POLISI ZANZIBAR WACHARUKA

SIKU mbili baada ya Padri
wa Kanisa Katoliki Parokia
ya Cheju, Mkoa wa Kusini
Unguja, Zanzibar, Joseph
Mwang'amba kumwagiwa
tindikali na watu
wasiofahamika, Jeshi la
Polisi li metoa tamko la
kuwasaka wahusika usiku
na mchana.


Padri Mwang'amba
ambaye amelazwa katika
Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Dar es
Salaam, akipatiwa
matibabu, alipatwa na
tukio hilo mwishoni mwa
wiki wakati akitoka
kwenye duka linalotoa hu
duma ya mawasiliano ya
mtandao(intaneti), lililopo
eneo la Mlandege,wilayani
Ung uja.


Taarifa iliyotolewa Dar
es Salaam jana na
Msemaji wa Jeshi la Polisi
nchini, Advera Senso, alisema kutokana na
ongezeko la vitendo hivyo,
jeshi hilo, Mkemia Mkuu
wa Serikali na kikosi
Maalumu cha kuzuia
uchochezi na ugaidi,
wamejipanga kufanya
operesheni maalumu.

Operesheni hiyo ni ile ya
kuwafuatilia watu wote
wanaoingiza , kusambaza
na kuuza vimiminika vya
tindikali kama
wanazingatia sheria
zilizowekwa dhidi ya
vimiminika hivyo.

"Yeyote ambaye
itabainika kwenda
kinyume hatua za kisheria
zitachukuliwa dhidi yake
na k ufikishwa
mahakamani, tutaendelea
kuwasaka watu
wanaofanya vitendo hivi,
tunaomba wananchi
wenye taarifa nao, wazitoe
na zitakuwa siri,"alisema.

Juzi Padri Mwa ng 'amba
alitembelewa hospitali na
Rais wa Zanzibar, Dkt.Ali
Mohamed Shein na
kumwe leza kuwa, miezi
mitatu iliyopita alitishiwa
kuuawa. Katika tukio
lililomkuta mwishoni m
wa wiki, Padri
Mwang'amba alijeruhiwa
usoni, mikononi na
kifuani.