WABUNGE WAZICHAPA KAVUKAVU BUNGENI

Wabunge wa bunge la
waakilishi Nigeria
wamerushiana ngumi wakati
wa vikao vya Jumanne
baada ya kuzuka bungeni
suitofahamu kuhusu
mrengo wa wabunge
waliojitenga na chama
tawala. Taarifa hizi ni kwa
mujibu wa vyombo vya
habari nchini humo.

Kituo kimoja cha kibinafsi
cha televisheni, pamoja na
vituo vingine vilionyesha
picha za mbunge
mwanamke akimtosa kidole
usoni kwa ghadhabu
mbunge mwenzake wakati
mbunge mwanamume
akionekana akichukua kiti
nusura kumgonga
mwenzake.
Wabunge wengine
walionekana wakipigana
ngumi.


Mgogoro inasemekana
ulianza baada ya
mwenyekiti wa mrengo wa
wabunge waliojiondoa
kutoka kwa chama tawala,
Kawu Baraje, kuingia
bungeni akiandamana na
magavana wanaomuunga
mkono.

Inaarifiwa spika wa bunge la
waakilishi ,Aminu
Tambuwal, aliambia
wabunge kuwa Baraje
aliomba ruhusa
kuwahutubia wabunge wa
mrengo wake kabla ya
bunge kuanza vikao vyake.


Lakini kuwepo kwa wabunge
hao bungeni kuliwaghabisha
mno wafuasi wa chama
tawala, PDP,kiasi cha kuzuka
sokomoko bungeni kati ya
pande hizo mbili na
kumlazimisha bwana Baraje
kukatiza hotuba yake
kutokana na kelele bungeni.


Chama tawala PDP kina
wabunge wengi zaidi
bungeni wakiwa 23 kati ya
wabunge wote 36
Aidha chama hicho
kimetawala Nigeria tangu
kupata uhuru mwaka 1999
lakini hivi kribuni
kimezongwa na migogoro ya
ndani ya chama pamoja na
kukabiliwa na upizani wenye
ushawishi.

Wananchi wanajiandaa kwa
uchaguzi mwaka 2015, lakini
wadadisi wana wasiwai ikiwa
chama tawala kitakuwa
kimesuluhisha migogoro
yake, huku kikikabiliwa na
upinzani mkali.


Mgogoro huu umekuwa
ukitokota kwa miezi kadhaa
huku baadhi ya wabunge
wakitofautiana kuhusu ikiwa
Rais Goodluck Jonathan
aidhinishwe na chama
kugombea urais kwa mara
nyingine wakati kuna
wanasiasa wengine
wanaotaka kugombea urais.

Hii ni mara ya kwanza kwa
wabunge wa Nigeria
kurushiana ngumi bungeni.