JWTZ YATOA UFAFANUZI USHIRIKI WAKE CONGO NA KUKANUSHA UVUMI UNAOENEZWA NA BLOGS

JESHI la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania
limetoa taarifa ya
maendeleo ya wanajeshi
wanaoshiriki kulinda
amani kwa nchi
mwanachama wa maziwa
makuu Jamuhuri ya
Demokrasia ya Kongo
eneo la Goma.
Taarifa hiyo imetolewa na
msemaji wa Jeshi hilo
Meja Erick Komba
alipokuwa akiongea na
waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam.
Meja Komba alisema
kuwa baadhi ya vyombo
vya habari na mitandao ya
Kijamii hususan "blogs"
kuandika taarifa zisizo
rasmi ambazo zinapotosha
umma kuhusu ushiriki wa
Jeshi la Tanzania katika
nchi ya Kongo.

Alieleza kuwa jeshi la
Tanzania linashiriki
kulinda amani Nchini
Kongo kutokana na Rais
wa nchi hiyo Mhe. Joseph
Kabila kuwasilisha ombi
katika kikao cha nchi za
maziwa makuu
kilichofanyika Julai 12
mwaka jana mjini Addis
Ababa, Ethiopia baada ya
waasi wa M23 kujitenga na
Serikali na kuanzisha
mapambano.
"Ushiriki wa Jeshi la
Tanzania katika kulinda
amani nchini Kongo
umetokana na ombi
liliwasilishwa na Rais Mhe.
Joseph Kabila kwa nchi
wanachama wa maziwa
makuu ambazo ni
Rwanda,Uganda,Tanzania
na DRC kusaidia kulinda
amani na kuwapokonya
waasi wa M23
silaha"alisema Meja
Komba.
Meja Komba aliongeza
kuwa, jeshi la Tanzania ni
sehemu ya SADC Standby
brigade iliyotoa mchango
wake katika jeshi la Umoja
wa Mataifa (MUNUSCO)
kinachofanya kazi chini ya
"Force Commonder"
ambapo majukumu yake
makubwa ni kuzuia waasi
kujitanua, kuvunja nguvu
za waasi na kuwapokonya
silaha makundi yote ya
waasi.

Naye Msemaji wa Serikali
ambaye pia ni Mkurugenzi
wa Idara ya Habari
Maelezo Bw. Assah
aliwaomba waandishi na
wadau mbalimbali wa
habari kuandika habari
zenye uhakika na ambazo
hazitapotosha umma.
"Nawaomba waandishi na
wadau wa habari tuwe
tunatoa taarifa zilizo
sahihi ili tusipotoshe
umma ukizingatia jeshi
letu lipo huko kwa ajili ya
kulinda amani na siyo
kupigana na M23," alisema
Mwambene.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi
Kikosi cha Tanzania kiko
chini ya MUNUSCO ambao
ndio wanaoendesha
operasheni ya kulinda
amani na Tanzania
haipigani na M23 wala
haina tatizo na Rwanda
kuhusiana na operesheni
hiyo.
Pia Rwanda imesaidia
Tanzania kwa kuruhusu
kikosi kupitisha watu, vifaa
na zana kuelekea
Jamuhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo.