WABUNGE WA KENYA WAKUBALI KENYA KUJITOA ICC

Baada ya mjadala mkali Jana bunge la kenya lilipitisha mswaada wa kuitaka kenya kujiondoa katika mkataba wa Roma unaounda mahakama ya kimataiafa ya uhalifu wa jinai- ICC.
Hatua hii inakuja wakati Naibu rais William Ruto akijiandaa kuelekea Katika makao makuu ya mahakama hiyo mjini Heague Uholanzi kukabiliana na kesi ya uhalifu dhidi ya binadamuBaadhi ya wabunge wa upinzani nchini Kenya waliondoka kwa hasira bungeni wakati mjadala huo ulipokuwa unaendelea.
Wabunge hao waliondoka baada ya kusema kuwa kamwe hawataunganana upande wa serikali kuunga mkono hoja hii ya kujiondoa kutoka katika mahakama ya ICC.

Ni kutokana na kuwa kwamba upinzani una idadi ndogo zaidi ya wabunge bungeni.Wengi waliounga mkono hoja hiyo walikuwa wabunge wa muungano tawala wa Jubilee unaoongozwa na vigogo Rais Uhuru Kenyata na naibuwake William Ruto.
Naibu kiranja wa wabunge wa upinzani bungeni Jakoyo Midiwo, alisema kuwa wabunge wa upande wa serikali wanaotetea hoja hii ya kujiondoa Hague watakuja kujuta.
Mjadala huu unatokana na hatua ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kukabiliwa na kesi za uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama hiyo wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007-2008 Hatua hii ya wabunge pia inakuja ikiwa imesalia chini ya wiki moja kabla ya kuanza kwa kesi dhidi ya naibu Rais wa Kenya Williiam Ruto kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2008.
Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Rais Uhuru Kenyatta pia anatarajiwakufika katika mahakama hiyo mweziNovemba kwa kesi dhidi yake.Wawili hao wanashtakiwa kwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka 2007.
Msemaji wa ICC ameambia BBC kuwa kesi hiyo itaendelea hata ikiwa Kenya itajiondoa kwenye mkataba wa Roma uliopelekea kuanzishwa kwa mahakama hiyo.
Bwana Fadi El Abdallah, alisema kuwa itachukua karibu mwaka mmoja kwa mchakato wa nchi yoyote ile kujiondoa kutoka katika mahakama ya ICC na hii bila shaka inaathiri tu kesi zilizokuwa mbele ya mahakama hiyo kwa wakati huo.
Hii ni hatua ya dharura inayochukuaserikali kujitoa katika Mkataba wa Roma wa mahakama hiyo ulioidhinishwa na Umoja wa mataifamnamo tarehe 17 July, mwaka1998.Kenya inataka kutoa mfano wa kuwanchi ya kwanza Afrika kuchukua hatua hiyo licha ya kwamba uamuzi huu hautoathiri kwa namna yoyote kesi zinazoendelea sasa katika mahakama ya ICC.
Mahakama hiyo ya kimataifa imesema kwamba kesi hizo zitaendelea hata iwapo Kenya itajitoa.Imesema itaichukua Kenya kiasi ya mwaka mmoja kabla ya kukubaliwa ombi hilo la kutaka kujiondoa katikamkataba wa Roma na hilo litaathiri tu kesi zitakazozuka baada ya muda huo.

Haya yanajiri wakati makamu wa rais William Ruto anatarajiwa kuondoka Kenya kueleka Hague Uholanzi wiki ijayo kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadaamu katika mahakama hiyo ya ICC, kesi inayoanza tarehe 10 mwezi huu.
Wote wameshtakiwa kwa kuhusika katika ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Kesidhidi ya rais Uhuru Kenyatta inatarajiwa kuanza tarehe 12 mweziNovemba.