TFF YAMFUNGIA REFEREE KWA KUBORONGA MECHI.

Kamati ya ligi ya Shirikisho la soka Tanzania-(TFF)imemfungia mwamuzi Martin Saanya kuchezesha mechi katika kipindi cha mwaka mmoja kwa madai ya kushindwa kuumudu mchezo wa ligi kuu ya vodacom baina ya yangadhidi ya coastal union ya Tanga uliochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ambapo timu hizo zilitoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bao 1-1.

Mwamuzi huyo amekumbana na adhabu hiyo kufuatia kikao cha kamati ya ligi kilichoketi mwishoni na wiki iliyopita kwa ajili ya kupitia ripoti mbalimbali za makamishna wa mechi ambapo mwamuzi huyo alizua kizazaa baada ya kuipa coastal union penati ya dakika za lala salama ambapo tukio hilo lilionekana kuwakera mashabiki wayanga ambao walivunja vioo vya basi la coastal union baada ya mchezo kumalizika.

Mbali na adhabu hiyo, kamati ya ligi pia imemfungia miezi mitatu na faini la shilingi moja kocha wa makipa wa coastal union Juma Pondamali Mensah kwa madai ya kuwatukana mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa simba huku yanga ikipigwa faini ya shilingi milioni moja baada ya mashabiki wake kumrushia chupa za plastiki mwamuzi Martin Saanyawakati Coastakl Union ikitakiwa kulipa faini ya shilingi laki moja kwa kosa la kuchelewa kwenye kikao cha maandalizi ya mechi.