waliosajiliwa kupiga kura,
hii leo wanawachagua
wabunge katika mfumo wa
vyama vingi vya kisiasa.
Rwanda inasifika sana kwa
kuwa na wanamama wengi
kwenye nyadhifa za uongozi
wa kitaifa.
Uchaguzi huu usio na
upinzani mkubwa ni kama
kupiga muhuri tu uongozi
wa chama cha RPF chake
Rais Paul Kagame ambacho
kimekuwa uongozini tangu
kumalizika kwa mauaji ya
Kimbari mwaka 1994.
Kiongozi wa Chama rasmi
cha upinzani FDU, Victoire
Ingabire yuko jela na
wafuasi wake wanasema
kuwa serikali imefanya
mazingira kuwa magumu
sana kwao hata kusajiliwa
rasmi kama chama cha
kisiasa.
Kwa sababu ya mfumo wa
kuhakikisha kuwa wanawake
wanawakilishwa vyema
katika nyadhifa za kisiasa,
Rwanda ndiyo nchi pekee
duniani yenye wanawake
wengi bungeni.
Inasemekana kuwa wapiga
kura wengi huenda
wakajitokeza licha ya kuwa
kampeini za uchaguzi
hazikufanywa kwa kishindo
pamoja na kukosekana kwa
upinzani mkubwa kwa
chama cha RPF.
Shughuli ya kupiga kura
ilionekana kuwa tulivu ,
foleni zikiwa zimepangwa
vyema huku vipaza sauti
vikisikika kuwaambia
wananchi kutosahahu kadi
zao za kujitambulisha
wakati wakienda kupiga
kura.
Mwishoni mwa wiki, tukio
pekee la kutishia usalama
lililoripotiwa ni shambulizi
la maguruneti, katika soko
moja mjini Kigali , mji
ambao unasifika kwa
usalama wake barani
Afrikia.
Tangu kutokea kwa
shambulizi hilo, hakuna
mtu yeyote aliyekiri
kuhusika nalo, lakini serikali
ililaumu waasi wenye
uhusiano na kundi la waasi
la (FDLR), ambao huendesha
harakati zao maeneo ya
mpakani na Jamuhuri ya
kidemokrasia ya Congo
Kundi hilo linajumuisha
waasi wa zamani wa kihutu
wanaolaumiwa kwa mauaji
ya Kimbari ya mwaka 1994
ingawa waliondoshwa na
waliokuwa wanachama wa
waliokuwa wanajeshi waasi
wa RPF.