ARSENAL, GARETH BALE WAVUNJA REKODI USAJILI ULAYA

Kunako siku ya mwisho kwa
vilabu vya mpira wa miguu
kukamilisha usajili wa
wachezaji klabu ya Arsenal
imeafikiana na mchezaji
Mesut Ozil wa Ujerumani
anayechezea klabu ya Real
Madrid kwa kitita cha pauni
za Uingereza milioni £42.4.

Kwa mujibu wa taarifa
zilizopatikana, klabu ya
Arsenal imekubaliana na
Real Madrid kuilipa pauni za
Uingereza milioni £42.4m
sawa na Euro milioni 50
kumsajili Mjerumani Mesut
Ozil.

Kijana huyo menye umri wa
miaka 24 amefikia
makubaliano na Arsenal
kuhusu maslahi yake binafsi
ingawa sharti apitie
mchakato wa vipimo vya
afya yake kabla ya Arsenal
kukamilisha usajili ambao
katika historia ya klabu hio
haujawahi kufanyika
kumsajili mchezaji kwa zaidi
ya pauni milioni 22.

Kwa wakati huu Ozil yuko
pamoja na kikosi cha Timu
ya Taifa ya Ujerumani na
itabidi afanyiwe vipimo
huko huko Ujerumani.

Kwa kipindi cha msimu wa
likizo na usajili wa
wachezaji Arsenal
imeshindwa kuwasajili
wachezaji wa kiwango
anachokitaka Arsene Wenger
kama mshambuliaji wa
Liverpool Luis Suarez na
Gonzalo Higuain, mchezaji
mwingine aliyekua huko
Real Madrid.
Lakini kwa sasa yumkini Ozil
anaelekea uwanja wa
Emirates kufuatia usajili wa
Gareth Bale kwa kitita
kikubwa cha pauni milioni
85.3.
Kabla ya kujiunga na Real
Ozil alikua akichezea klabu
ya Werder Bremen
alikosajiliwa na Real kwa
takriban pauni milioni 12.4
na kuichezea Real mara 155.

Wakati Arsenal ikijitahidi
kusajili kabla ya dakika ya
mwisho ya shughuli ya
usajili Liverpool pia
imetiliana saini na
Mamadou Sakho na Tiago
Ilori kwa jumla ya pauni
milioni 25.

Sakho mwenye umri wa
miaka 23 ameichezea Timu
ya Taifa ya Ufaransa mara
14 France na amegharimu
pauni milioni £18m kutoka
klabu ya Paris St-Germain.

Ilori alizaliwa mjini London
na ameiwakilisha Timu ya
Ureno ya vijana ingawa
bado anaweza kuiwakilisha
England.

Liverpool haikuishia hapo
ila imemzoa Mnaijeria
Victor Moses kutoka
Chelsea.

Mshambuliaji huyo alifunga
mabao 10 akishiriki mechi
42 za Cheslea lakini
amekabiliwa na ushindani
mkali wa kuweza kuingia
uwanjani kufuatia usajili wa
mcheza kiungo kutoka Brazil
Willian, Mjerumani Schurrle
pamoja na mkongwe wa
Cameroon Samuel Eto'o.

Real Madrid imevunja
rekodi ya dunia ya
uhamisho wa wachezaji kwa
kumsajili mshambuliaji wa
Tottenham Gareth Bale.

Mchezaji huyo wa kimataifa
wa Wales ametia saini
mkataba wa kuichezea Real
Madrid wa miaka 6 kwa
kununuliwa kitita cha pouni
milioni 85,3.

Rekodi iliyokuwepo ilikuwa
ya Cristiano Ronaldo
aliponunuliwa na Real
Madrid toka Manchester
United kwa pouni milioni 80
mwaka 2009.

"nilikuwa na furaha ya
miaka 6 niliyochezea
Spurs,lakini huu ni wakati
mwafaka kwangu kusema
kwa heri "alisema Bale
mwenye umri wa miaka 24.

Bale aliyeshinda tuzo ya
mchezaji bora wa msimu
uliopita katika ligi kuu ya
England alijiunga na
Tottenham kutoka
Southampton kwa pouni
milioni 10 mwaka 2007 na
alifunga magoli 26 msimu
uliopita.