15 WADAKWA BAADA YA KUSHUKIWA KUHUSIKA NA MATUKIO YA TINDIKALI

Mkuu wa polisi nchini
humo, Mussa Ali Mussa,
alidai kuwa baadhi ya
washukiwa wana uhusiano
na kundi la wapiganaji wa Al
Shabaab nchini Somalia.

Wiki jana kasisi wa kanisa
katoliki alishambuliwa kwa
kumwagiwa tindi kali katika
mji wa kale.


Shambulizi hilo linakuja
baada ya wasichana wawili
wa uingereza kushambuliwa
mwezi jana.

Kirstie Trup na Katie Gee,
wote wenye umri wa miaka
18, walimwagiwa tindi kali
wakiwa wanatembea mjini
humo.

Maafisa nchini Zanzibari,
wametangaza kumzawadi
mtu atayetoa taarifa kuhusu
shambulizi hilo.

Katika shambulizi
lililofanyika siku ya Ijumaa,
kasisi Joseph Anselmo
Mwangamba alimwagiwa
tindi kali alipokuwa
anaondoka kwenye duka la
huduma za internet katika
mji wa kale.


Shambulizi hilo ni la tano la
aina yake visiwani humo
tangu Novemba mwaka jana.

Bwana Mussa alisema kuwa
polisi walinasa mitungi
iliyokuwa na lita 29 za Tindikali wakati wa msako wao.


Kwa mujibu wa polisi,
washukiwa walikamatwa
wakiwa katika harakati za
kujiandaa kwa mapigano
kwengineko nje ya Tanzania.

Hadi sasa polisi
wanakamilisha uchunguzi
wao kabla ya kuwafungulia
mashtaka washukiwa watatu
waliowashambulia
wasichana wawili raia wa
Uingereza.

Hata hivyo haijulikani ikiwa
washukiwa hao 15
waliokamatwa
wamehusishwa na
shambulizi walilofanyiwa
wasichana hao wawili au
ikiwa ni wao
waliomshambulia kasisi
Mwangamba.

Visiwa vya Zanzibar hupokea
watalii wengi na wenyeji
wansema kuwa
mashambulizi dhidi ya raia
wa kigeni sio jambo la
kawaida.