Watu waliouawa ni baba wa familia, Jonas Lulinga (44) aliyechinjwa, mkewake Lucia Jonas (35) aliyeuawa kwakunyongwa kama ilivyokuwa kwa mtoto wao mwenye umri wa mwaka mmoja, Eliud.Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) katika Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Joseph Konyo aliyesema wanamsaka fundi ujenzi anayetuhumiwa kusababisha vifo hivyo. "Kwa sasa Polisi inaendelea na upelelezi wa kina juu ya tukio hilo na hatuwezi kumtaja jina fundi ujenzi huyo, ili kuepuka kutoroka natunawaomba wananchi wawe makinina watu ambao hawawafahamu vyema," alisema Konyo.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Ihila, Joseph Kabadi akizungumza jana eneo la tukio, alisema vifo hivyo vilitokea usiku wakati wanafamilia wakiwa wamelala.
Baadhi ya majirani walimhusisha fundi na mauaji ikielezwa huenda aliiba fedha za marehemu aliyekuwa ameuza kiwanja kingine na kuanza ujenzi wa nyumba ambayo fundi huyo alipewa jukumula kuijenga, huku tayari akiwa ameshakamilisha ujenzi wa msingi.