PADRI AMWAGIWA TINDIKALI HUKO ZANZIBAR

Polisi huko visiwani
Zanzibar wanachunguza
tukio la kasisi wa kanisa
katoliki kushambuliwa kwa
tindikali.

Imeelezwa kuwa Kasisi huyo
Anselmo Mwang'amba,
alimwagiwa tindikali akitoka
mgahawa mmoja wa
kutumia mtandao mjini
Zanzibar. Tukio hilo
linatokea ndani ya mwezi
mmoja tangu wasichana
wawili wa kiingereza
kushambuliwa.

Hili ni janga jingine kwa
Zanzibar ambayo imekuwa
ikizongwa na matukio ya
aina hii kwa muda sasa.

Mkurugenzi wa upelelezi wa
Zanzibar, Yusufu Ilembo
ameieleza kuwa bado
hawajakamata mtu yoyote
kuhusika na tukio hilo
ingawa amethibitisha kuwa
uchunguzi tayari umeanza.

Ameeleza kuwa Kasisi
Mwang'amba aliungua
usoni na mabegani na
kwamba anaendelea
kutibiwa.

Katika miaka ya karibuni
Zanzibar imekabiliwa na
mikasa ya watu
kushambuliwa hivi na kuzua
hisia kuwa chuki za kidini.

Mapema mwaka huu kasisi
mwingine wa kanisa katoliki
alishambuliwa kwa risasi na
kuuawa.

Mwezi uliopita Zanzibar
ilitikisika kutokana na
wasichana wawili wangereza
kushambuliwa kwa tindikali
na watu wasiojulikana.

Kiongozi mmoja wa dini ya
kiislamu pia alimwagiwa
tindikali na watu
wasiojulikana.