WILLIAM RUTO NA JOSHUA ARAP WASOMEWA MASHITAKA ICC

Naibu rais wa Kenya William Ruto pamoja na mshukiwa mwenzake Joshua Arap Sang wamesomewa mashtaka yanayowakabili katika mahakama ya kimataifa ya ICC

12:01 Upande wa mashtaka unasimulia ambavyo unapanga kuthibitisha kuwa kesi yao ni ya uhakika, ushahidi utakaotolewa , na nani atakayetoa ushahidi huo. Mashahidi inasemekana watawataja wahusika wengine kwenye kesi hiyohasa walioshirkiana na washtakiwa kuendesha

11: Upande wa mashtaka kupitia kwa wakili Steynberg umeiambia mahakama kuwa kila mshukiwa anakabiliwa na mashtaka matatu ya kuwalazimisha watu kuondoka makwao kwa lazima, mauaji na kuchochea ghasia

11:51 Bensouda aambia mahakama kuwa amekuwa na wakati mgumu sana kukusanya ushahidi wa kesi yake akisema kuwa wengi wa mashahidi wamejiondoa katika kesi hiyo wakisema wanahofia maisha yao na kuongeza kuwa baadhi pia wamehongwa ili wasitoe ushahidi wao

11:41 Fatou Bensuda mwendesha mkuu wa mashtaka katika mahakama hiyo aelezea mahakama kuhusu tuhuma zinazowakabili Ruto na Sang kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007-2008. Bansuda amesema kuwa Ruto alifanya mauaji kwa sababu za kisiasa huku Sang akimsaidia kuchochea ghasia ili kumsaidia kufanikisha ajenda yake ya kuingia mamlakani

11:35 Joshua Sang pia amekanusha mashtaka yote dhidi yake

11:33 Ruto amekana mashtaka yotealiyosomewa na upande wa mashtaka kuwa alihusika na uhalifu dhidi ya binadamu , mauaji, dhulmana kuwaondosha watu makwao kwa lazimaRuto akiwa na Joshua Arap Sang wakati kesi dhidi yao ilipowasilishwakatika mahakama ya ICC

11:24 Naye Joshua alisomewa mashtaka dhidi yake ya kuchochea ghasia katika mkoa wa Rift Valley kwa kutumia kituo cha redio alichokuwa anafanyia kazi kueneza chuki na ukabila

11:23 Ruto asomewa mashtaka dhidi yake na kuambiwa kuwa alihusika na mauaji ya watu katika mkoa wa Rift Valley

11:20 Kesi dhidi ya mshukiwa mkuuwa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya Naibu Rais William Ruto imeanza kusikilizwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC.

11:00 Wahusika wote kwenye kesi hii kutoka upande wa naibu rais Ruto, mshukiwa mwengine Joshua Arap Sang na upande wa mashtaka wake Fatou Bensauda walijitambulisha mahakamani kwa ombi la mmoja wa majaji kwenye jopo la majaji.