"NYIE WATU WABAYA" KAULI ALIYOTOA MTOTO ELLIOT PRIOR KWA MAGAIDI WA AL SHABAAB

Mtoto wa miaka minne ambaye ni raia wa Uingereza, Elliott Prior ameonyesha ushujaa wa hali ya juu baada ya kuweza kuwatolea maneno makali na ya kugusa magaidi waliovamia jengo la maduka la Westgate.

Baada ya maneno hayo, baadhi ya taarifa zilizochapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya kimataifa, vinasema magaidi hao waliomba mtoto huyo awasamehe kwa maelezo kuwa wao siyo watu wabaya.

Inaelezwa kuwa, kitendo cha mtotohuyo kilikuwa cha kishujaa kwani aliweza kuwaeleza magaidi hao maneno hayo, bila kuogopa silaha nzito walizokuwa wameshika mkononi huku baadhi ya watu wakiwa wameshauuawa.

Mtandao wa Daily Mail unasema mtoto huyo alimwambia mmoja wamagaini hao kuwa 'Nyie ni watu wabaya sana'.

Mtandao huo unasema mtoto huyo aliyasema maneno hayo kama njia ya kumkinga mama yake Amber, aliyekuwa amepigwa risasi mguuni pamoja na dada yake Amelie, mwenye umri wa miaka sita ambaye walikuwa wote ndani ya duka hilo.

Katika kile kilichotafsiriwa kuwa ni kuumizwa na maneno hayo, magaidi hao walimpa Elliott pamojana dada yake mifuko miwili miwili ya chokleti na kuwaomba msamaha. Taarifa hizo zinasema kuwa, gaidi huyo alisema "Samahani nisamehe,sisi siyo watu wabaya".

Mama huyo anasema kuwa, kabla ya kukamatwa na magaidi hao, yeye na watoto wake walikuwa wamejificha kwenye jokofu la kuhifadhi nyama lililopo ndani ya duka la Nakumatt kwa zaidi ya saa moja na nusu.

Anasema kuwa, baada ya kukamatwa na magaidi hayo, walimpiga risasi ya paja.

Mjomba wa watoto hao aliliambia gazeti la The Sun la Uingereza kuwa"Walikuwa na bahati kuweza kutokakwenye mikono ya hao magaidi. Hao magaidi walisema kuwa, kama kuna mtoto yeyote aliye hai ndani ya jengo hilo wanaweza kuondoka.

'Mama yao alisimama na kusema 'ndio' , binamu yangu aliweza kupata ujasiri wa kusimama na kuwaambia kuwa, nyie ni watu wabaya sana'.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, baada ya magaidi hao kujua kuwa mama huyo na watoto wake hawakuwa kati ya watu waliowalenga, hawakuwaua.