MAUWAJI KATIKA KAMBI YA JESHI WASHINGTON DC

Mtu aliyewaua watu 12
katika kambi ya kijeshi
nchini Marekani na kisha
mwenyewe kuuawa, katika
makabiliano na polisi,
ametajwa kuwa mwanajeshi
wa zamaji wa jeshi la
wanamaji.

Aaron Alexis, 34, kutoka Fort
Worth, Texas, aliuawa na
polisi baada ya kuvamia
kambi hiyo na kuwaua watu
kiholela , mjini Washington
DC.

Watu wengine wanane
walijeruhiwa kwenye
uvamizi huo ulioanza
mapema asubuhi mnamo
Jumatatu.


Rais Barack Obama
aliamuru bendera
kupeperushwa nusu
mlingoti katika Ikilu ya
White House na Capitol Hill.

Alisema anaomboleza kwa
sababu ya mauaji mengine
ya halaiki na kulaani
kitendo hicho cha uoga.

Haijulikani kwa nini Aaron
Alexis aliamua kufanya
shambulizi hilo na kuwaua
watu kati ya umri wa miaka
46-73.

Awali polisi walichukua
hatua baada ya ripoti za
watu wengine kujihami
wakishirikiana na Alexis,
lakini baada ya msako mkali
wakasema kuwa hakuna
dalili kwamba Alexis alikuwa
na wenzake..

Valerie Parlave wa shirika la
ujasusi la FBI alisema kuwa
Alexis, aliyekuwa ameajiriwa
na mwanakandarasi
aliyekuwa anafanya kazi
kwenye mtandao wa
internet wa FBI, alikuwa na
pasi ya kuingia kwenye eneo
hilo.