AFUNULIWA USO KWA KUNG'ATWA NA BOSI WAKE

KATIKA hali isiyokuwa ya
kawaida mkazi wa Kijiji
cha Nyabibuye Kakongo
katika Wilaya ya Kibondo
mkoani Kigoma, Susuluka
(16) anadaiwa kujeruhiwa
vibaya usoni na bosi
wake, Imani Paulo (36)
kwa kung'atwa ng'atwa
usoni na kisha
kunyofolewa macho, pua
na meno kubaki nje, kama
ambavyo anaonekana
pichani.

Tukio hilo ambalo
tunaweza kulifananisha
na dunia kuelekea kufika
mwisho, limegusa hisia za
watu wengi hasa wakazi
wa Kibondo, huku
wengine wakitokwa na
machozi kutokana na
kuguswa na ukatili ambao
amefanyiwa kijana
huyo.

Tunaweza kufikiria
kuwa tukio hilo ni sinema,
lakini Mkuu wa Wilaya ya
Kibondo, Venance
Mwamotto, ameliambia
Majira kuwa tukio hilo
limetokea miezi miwili
iliyopita.

Akizungumza na Majira
katika mahojiano
maalumu, Mwamotto,
alisema kuwa kabla ya
kijana huyo kujeruhiwa
na bosi wake, alimtuma
dukani ili akamnunulie
soda. Aliliambia Majira
kuwa baada ya kufika
nyumbani alimkuta bosi
wake akiwa amemkaba
koo mbwa na kutokana na
maumivu aliyokuwa
akiyapata mbwa huyo,
alianza kuhema akitoa
ulimi nje.

DC Mwamotto alisema
kuwa mtuhumiwa huyo
ghafla alianza kuung'ata
ulimi wa mbwa na kisha
kumeza vipande jambo
lililosababisha mbwa huyo
kupiga kelele kutokana na
maumivu. Aliongeza kuwa
aliendelea kula vipande
vya ulimi huo wa mbwa
hadi alipoumaliza.

"Unaweza kusema kuwa
ni uongo, lakini ni tukio la
kweli kabisa kwani
mshtakiwa huyo
aliendelea kula ulimi wote
wa mbwa, huku kijana
huyo akiendelea
kumshangaa bosi wake
kutokana na kitendo hicho
kilichosababisha mbwa
huyo kufa,"Wakati
akiendelea kumshangaa
bosi wake ghafla
alimrukia na kumkamata
kwa nguvu na kuanza
kumng'ata kama mtu
anayetafuna hindi la
kuchoma.

"Mshtakiwa huyo alianza
kumtafuna jicho moja na
kufuatia jicho la pili na
kisha kumeza vipande vya
macho huku akiendelea
kumshika kwa nguvu,"
alisema DC Mwamotto
wakati wa mahojiano na
Majira.
Baada ya kumaliza
kitendo hicho alisema
kuwa mshtakiwa huyo
alianza kumng'ata pua na
kisha kumeza na vipande.

Alisema kuwa wakati
anaendelea na kitendo
hicho majeruhi huyo
alikuwa akipiga kelele za
kuomba msaada, lakini
mshtakiwa huyo alianza
kumng'ata tena kipande
cha mdomo wa chini na
kisha kusababisha meno
kubaki nje.

"Kutokana na
kelele hizo wananchi
waliamua kusogea karibu,
lakini walikuta tayari,
Susuluka amejeruhiwa
vibaya usoni huku damu
zikimtoka kwa wingi,"
alisema.

Mwamotto alisema kuwa
kutokana na hali hiyo
wananchi walimvamia na
kumpiga na kumpeleka
katika Kituo cha Polisi cha
Kibondo na majeruhi
walimkimbiza katika
Hospitali ya Wilaya ya
Kibondo.

Majira iliendelea na
mahojiano hayo ambapo,
mshtakiwa huyo
alifikishwa katika
Mahakama ya Wilaya na
kufunguliwa mashtaka ya
kudhulu mwili."Hivi sasa
mshtakiwa yupo katika
Gereza la Nyamisivi
Kibondo, lakini cha
kusikitisha tena akiwa
huko alimng'ata na kula
vipande vya nyama vya
mguu mshtakiwa
mwenzake," alisema.

Alisema kuwa mshtakiwa
mwenzake alimjeruhi
vibaya na kupelekwa
hospitalini hali
iliyosababisha mshtakiwa
huyo kutengwa na
washtakiwa
wenzake.

"Mimi
nimelazimika kwenda hadi
gerezani na kufanya
mahojiano na mshtakiwa
huyu, kwani hili tukio
linasikitisha sana lakini
cha ajabu alitaka
kufahamu je ameshtakiwa
kwa makosa gani ya kuua
mbwa au kumng'ata mtu,"
alisema.

Alisema kuwa pia
amelazimika kwenda
kumjulia hali majeruhi
huyo ambapo madaktari
katika hospitali hiyo
walishindwa
kumtibia.

"Nimeomba
msaada kutoka Wizara ya
Afya ili mgonjwa huyu
akatibiwe India na tayari
maandalizi yameanza
kufanyika kwa
kushirikiana na Hospitali
ya Kibondo," alisema.
Mwamotto alisema kuwa
mgonjwa huyo hana pua,
macho yamefumba,
mdomo kwa kujeruhiwa
vibaya usoni hali ambayo
anahitaji matibabu
zaidi.

Amewaomba
Watanzania kumsaidia
kijana huyo ili aweze
kwenda kutibiwa haraka
nje pamoja na kupata
msaada mbalimbali kwa
kuwasiliana na mganga
mkuu wa hospitali ya
Kibondo ama kuwasiliana
na Mhariri mtendaji wa
gazeti hili la Majira.
Source: Majira