MSHUKIWA WA MAUWAJI YA KIMBARI AACHIWA HURU

Mahakama moja nchini
Ufaransa imeamuru
kuachiliwa kwa aliyekuwa
Kanali wa jeshi la Rwanda ,
anayesakwa na taifa hilo
kwa kuhusika katika mauaji
ya kimbari ya mwaka 1994
nchini humo.
Rwanda iliwasilisha ombi la
kutaka Kanali huyo Laurent
Serubuga, wa kabila la
Hutu, na ambaye alihudumu
kama naibu mkuu wa
majeshi kurejeshwa nchini
humo.

Kanali Serubuga mwenye
umri wa miaka 77,
alikamatwa mwezi Julai
Kaskazini mwa Ufaransa
baada ya Rwanda kutoa
kibali cha kumkamata.

Takriban watu 800,000
wengi wao wakiwa wa kabila
la Tutsi, waliuawa na
wahutu ambao ni wengi kwa
idadi nchini Rwanda mnamo
mwaka 1994.

Mwanawe Serubuga alikuwa
mahakamani kushuhudia
kesi hiyo. Wakati jaji akitoa
uamuzi wake, alisema kuwa
wameridhishwa na uamuzi
wa kumwachilia huru
babake.

"tulirajaria kesi ya kisiasa.
Uongo wa Rwanda
haujasikika mbele ya
mahakama hii," alinukuliwa
akisema na shirika la habari
la AFP.

Mahakama iligundua kuwa
wakati wa mauaji ya
kimbari, uhalifu wa mauaji
ya halaiki na uhalifu dhidi
ya binadamu haungeweza
kuadhibiwa chini ya sheria
ya Rwanda, kwa hivyo,
bwana Serubuga hangeweza
kuchukuliwa hatua zozote
kwa makosa ambayo
hayakuwa na adhabu.

Sheria za Ufaransa,
haziruhusu mshukiwa au
mhalifu kurejeshwa kwao
hasa ambapo mshukiwa ana
wasiwasi ikiwa haki zake
zinaweza kulindwa, alisema
wakili wa Bwana Serubuga.

Wakili aliyekuwa anatetea
maslahi ya Rwanda alisema
kuwa hakushangazwa na
uamuzi huo kwani Ufaransa
mara kwa mara imekataa
kuwarejesha washukiwa wa
mauaji hayo nchini Rwanda
ili wakabiliwe na sheria.