MAELFU WAJITOKEZA MKUTANO WA CDM, CUF NA NCCR

Maelfu wakazi wa jiji la
Dar es salaam wengi wao
wakiwa ni wafuasi wa
vyama vya Chadema ,Cuf
na NCCR Mageuzi
wemefurika katika
viwanja vya jangwani
kuwasilikza viongozi
wakuu wa vyama hivyo
ambapo kwa pamoja
viongozi hao wanapinga
hatua ya serikali kuingiza
baadhi ya vipengele katika
mswada wa sheria ya
marekebisho ya sheria
ya mabadiliko ya katiba.


Viongozi hao wanadai
kuwa vipengele hivyo
vitapelekea kupatikana kwa
katiba ya upande mmoja
na kuongeza kuwa kama
mswada huo hautafanyiwa
marekebisho, basi wao
hawatashiriki katika bunge
la katiba.


Katika viwanja hivyo ulinzi
uliimarishwa kutoka katika
vikundi mbalimbali
vinavyomilikiwa na vyama
hivyo huku shamra
shamra za huko na kule
zikiwa hazikosekani ili
mradi kunogesha mkutano.


Mwenyekiti wa taifa wa
Chadema na ambaye ni
kiongozi wa kambi ya
upinzani bungeni Mh
Freeman Mbowe
amewataka watanzania
kuacha uoga na wasimame
imara kudai katiba bora.


Naye mwenyekiti wa Cuf
Mh Profesa Ibrahim
Lipumba amesema
Tanzani inahitaji katiba
ambayo italinda na
kusimamia rasilimali za
taifa kuweza kutimia kwa
usawa na kuzingatia
mahitaji ya watanzania
wenyewe.


Kwa upande wake
mwenyekiti wa NCCR
Mageuzi na mbuge wa
kuteuliwa amesema
hakuna haja ya kutumia
mabavu na badala yake
ameitaka serikali itumie
busara zaidi ili kuweza
kufikia mwafaka wa jambo
hili.


-ITV