JKT YAWATOA HOFU WANAOJIUNGA NA VYUO

JESHI la Kujenga Taifa (JKT), limewatoa hofu vijana waliotakiwa kujiunga na jeshi hilo kwa awamu yatatu, huku wakiwa tayari wamedahiliwa na kulipa ada vyuoni kwamba watachagua moja.

Vijana hao waliochaguliwa kujiunga JKT awamu ya tatu wanatakiwa kuripoti makambini Jumamosi Oktoba 28, jambo lililozua hali ya sintofahamu kwa wazazi wao ambaowalikwisha kuwalipia ada vyuoni.


Kwa mujibu wa JKT utaratibu utakuwa kwamba vijana wanaotaka kuendelea na masomo ya elimu ya juu kwa wakati huu lakini wamo kwenye orodha ya kujiunga na jeshihilo, watalazimika kuandika barua makao makuu kuomba kuahirisha mkataba wa mafunzo.

"Masharti waliyowekewa kwa ajili yakuomba kuahirisha kujiunga na JKT kwa sasa ni kuandika barua binafsi ya kuomba kuahirisha mkataba na barua iwe na picha ya mhusika anayeomba," ilisema taarifa hiyo.

Pia mhusika atatakiwa awe na nakala ya barua ya kuchaguliwa kujiunga na chuo, aeleze katika barua yake kuwa atajiunga na JKT baada ya kuhitimu masomo na kisha barua hiyo ifike makao makuukabla ya Oktoba 2, mwaka huu.

Taarifa hiyo ilisema kuwa suala la vijana wanaomaliza kidato cha sita kujiunga na JKT ni la lazima na kwamba ni wajibu wa kila mhitimu kuhudhuria mafunzo hayo.