwe mwenzao aitwaye Mwamini Luholi (70) kucheza ngoma hiyo ya matambiko nyumbani kwake.

Alisema jioni hiyo ya tukio, Mwamini alitengeneza pombe ya kienyeji kwa ajili ya matambiko ya mila na desturi za kabila la Kebende ambapo pia aliwataarifu na kuwaalika Mwenyekiti wa Kijiji hicho Steven Ismail (51), na pia ndugu, jamaa na majirani zake.

Inadaiwa ilipofika saa 11 jioni Mwamini alifika kwenye shughuli hiyo na kujumuika na wageni wengine kwa kucheza ngoma ya pamoja ambapo baada ya muda mfupi hali yake ilibadilika na kuanza kijisikia vibaya huku akitetemeka ambapo alidondoka chini.

Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari ilipofika saa 12 jioni kikongwe huyo alifariki dunia kutokana na hali yake kuzidi kuwa mbaya bila kupatiwa huduma yoyote ya kiafya.

"Hadi sasa chanzo kilichopelekea umauti wa kikongwe huyo hakijafahamika na uchunguzi wa kitabibu unaendelea ili kubaini sababu zilizopelekea Mwamini kufariki katika mazingira hayo," alisema Kamanda Kidavashari.

Alisema hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na kuongeza kuwa kama itabainika kuna aliyehusika atakamatwa na kuchukulia hatua za kisheria.

AL SHABAAB WASHAMBULIA TENA SOMALIA WAUWA ISHIRINI

Karibu watu ishirini wameuawa katika shambulio la kujitoa mhanga kwenye kituo cha polisi nchini Somalia.

Shambulio hilo limetokea katika mji wa Beledweyne karibu na mpaka na Ethiopia.

Mashuhuda wameiambia BBC kuwa gari lilipiga lango kuu la kuingia kwenye jengo lapolisi na kulipuka kabla ya watu wenye silaha kushuka na kushambulia jengo hilo kwa risasi. Taarifa zinasema wengi waliofariki katika shambulio hilo ni maafisawa polisi.

Mwandishi wa habari wa BBC nchini Somalia Mohammed Moalimu amesema kituo hicho cha polisi kipo karibu na ngome ya majeshi ya Umoja wa mataifa yaliyopo nchini Somalia AMISOM.

Wapiganaji wa kiislamu wa Al Shabaab wamekiri kuhusika na shambulio hilo. Mwezi uliopita wapiganaji hao wa Al Shabaab pia walikiri kuhusika na shambulio jingine ambapo watu 16 waliuawa katika hoteli moja maarufu mjini Mogadishu.

Maafisa wa polisi nchini Somalia wamesema mlipuko huo ulikuwa ni mkubwa na umesababisha majeruhi kadhaa.

"Mlipuko ulikuwa ni mkubwa na pia wapo majeruhi kadhaa, hata hivyo hali imedhibitiwa," amesema Kanali AbdulkadirAli, kamanda wa polisi wa mji huo wakati akiongea na shirika la habari la AFP.

Kamanda wa kundi la Al Shabaab Mohamed Abu Suleiman ameliambia shirika la AFP kuwa makomandoo wa Al Shabaab ndio waliofanya shambulio hilo.

Naye Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema shambulilo hilo ni la kujimaliza na linaonyesha kutojali maisha.

"Kipau mbele changu cha kwanza ni kutuma salamu za rambi rambi kwa waathirika na familia zilizoguswa na tukio hilo la kipumbavu", alisema katika taarifa yake "Nimesema ni shambulio la kipumbavu kwa sababu maadui zetu wanapaswa kuelewa kwamba mashambulizi hayatawasaidia kuendeleza harakati zao zaidi sana yanawapotosha "Mwezi Septemba, kundi la Al Shabaab lilisema kuwa lilifanya shambulizi la kigaindi katika kituo cha biashara cha Westgate nchini Kenya ambapo watu wapatao 67 waliuawa.

DROO YA KUPANGA MAKUNDI KOMBE LA DUNIA KUFANYIKA DECEMBER 6

Droo ya kupanga makundi ya kombe la dunia 2014 hufanyika December 6 2013:

Katika michuano hiyo itakayo fanyika Brazil, timu zilizofuzu tayari ni kama ifuatavyo

EUROPE/Ulaya
Netherlands, Italy, Belgium, Germany, Switzerland, Spain, England, Russia, Bosnia-Herzegovina, Croatia, Greece, Portugal, France


ASIA
Japan, Australia, Iran, South Korea(Jordan involved in a two-leg play-off with Uruguay. Uruguay won first leg 5-0; 2nd leg on Wednesday)


SOUTH AMERICA/Amerika kusini
Brazil (hosts), Argentina, Colombia,Chile and Ecuador (Uruguay involved in a two-leg play-off with Jordan. Uruguay won first leg 5-0; 2nd leg on Wednesday. Winners will qualify)

CONCACAF/Amerika ya kati na kaskazini.
United States, Costa Rica, Honduras (Mexico involved in a two-leg play-off with New Zealand. Mexico won first leg 5-1; 2nd leg on Wednesday. Winners will qualify)

AFRICA/Afrika
Nigeria, Ivory Coast, Cameroon, Ghana, Algeria

OCEANIA
Inasubiriwa kati ya Mexico vs New zealand ambapo mchezo wa kwanza Mexico 5-1 New zealand

WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE WATATU KUJERUHIWA KWA RISASI JIJINI DAR

Watu wawili wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi na kijana aliyetambulika kwa jina la Gabriel Munisi mfanyabiashara wa jijini Mwanza ambaye naye alijiua baadaya kufanya mauaji hayo.

Mkasa huo unaodaiwa kusababishwa na wivu wa kimapenzi umetokea Jumanne hii majira ya saa 2 asubuhi katika eneo la Ilala Sharifu shamba Jijini Dar es Salaam.

Ni nyumba iliyopo karibu klabu ya Wazee Ilala Dar es Salaam yalipofanyika mauaji hayo ambapo baadhi ya wakazi walioshuhudia wamesema walisikia milio ya risasi na kisha majeruhi walikimbizwa hosptali ya Amana na baadaye ya Taifa Muhimbili kutokana na hali zao kuwa mbaya.

Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Ilala amezungumza na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akimtaja mwingine aliyefariki dunia kuwa ni Christina Alfred.

Kamanda Minangi akatoa wito kwa jamii kuacha kuchukua maamuzi ambayo yanaweza kusababisha kutoelewana miongoni mwa jamii na kushangazwa kujitokeza kwa vitendo hivyo

NAIBU MKUU WA USALAMA LIBYA AACHIWA BAADA YA KUTEKWA

Naibu mkuu wa usalama wa taifa nchini Libya, Mustafa Noah, ameachiliwa huru siku moja baada ya kutekwa na watu wasiojulikana wakiwa na silaha karibu na uwanja wa ndege wa Tripoli.

Wakati akitekwa hakuwa na walinzi wake.

Libya imekuwa katika hali ya wasiwasi tangu watu arobaini wauawe na mamia wengine kujeruhiwa katika mapigano makali Ijumaa iliyopita.

Mapigano hayo yaliwahusisha wanamgambo na waandamanaji, ambao walikuwa wakijaribu kuwafukuza wanamgambo kutoka mji mkuu Tripoli.

Serikali imekuwa ikijitahidi kuwafukuza wanamgambo hao.

Mgomo wa kutaka wanamgambo waondolewe kutoka Tripoli, umedumu kwasiku tatu.

Waziri Mkuu, Ali Zeidan, alitekwa nyara kwamuda mfupi mwezi uliopita.

NDEGE YAANGUKA NCHINI URUSI NA KUUWA WATU WOTE

Ndege ya abiria imeanguka katika uwanja wa ndege katika mji wa Kazan, nchini Urusi na kuua watu wote 50 waliokuwa katika ndege hiyo.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737 iliruka kutoka mji wa Moscow na ilikuwa ikijaribu kutua lakini ikawaka moto saa moja usiku kwa saa za huko.

Wizara ya matukio ya dharura imesema kulikuwa na abiria 44 na wafanyakazi sita wa ndege hiyo ya shirika la Tatarstan Airlines.

Wachunguzi wanajaribu kuona kama kulikuwa na makosa ya kiufundi au huendaya kibinadamu yaliyosababisha ajali hiyo.

Afisa wa kamati ya uchunguzi Vladimir Markin ameiambia Televisheni moja nchini Urusi, Rossiya 24 TV, kwamba wataalam wanachunguza kubaini kama ajali hiyo imesababishwa na matumizi ya mafuta mabaya, au hali mbaya ya hewa.

Mvua ilikuwa ikinyesha katika mji wa Kazan wakati ndege hiyo ilipoanguka.

Kwa mujibu wa orodha rasmi ya wasafiri wa ndege hiyo, miongoni mwa waliokufa niIrek Minnikhanov, mtoto wa kiume wa rais wa Jamhuri ya Tatarstan,nchini Urusi.

Aleksander Antonov, ambaye aliongoza Idara ya Usalama ya Shirikisho la Urusi, ni miongoni mwa abairia wa ndege iliyoanguka.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza, imethibitisha kuwa raia mmoja wa Uingereza amekufa katika ajali hiyo.

Miongoni mwa waliokufa wamo watoto wawili.


Rais Vladimir Putin wa Urusi ametuma salaama zake za rambirambi kwa ndugu najamaa wa waathirika.

Tume ya serikali imeundwa kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.

Taarifa zinasema, rubani wa ndege hiyo Rustem Salikhov mwenye umri wa miaka 47, alijaribu mara kadhaa kutua kabla ya kuanguka kwa ndege hiyo.

Shirika la habari la Urusi limeripoti kuwa wafanyakazi walisema hawa kuwa tayari kutua kwa sababu ya matatizo ya kiufundi.

Mwandishi mmoja wa habari ambaye alisafiria ndege hiyo mapema Jumapili kabla ya safari iliyotokea ajali, kutoka Kazan kwenda Moscow ameiambia televisheni moja nchini Urusi kwamba kulikuwa na mtetemo mkubwa wakati ndege hiyo ikitua mjini Moscow.

"Tulipokuwa tukitua haikujulikana kama kulikuwa na upepo mkali, japokuwa mjini Moscow, hali ya hewa ilikuwa nzuri au kulikuwa na tatizo la kiufundi au ndege yenyewe," amesema Lenara Kashafutdinova.

"Tulisukwasukwa huku na kule, ndege ilitua. Mtu aliyekuwa amekaa karibu nami alikuwa mweupe kama shuka kutokana woga uliompata.

"Ndege hiyo imekuwa ikitoa huduma tangu mwaka 1990.

Uwanja wa ndege wa Kazan - mji mkuu wa Tatarstan - umefungwa tangu kutokea jali hiyo na hautarajiwi kufunguliwa hadi Jumatatu mchana.

Mji wa Kazan upo kilomita 720 mashariki mwa Moscow.

24 WAFARIKI AJALI YA TRENI MISRI

Takriban watu 24 wamefariki na wengine 28 kujeruhiwa katika ajali ya treni na basi ndogo iliyohusisha magari mengine Kusini mwa mji mkuu wa Misri Cairo.

Treni iligongana na basi ilipokua inatoka mjini Bani Swaif, na kisha kugonga mahari mengine katika makutano ya njia ya reli umbali wa kilomita 40 kutoka mji mkuu Cairo.

Taarifa za vyombo vya habari nchini humo zilisema kuwa wengi wa waliofariki walikuwa jamaa wa familia moja waliokuwa wanarejea kutoka harusini.

Ajali hiyo ilitokea karibu na kijiji cha Dahshur Jumatatu asubuhi huku taarifa zikisema kuwa ajali hiyo pia ilihusisha basi ndogo na magari mengine.

Maafisa wakuu walisema kuwa milango ya magari kuvukia njia ya reli ilikuwa imefungwa lakini dereva wa treni alishangazwa kuona magari yakipita kwenye njia hiyo.

Magari ya kuwabeba wagonjwa ya Ambulance, yaliwasili katika eneo la tukio kuwabeba waliojeruhiwa.

Taarifa zinasema kuna hofu kuwa idadi ya waliojeruhiwa huenda ikaongezeka.

Mnamo mwezi Januari, treni iliyokuwa imewabeba makurutu wa jeshi, ilianguka na kusababisha vifo vya watu 19 na kuwajeruhi zaidi ya 100.

Novemba mwaka jana watoto 50 walifariki wakati treni ilipogonga basi yao ya shule.

Waziri wa usafiri alijiuzulu baada ya ajali hiyo.

Ajali mbaya zaidi ya gari moshi kuwahi kutokea Misri, ilishuhudiwa mwaka 2002, ambapo treni ilishika moto na kuwaua watu 373

CAMEROON YAUNGANA NA IVORY COAST NA NIGERIA SAFARI YA BRAZIL 2014

Cameroon qualified for the World Cup finals after beating Tunisia 4-1in Yaounde on Sunday to win their two-legged play off tie and book their place in Brazil next year.

A third-minute goal from Pierre Webo broke the deadlock after a goalless draw in last month's first leg before Benjamin Moukandjo's made it 2-0 in the 30th minute.

Tunisia pulled a goal back from substitute Ahmed Akaichi with a left-foot volley in the 50th minute but Jean Makoun scored twice in the second half to settle the tie.

MZEE MANDELA HAWEZI KUZUNGUMZA

Mke wa zamani wa Nelson Mandela, amesema rais huyo wa zamani hawezi kuzungumza, lakini anatumia uso kuwasiliana na watu.

Winnie Madikizela-Mandela alieleza kuwa Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 95, ni mgonjwa kweli lakini alikanusha tetesi kuwa mashini ndio inamsaidia kupumua.

Mwezi wa Septemba Bwana Mandela alirudi nyumbani baada ya kulazwa hospitali mjini Pretoria kwa karibu miezi mitatu akitibiwa ugonjwa wa mapafu.

Serikali ya Afrika Kusini imesema hali yake bado ni ya kutia wasi-wasi na wakati mwengine hubadilika.

AUWAWA KWA KUKATWA NA PANGA KICHWANI

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mele Seni (60) Mkazi wa Kijiji cha Kapalala Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ameuwawa kwa kukatwa na panga kichwani na mgongoni na watu wasio fahamika wakati akiw nyumbani kwake akiota moto.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari tukio hilo la mauwaji ya kinyama yalitokea hapo jana majira ya saa moja na nusu usiku nyumbani kwa marehemu huyo kijijini hapo.

Alisema siku hiyo ya tukio marehemu akiwa nyumbani kwake amejipumzisha akiota moto ghafla walitokea watu wasiofahamika na kupiga hodi nyumbani kwa marehemu ambae nae aliwakaribisha watu hao kwa kujua ni watu wema.

Alieleza ndipo watu hao walipoanza kumshambulia marehemu kwa kumkata kwa panga kwenye kichwa na mgongoni huku marehemu akiwa anapiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani zake.

Kidavashari alisema licha ya marehemu kupiga moyowe majirani zake hawakuweza kujitokeza mapema kuweza kumpatia msaada na ndipo watu hao walipoona Mele Seni amefariki dunia walitokomea kusiko julikana.

Majirani waliweza kufika nyumbani kwa marehemu baadaya muda mrefu wa kutokea kwa tukio hilo ambapo walimkuta marehemu akiwa ameisha fariki dunia huku mwili wake ukiwa na majeraha ya panga kichwani na mgongoni na kisha walitowa taarifa kwa uongozi wa serikali ya kijiji ambao nao walitowa taarifa kwa jeshi la polisi.

Kamanda Kidavashari alieleza kabla ya tukio hilo marehemu alikuwa akilalamikiwa na majirani zake na wanakijiji hichokuwa amekuwa akijihusisha na vitendo vya kishirikina kwa kuwaroga watu kijijini hapo.

Hivyo uchunguzi wa awali uliofanywa na jeshi la Polisi umebaini kifo hicho kametokanana imani ya ushirikina ulisababisha wanakijiji hicho kumjengea chuki marehemu huyo.

Mpaka sasa hakuna mtu au watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hili na jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ili kuwakamata na kuwafikisha mahakamani waliohusika katika tukio hili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi ametowa wito kwa wananchi kutojichukilia sheria mkononi kutokana na kuwahusisha watu na imani za kishirikina na matokeo yake wamekuwa wakiua watu pasipo sababu.


Source:Katavi Yetu Blog

SAMATTA KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA

Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF limetangaza majina ya wachezaji wa kiafrika watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2013 na Mchezaji bora wa Afrika anayechezea vilabu vya ndani ya Afrika mwaka 2013.

Katika majina hayo yapo majina mawili ya wachezaji wanaotoka Afrika Mashariki ambao ni Victor Wanyama raia wa Kenya anachezea Southampton FC ya England ambaye ni miongoni mwa wachezaji 25 watakaowania tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika, huku Mbwana Samatta raia wa Tanzania anayechezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo yeye ameteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika anayechezea timu za Afrika.

Wachezaji 25 watawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika na 21 Mchezaji bora wa Afrika anachezea timu za ndani ya Afrika.

Washindi wa tuzo hizo wanatarajiwa kutangazwa Januari 9, mwaka 2014 mjini Lagos nchini Nigeria.

Orodha kamili ya wachezaji waliotangazwa na CAF na timu wanazotoka hii hapa chini.


Mchezaji wa bora wa CAF Afrika

1. Ahmed Musa - Nigeria - CSKA Moscow

2. Asamoah Gyan - Ghana - Al Ain

3.Dame N'Doye - Senegal - Locomotiv Moscow

4. Didier Drogba - Cote d'Ivoire - Galatasaray

5. Emmanuel Emenike - Nigeria - Fenerbahce

6. Islam Slimani - Algeria - Sporting Lisbon

7. John Mikel Obi - Nigeria - Chelsea

8. Jonathan Pitroipa - Burkina Faso - Stade Rennais

9. Kévin Constant - Guinea - AC Milan

10. Kwadwo Asamoah - Ghana - Juventus

11. Luís Carlos Almada Soares (platini) - Cape Verde - AC Omonia

12. Mehdi Benattia - Morocco - AS Roma

13. Mohamed Aboutrika - Egypt - Al Ahly

14. Mohamed Salah - Egypt - Basel FC

15. Nicolas Nkoulou - Cameroon - Marseille

16. Pierre-Emerick Aubameyang - Gabon - Borussia Dortmund

17. Ryan Isaac Mendes da Graça - Cape Verde - Lille

18. Saladin Said - Ethiopia - Wadi Degla FC

19. Seydou Keita - Mali - Dalian Aerbin F.C

20. Sofiane Feghouli - Algeria - Valencia

21. Sunday Mba - Nigeria - Warri Wolves

22. Victor Wanyama - Kenya - Southampton FC

23. Vincent Enyeama - Nigeria - Lille

24. Yao Kouassi Gervais 'Gervinho' - Cote d'Ivoire - AS Roma

25. Yaya Toure - Cote d'Ivoire - ManchesterCity


Mchezaji bora Afrika anacheza vilabu ndaniya Afrika

1. Adane Girma - Ethiopia - St George

2.Ahmed Fathi - Egypt - Al Ahly

3. Alexis Yougouda Kada - Cameroon - Coton Sport

4. Ali Machani - Tunisia - CAB

5. Bapidi Fils Jean Jules - Cameroon - Coton Sport

6. Daine Marcelle-Klate - South Africa - Orlando Pirates

7. Fakhreddine Ben Youssef - Tunisia - CSS

8. Getaneh Kebede - Ethiopia - Bidvest Wits

9. Idrissa Kouyate - Cote d'Ivoire - CS Sfaxien

10. Iheb Msakni - Tunisia - Esperance

11. Luyanda Lennox Bacela - South Africa - Orlando Pirates

12. Mbwana Samatta - Tanzania - TP Mazembe

13. Moez Ben Cherifia - Tunisia - EST

14. Mohamed Aboutrika - Egypt - Ahly

15. Rainford Kalaba - Zambia - TP Mazembe

16. Senzo Meyiwa - South Africa - Orlando Pirates

17. Soumbeila Diakite - Mali - Stade Malien

18. Sunday Mba - Nigeria - Warri Wolves

19. Tresor Mputu - DR Congo - TP Mazembe

20. Waleed Soliman - Egypt - Al Ahly

21. Yannick N'djeng - Cameroon - EST

AUWAWA KWA KUKATWA KOLOMEO AKIWA AMELALA

Mpanda Katavi

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ngoro Nyengera (60) mkazi wa Kijiji cha Mirumba Tarafa ya Usevya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ameuwawa kwa kukatwa kolomeo na kitu chenye ncha kali nyumbani kwake wakati akiwa amelala kitandani na mume wake.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo la mauwaji ya mwanamke huyo ya kusikitisha lilitokea hapo juzi majira ya saa saba na nusu usiku nyumbani kwa marehemu ambae alikuwa akiishi na mume wake aitwaye Rina Kuzenza (70) Alisema siku ya tukio marehemu alikuwa amelala na mumewe kitandani katika nyumba waliokuwa wakiishi pamoja na kijana wao aitwaye Ndura Kusenza (20) ambae yeye alikuwa akilala chumba kinachotazamana na chumba cha wazazi wake.

Kamanda Kidavashari alieleza ghafla watu wawili walivunja mlango wa chumba alichokuwa amelala marehemu na mumewe na kuingia ndani huku wakiwa na tochi kubwa mbili zenye mwanga mkali na kuwaweka chini ya ulinzi wao marehemu na mumewe.

Alisema ndipo walipomwamuru mume wa Marehemu akifunike usoni kwa shuka yake na kisha walimlazimisha alale akiwa amelala kifudifudi.

Kidavashari alieleza kuwa baada ya kulazimisha hivyo mumewe alitekeleza amri hiyo na ndipo watu hao walipoanza kumkata Ngoro Nyengera kolomeo hadi kufariki dunia Kamanda Kidavashari alisema siku za nyuma marehemu alikuwa akilalamikiwa na wanakijiji wenzake kuwa ni mshilikina na amekuwa akituhumiwa kuwaloga wanakijiji wenzake hari ambayo ilipelekea marehemu kuchukiwa na kukosa mahusiano mazuri baina yake na wanakijiji wenzake.

Alisema katika tukio hilo hakuna mtu wala watu waliokamatwa na jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa kuwabaini waliohusika katika mauwaji hayo ili kuweza kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma hii ya mauwaji ya kinyama.

Source: Katavi Yetu Blog

AKATWA SEHEMU ZA SIRI AKIWA AMELALA KWA SHEMEJI YAKE

Mpanda Katavi

Mtu mmoja Mkazi wa Kijii cha Majimoto Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi MwamiM wanalusi (31) amekatwa nakisu katika sehemu zake za siri na watu wasiojurikana wakati akiwa amelala ndani ya nyumba ya shemeji yake na watu wasio julikan.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea hapo jana majira ya saa nane usiku nyumbani kwa shemeji yake.

Alisema siku ya tukio Mwami alikuwa ameenda kumtembelea shemeji yake aitwaye Anset Kapampala (36) ambae alikuwa akiishi katika kijiji hicho cha Majimoto.

Baada ya mlo wa usiku mwenyeji wake alimuonyesha chumba cha kulala ambacho hata hivyo hakikuwa na godoro wala kitanda bali kulikuwa na Benchi la kupumzikia ambalo shemeji yake ambae ni mwenyeji wake alimweleza Benchi hilo ndilo alitumie kama kitanda cha kulalia kutokana na hari yake ya kiuchumi kutokuwa nzuri.

Alisema wakati Mwami yuko ndani ghafla walitokea watu asio wafahamu ambao waliingia ndani ya chumba hicho na wala hawakumsemesha chochote hari ambayo ilimfanya ashikwe na butwaa.

Alieleza ndipo watu hao walipo anza kumkata kwa kisu sehemu zake za ume hadi ume ukawa umeharibika vibaya na kisha watu hao wakatokomea kusiko julikanana kumfaya yeye apige mayowe ambapo shemeji yake ambae alikuwa amelala kwenye nyumba yake nyingine alishituka na ndipo alipoingia ndani na kumkuta mgeni wake akiwa ameharibiwa vibaya sehemu zake za siri.

Kamanda Kamanda Kidavashari alisema chanzo cha tukio hilo bado hakijulikana na polisi wanaendelea na epelelezi ili kuwabaini na kuwakamata waliohusika ili sheria ichukuwe mkondo wake.

Source: Katavi Yetu blog

WATUPWA JELA MIAKA 70 KWA KUKAMATWA NA MENO YA TEMBO

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imewahukumu watu watatu kutumikia kifungo cha jumla ya miaka sabini jela bada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na meno ya tembo manne yenye thamaniya shilingi milioni 45.

Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya kulidhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka na upande wa utetezi.

Waliohukumiwa kifungo hicho ni Gwabi Mayala (39) mkazi wa kijiji cha Majimoto Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi ambae alikuwa mshitakiwa wa kwanza amehukumiwa kifungo cha miaka 30 na kulipa fidia ya shilingi milioni 45 Washitakiwa wengine waliohukumiwa ni Mashaka Mabanga (33) Mkazi wa Sumbawanga Mkoa wa Rukwa na Adamu Kalinzi (30)Mkazi wa Kijiji cha majimoto Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wamehukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka ishirini jela.

Awali katika kesi hiyo ilidaiwana mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Fadhili Mwandoloma kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo hapo Oktoba 10 mwaka huu majira ya saa nne usiku katika Kijiji cha Majimoto Wilayani Mlele Wanadaiwa siku hiyo ya tukio washitakiwa walikamatwa wakiwa na meno manne ya Tembo yenye uzito wa kilo kumi na sita yenye thamani ya shilingi milioni 45 wakiwa katika harakati ya kuyauza.


Mwanasheria huyo wa Serikali aliiambia mahakama kuwa Mshitakiwa wa kwanza Gwabi Mayala ndiye aliyekuwa mwenye meno hayo ya Tembo na aliwashirikisha wenzake hao wawili kwa ajiri ya kumtafutia wateja ambao wangeyanunua meno hayo ya Tembo Aliiambia mahakama baada ya washitakiwa hao kukamatwa na Askari wa Hifadhi ya wanyama pori ya Katavi walioshirikiana na polisi washitakiwa walipofikishwa polisi mshitakiwa wa pili na watatu walikiri kuhusika na meno hayo ya tembo na kudai kuwa meno hayo ni ya mshitakiwa wa kwanza Gwabi Mayala.


Hakimu mkazi mfawidhi Chiganga baada ya kusikiliza mwenendo mzima wa kesi hiyo aliiambi mahakama kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo wa pande mbili za mashitaka na utetezi mahakama imewaona washitakiwa wote watatu wanahatia hivyo kabla ya mahakama haijatowa adhabu inatowa nafasi kwa washitakiwa kujitetea Katika utetezi washitakiwa Mashaka na Adamu walikiri kukamatwa na meno hayo ya Tembo lakini walidaikuwa meno hayo ya Tembo yalikuwa ni ya mshitakiwa wakwanza Gwabi Mayala ambae alikuwa amewaomba wamtafutie wateja wa kuyanunua kwa upande wake mshitakiwa Gwabi aliiomba mahakama isikubaliane na maelezo ya washitakiwa wenzake kuwa meno hayo yalikuwa sio ya kwake.


Hakimu Chiganga alieleza mahakama kuwa washitakiwa wamevunja sheria ya kifungunamba 86 (1) (2) cha sheria ya huifadhi ya mwaka 2009 na kifungu namba 57 na 60 ya sheria ya kuhujumu uchumi sura ya 200 ya mwaka 2002 hivyo mahakama imetowa adhabu kwa mshitakiwa wa kwanza Gwabi Mayala kutumikia kifungo cha miaka 30 jela la kulipa fidia ya shilingi milioni 45 ambayo ni thamani ya meno hayo ya TemboPia washitakiwa Mashaka Mabanga na Adamu Kalinzi wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kushirikiana na mshitakiwa wa kwanza katika biashara ya kumtafutia wateja wa kununua meno ya Tembo.

Kwa hisani ya: Katavi yetu blog

UN YAGOMA KUWAUNGA MKONO RUTO NA KENYATTA

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, limekatalia mbali ombi la kuahirishwa kwa kesi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.

Azimio hilo lililokuwa limependekezwa liliungwa mkono na nchi wanachama wa Muungano wa Afrika.

Viongozi hao wawili wanatuhumiwa kwa kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia za baadaya uchaguzi mwaka 2007-08 nchini Kenya.

Kukataliwa kwa azimio hili ni changamoto ya hivi punde kwa kesi inayowakabili Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto wanaotuhumiwa kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007-08.

Lakini azimio hilo lilipata tu kura saba badala ya angalau tisa ambazo zilihitajika kupitishwa na baraza la usalama la UN.

Nchi nane wanachama wa baraza la usalama la UN, nchi wanachama wote wa ICC, Uingereza, Ufaransa na Marekani zote zilijizuia kupiga kura kuhakikisha kuwa azimio hilo halipiti.

Ilikuwa mara ya kwanza katika miaka kumi kwa baraza la usalama la UN kukosa kupigia kura azimio kama hilo bila ya kutumiwa kwa kura ya turufu na mwanachama wa kudumu wa UN.

Mataifa ya Afrika yakiongozwa na Rwanda, iliyopendekeza azimio hilo, yalikosolewa vikali kwa kupendekeza azimio hilo na kulazimisha baraza la Usalama la UN kupiga kura.

Balozi wa Guatemala katika Umoja wa Mataifa, alisema kuwa jaribio la kutaka kuahirisha kesi hiyo ilikuwa njama ya hujuma dhidi ya nchi zinazotaka kusaidia Afrika na juhudi za amani pamoja na kuimarisha uwajibikaji wa viongozi katika mataifa hayo.

Kenyatta na Ruto wanatuhumiwa kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi Kenya, mwaka 2007 ambapo takriban watu 1,100 walifariki.

Kenyatta na Ruto walichukua hatamu za uongozi baada ya uchaguzi uliofuata mwaka 2013

DUMA WAKIONA CHA MTEMAKUNI TOKA KWA WANAKIJIJI

Wanakijiji Kaskazini Mashariki mwa Kenya wamewakimbiza Duma wawili ambao wamekuwa wakiwaua Mbuzi wao na kuwakamata.

Wakaazi hao wanaoishi karibu na mji wa Wajir walisubiri hadi majira ya joto nyakati za mchana kuwafukuza Duma hao ambao baada ya kilomita sita walichoka na kusalimu amri.

Jamaa aliyeongoza uwindaji huo amesema aliamua kuchukua hatua baada ya Duma hao kuwaua mbuzi wake 15.

Duma hao walikamatwa wakiwa hai na wamekabidhiwa shirika la wanayapori KWS huku wana kijiji hao wakitaka kulipwa fidia ya mbuzi waliouawa.

Wanakiji hao waliambia BBC kuwa wanyama hao walikuwa wakiwashika Mbuzi wao mmoja baad ya mwingine kila siku.

"Nahitaji kulipwa fidia kwa sababu Duma hawa waliwala mifugo wangu wengi,'' alisema Nur Osman Hassan.

Mifugo ndio njia kubwa zaidi ya kujikimu katika jamii ya wasomali wakenya wanaoishi Kaskazini Mashariki mwa nchi ambako ukamendio hali ya maisha ya kawaida kwao.

Mzee Hassan alisema kuwa Duma hao waliwaua Mbuzi wake 15 na kuwa walikuwa wakija nyumbani kwake kila siku.

Aliongeza kwamba, aliamua kurejea kijijini kuapanga ambavyo angewakamata Duma hao wakati wamchana ambapo Duma hao huwa wachovu.

"Nilikuwa nakunywa chai wakati nilipowaona wakimla Mbuzi mwingine, '' aliongeza kusema kuwaulikuwa wakati wa asubuhi.

Alisema alisubiri hadi jua lilipokuwakali mno na ndiposa walianza kuwakimbiza.

"Niliwaita vijana na kisha tukawakimbiza Mbuzi hao,'' alisema mzee Hassan.

''Tuliwakamata na kisha kuwaleta kwa maafisa wakuu kijijini mwetu.''

MFUNGWA ANAETARAJIA KUNYONGWA AOMBA ATOE ZIUNGO VYA NDANI KUNUSURU UHAI WA MAMA YAKE

Ronaldo Phillips mfungwa anayetarajiwa kunyongwa Marekani Hukumu ya kunyongwa kwa Ronald Philllips aliyepatikana na hatia ya kumuua mtoto wa miaka mitatu katika jimbo la Ohio nchini Marekan imeahirishwa kutokana na mshitakiwa huyo kuomba kuchangiabaadhi ya viungo vyake vya mwili zikiwemo figo ili kunusuru uhai wa mama anayeumwa.

Ronald Phillips alitarajiwa kunyongwa Alhamis kwa njia ya sindano ya sumu baada ya kupatiakana na hatia ya kumuua mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu mwaka 1993.

Gavana wa jimbo la Ohio John Kasich amesema kama ombi hilo la mshitakiwa litasaidia kuokoa uhai wa mtu mwingine basi na likubalike, lakini litakuwa jambo geni kuahirishwa kwa adhabu iliyokwisha kupitishwa japo kuwa madaktari wanapaswa kuthibitisha.

Phillips mwenye umri wa miaka 40 alihukumiwa kifo kutokana na makosa ya ubakaji na mauaji ya binti wa rafiki yake wa kike Sheila Marie Evans.

Dawa ya sumu iliyotarajiwa kutumika kumuua Phillips ni aina ya midazolam na hydromorphone, mchanganyiko wa dawa ambayo ingetumika kwa mara ya kwanza nchini Marekani kunyonga watuJimbo la Ohio liliamua kutumia mchanganyiko wa dawa hii kwa sababu haikuwa na kiasi cha kutoshacha dawa ya kawaida inayotumika kunyongea watu ijulikanayo kama pentobarbital.

Mama mzazi wa Phillips amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya figo nadada yake Phillips pia anasumbuliwa na maradhi ya moyo ambapo anasema anahitaji kutoa viungo vyake haraka iwezekanavyo.

KIM POULSEN AITA 32 WAKAOCHEZA MECHI ZA KIRAFIKI

Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameunda kikosi cha wachezaji 32 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Kenya itakayochezwa Jumanne, Novemba 19 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wachezaji walioitwani makipa wanne; Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said Moradi (Azam).


Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo, Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian(Simba).


Viungo washambuliaji ni Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).


Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa SugarMbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

BOKO HARAM NA ANSARU WAJUMUISHWA KAMA VIKUNDI VYA UGAIDI NA MAREKANI

Serikali ya Marekani imeweka makundi ya wapiganji wa Kiislam ya Boko Haram na lile la Ansaru katika orodha yake ya ugaidi.

kutokana na sheria za Marekani sasa itakuwa kosa la jinai kutoa msaada wowote kwa makundi hayo yanayotuhumiwa kusababisha vifo vya watu wengi nchini Nigeria.

Marekani imesisitiza kuwa hii ni hatua muhimu katika kuisaidia Nigeria na mashambulizi kutoka katika makundi hayo mawali na kwamba sasa yatambulike kama makundi ya kigaid kama ilivyo kwa Al Qaeda.


Kutokana na hatua hiyo ya Marekani idara zake zinapaswa kusitisha biashara zote zinazoendeshwa mtandao huo wa kigaidi na kudhibiti usafirishaji wa fedha ndani ya makundi hayo Pamoja na kundi hilo kuwepo zaidi nchini Nigeria lakini Marekani inasema limekuwa likishirikiana na mtandao wa kimataifa wa Ugaidi wa Al Qaeda ambapo matawi yake yapo pia Afrika Magharibi na Mali Kundi hili la Boko Haram lilianzishwa mwaka 2009 huku mashambulizi yake yakielekezwa katika vituo vya jeshi, katika shule na kuendesha mapigano na vikosi vya ulinzi nchini Nigeria.

RROFESA KAPUYA MATATANI BAADA YA KUDAIWA KUMBAKA MWANAFUNZI

MBUNGE wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), ameingia katika matata. Katika kujaribu kudhibiti mtoto wa shule ambaye anadai alibakwa naye na kuambukiwa virusi vya ukimwi, mbunge huyo ametoa vitisho vya kuua mtoto huyo na kujiua kama njia ya kuepuka dhahama inayoelekea kumkabili.Siku moja baada ya gazeti hili kuripoti habari za mbunge mmoja (bila kumtaja jina), jana asubuhi Profesa Kapuya ameibuka na kumtisha mwanafunzi huyo mwenye miaka 16 anayesoma Shule ya Sekondari Turiani iliyoko Magomeni jijini Dar es Salaam.

Baada ya kujua kuwa mtoto huyo ndiye alitoa habari za masahibu hayo, ambayo mbunge hakutaka yajulikane, alimpigia simu mtoto huyo, na baadaye kutuma meseji kadhaa za vitisho.

Jana Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Profesa Kapuya kwenda kwa mtoto huyo.

Alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake ya mkononi yenye namba 0784993930, Profesa Kapuya alituma ujumbe ufuatao kwa mtoto huyo: "chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?" Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyohiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: "Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu.

"Mwambieni Mbowe mwenye hilo gazeti awape nyumba ya kuishi. Si mmemuingizia hela leo? Mnatumika bure watu wanaingiza hela nyingi, mmenitibua lazima niwauwe wiki hiii haitaisha, nitapanga kambi popote."Jana si wamekuficha? Tuone kama utalindwa milele.

Kazi ya kulindwa imeisha, maana wameshatengenezahela. Lazima mvae sanda. Hilo sio ombi, ni wajibu wenu. Mnajitia mafia watoto sio? Watoto wetu wanauza unga, nani anawakamata? Nani atapigana nasi?

"Hata hivyo, baada ya kuhisi kuwa watoto hao wamedhamiria kumchukulia hatua, na wamewasiliana na taasisi mbalimbali za kiraia na serikali zenye uwezo wa kumtia adabu, mbunge huyo alimtumia mtoto huyo ujumbe wa kuonyesha alikuwaanafikiria kunywa sumu.. Ujumbe huo uliotumwa kwa mtoto huyo saa 11:2 3 ulisema: "nimwakosea sana, acha nife mie nakunywa sumu nijiue, na nyie mje mnizike.

"Hasira za Profesa Kapuya dhidi ya mtoto hao zilitokana na hatua ya mtoto huyo na dada yake kufichua unyama wanaodai kutendewa na mbunge huyo, ambaye amewahi kushika nyadhifa kadhaa za uwaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Tangu alipogundua kuwa mtoto huyo alizungumza na gazeti hili juzi, saa 5:17 usiku wa kuamkia jana alituma ujumbe usemao: "Si mpo Bilz? Sasa tupo pamoja na nyie mpaka usiku.

"Baadaye saa 5:31 alituma ujumbe huu: "Hivi hamkubali kushindwa? Leo ulifuata nini ofisi ya CCM?" Ujumbe huo ulitokana na ukweli kwamba dada wa mtoto anayedaiwa kubakwa alifika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) juzi asubuhi kuonana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, ili kuomba chama kimsaidie kumbana Profesa Kapuya, ambaye alikuwa ameanza kuwatisha yeye namdogo wake.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mtoto huyo, Kinana alisema suala hilo si lachama bali la Profesa Kapuya binafsi.

Mtoto huyo alikataa ushauri wa kupeleka shauri hilo mbele ya vyombo vya sheria, akidai kuwa jitihada zake zimekuwa zinazimwa na mbunge huyo anayedai serikali haiwezi kumfanya lolote.Alisisitiza kuwa hana imani na serikali, lakini akasema yupo tayari kuchukua hatua kali dhidi ya Profesa Kapuya iwapo atasimamiwana watetezi wa haki za binadamu.

Baadhi ya mashirika yanayotetea makundi kadhaa yakiwamo Kituo cha Sheria na Haki za BInadamu (LHRC) na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) yalijitokeza kumsaidia watoto hao, ambao ni yatima.

Mtoto huyo na dada yake, wakizungumza na gazeti hili kwa hofu mafichoni, walisema kwa sasa hawana imani tena kama kuna serikali nchini Tanzania kwa kuwa wamedhalilishwa, wametembezwa hadi Bungeni na wabunge bila hatuakuchukuliwa, licha ya kutoa taarifa katika kituo cha polisi Oysterbay tangu mwaka jana.

Hata hivyo, kabla ya tukio la watoto hao kuripoti, ofisi za gazeti hili juzi usiku kulikuwa na watu waliokuja wakiwatafuta watoto hao, huku wakiwatisha kwa simu na kuwatoleamaneno ya kejeli, wakidai watawamwagia tindikali.

Mmoja wa watoto hao, alidai kuwa miongoni mwa vijana waliokuwa wanawatisha juzi walikuwa katika gari T170 BGY, Benz, Cream Metalic, ambayo inamilikiwa na mbaya wao.

Jana gazeti hili lilichapisha habari kuwa mwanafunzi huyo aliyesema kuwa waziri huyo alimbaka kwenyehoteli moja ya kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipoitwa kwenda kuchua ada kwa mara ya pili.

Akizungumza kwa uchungu, alisemambunge huyo alifanya kitendo hicho kwenye Hoteli ya Giraffe, Jijini Dar es Salaam mwaka 2011.

Alisema kuwa yeye alikuwa na urafiki na mwanafunzi mwenzake Zuhura Mwaking'inda. Mwaking'inda amewahi kuwa Diwani wa Kata ya Sinza Jimbo la Ubungo, Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, rafiki yake (mtoto wa Mwaking'ida) alikuwa amepooza hivyo alikuwa analazimika kumhudumia hali iliyowaunganisha hadi huyo mtoto alipochukua jukumu la kumtambulisha kwa baba yake ambaye naye alimtambulisha kwa Kapuya ili aweze kumsaidia fedha kwa jili ada.

Mwanafunzi huyo alisema baada ya kutambulishwa aliitwa katika hoteli moja jijini Dar ambapo baada ya kufika mapokezi wafanyakazi wa hoteli hiyo walimkataza kuingia chumbani katika maana kwamba umri wake alikuwa mdogo (mwaka 2011 alikuwa na miaka 14), lakini Kapuya aliamrisha aje chumbani pamoja na dereva na kumwingiza kwa nguvu.

Akiwa chumbani alimlazimisha kulala naye kisha kumpa sh laki saba, badala ya sh elfu sitini na sabakiasi ambacho kilikuwa ndio mahitaji halisi ya ada.


Mwanafunzi huyo amesema baada ya muhula mmoja aliitwa tena na mbunge huyo katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala tarehe 3 June 2012, ambapo pia alimlazimisha kulala naye kwenye zulia la ofisi yake, kisha kumpa sh 350,000/.


Alisimulia kwamba wakati anatoka kwa huzuni ofisini kwa mbunge huyo, mmoja wa wahudumu wa hapo alimuuliza kwanini anatoka kwa huzuni, alimweleza kisa hicho, na huyo mama aliangua kilio kwa kumwambia "mwanangu umekufa pole tu, huyu baba ni muathirika waukimwi".

Aliongeza kuwa baada ya kuambiwa vile alilia na kufanya fujo hapo mapokezi hadi alipokamatwa na walinzi wa kisha kupelekwa kituo cha polisi kufunguliwa mashtaka, lakini akiwa polisi alipoeleza mkasa wote, Polisi walilazimika kumwita Kapuya na wakawasuluhisha kwa makubaliano kwamba Kapuya atakuwa anamlipia ada, na kumpa pesa za matumizi sh. laki tatu kila mwezi, jambo ambalo amekuwa akilitekeleza kupitia simu yake ya mkononi 0755993930.


Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, 24 Januari 2013, alifika mtu nyumbani kwao mtu mmoja (jina tunalihifadhi) na kujitambulisha kuwa yeye ni jambazi na kuwa alitumwa kwenda kuwaua kwa malipo ya sh. milioni 50, lakini alipokuta ni watoto wadogo aliwasamehe, na kusema yeye ni jambazi sugu hawezi kupoteza nguvu zake kuua vitoto.

Alienda akiwa na bastola, maji kwenye chupa yanayodhaniwa kuwani tindikali na bomba la sindano. Kwa mujibu wa mtoto huyo, jambazi huyo anasema kuwa tayari alilipwa milioni 15 za awali.


Mtoto huyo alisema jambazi huyo aliwambia kuwa yeye ni rafiki wa mtoto wa Kapuya na wanamfahamuvizuri, lakini hataweza kuaua baada ya kubaini kuwa wao ni yatima tu.

Hata hivyo kufikia mwezi Februari mwaka huu, mtu asiyefahamika alienda nyumbani na kutelekeza gari aina ya T.199 BGY Mercedes Benzi ya Blue wakati wanafunzi hao wakiwa shuleni, kisha kuacha ufunguo kwa jirani yao kwa maelekezo kuwa wakifika awapatie.

Na Kapuya aliwapigia simu kuwaarifu kuwa amempa zawadi ya gari kwa ajili ya matumizi ila yeye na dada yake wanaruhusiwa kuuza ili wapate pesa kwa ajili ya mahitaji yake siku zilizosalia, kwani muda siomrefu baada ya uchguzi mkuu 2015, Kapuya atakuwa Waziri Mkuu,hivyo itakuwa ngumu yeye kumtumia huyo binti pesa kama alivyoelekezwa na jeshi la polisi kituo cha Oysterbay.

Baada ya mwanafunzi huyo na dada yake ambaye ana umri wa miaka 20, kupewa gari walishindwa kulitumia hivyo kutoa taarifa polisi kwani kwa kupokea gari hilo ilikuwa ni kuwatelekeza kwani yeye hana hata hela ya kuweka mafuta yagari, hivyo walienda polisi ili kesi ipelekwe mahakamani kumshtaki kapuya.


Polisi wa Oysterbay walikubali kulipeleka tatizo hilo kwa Katibu waBunge, ambaye alimwita mwanafunzi huyo na mdogo wake waende Dodoma kukutana na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ingawa walipofika Dodoma walikaa na kamati ya hiyo kwa maelezo kuwa Kapuya hakuwepo hadi Bunge lilipoisha walirejeshwa Dar es Salaam.


Mtoto huyo na dada yake alitoka ofisi za CCM lakini akiwa anaelekea kituo cha basi alithadharishwa na mwanafunzi mwingine kwa haraka kuwa akimbie kwa kuwa atamwagiwa tindikali na watu waliokuwa wanamfuata nyuma, alikimbilia katika mtaa wa Hoteli ya Star light kisha aliomba msaada baada ya kupotea njia na hivyo alisaidiwa na mama mmoja kufikishwa chumba cha habari cha Channel Ten.

Ni katika chumba hicho ndio mwandishi wa habari hizi alienda na kuwakuta watu wawili hao waliokuwa wanamhitaji binti huyo lakini walikatazwa kumchukua.


Chanzo: Tanzania Daima

AKAMATWA NA BASTOLA INAYODAIWA KUWA YA DK. MVUNGI

.Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia mtu mmoja (jina tunalihifadhi), kwa tuhuma za kukutwa na bastola inayodaiwa kuwa ilikuwa inamilikiwa na marehemu Dk Sengondo Mvungi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova alidai jana kuwa mkazi huyo wa Kiwalani, Dar es Salaam alikutwa na bastola aina ya Revolver yenye namba BDN 6111 ikiwa na risasi 21 na baada ya kufuatilia kumbukumbu zao na kuwasiliana na familia ya Dk Mvungi walibaini kwamba ilikuwa niya mwanasheria huyo nguli.

Huyo anakuwa mtuhumiwa wa 10 kukamatwa tangu kutokea kwa tukio la kushambuliwa kulikosababisha kifo cha Mjumbe huyo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Dk Mvungi alivamiwa nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, Dar es Salaam usiku wa kuamkia Novemba3, mwaka huu.

Mbali ya kushambuliwa, wavamizi pia waliiba bastola, kompyuta mpakato(laptop) na simu tano za mkononi.

Kamishna Kova alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi saa 12 jioni Mitaa ya Twiga na Jangwani alipokuwa akiangalia runinga na akifuatilia taarifa za matukio ya tukio hilo. Alisema kukamatwa kwake kulitokana na taarifa za msamaria mwema.

Alidai kwamba baada ya kukamatwa aliwaongoza polisi hadi nyumbani kwake Kiwalani ambako walikuta bastola moja na risasi hizo.


Kutoka:Mwananchi

KONTENA LA MENO YA TEMBO LAKAMATWA ZANZIBAR

Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar, vimekamata kontena la futi 40 likiwa limepakia meno ya tembo yaliyohifadhiwa kwenye mifuko ya nailoni yenye ujazo wa kilo 50, yakisafirishwa nje ya nchi.

Meno hayo yalikamatwa Bandari yaMalindi majira ya alasiri jana na polisi, Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM), Maofisa wa Usalama wa Taifa na raia wema waliotoa taarifa kuhusiana na mpango huo.

Akizungumza mjini hapa jana, Kamishna wa Polisi Zanzibar, MussaAli Mussa alisema uchunguzi wa tukio hilo umeanza ikiwamo kuwasaka wamiliki wa mzigo huo kupitia Kampuni ya Wakala wa Kusafirisha Mzigo, iliyopewa kazi hiyo.


Kamishna Mussa alisema kazi ya kupakua mzigo na kuchana gunia moja baada ya jingine tayari imeanza chini ya ulinzi mkali wa askari ili kujua idadi ya meno na thamani yake. Alisema mzigo huo ulikamatwa kupitia taarifa za siri zilizofanikisha kugundua kontena hilo lililokuwa na meno hayo yaliyochanganywa na kuwekwa katikati ya makombe (sea shells).

Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki alisema wakati umefika kwa Watanzania kushiriki na kuvikabili vitendo vya ujangili vyenye lengo la kuangamiza wanyamapori hasa Tembo na Faru.

Balozi Kagasheki alisema kazi inayofanywa na askari ni sehemu ya utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili, huku akiwapongeza askari kwa
kufanikisha jukumu lao.

Naye Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais (Idara Maalumu na Vikosi vya SMZ) Haji Omar Kheir alisema hakuna sheria za nyara za Serikali kutokana na visiwa hivyo kutokuwa na wanyamapori wa aina hiyo, lakini wahusika wanaweza kushtakiwa kwa kuhujumu uchumi ya Zanzibar iliopitishwa mwaka huu.

MWALIMU ALA NJAMA ZA KUMLAWITI MWANAFUNZI

Katika hali isiyo ya kawaida, mwalimu wa Shule ya Sekondari Nyerere iliyopo wilayani hapa mkoani Kilimanjaro anatuhumiwa kuwakodi vijana watatu wamlawiti mwanafunzi wa kidato cha tatu na kumsababishia maumivu makali huku mwalimu huyo akidaiwa kupiga picha unyamahuo.

Akizungumza na gazeti hili mwanafunzi aliyefanyiwa unyama huo alidai, bila kujua njama za mwalimu wake alikubali kuitika wito na alipomfuata walitokea waendesha bodaboda na kumteka na kumpeleka katika moja ya nyumba zao, ambapo walimpiga na shoti ya umeme, baadaye alipokuwa hajielewi walimwingiza karoti na baadaye kumlawiti kwa zamu.

Mwanafunzi huyo amesema hajui kosa lake na anasikitika kwa unyama huo na kuiomba Serikali ichukue hatua stahiki kwa wahusika.

Kwa sasa mwanafunzi huyo anaendelea vizuri na matibabu.

Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa alisema, mwanafunzi huyo amekutwa na balaa hilo kufuatia mwalimu anayetuhumiwa kurudi nyumbani na kukuta mtoto wake wa kike wa miaka mitatu akiwa chumbani kwa mwalimu mwenzake anayeishi na mwanafunzi huyo. "Alipomwita mtoto wake alidai alichelewa kutoka na akahisi huenda mwanae amefanyiwa kitendo kibaya lakini alipompeleka hospitali kwa vipimo hakukutwa na dalili ya kubakwa," alisema mwalimu huyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz alithibitisha kutokea kwa tukio hilo Novemba 3, mwaka huu saa 12 jioni katika maeneo ya Lembeni wilayani hapa.

Alisema mwalimu na wanaume waliomfanyia kitendo hicho mwanafunzi huyo wanashikiliwa na kwamba watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma.


Kutoka:Mwananchi

ATUPWA NJE YA TIMU KWA KUONESHA ISHARA YA KUMUUNGA MKONO MOSRI

Mchezaji soka mmoja katika moja ya vilabumaarufu nchini Misri ametupwa nje ya mechi za klabu hiyo baada ya kuonekana kumuunga mkono rais aliyeondolewa mamlakani Mohammed Morsi.

Klabu ya Al Ahly, imesema kuwa Ahmed Abdul Zaher, hatashiriki mchuano wa FIFA wa klabu bingwa duniani baada ya kupiga saluti ya vidole vinne mnamo siku ya Jumapili.

Mchezaji huyo alikuwa anasherehekea bao lake la mchuano wa mabingwa wa Afrika ambapo Al Ahly ilishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Orlando Pirates wa Afrika Kusini.

Ishara hio imekuwa ikitumika kama ishara ya kumuunga mkono bwana Morsi.

Ishara hiyo pia ilitokana na maandamano ya wafuasi wa Morsi waliotawanywa na maafisa wa usalama mnamo mwezi Agosti baada ya kukesha katika eneo walilosema alikuwa amezuiliwa Morsi.

Rais Morsi alikuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo kuchaguliwa kidemokrasia, na sasa anakabiliwa na kesi ya kuchochea mauaji ya waandamanaji wakati wa ghasia zilizotokea mjini Cairo mwaka jana.

Yeye mwenyewe aling'olewa kutoka uongozini mwezi Julai.

Abdul Zaher alisherehekea kwa ishara ya vidole vinne baada ya kuingiza bao la Al Ahly la pili ambapo waliibuka washindi dhidi ya Orlando Pirates.

"ndio nilitoa ishara hiyo ya Rabaa," alinukuliwa akisema kwenye mtandao wa FilGoal.

"lakini sikunuia kuzua hisia za kisiasa kwa mtu yeyote, nilichonuia ni kumkumbuka mtu yeyote aliyefariki, awe raia wa kawaidaau hata polisi.

''Mnamo siku ya Jumatatu maafisa wa klabu ya Al Ahly, walisema kuwa Ahmed Abdul Zaher hatashirikishwa kwenye mechi itakayochezwa nchini Morocco.

WAFILIPINO BADO HAWAJAPATA MSAADA

Siku nne baada ya Kimbunga Haiyan kupigamji wa Tacloban ,Ufilipino, maelfu ya watu wangali wanasubiri msaada wa dharura.

Umoja wa mataifa umetoa wito kwa jamii ya kimataifa kutoa msaada wa dola millioni 301 ili kuwasaidia watu nchini Ufilipino.

Wakitoa ombi hilo mjni Geneva,wafanyikazi wa umoja huo wamesema maswala yanayopewa kipaumbele ni chakula, maji na dawa licha ya kuwa maeneo mengi bado hayawezi kufikiwa.

Wakati huohuo, Meli za Marekani na Uingereza zinaelekea nchini Ufilipino huku Umoja wa Mataifa ukiomba msaada kupelekwa nchini humo kukiwa na taarifa za uharibifu mkubwa uliosababishwa na kimbunga Haiyan.

Marekani imepeleka ndege na meli za mizigo kwenda Ufilipino, wakati ambapo Uingereza imepeleka meli ya kivita.

Watu wapatao 10,000 wanahofiwa kufa, namaelfu ya walionusurika katika kimbunga Haiyan wanahitaji msaada.

Rais wa Ufilipino Benigno Aquino ametangaza hali hiyo kuwa janga la kitaifa.

Katika taarifa yake, Rais Aquino,amesema majimbo mawili ya Leyte na Samar yameathirika zaidi kutokana na kimbunga hicho, ikiwemo watu wengi kupoteza maisha.

Juhudi kubwa za kimataifa zinafanyika ili kutoa msaada wa dharura kwa Ufilipino, lakini wafanyakazi wa mashirika ya kutoa msaada wanakwama kuyafikia maeneo yaliyokumbwa na kimbunga.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amezielezea picha zinazoonyesha ya kimbunga hicho kuwa zinatisha na kukatisha tamaa.

Umoja wa Mataifa utazindua mpango mkubwa wa msaada wa kibinadamu, na kutenga dola milioni 25 kusaidia jitihada zamisaada ya dharura.

"Maelfu ya watu wameripotiwa kufa na watu wapatao milioni kumi wameathirika kutokana na kimbunga hicho. Hebu tuonyeshe mshikamano wetu na watu wa Ufilipino katika kipindi hiki cha kuhitaji msaada," amesema.

Mbali na Marekani na Uingereza, nchi nyingine pia zimeahidi mamilioni ya dola ukiwa ni msaada kwa Ufilipino. Australia imeidhinisha dola milioni 9, wakati ambapo New Zealand imeahidi zaidi ya dola milioni moja, huku Uchina ikiahidi kutoa dola laki moja. ($100,000)

JUHUDI ZA KUTIA SAINI MKATABA WA AMANI DR CONGO WAGONGA MWAMBA

Shughuli ya kutia saini mkataba wa amani kati ya waasi wa M23 na serikali na Jamhuriya kidemokrasia ya Congo, iliyokukuwa imepangwa kufanyika Jumatatu, iligonga mwamba.

Hii ni kutokana na serikali ya Congo kusema kuwa mkataba huo uangaliwe upya na hivyo kulazimisha shughuli hiyo kuahirishwa.

Mpatanishi wa pande hizo mbili Ofuono Opondo wa Uganda, alisema kuwa pande hizo hazikuwa tayari kuonana ana kwa ana baada ya DRC kusema kuwa M23 watie saini mkataba katika chumba tofauti na kisha wapewe wao kuusaini.Hata hivyo mpatanishi alisema haiwezekeni kwa hilo kufanyika kwa sababu pande zinazozozana lazima zikae katika chumba kimoja kwa ajili ya kufanikisha juhudi za upatanishi.

Kundi la waasi la M23 lilisitisha uasi wao baada ya kupata kipigo kutoka kwa wanajeshi wa DRC wakisaidiwa na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa waliowafurusha kutoka maficho yao ya milimani katika mpaka wa Rwanda na Uganda.

Mkataba huo ulistahili kutiwa saini mjini Kampala Uganda, ingawa shughuli yenyeweilicheleweshwa bila ya kujua itafanyika lini.

Mwandishi wa BBC mjini Kampala, Ali Mutasa anasema kuwa mpatanishi mkuu Ofwono Opondo alisema mkataba hautatiwa saini na kwamba haijulikani ni lini makubaliano hayo yatasainiwa.

AlisemaUpande wa M23 uko tayari kwa shughuli hiyo na kuwa kizungumkuti kimetokana upande wa DRC.

Serikali ya DRC kupitia kwa msemaji wake, Lambert Mende ilisema kuwa Kinshasa iko tayari kutia saini makubaliano hayo, lakini sio mkataba unaosema ni makubaliano ya amani kwa sababu ni kama kundi hilo bado lipo.

Duru zinasema kuwa Rais Yoweri Museveni pamoja na wanadiplomasia wa nchi za Magharibi, walisburi mkataba kutiwa saini lakini wajumbe wa DRC hawakuingia katika chumba cha hafla hiyo ya kutia saini.

KENYA YAJIRUDISHA KWA TANZANIA KUIMARISHA EAC

Bila shaka hakuna Mtanzania hata mmoja ambaye hakuipongeza hatua ya Serikali ya Kenya kutuma ujumbe wa kuunga mkono msimamo wa Tanzania wa kutojitoakatika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), licha ya nchi za Uganda, Kenya na Rwanda kufanya mikutanokujadili mipango na masuala yanayohusu jumuiya hiyo pasipo kuihusisha Tanzania, kinyume kabisa na Mkataba wa Jumuiya hiyo.

Tanzania ilipinga kwa nguvu zote hatua ya nchi hizo kuitenga hata katika masuala yaliyo chini ya jumuiya hiyo, ambayo kwa mujibu wa mkataba huo yanapaswa kujadiliwa na kutekelezwa kwa pamoja na nchi zote wanachama. Rais Jakaya Kikwete alilazimika kulihutubia Bunge wiki iliyopita na kuelezea kwa kirefu ukiukwaji wa mkataba huo na athari za kuzitenga Burundi na Tanzania katika mikutano inayojadili masuala ya EAC.

Pamoja na kuzikosoa na kuzilaumu vikali nchi hizo tatu kwa kukiuka mkataba huo pamoja na itifaki zakembalimbali, Rais Kikwete aliweka wazi msimamo kwamba Tanzania kamwe haitajitoa katika Jumuiya hiyo na itaendelea kuwa mshirika mwaminifu wa Jumuiya hiyo pasipokutetereka. Msimamo huo bila shaka uliondoa hofu iliyokuwa imetanda miongoni mwa wananchi katika nchi zote wanachama wa EAC, kwamba Tanzania ingejitoa katika Jumuiya hiyo kutokana na kutengwa na nchi hizo tatu zilizokuwa zikiunda kile kilichoitwa 'Coalition of the willing' (Ushirikiano wa wenye hiari).

Hotuba ya Rais Kikwete ilifikisha ujumbe kule kulikotarajiwa.

Ikiwa ni siku nne baada ya Rais kulihutubia Bunge akilalamikia nchihizo kuitenga Tanzania, Kenya imemtuma Waziri wake wa Mamboya Nje, Amina Mohamed kuja hapa nchini kuwasilisha ujumbe wa Rais Uhuru Kenyatta kwamba nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania kwa kutambua umuhimu wake kama moja ya waanzilishi wa Jumuiya hiyo. Waziri huyo alisema kuwa, kuja kwake hapa nchini kunafuatia Serikali ya Kenya kusoma kwa undani hotuba ya Rais Kikwete ambayo alisema, ilikuwa nzuri na ilitolewa kwa nia njema tu ya kuimarisha Jumuiya hiyo na siyo kuidhoofisha.

Sisi tunadhani hatua ya Kenya ya kutafuta maridhiano na Tanzania ni ya kupongeza, hasa tukitilia maanani ukweli kwamba moja ya sababu kubwa zilizosababisha kuvunjika kwa EAC mwaka 1977 ilikuwa ni kutokuwapo utamaduni wa nchi wanachama kujikosoa na kuona umuhimu wa kumaliza tofauti zao kwa njia ya mazungumzo.

Hatua hiyo ya Kenya yafaa iwe mfano kwa nchi nyingine ndani ya Jumuiya hiyo, kwamba zijisahihishe pale zinapojiridhisha kwamba zimekosea hapa au pale.

Hapa hatuna maana kwamba Tanzania haikuchangia lolote katika kufikiwa kwa hali hiyo ya kutengwa.

Kwa mfano, mbali na wafanyabiashara wa ndani na nje yanchi imekuwa ikilalamikiwa na nchi nyingi jirani zinazotumia Bandari yaDar es Salaam. Yamekuwapo malalamiko mengi na ya muda mrefu kuhusu ucheleweshaji wa kupakua na kupakia shehena za mizigo, ukubwa wa tozo za bandari na barabara pamoja na uchakachuaji wa mafuta. Ndiyo maana baadhi ya nchi hizo zimeamua kutumia Bandari ya Mombasa.

Ni matumaini yetu kwamba nchi wanachama wa EAC zitachukulia mvutano uliokuwapo kati yao na Tanzania kama changamoto ya kuzisukuma kushirikiana zaidi ili kujenga Jumuiya yenye nguvu kubwa kiuchumi. Wakati huohuo, hatua hiyo ya Kenya ni ya kijasiri, siyo udhaifu.

MWASISI WA CHADEMA MZEE MTEI ANENA JUU YA YANAYOENDELEA NDANI YA CHADEMA

Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei amesema kuna baadhi ya watu nchini wanakesha usiku na mchana kuhakikisha wanafanya njama za kukidhoofisha na hata kukipoteza kabisa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Mtei,alitoa kauli hiyo wakati chama hicho kikiwa katika wakati mgumu baada ya baadhi ya viongozi wake kushambuliana kupitia mitandao ya kijamii, huku aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba akisimamishwa kwa madai ya kukiuka kanuni za chama hicho.

Mtei alisema kuna baadhi ya watu kutoka Chama Tawala cha CCM wanahakikisha wanatengeneza mifarakano kila kukicha ili kukivuruga Chadema.

Alisema mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa kauli kuwa huenda CCM ikang'oka mwaka 2015, baadhi ya makada na viongozi wameanza kukesha wakifanya mbinu ya kukivuruga ili Chadema kisishike dola.

"Kuna watu wa CCM wanakesha usiku na mchana kuhakikisha wanatuvuruga, ili tusishike dola mimi nasema hawatuwezi" alisema Mtei Hata hivyo, alisema kitendo cha kusimamishwa na hata kufukuzwa baadhi ya makada wa Chadema kimetokana na usaliti ndani ya chama hicho huku wengine wakikubali kutumiwa na CCM.

DK. MVUNGI AFARIKI DUNIA

Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi amefariki dunia leo alasiri nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Dk Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko yaKatiba alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.

WACHINA ZAIDI YA 150 WAKAMATWA GHANA KWA UCHIMBAJI WA DHAHABU KINYUME NA SHERIA

Maafisa wa uhamiaji nchini Ghana wanasema kuwa polisi wamewakamata zaidi ya raia 150 wa uchina ambao wanashukiwa kuhusika na uchimbaji wa dhahabu kinyume na sheria.

Kulingana na Francis Palmdeti kutoka idara ya uhamiaji nchini Ghana, raia hao wanazuiliwa katika migodi minne tofauti nchini humo.

Mamlaka nchini Ghana ilikuwa imewataka raia wote wa kigeni kutohusika katika uchimbaji madini.

Taarifa zinasema kuwa raia wengi wa uchina wamekuwa wakihusishwa na uchimbaji madini wa kiwango cha chini nchini humo baada ya kuingia kinyume cha sheria kupitia mataifa jirani.

Hata hivyo msemaji wa ubalozi wa uchina nchini Ghana anasema kwamba anataraji kuwa raia hao watarudishwa makwao.

Wakati huohuo, wizara ya mambo ya kigeni ya Uchina imelalamikia serikali ya Ghana baada ya wafanyakazi hao wa China kuzuiliwa kufuatia msako uliofanywa wa wachimbaji haramu wa madini.Ghana ndiyo nchi yenye kuzalisha kiwango kikubwa cha Dhahabu baada ya Afrika Kusini barani Afrika.

Huku bei ya dhahabu ikiendelea kupanda katika miaka ya hivi karibuni, sekta hiyo imekuwa ikikumbwa na wachimbaji haramu wa madini hayo ikiwemo, idadi kubwa ya wafanyakazi wa kichina inayoendelea kuongezeka.

China imesema kuwa intaka watu hao kutoteswa na kutoibiwa wakati wa msako huo.

RAIA WA ITALIA ISHIE BURUNDI AKAMATWA NA MAFUVU YA BINADAMU

Polisi nchini Burundi wanasema zaidi ya mafuvu 40 ya binadam yamepatikana katika makao ya raia mmoja wa Italia anayefanya kazi nchini humo.

Giussepe Favaro alikamatwa mwezi uliopita baada ya mafuvu mawili yaliyonuiwa kusafirishwa kwa ndegekunaswa katika uwanja wa ndege nchini Burundi.

Kwa mujibu wa polisi mafuvu hayo yalinuiwa kusafirishwa hadi nchini Thailand.

Polisi hata hivyo hawajatoa taarifa zaidi na mwandishi wa BBC nchini Burundi anasema watu wana shaukuya kutaka kujua mafuvu hayo yalitoka wapi na yalikua yatumike kivipi.

Kumekuwepo ripoti za sehemu za miili ya binadam kutumika katika ushirikina hasa katika nchi jirani ya Tanzania, lakini haifahamiki kwanini mafuvu yaliyopatikana hapo awali yalikua yakipelekwa Thailand.

Bwana Favaro amekua akiishi nchini Burundi kwa miaka kadhaa.

AFARIKI DUNIA BAADA YA PIPI ZINAZOZANIWA KUWA ZA DAWA ZA KULEVYA KUPASUKIA TUMBONI

MNAMO TAREHE 07.11.2013 MAJIRA YA SAA11: 00 HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA.

KASSIM SAIDI MBOYA, MIAKA 36, MKAZI WA DSM ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.

MAREHEMU ALIFAHAMIKA JINA KWA MUJIBU WA HATI YAKE YA KUSAFIRIA NAMBA – AB 051010 KUTOKA DSM KUELEKEA LILONGWE NCHINI MALAWI.

MAREHEMU ALIKUWA ANASAFIRI AKIWA KATIKA BASI LA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJIRI T.319 BLZ AINA YA NISSAN KWA MUJIBU WA TIKETI YAKE ILIYOKUWA NA JINA LA KASSIM MUECK MICHAEL, AKIWA NA BEGI DOGO LENYE SURUALI MOJA AINA YA JEANS, T-SHIRT MOJA NYEUSI, RABA JOZI MOJA RANGI NYEKUNDU, MKATE MMOJA , MKOBA MDOGO WA KIUNONI, VACCINATION CARD MBILI ZA KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RANDI MBILI SARAFU ZA AFRIKA KUSINI NA MIFUKO SITA YA RAMBO RANGI NYEUSI.

AWALI BASI HILO BAADA YA KUFIKA MPAKANI KASUMULU NA ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE GARI HILO NA KUANZA KUFANYA TARATIBU ZA KUVUKA MPAKA KUINGIA NCHINI MALAWI, MAREHEMU ALIBAKI NDANI YAGARI HUKU HALI YAKE YA KIAFYA IKIZIDI KUDHOOFIKA.

WAHUSIKA WA GARI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO MAREHEMU ALICHUKULIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA KWA MATIBABU. HATA HIVYO KABLA HAJAPATA MATIBABU ALIFARIKI DUNIA.

KUFUATIA DALILI ALIZOKUWA NAZO KABLA YA KUFARIKI ILIBIDI MWILI WA MAREHEMU USAFIRISHWE HADI HOSPITALI YARUFAA MBEYA NA KUFANYIWA UPASUAJI AMBAPO ZILIPATIKANA PIPI 65 ZA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA KULEVYA ZIKIWA TUMBONI KWA MAREHEMU NAMOJA KATI YAPIPI HIZO IKIWA IMEPASUKA.

TARATIBU ZINAFANYWA ILI DAWA HIZO ZIPELEKWE OFISI YAMKEMIA MKUU WA SERIKALI KWA UCHUNGUZI WA KITAALAM IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA AINA YA DAWA.

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO.

KAMANDA WA POLISI. MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA KWANI SIO TU NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI BALI PIA NI HATARI KWA AFYA YAMTUMIAJI.

AIDHA ANATOA RAI KWA WAKAZI WA MBEYA NA TANZANIA KWA JUMLA KUFIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA AJILI YA UTAMBUZI WA MWILI WA MAREHEMU.

[DIWANI ATHUMANI- ACP]KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Source: Mbeya Yetu

AZAM NA STEWART HALL WATENGATA TENA KWA MARA YA PILI

Huku ligi kuu soka Tanzania Bara ikiwa imekamilisha mzunguko wake wa kwanza hii leo, timu ya Azam FC ya Dar es Salaam imetangaza kusitisha mkataba na kocha wake mkuu Stewart Hall wa Uingereza kwa kile kilichoelezwa kama makubaliano ya pamoja.

Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa klabu hiyo jijini Dar es Salaam, hii itakuwa ni mara ya pili kwa kocha huyo kuachana na klabu ya Azam na ameafikiana na uongozi wa klabu hiyo baada ya kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ambapo timu ya Azam sasa inashika nafasi ya Pili baada ya kwenda sare ya mabao 3-3 na timu ya Mbeya City ambapo zote sasa zina Pointi 27.

Bingwa mtetezi timu ya Yanga inaongoza ligi hiyo kwa sasa ikiwa na pointi 28 baada ya kuinyuka Oljoro JKT mabao 3-0 katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo, maaruf kama Vodacom Premier League.

Klabu ya Azam FC inayoinukia kwa ubora wa miundo mbinu huku ikiendeshwa kisasa kwa mipango inayoeleweka kinyume na klabu nyingi nchini Tanzania imekuwa ikifanya vema chini ya mwalimu huyo ambapo msimu uliopita aliiwezesha kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kushika nafasi ya Pili katika Ligi kuu msimu uliopita.

Klabu hiyo inao wachezaji kadhaa wa Kulipwa kutoka nchi za Ivory Coast, Kenya na Uganda. Kuachia ngazi kwa kocha huyo kunaelezwa kuwa kumekuwa kwa mkakati ili kusiathiri mwenendo wa timu hususa ni wakati ligi ikiendelea na sasa kutaiwezesha Azam FC Kutafuta kocha mwingine hususan wakati huu ambapo ligi imefikia mapumziko.